Thursday, 23 June 2016

MAHUSIANO BAADA YA USALITI.


Baada ya affair kutokea au kugundulika huwa ni wakati mgumu kwa wanandoa; jambo la msingi ni kwamba kuaminiana kulikoyeyuka huweza kurudi hasa baada ya hasira kwisha na wanandoa kuanza kuwa karibu kihisia tena.
Hii hutokea tu na pale tu kama wahusika wameelezana na kufahamu sababu za kwa nini affair ilitokea.
Ukweli ni kwamba kuelezea sababu za kwa nini affair ilitokea ni moja ya jambo gumu sana na pia ni moja ya jambo muhimu sana katika kuiponya ndoa.
Ni muhimu kujua sababu za affair kwa kuwa kama wewe ni uliyesalitiwa na mwenzako utatakiwa kujifunza kwa mapana yote kwa nini mwenzako alichepuka (affair) ili kuweza kurudisha ukaribu wa kimapenzi na kuaminiana upya.
Kama wewe ndiye umesaliti ni vizuri kuelezea sababu za kuchepuka kwako kwa sababu ndicho mwenzako anapenda kufahamu.
Kujua sababu za affair ni kuchambua au kuweka wazi sababu zilizofanya mwingine achepuke.
Ili kufahamu vizuri maana ya kwa nini affair ilitokea hebu tujaribu kuweka suala la affair katika ndoa kama vile nyumba inavyoingiliwa na majambazi usiku.

Baada ya nyumba kuvunjwa ni muhimu kuchunguza nini kilifanya majambazi kuvunja na kuingia kuiba kirahisi, ni mianya ipi ilisababisha hao wezi kuvunja na kuingia kirahisi?
Je, tatizo ni majirani hatari?
Na je, ulichukua hatua gani kujilinda na hao majirani ambao wamesaidia kuwapa majambazi data au siri na namna ya kuvunja na kuingia katika nyumba yako?
Je, uliwaona watu wageni ambao walikuwa wanapita karibu na nyumba na hukutilia maanani na ukaona ni jambo la kawaida?
Je, nyumba yako haikuwa na milango ya uhakika?

Kuingiliwa na majambazi na kuibiwa haina maana kwamba unawajibika na tabia mbaya za wale majambazi.
Hata hivyo ukihamia nyumba nyingine utajisikia secured kama utafahamu sababu zilizofanya majambazi kupata mwanya wa kuvunja na kuingia kukuibia nyumba yako ya kwanza.
Hutakuwa na uhakika wa usalama wako kuibiwa na majambazi kama hutafahamu sababu zilizofanya uibiwe mara ya kwanza.
Trust na usalama wa kuwa karibu kimapenzi katika ndoa umeharibiwa na mwenzako ambaye amekusaliti, kama majambazi walivyoingia na kuvunja nyumba na kuiba, hutakuwa salama hadi ujue sababu zilizochangia.
Au inawezekana mmoja wenu alikuwa na urafiki na mtu wa nje ambaye alikuwa hana heshima na ndoa yenu.
Pia inawezekana kulikuwa na dalili za mwenzako kutoka nje na wewe ukapuuzia. Inawezekana hakukuwa na ukaribu wa kimapenzi kati yenu na hiyo ikatoa mwanya kwa yeye kuvutiwa kihisia na mtu wa nje.
Inawezekana kuzozana kwenu kila siku kumefanya muwe mbali kimapenzi na kihisia hivyo kutoa mwanya kwa mwingine kutoka nje.
Inawezekana mmoja alikuwa hamheshimu mwenzake na alipopata anayemheshimu nje akaishia kuchepuka.
Inawezekana kulikuwa na ukame wa tendo la ndoa ndani ya ndoa yenu na mwingine akajikuta anapenda kutuliza kiu nje.
Au inawezekana ni shetani tu.............................
Ukishajua sababu basi inakuwa rahisi kubadilisha mambo na si wanandoa wote huwa tayari kukubaliana na hizi changamoto.

Wednesday, 22 June 2016

NI VIZURI KUZINGATIA KWANZA..


Inakuwaje watu wawili waliopendana deep idara zote inafika siku wanakuwa baridi na wanajiona ni watu wawili tofauti kabisa kwenye ndoa yao?

Kuna mambo mengi sana husababisha kuanzia na yale yaliyo ndani ya ndoa yao na yale yaliyo nje ya ndoa yao hata hivyo ukweli love is so terrible and is so important, kuna wakati mwingine mpenzi (mke au mume) anaweza kukupa au kukunulia gari au kukujengea nyumba ya uhakika lakini bado ikawa haina maana kama hatatimiza mambo ya msingi kuhusiana na upendo wake kwako.

Ndiyo unakuja ule usemi
“Buying very expensive gifts doesn’t make woman happy but real love and affections”

Kuna aina tofauti za migogoro na jinsi ya kukabiliana nayo, wengine mgogoro ukizuka hata majirani wanajua leo kuna vita kati ya Mr na Mrs wake na baada ya muda wanarudi kwenye mstari. Wengine vita vyao huwa slow, kimya kimya, hakuna kelele ni cold war na kila mmoja huanza mbali na mwenzake kihisia, kiroho na kimwili polepole ila matokeo yake ni hatari tupu.

Kama ni mwanandoa mpya ni vizuri kuwa makini katika maamuzi mbalimbali mnayofanya na kufikiria kwa makini huku ukiangalia zaidi ya miaka 5 ijayo, kwa mfano;

Jerry na Judy wameamua baada ya kuoana tu wanazaa mtoto haraka iwezekanavyo kwa kuwa kila mmoja ana kazi hivyo shida ipo wapi kama pesa zipo. (Ingawa ukweli pesa huwa hazitatui matatizo yote)

Hata hivyo uamuzi wa kuwa na mtoto haraka kabla hawajajuana vizuri na kufikia mahali wakawa wanafahamiana tofauti na uchumba ni jambo la msingi. (siyo lazima ukubali huu ushauri kwani inatokana mmejuana kiasi gani na mchumba wako)

Kuna watoto wakizaliwa huja na package ambayo mzazi hulali kama vile kulia (cry) muda wote na mke kumtumikia huyo mtoto all the time (acha ile ya kumaliza madaktari wote kujua kwa nini mtoto analia usiku mzima na wanakwambia hakuna tatizo) na kufikia mahali mume akawekwa pembeni kwani mtoto kwanza na wakati huohuo ndoa bado changa.

Mke hujikuta mtoto anamuhitaji na mume anamuhitaji na hawawezi kubalance kwani bado ni mgeni na hii institution.


Watoto wengine huwa na matatizo ya kula, kiasi kwamba mama hujikuta hawezi hata kumwachia mtu yeyote amtunzie mtoto na matokeo yake mama hujikuta muda wote anatumikia mtoto na wakati mwingine kuacha kazi (ajira) na pia mume kuwekwa pembeni.

Matokeo yake wanandoa hujikuta wanakuwa mbali na feelings kufa na kila mmoja anaanza kuona ndoa hairidhishi wakati hata miaka 2 haijamaliza.

Jambo la msingi ni mwanamke kufahamu vizuri aina ya mume uliyenaye kwani kuna wanaume ambao wanaweza kuwa baba na kuna wengine ni kazi, wanaendana na usemi kwamba:

“Men don’t become fathers overnight, where as women have strong maternal instinct in them”

Suala la kule mtoto linahitaji mke na mume wote kushirikiana kuhakikisha si mmoja ndiye anakuwa na mzigo zaidi.

Tuesday, 21 June 2016

KUPENDELEA MTOTO MMOJA ZAIDI YA WENGINE.


Tabia ya kumpendelea mtoto mmoja au kila mzazi kuwa na mtoto wake ambaye anagusa zaidi moyo wake ipo sana katika familia zetu.Wengi huwa hawataki kulitaja au kuliongelea kwa undani ingawa ni kweli familia nyingi zitakiri kwamba hili ni tatizo sugu na pia inawezekana wewe ni mmoja ya watoto waliopendwa au ambao hawakupendwa na moja ya wazazi wenu.

1.Kwa nini upendeleo hutokea kwa mtoto mmoja?

Inawezekana tabia ya huyo mtoto ni njema zaidi kuliko wengine, wakipewa kazi mmoja anafanya na mwingine hafanyi mara zote, anayetii hujikuta anapendwa zaidi.
Inawezekana tabia ya huyo mtoto ni rahisi na mwenzake au wenzake ni ngumu.
Inawezekana mtoto anafanana na mzazi zaidi kuliko wengine (tabia na mwonekano).
Inawezekana huyo mtoto anafanikisha matarajio ya wazazi wake au mzazi mmoja.

Inawezekana kwa sababu ni mvulana peke yake au msichana peke yake mzazi hujikuta anampenda zaidi.
Pia inawezekana talents zake au vipaji vyake vinafanana na vile mzazi anataka mtoto awe au inawezekana ndiyo values za familia.
Pia inawezekana mtoto asiyependwa ni mtoto ambaye ni mbishi au ni mtoa hamasa (challenge authority) kuliko mwenzake au wenzake. Mtoto ana njia zake au mitazamo yake kuhusu maisha na vitu hivyo wazazi au mzazi hujikutana wanabishana kila kitu.

Pia kuna mazingira ya kuzaliwa ambayo hufanya mtoto kupendelewa zaidi ya wenzake kama vile mtoto kuzaliwa siku au wakati (huohuo) ambao mzazi wa baba au mama (babu au bibi) yake anafariki, ingawa haina ushahidi wa kisayansi ila matukio mengi huonesha kwamba mtoto wa aina hii huonekana wa thamani kuliko wengine na ni kama vile roho ya babu au bibi huenda kwa mtoto anayezaliwa na wazazi kujikuta wanampenda kuliko kawaida.
Au inaweza kuwa ngumu sana mzazi kuweka bond na huyo mtoto kutokana na huzuni, stress na depression mzazi alipata wakati anazaa na wakati huohuo mzazi wake mwenyewe (baba au mama) naye anafariki.

Mtoto kuzaliwa bila kutegemea hasa baada ya wazazi kudhani wamemaliza kuzaa.
Mtoto kuwa na matatizo ya afya hivyo wazazi kutumia muda mwingi kwake na wengine kujiona mwenzao anapendelewa.
Wakati mwingine inatokea tu mzazi hujikuta anampenda mtoto fulani katika familia kuliko wengine.

2. Nini mojawapo ya Dalili za mtoto kupendelewa?

Kununuliwa zawadi zaidi ya wenzake.
Kutoa adhabu rahisi kuliko wenzake kwa kosa moja, wenzake wanakula fimbo yeye anaonywa tu.
Sherehe au sikukuu zake kuwa tofauti na wenzake kwa jinsi zinavyoandaliwa nk.
Wenzake wakiomba kitu hichohicho wanakataliwa lakini yeye anapewa au kuruhusiwa.
Mzazi kutumia jina lake kumaanisha watoto wake wote kama vile baba anarudi kazini na watoto hawapo na mtoto anayempenda anaitwa Ben na badala ya kuuliza watoto wapo wapi yeye anauliza “akina Ben wako wapi?”

Tumia muda mwingi na mtoto mmoja.
Kuonesha upendo wa dhahiri kwa mtoto mmoja nk nk nk.

3.Je, mtoto ambaye anajisikia hapendelewi na mzazi au wazazi hujisikiaje?

Mtoto anakuwa na wakati mgumu sana kujikubali na kujipenda mwenyewe kwa kuwa anaamini mzazi/wazazi hawampendi na anaweza kuwa na tatizo sugu la kutojiamini (chronic low self-esteem)
Mtoto hujiona duniani hakuna haki na kwa kuwa hatendewi haki na yeye anaweza kuanza kutowatendea haki wengine.

4.Je, mtoto anayependwa anaweza kupata madhara yoyote?

Ukweli ni kwamba hata mtoto ambaye anajiona anapendwa pia anaweza kupata tatizo la kukosa kujiamini kwani anakuwa too much spoiled.
Kwa kuwa anapendwa basi atajitahidi kufanya zaidi kwani anaamini asipofanya kila kitu juu anaweza kupoteza kuendelea kupata upendeleo hivyo kama ni shule atajitahidi kupata grades za juu, kama ni tabia atajitahidi asikasirike nk na matokeo yake atakuwa hajiamini na anaweza kupota msongo mawazo.

Mtoto anayependelewa anaweza kuwa si mzuri sana linapokuja suala la wenzake wa rika moja au walimu au watu wengine kwenye maisha kwani kile kitendo cha kujiona anapendelewa na wazazi au mzazi humpa kakiburi Fulani.

Mtoto anayependwa hujiona yeye ndo mzuri na huwa hakosei hata hivyo maisha hayako hivyo na matokeo yake atakuwa na wakati mgumu mbele ya maisha hasa llikija suala la kupambana na matatizo.

Hasara ya kumpendelea mtoto mmoja huendelea hadi kwa wajukuu na inaweza kuleta matatizo na migogoro kwa kuwa wajukuu wa watoto wote huanza kuzozana kwa kuwa mmoja wa wazazi wao alikuwa anapendwa zaidi na babu au bibi.


5.Je, kwa mume na mke ni tatizo?

Ndiyo kunaweza kutokea mgogoro kati ya mke na mume hasa kwa mtoto mmoja kupendelewa na mzazi mmoja, kwa mfano baba anampa fedha nyingi zaidi mtoto mmoja anayempenda bila kujali ni mdogo kuliko wenzake, mama akiona au kusikia naye huja juuu kitendo ambacho kitafanya ndoa iwe katika mzozo.

6.Je, unaweza kuepuka vipi kumpendelea mtoto mmoja?

Kwanza wewe mzazi jikubali kwamba wewe ni binadamu na kwamba katika watoto wako mmoja anakubalika kwako zaidi kuliko wengine.
Wasikilize watoto wengine ambao wanakwambia unampendelea mwenzao na usijilinde, wasikilize na anza kufanyia kazi yale wanasema (kuacha kumpendelea mmoja)

Gundua utofauti wa kila mtoto na kile anapenda kufanya (characteristics, skills, interest) na mhudumie kutokana na vile anavipenda.

Usiwalinganishe au kumsema mmoja kwa sababu ya mwingine kwani kila mtoto yupo tofauti, sentensi kama “mwenzako Ben akirudi shule anafanya homework yake vizuri na anamaliza wewe hadi ulazimishwe!”
Ni kweli amekosea hata hivyo kila mtoto yupo tofauti na kila mtoto anatakiwa kuambiwa kama yeye na si mwingine.
Kama unanunua zawadi ni vizuri kununua zawadi zinazolingana siyo mmoja unanunua zawadi ya Tsh. 100,000 na mwingine Tsh. 20,000
Tumia muda vizuri na sawa kwa watoto wote.

Kumbuka jinsi unavyozidi kuwa na watoto wengi ndivyo utakuwa na kibarua kigumu zaidi, kwani unahitaji kutafuta muda maalumu kwa kila mtoto na kugundua kipaji chake na kuhakikisha unakiendeleza sawa na watoto wengine.

Jambo la msingi ni kila mzazi kumpa (treat) kila mtoto sawa katika hali zote na juhudi za ziada zinahitaji katika mazingira ya nyumbani kuhakikisha watoto wote wanalelewa sawa na kila mmoja kujiona ana thamani sawa kwa wazazi mmoja mmoja na kwa pamoja.

Thursday, 16 June 2016

NDOA IMARA NA ZINAZODUMU.


Ukiona kosa moja kwa mke wako au mume wako, hutakiwa kuliangalia na kuliwekea sura kamili au hutakiwi kulipa uhai badala yake lipe jina na liweke kando kwa kujaribu kulinganisha na uzuri wake au mambo matano mazuri kuhusu yeye(positive traits).


Kwa mfano unajikuta mume wako au mke wako amewaka hasira kwa jambo dogo tu hadi unahisi dunia umebadili mwelekeo, hata hivyo badala ya kuanza kufikiria hizo hasira zake Unachotakiwa kufanya ni kujiambia mwenyewe kwamba:

“ Ni kweli ana hasira hata hivyo ni mwanamke/mwanaume anayenijali, anayenipenda, anayewajibika, ni mbunifu na anajua kuniridhisha chumbani”.

Kumbuka strongest relationships ni zile ambazo partners wanaweza kujenga picha ya uzuri wa mwenzake (idealized/illusioned) kuhusu uwezo wake na si udhaifu.


Kwa kuufuta udhaifu au kuondoa mawazo kuhusu udhaifu wake na kuweka uwezo wake au uimara wake unahusanisha information muhimu za kufanya mke wako au mume wako awe mzuri zaidi na ukampenda zaidi.

Kwa miaka zaidi ya 100 hekima na busara iliyodumu na ambayo hata wengine wanaamini ni ile kwamba kinyume cha uzuri ni ubaya.

Hii ina maana kwamba Ukitaka kujua uzuri wa kitu basi unatafuta ubaya wake kwanza.

Ukitaka kujua furaha ni kitu gani au ina thamani kiasi gani unajaribu kumchunguza mtu mwenye huzuni kwanza.

Watoto ambao wanatumia madawa ya kulevya hutumika kujua namna ya kuwalinda watoto wasiotumia madawa ya kulevya wasijiingize kwenye hivyo vitendo.


Watoto ambao ni watoro shuleni hutumika kujifunza kuwafanya watoto wengine wawe na mahudhurio mazuri.


Linapokuja suala la ndoa si kweli kwamba ili kujifunza ndoa kuwa nzuri au kusiwe na talaka basi ni vizuri kujifunza ndoa ovyo au ndoa ambazo zimeishia kwenye talaka.

“Bad is not always the opposite of good”

Ukweli ni kwamba linapokuja suala la ndoa Ukitaka kujenga ndoa nzuri au imara unahitaji kujifunza kutoka ndoa imara na si ndoa ovyo au zile zimeishia kwenye talaka.

Vitu vinavyopatikana kwenye ndoa imara havina uhusiano na vitu vilivyosababisha ndoa ovyo kuwa ovyo kwani ndoa imara zina siri yake ambayo si kinyume cha ndoa ovyo.


Ndoa imara ni zile ambazo mwanandoa mmoja au wote huwa na picha kamili ya mwenzi wake, huwa na sifa ambazo amezijenga kwa mwenzi wake ambazo ukweli ni kwamba inawezekana kwamba mwenzi wake hana ila yeye huamini anazo na ni kuwa positive kwamba anamfaa.

Ndoa imara na zinazodumu ni zile ambazo mwanandoa huamini katika uimara au uwezo wa mke wake au mume wake hata kama huo uwezo hana.

Unaweza kuona kama ni utani au contradiction hata hivyo ndio ukweli.

Nina amini mke wangu ni caring, nina amini mke wangu ni sweetie, nina amini mke wangu ananifaa, nina amini mke wangu ni mzuri, nina amini mke wangu ni mchapa kazi, nina amini mke wangu ni mrembo, nina amini mke wangu ananifaa hata kama hizo sifa hana kwa kuwa naamini basi ninavyoamini ndivyo itakuwa na nitakuwa na furaha kuliko kuwaza vinginevyo.

NI VIZURI KUWA WAZI.


Kawaida linapokuja suala la mapenzi opposite attract na the same repel kwa maana kwamba mara nyingi huwa tunavutiwa na strength za mwingine kwa kuwa hufanana na weakness zetu.
Watu ambao hutuvutia sana ni wale ambao huonesha strength katika maeneo ambayo sisi tupo weak.

Ukikutana na mtu wa jinsia tofauti na wewe na mkawa pamoja kwa muda mrefu pamoja na ukavutwa kutokana na strength zake ambazo zinakubaliana kwenye weakness zako penzi huzaliwa na baadae inaweza kuwa ndoa

Ndoa ni kuwekana wazi.

Wakati Bwana harusi na Bibi harusi wanaposimama mbele ya Mhubiri kanisani na kutoa ahadi zao kwa Mungu na wageni wote walioalikwa huwa wanaahidiana kwamba
“Ninakuahidi kukupenda na kukunyenyekea kwa muda wote wa uhai wetu”
Hii ina maana kwamba maharusi huwa wanakazia kwamba kwa kuwa nakubali kiapo chako na unyenyekevu wako kwangu leo basi nitajifunua kwako mzimamzima kuanzia sasa si kimwili tu bali kisaikolojia pia kwani hadi hapa nimejidhihirisha/nimejifunua kwako katika upande ule wa mazuri tu (strength) kuhusu mimi.
Sasa kwa kuwa tunaoana nitajiweka wazi kwako mzimamzima na nina imani kubwa na wewe kwamba utaendelea kunipenda kama nilivyo.

Ndoa ni kuwekana wazi, ni kila mmoja kujidhihirisha kwa mwenzake kama alivyo pamoja na weaknesses zake.
Vitu vyote ambavyo vilikuwa vimejificha wakati wa uchumba hadi honeymoon basi kuanza kwa ndoa vyote huwa mezani juu kwa kila mmoja kuona.
Na hapo ndipo kwenye mtihani wa kwanza wa wanandoa wapya.
Honeymoon siyo residence ya kudumu ya ndoa, baada ya honeymoon (na wengine hata wakati wa honeymoon) wanandoa wapya hushikwa na mshangao wa partner anavyobadilika na kuwa kama mwingine kabisa.
Ukweli ni kwamba unapoona partner wako anaonekana kama mwingine tofauti na yule wa wakati wa uchumba, ukweli ni kwamba sasa matching inaanza, kufahamiana kikwelikweli kunaanza na wenye hekima na busara huwa makini katika kukabiliana na hizo tofauti na kuendelea kusherehekea hizo tofauti kwa upendo na kuvumiliana kwani huwezi kumbadilisha na kumbadilisha ni kupoteza muda wako.

LOVE MAY BE BLIND BUT MARRIAGE IS A REAL EYE-OPENER.

Wednesday, 15 June 2016

TOFAUTI HUWA HAZIKOSEKANI.


Wanandoa imara au waliofanikiwa katika ndoa yao ni wale ambao wanaweza kukaa pamoja na kujadili tofauti zao katika namna ambayo huwezesha kujenga ukaribu kimapenzi (intimacy) zaidi.

Wanafahamu jinsi ya kukubaliana na kutokukubaliana, wanafahamu namna ya kuhakikisha kutokukubaliana hakusababishi maafa kwenye maeneo mengine ya mahusiano yao.

Si kweli kwamba tunaolewa au kuona ili kuchukuliana katika migogoro hata hivyo kutofahamu namna ya kupambana na migogoro huweza kusababisha kutofanya vizuri katika mambo mengine ambayo ndo sababu za kuoana.

Kukwepa migogoro au kukwepa kuongea pamoja eti kunaweza sababisha mgogoro mzito si hekima wala busara kwani njia bora ni kuwa wazi kuongea pamoja ili kujadili tofauti au kutokuelewana kunakojitokeza ili wanandoa waweze kufahamiana zaidi.

Kwa lugha nyingine si rahisi mke kufahamu mume anapenda chakula gani bila kuongea kwanza, pia haina maana kukaa kimya kwa kuwa mke anapika chakula usichopenda basi atabadilisha na kukupikia chakula unapenda. Si rahisi mume kukupeleka outing kama hamuongei.

Wapo wanandoa ili kuepuka migogoro huacha kuongea na kuwa kimya, ni muhimu sana wanandoa kufahamu utafiti wa ndoa imara unasemaje.
Kila ndoa imara kwa wastani ina maeneo 10 ambayo wanandoa hawafanani au hawawezi kukubaliana au kwa lugha nyingine hawataweza kufikia muafaka maishani mwao.

Kwa nini hizi ndoa imara pamoja na tofauti 10 na bado zinaitwa ndoa imara?

Jambo la msingi au siri kubwa ni kwamba wanandoa wanafahamu namna ya kukabiliana na hizo tofauti na kuishi nazo, kupendana pamoja na kutofautiana na zaidi kila mmoja anamuelewa mwenzake na kukubaliana kihisia na kuchukua nafasi yake kama ni yeye.

Wanandoa imara hufurahia na kusherehekea tofauti zao na hufarijika kwa kuwa sasa anamfahamu mwenzake, anajua eneo ambalo wapo tofauti then wanaaendelea kupendana huku kila mmoja akifahamu namna ya kukabiliana na hizo tofauti.

Hawa wanandoa imara wanafahamu wazi kabisa kwamba hata kama watabadilisha partners bado watapata matatizo mapya katika maeneo ya kutokukubaliana, kuwa tofauti na kwa huzuni kubwa kazi kubwa itakuwa ni mizigo waliyotoka nayo kwenye ndoa zao za kwanza kama vile watoto nk ndiyo maana kwao talaka haina sauti wala nguvu na huwa haizungumzwi, ni neno lililofutwa katika maongezi.
Zaidi ya kukabiliana na tofauti na kutokukubaliana pia ni muhimu sana kusherehekea/kumbatia (embrace) mabadiliko.
Wakati tunaoana huwa tunaahidi kukaa pamoja hadi kifo kitakapo tutenganisha hata hivyo huwa hatuahidi kubaki vilevile bila mabadiliko yoyote, tunahitaji kukua, kuongezeka skills, kwa wabunifu na wazuri zaidi kila siku zinavyozidi kwenda.
Kuna mambo mengi tunaweza kujifunza kadri ziku zinavyozidi kwenda kama vile kusema asante, kuomba msamaha.
Hivyo inawezekana kujifunza tabia njema ambazo zinaweza kujenga ndoa na kuziacha tabia mbaya ambazo zinaweza kuharibu ndoa.

MTAZAMO WAKO UKOJE?


Huwezi kuongelewa mapenzi bila kutaja suala la pesa. Wapo watu ambao wanaamini kuwa na pesa nyingi, nyingi kabisa za kutosha husaidia pesa kuwa imara na linaloridhisha.
Hata hivyo tumeona penzi la uhakika hata wakati pesa zikiwa hazipo au tumeona penzi la kweli hata katikati ya umaskini uliokithiri.
Hii haina maana kwamba pesa siyo muhimu, pesa ni muhimu sana. Na pesa ina umuhimu kwa kila mahusiano hata, hivyo inabidi ujiulize mwenyewe je, upo kwa ajili ya pesa au kwa ajili ya penzi la kweli.
Utakuwa mtu wa maana sana kama utakuwa unatazama na kuwekeza kwenye penzi la kweli na si pesa.
Pia ni vizuri kuwa makini na mtazamo wa mpenzi wako je yupo kwako kwa ajili ya pesa au kwa ajili ya penzi la kweli.
Mtazamo wake kuhusu pesa ni muhimu sana.

Saturday, 11 June 2016

TABIA HIZI WAKATI MWINGINE ZINAKERA KTK NDOA.


Kuna wakati mwanandoa mmoja anajikuta yupo ndani ya ganda la yai kwa maana kwamba anajikuta anakabiliana na mke au mume ambaye anadhibiti, anayeamulisha, anapenda ufyate ulimi, anakukalia kooni, huna hiari yako na anakusimamia kila kitu.


Judy ni mmoja ya wanawake ambao wanatabia ya kufanya auditing hadi chumbani.

Kwanza mumewe huambiwa asahau tendo la ndoa siku za wiki (weekdays), labda Ijumaa usiku au Jumamosi usiku, pia watoto lazima wawe wamelala dakika 90 zilizopita na wawe kweli wamelala fofofo kwa kukaguliwa zaidi ya mara tatu na kuthibitisha kwamba kweli wamelala folilo kabla ya wao kuingia kwenye sita kwa sita.


Mume wake lazima ahakikishe ameoga kwa dakika 30, ahakikishe ametumia sabuni, kitamba (washcloth) na kupiga mswaki, akitumia dakika pungufu ya hizo lazima ataambiwa hajaoga akawa safi (amelipua) hivyo hawezi kupata unyumba (kama una hasira hapa nyumba haitoshi).

Pia mume anatakiwa ahakikishe anatandika taulo sehemu ambayo yeye Judy atalala wakati wa tendo la ndoa kitu kinachofanya eneo la kufanyia mapenzi kuwa dogo.


Anatakiwa kuhakikisha taa zimezimwa wakati wa tendo la ndoa na wanaenda kulala kabla ya saa nne usiku siku ya kupeana unyumba.

Pia kunatakiwa kusiwe na sauti ya binadamu au kitu chochote ndani ya mita 500 vinginevyo hakuna unyumba.

Ni kweli ni muhimu sana binadamu kuwa na taratibu lakini taratibu zingine badala ya kuwajenga wanandoa huwabomoa na kuwa vipande vipanda ambavyo kuvirudisha inakuwa ngumu maradufu.


Mume wa Judy itafika siku atasema “enough is enough”


Jeffy ni mwanaume ambaye kwake kila kitu ni utaratibu, akikwambia anapiga simu saa mbili kamili ni kweli atakupigia saa mbili kamili. Akikwambia atakuwa mahali fulani saa fulani, count him there. Jumamosi anakata majani kuzunguka nyumba yake na Jumapili jioni anaosha gari lake, kwa ufupi shughuli zake zinafanywa kwa mtindo wa saa.


Likija suala la tendo la ndoa na mke wake basi utaratibu wake ni kila baada ya siku tano, penda usipende mwanamke awe anataka au hataki period.

Kutokana na tabia za controlling wapo wanaume wamefanya wanawake kujisikia baridi kali mwilini kila mlango ukigongwa mume anapofika nyumbani kutoka kazini na kumfanya mwanamke kuwa turned off ile jioni na usiku mzima.


Hapa haijalishi umesoma au hujasoma, upo smart au ovyo, tajiri au maskini, kumbuka skills zinazokufanya ufanikiwe kazini kwako wakati mwingine ndo skills zinazofanya ushindwe masuala la chumbani kwako na mke wako au mume wako.

Tabia za kudhibiti na kutaka kila kitu kufanyika kwa umakini wa kupindukia (Control & Perfection) wakati mwingine huharibu mapenzi na ndoa badala ya kujenga.

ANA MTAZAMO GANI KUHUSU PESA?


Watu tunatofautiana katika mitazamo kuhusu fedha, baadhi huiangalia fedha kwa jicho la kutoa (giving) na wengine kwa jicho la kuitunza (saving) na wengine kutumia (spending)

Kama wewe ni kijana wa kiume au kike ambaye upo katika harakati za kusaka mwenzi wa maisha basi ni muhimu sana kuwa na makubaliano au kufahamu mtazamo wa huyo mtarajiwa kuhusu fedha.


Judy ni mwanamke ambaye mume wake Jeffy akipata mshahara huamuriwa akabidhiwe na anachofanya ni kugawa zile pesa na kuziweka kwenye bahasha tofauti tofauti, bahasha moja kwa ajili ya kununua chakula, bahasha nyingine usafiri, nyingine pango la nyumba, nyingine kununua nguo na nyingine sadaka kanisani na nyingine kwa ajili ya dharura.


Mume akitumia pesa kutoka moja ya bahasha lazima aeleze ni bahasha ipi alichukua pesa, na amefanyia kitu gani, na risiti ziko wapi na change zipo wapi na duka gani alienda kununua na alikuwa na nani na ametumia usafiri gani na amelipa kiasi gani.

Jeffy hujikuta oppressed, frustrated na hawezi kuvumilia tena!


Je, unadhani hiyo ndoa itadumu kwa muda gani?


Kumbuka wengine hutumia pesa kama emotional agenda, kama kwenye huo mfano bahasha za Judy si bahasha tu bali ni mfuko anaotumia ku-mcontrol Jeffy.

Kuna watu walitembelea ndoa moja na ilikuwa ni summer time na joto lilikuwa limepanda nyuzi 40 centigrade.

Ikafika mahali watu wakawa wana sweat utadhani wapo ndani ya sauna wakati huohuo nyumba ilikuwa na viyoyozi vya uhakika ila vimezimwa kwa utaratibu kwamba hadi ifike tarehe iliyowekwa ndipo huwashwa.

Wanandoa walipoulizwa kwa nini kuzima wakati joto linatuua, wakawajibu tarehe tuliyoweka kuwasha viyoyozi haijafika bado na kuwasha sasa ni matumizi mabaya ya pesa.

Hawa wanandoa wanafurahia ndoa yao kwa kuwa wanamtazamo sawa kuhusu fedha na hakuna kulemba!

Kuna wanawake ambao kwao fedha za mume ni za familia, na pesa zake ni zake.

Hii ilitokea kwa Suzy na Simon wakati fulani ambapo Suzy alikuwa anafanya kazi na Simon naye alikuwa anafanya kazi.

Simon akipata mshahara, Suzy humkomalia na kupanga bajeti namna ya kutumia hizo fedha kwani anachojua ni kwamba mshahara wa mume ni wa familia na mshahara wake ni kwa ajili yake tu.

Hata Simon alipotaka kununua kitu kutokana na ule mshahara basi Suzy huja juu kwa kuanza kutoa lecture kwa Simon namna watoto wanavyohitaji nguo na vifaa vingine wakati huohuo yeye Suzy pesa anayopata kazini kwake anaila kisirisiri.

Mitazamo kama hii huweza kuharibu ndoa kwa kasi ya ajabu kama dhoruba.

Angalia kwa makini yule unategemea kuwa mke au mume anazielewaje fedha kama unaona mtazamo wake ni wa ajabu ajabu ushauri wangu ni kwamba fikiria kwa makini kabla ya kuchukua uamuzi wa kuwa naye.

NI KUJIDANGANYA.


Kuna usemi mmoja wa kingereza unaosema:

“Someone is better than no one”

Kwa maana kwamba wapo watu ambao (hasa wanawake wale ambao wanaona muda unaenda bila kuwa na mchumba au mpenzi wa kuwa naye katika maisha) huamua kushikana na bora mwanaume kwa imani kwamba ni heri kuwa na huyo mmoja (unfaithful, untrustworthy) kuliko kutokuwa na mwanaume yeyote.


Subiri kidogo nikwambie!

Kujiingiza kwa mwanaume ambaye moyo wako hauko radhi eti kwa sababu unataka na wewe uonekane una mpenzi au una mchumba au una mume ni kuumiza hisia zako.

Hata kama unaamini utafanikisha matakwa yako bila kuunganishwa emotionally, intellectually au affectionally utaishia kuumizwa.


Pia huyo someone ambaye unaona ni afadhari kuliko kuwa mwenyewe ni looser ambaye anakuzuia wewe kumpata anayefaa, kwa lugha nyingine huwezi kumpata mwanaume mwenye sifa njema kama utaendelea kukaa au kushikamana na huyo someone wako ambaye hata hivyo ana sifa ovyo.

Wengi wanajuta kwa sababu ya kuamini kwamba "someone is better than no one, hata hivyo waliokiri kwamba "no one is better than a relationship that lack respect" wanapeta.

JE,NIKIMPA HATANIKIMBIA?


Kaka asante sana kwa mafundisho yako na tunajifunza mambo mengi sana kuhusu ndoa na mahusiano.
Mimi ni mdada ambaye kweli Natamani kuolewa hata hivyo mchumba wangu anasisitiza kwamba tufanye mapenzi kwanza (sex) ili ajue nampenda.
Je, mapenzi kabla ya ndoa si ni jambo baya?

Dada asante kwa swali zuri na swali lako si mara ya kwanza kulijibu hapa hata hivyo kila siku tunajifunza kitu kipya.
Kwa ufupi ni kwamba kawaida mtu huhitaji kile ambacho hana.
Kama mchumba wako anakutaka kimapenzi (sex) kabla ya kuoana na wewe kwa ujinga wako ukamkubalia maana yake mkishamaliza kufanya mapenzi mwenzako atakuwa hana kitu cha kuhitaji kutoka kwako ili akuoe.
Umeshajiuza kwake kwa bei rahisi kabisa.
Kumbuka na fikiria upya, ukijirusha na mchumba wako kitandani hata kama mtakuwa mmejifunika shuka gubigubi ataona kila kitu mwilini mwako na atafahamu kila kitu kuhusu wewe.
Kwa mfano ataona alama mbalimbali mwilini mwako kama vile ukubwa wa matiti, chuchu, makovu ulivyonayo, tumbo, makalio, mapaja, sehemu za siri (kipara au msitu), mgongo wako, kiuno chako.
Atafahamu jinsi na namna unavyoguna kimapenzi, unavyobusu kwa kutetemeka, atajua harufu yako ukiwa uchi, atafahamu unavyolala kama gogo au ulivyo na kiuno kizito au ulivyo na aibu au ulivyo na maji au ukavu huko chini na mengine mengi.
Yaani ameona na uchi wako, una nini tena cha kumfanya akusubiri na kukuona special?

HUNA!

Kumbuka kwa kuwa anakutaka maana yake ameshatembea na mabinti wengi hivyo mambo yote nimeandika hapo juu atakuwa analinganisha na wale alitembea nao na kuangalia wewe umekuwa mshamba kiasi gani na kama anakuacha akuache lini.
Sasa hana shida tena kufikiria kuhusu wewe bali kukumbuka tu vile ulikuwa unafanya au ameona na anachofanya analinganisha na wanawake aliotembea nao na kuona wewe hakuna jipya cha maana ni kukubwaga chini na kutafuta mwingine.
Umeshaharibu maana ya vile alikuwa anategema kupata kutoka kwako au tuseme hana chochote cha kutegemea kutoka kwako maana umeshaonesha na kumpa kila kitu.
Kumbuka hana mkataba wowote na wewe na ana uhuru wa kukuacha kwani huna jipya kwake, hana kitu kinachomfanya ajisikie kukisubiri kutoka kwako maana anakujua ulivyo na Umeshajiuza kwa bei rahisi hivyo ana hiari ya kutafuta binti mwingine.
Mapenzi kabla ya ndoa ni dhambi, ni vibaya na ni sababu kubwa ya wengi kutooana na pia ni muhuri wa kukubaliana kwamba ndoa yenu haitakuwa na uaminifu.
Mchumba anayekutaka kimapenzi kabla ya ndoa mkimbie kwa kasi ya ajabu na usigeuke tena nyuma!

INAWAHUSU SANA WANAUME.


Kama mwanamke atajiona yupo appreciated nje ya chumbani basi akifika chumbani atakuwa mwenye furaha (excited), hivyo haina maana kusubiri umpe maneno matamu akiwa kitandani badala yake mpe maneno matamu kuanzia jikoni au sebuleni.

“Never tell a woman she is beautiful when lights are off”

Mwanamke ana hamu kubwa ya ukaribu wa kimapenzi (intimacy) kutoka kwa mume wake, kujisikia yupo karibu na connected.


Kwa mwanaume sex hutokea kule downstairs chini ya mkanda ulivaa, kwa mwanamke sex ni upstairs, kwenye kichwa chake (brain).

Ndiyo maana kwao foreplay ndiyo mfumo wa maisha ya mapenzi.

Na ndiyo maana hawafiki kileleni mara zote.


Wanawake hutumia muda mwingi kuwaza ni kitu gani wanaume wanahitaji katika mahusiano na tatizo kubwa ni kwamba wanaume wachache sana huwaza kuhusu nini wanawake wanahitaji katika mahusiano, basi unahitaji kuwa mmoja ya wanaume ambao si kuwaza tu bali wanafanya kile wanawake wanahitaji.


Mwanamke anapoongea usimkatishe kwani ndiyo njia pekee ya yeye kuwa karibu na wewe.

Kumbuka anapokwambia matatizo yake wakati mwingine hana maana umpe majibu namna ya kutatua (fix the problem) bali anahitaji wewe umsikilize tu na wewe kumsikiliza maana yake unamjali.


Kwa mwanaume fedha ni status hata, hivyo kwa mwanamke fedha ni security, hivyo usiseme fedha zangu, bali sema fedha zetu.

TOFAUTI YA MAWASILIANO KTK NDOA.


Mtazamo wa mwanaume na mwanamke kuhusiana na suala la mawasiliano ni vitu viwili tofauti kabisa.

Wanaume huwa na ulimwengu wao sawa na wanawake ambao nao huwa na ulimwengu wao linapokuja suala la kuwasiliana au maongezi kati ya mke na mume.


Wanaume huwa na ulimwengu wa ngazi (hierarchical social order) kwa kujiweka nafasi ya kutawala, kuwa na amri au kuonesha mafanikio au uhuru na mamlaka aliyonayo kwa wengine. Hii ina maana kwake kuongea ni pamoja na kuhakikisha hayo yametajwa ni jambo la msingi.


Lengo kubwa la mawasiliano au kuongea katika ulimwengu wa wanaume ni kutunza uhuru wao na kuimarisha nafasi yao katika ngazi ya kijamii.


Wanawake kwa upande wao, linapokuja suala la mawasiliano au kuongea ni yeye mwanamke binafsi kujihusanisha au kujijumuisha katika ulimwengu wa wengine (networking).

Kwa mwanamke kuongea ni kuimarisha ukaribu (intimacy) kwa maana kwamba kwa mwanamke kuongea ni suala la feelings.

Mawasiliano au kuongea ni gundi ambayo huwaunganisha wanawake pamoja wao wenyewe au mwanaume na kuongea humfanya kujisikia karibu na yule anaongea naye na wakati mwingine huondoa upweke.


Tangu wanawake wakiwa na umri mdogo, akitokea binti mwingine akawa haongei basi wenzake kumlaumu kwa tabia yake ya kuwa antisocial.


Kwa kuwa wanaume huongea ili kuimarisha status zao ndiyo maana utakuta wanaume wengi huongea kwenye public.

Wanapenda kutoa reports kwenye mikutano, hutoba katika makundi ya watu na kubadilishana habari kazini na wafanyakazi wengine na huko wanang’aa lakini wakifika nyumbani wanakuwa kimya kwani wanajua nyumbani ndipo kwenye uhuru wao wa kuwa silent.


Kwa wanawake nyumbani ni mahali pa kuongea kwa uhuru na ukaribu (intimately), nyumbani ni mahali mwanamke anasubiri kwa hamu kuongea na mume wake anayempenda.


Data nyingi zinaonesha wanaume wengi huongea kwenye public kuliko wanawake na wanawake wengi huchonga sana majumbani.


“Kumsikiliza mwanamke maana yake umesema unampenda”


Kwa mwanaume kuongea ni kuwasilisha habari, kuimarisha status au njia ya kutatua tatizo, kwa mwanamke kuongea ni kuhusisha ukaribu wa ndani (sharing) na mwingine.


Wanawake huwa wanawashangaa sana wanaume kuhusiana na suala la mawasiliano.

Mwanaume A na mwanaume B wanaweza kuangalia TV bila kuongea na kesho wakasema ni marafiki, kitu ambacho kwa wanawake ni vigumu kwani urafiki kwa mwanamke ni pamoja na kuongea.

Wanaume hutumia mfumo wa kuwasiliana kwa kutumia kitu cha tatu (triangulation)

Hii ina maana mwanaume A na mwanaume B ni marafiki kwa kuwa wametumia kitu cha tatu TV kuwapa attention na kujikuta wameunganishwa.


Hii ina maana gani?

Hii ina maana kwamba kama mwanamke ana mume ambaye anachonga sana kwenye public na akifika nyumbani anakuwa bubu ili huyu mwanaume aongee inabidi mke atafute kitu cha tatu inaweza kuwa kufanya kazi yoyote kitu ambacho wote pamoja watakuwa wanafanya na katika kufanya mwanaume utajikuta anaongea.

HUWA WANAANGALIA WENYE MAFANIKIO.


Ni kama miongo mitatu sasa wanaharakati wamejitahidi kuwafanya wanaume wajisikie aibu kuvutiwa kimwili na mwanamke anayevutia katika mwonekano wake.
Ingawa ni kweli wanaume walizaliwa kuona (born to see).
Ni kweli huvutiwa na kushtuka pale mwanaume akikutana na mwanamke anayependeza na kuvutia.
Macho mwanaume yanauwezo wa kuona (scanning) mwanamke anayevutia katika kundi la mamia ya Wanawake utadhani macho yana lensi za kivita kwa ajili ya kurusha makombora kwa usahihi.
Au mwanamke anayevutia akipishana na mwanaume (si wote) lazima afanye juhudi ya ziada kuhakikisha mboni ya jicho inakaza kule alikuwa anaangalia vinginevyo anaweza kusababisha ajali.
Tukija suala la Wanawake; ingawa wao hukataa ukiwauliza ila ndani yao ukweli hujieleza kwamba mwanamke huvutiwa na mwanaume kutokana na mafanikio au uwezo alionao katika jamii.
Kuna usemi wa kingereza kwamba:

“Men are evaluated by income and professional status while women are evaluated by their looks”

Hii ina maana mwanamke na mwanaume wapo wired tofauti linapokuja suala la kumpata mwenzi au mtu wa kuishi naye pamoja.

Mwanaume hutafuta mwanamke ambaye anavutia, mwanaume huona uzuri wa mwanamke kuliko akili ya mwanamke kichwani mwake.

Mwanamke hutafuta mwanaume ambaye ana mafanikio, mwanamke huona akili ya mwanaume kuliko uzuri wake wa sura.

Ndiyo maana kuna utani kwamba mwanaume akiwa na pesa hata kama ana sura inayofanana na chimpanzee bado Wanawake watamuona ni handsome wa nguvu.

Je, ukiwachukua mabinti wanaomaliza chuo na kuwauliza kama wapo tayari kuolewa na mwanaume ambaye atakuwa na kipato cha chini kuliko wao watakubali?

Je, ukimuuliza binti yeyote ambaye ana taaluma yake na anataka kuolewa kama atakubali kuoana na mwanaume asiyevutia ila ana kazi nzuri na kipato cha uhakika?
Si rahisi kwa mwanamke kukubali kwamba anahitaji mwanaume mwenye mafanikio au akili ya maisha ili aoane naye ingawa katika ukweli mwanaume mwenye mafanikio au akili ya maisha humfanya mwanamke kujiona yupo protected, ni mwanaume ambaye anayeonekana anaweza kuwajibika au kwa lugha nyingine si pesa alizonazo bali ule uwezo wa kupata pesa alionao ndiyo humvutia mwanamke.

Ndiyo, wapo wanawake huvutiwa na wanaume walichacha (pigika) au wengine hubeba mwanaume yeyote hata hivyo mwanaume kuwa na pesa ni sexy na mwanamke anajua kuwa na mwanaume asiye na akili ya maisha au uwezo kifedha atatumia muda wake kuishi naye huku akiwa na hofu na mashaka kuhusu pesa.
Kwa wanawake wengi “money is security” najua utabisha ila ndo ukweli!

KUFIKA KILELENI KWA MWANAMKE.


Je, kufika kileleni kwa mwanamke anapofanya mapenzi ni tofauti na mwanaume?

Tafiti nyingi zimefanyika na mojawapo ni ile iliyoruhusu Wanawake na wanaume wote kuandika vile wanajisikia wanapofika kileleni na baadae wakaruhusu watu wengine wasome na wapendekeze nani ameandika kati ya mwanamke au mwanaume hata hivyo ilikuwa vigumu kwa wasomaji kufahamu maelezo yaliyoandikwa yameandikwa na mwanaume au mwanamke.
Hii ina maana kufika kileleni kwa mwanaume na mwanamke huhusisha uzoefu unaofanana.
Hata hivyo kuna tofauti ya uzoefu wa kufika kileleni kwa Wanawake na hata mwanamke mmoja na hii tofauti hutokana na aina ya kusisimuliwa ili kufika kileleni kuanzia kisimi, uke, G-spot, matiti na hata picha za kizushi (fantasy/imagery)

Je, ni kweli kwamba kinachomfikisha kileleni mwanamke huyu ni tofauti na mwanamke yule?


Ni kweli pia hata mwanamke huyo mmoja kinachomfanya asisimuliwa kufika kileleni leo ni tofauti na wiki ijayo na mwezi ujao na hata miaka matano au kumi ijayo.
Wapo wanaopenda kusisimuliwa G-spot na wengine hawataki, wapo wanaopenda kusisimuliwa kisimi wengine hakuna lolote, wapo wanaopenda kusisimuliwa uke na wengine hawataki. Wengine matiti au masikio au shingo nk kila mmoja au hata huyo mmoja uliyenaye anatofautiana kutokana na mzunguko wake wa siku kwa mwezi.
Kama tunavyopenda vyakula tofauti na nguo tofauti na usisimuliwe wapi kwa mwanamke kufika kileleni ni tofauti.
Kuamini kwamba kumsisimua mwanamke Mahali fulani ndipo huweza kumfikisha kileleni bila kuwasiliana naye wakati mwingine huweza kuwa kero.

Je, mazoezi ya Kukaza misuli ya uke huweza kuongeza uwezekano wa mwanamke kufika kileleni kirahisi?

Mazoezi ya kege



Mazoezi ya kukaza misuli ya uke ni muhimu mno. Uwezo na uimara wa misuli ya PC (puboccoccygeus) unahusiana mno na mwanamke kufika au kufurahia tendo la ndoa.
Wanawake ambao hawawezi kufika kileleni kirahisi wana misuli ya PC iliyodhaifu (loose).
Mwanamke anayeweza kufika kileleni kwa kusisimuliwa kisimi ana misuli imara hata hivyo mwenye misuli imara zaidi ni yule anayeweza kufika kileleni kirahisi kwa uke wake.

Je, ina maana kuna Wanawake huweza kufika kileleni kwa kulala na kuanza kufikiria picha za kizushi (fantasy) hata kama yupo peke yake?

Ni kweli.
Beverly Whipple, R. N. PhD katika maabara yake aliwaalika Wanawake 10 ambao walisema wana uzoefu na kufika kileleni kwa picha za kizushi (fantasy) na hao Wanawake walionesha mgandamizo wa damu, mapigo ya moyo, kubadilika kipenyo cha macho sawa na kufika kileleni kwa njia zingine kama uke na kisimi.


Wanawake huwa na tofauti za kufika kileleni kutokana na aina ya kusisimuliwa pamoja na sababu zingine kama vile anavyojisikia huo wakati, kiwango cha homoni.
Si suala la kubonyeza button na mwanamke akafika kileleni. Kufika kileleni si conditioned reflex.
Mara nyingi lengo la mume katika sex ni kuhakikisha mke anafika kileleni je kuna tatizo kuwa na mtazamo kama huo?
Kawaida tunapozungumzia maisha huwezi kukwepa kuweka malengo.
Linapokuwa suala la sex ni kweli kwamba wanaume huwa goal-directed na Wanawake huwa pleasure-directed.
Tatizo huja pale watu wameshindwa kufahamu hiyo siri na hasa wanaposhindwa kuwasiliana na wapenzi wao.
Mwanamke anaweza kufika kileleni kwa kusisimuliwa sehemu zingine za mwili kama vile masikio nk bila kuwasiliana inaweza kuleta shida kwani we are all unique.

Friday, 10 June 2016

NDOA NI KAZI..


Ndoa ni kazi.
Inayochukua muda, jitihada na commitment na wakati mwingine huhitaji professional counselling.
Kama umefika Mahali ambapo wewe na mume wako au mke wako hamuwezi hata kuwasiliana (kuongea) bila kuvurugana na umeanza kufikiria kuachana kama njia bora zaidi basi unahitaji msaada kwani kuachana bado si jibu la matatizo yote.
Katika ndoa mwanaume na mwanamke ni tofauti na kila mmoja ana mahitaji muhimu ambayo ni lazima mwenzake ayatimize na kutotimizwa hayo mahitaji husaidia kukwetua njia ya kila mmoja kutoridhika na mwenzake.
Kwa ufupi mahitaji muhimu ya mwanaume (yale anapenda mke wake amtimizie) ni kama ifuatavyo

1. HITAJI LA KURIDHISHWA KIMAPENZI (SEX).

2. HITAJI LA KUBURUDISHWA, RAHA, KUSTAREHE, KUPUMZIKA, NAFASI YA KUPUMUA, BURUDANI.

3. HITAJI LA KUWA NA MKE ANAYEVUTIA.

4. HITAJI LA KUWA NA AMANI NA UTULIVU.

5. HITAJI LA KUAMINIWA, KUHUSUDIWA NA KUHESHIMIWA.

Mahitaji ya mwanamke katika maisha ya ndoa (vile mwanamke anapenda mume amfanyie au kumtimizia) ni kama ifuatavyo:

1. HITAJI LA UPENDO, KUPENDWA, MAHABA NA HURUMA.

2. HITAJI LA MAONGEZI, MAZUNGUMZO, MISEMO, POROJO, KUSIMULIANA NA SOGA.

3. HITAJI LA UKWELI, UADILIFU, KUAMINIANA, UNYOFU, WIMA NA UWAZI.

4. HITAJI LA UHAKIKA WA KIFEDHA, AMANA KIFEDHA, UHAKIKISHO KIFEDHA, ULINZI KIFEDHA, USALAMA KIFEDHA, UTHABITI NA AMANI KIFEDHA.

5. HITAJI LA KUJITOA KWA AJILI YA FAMILIA.

Kwa ufafanuzi ni kwamba mwanamke hupenda mume akimaliza kazi jioni kwanza ajithidi kuwahi nyumbani ili ale chakula (supper/dinner) na mke na watoto, akae na mke na kuongea masuala ya familia kama watoto, matumizi ya fedha nk na hupendelea baba kutumia muda na watoto na mke na si kuangalia TV.
Mume naye hupenda anaporudi kazini mke ampe angalau dakika 15 apumue ndipo aanze kuuliza maswali na kuelezea siku ulivyokuwa na ikifika muda wa kulala mke aanzishe kwamba anahitaji tendo la ndoa.

MIMBA NA TABIA ZAKE..



Naitwa Jeffy na mke wangu anaitwa Judy, nipo nyumbani nafanya kazi zangu na mke wangu Judy ameenda kwa Daktari ili kujua inakuwaje mbona amejikuta asubuhi mambo si ndivyo kama kuchoka si kuchoka, anajisikia kichefuchefu na kuna dalili lile zoezi letu la kupata first born limewezekana.

Judy amerudi na Daktari amemwambia mke wangu ana mimba ya wiki mbili na ndani ya miezi tisa tutakuwa na mtoto.

Nipo excited ila nawaza sana namna ya kuwa baba na kuitwa baba, mikikimikiki ya nepi usiku na mchana.

Ni wiki sasa naona mke wangu iwe mchana iwe usiku iwe lunch, breakfast au supper yeye anataka ale embe na kibaya zaidi lisiwe limeiva sana wala lisiwe halijaiva sana.

Anafakamia maembe kiasi cha kunifanya nihisi anaweza kuzaa maembe badala ya mtoto.

Kinachonishangaza hata moon yake inabadilika kila wakati, dakika moja ni chakalamu na dakika inayofuata ni balaa, mkali kama nyuki na ngumu kuishi naye, alikuwa anapenda juice ya machungwa, nanasi sasa hataki hata kusikia harufu yake, cha ajabu hataki hata juice ya maembe wakati anapenda kula embe (lisilo bichi sana na ambalo halijaiva sana).

Akiniona nafakamia juice basi ananiambia kwamba kwa nini sijali hisia zake.

Kibaya zaidi sasa hata majirani hawapendi inafikia muda anataka tuhame muda huohuo na kila ninapojitahidi kumwambia haitawezekana anaiita mimi ni selfish na kwamba kila ninachojali ni mimi mwenyewe na si yeye.

Mara ananiambia anahitaji ale mishikaki na mimi naondoka kiguu na njia hadi km 4 kufuata mishikaki ili mzazi mtarajiwa ale, ile nikifika nyumbani tu na kufungua ili nimpe ile mishikaki anabadilika ghafla eti nimetumia muda mrefu mno na sasa hahitaji.

Sasa ameanza mtindo anaamka saa tisa au nane au kumi usiku na kuniomba tuongee, namuuliza na huu usiku wa manane tuongee kitu gani, majibu ananipa analalamika kwamba sijali tena kuongea na yeye na kwamba nilichokuwa napenda ni kumtia mimba.

Finally, mtoto wetu akazaliwa na kila kitu kikaanza kurudi katika hali ya kawaida..

Unaweza kujifunza kitu kama mke wako atakuwa na tabia hizo wakati akiwa mjamzito..Mvumilie kwani ni kipindi cha mpito tu.

Thursday, 9 June 2016

NDOA NI UVUMILIVU


Moja ya siri kubwa ya mahusiano ya binadamu ni jinsi Mungu anavyo weza kufanya miujiza kwa mwanaume na mwanamke ambao wanaamua kufuata njia za kimungu ili ndoa yao iwe ya kuridhisha na mpya kila siku.

Ni pale tu tunapotii mpango wa Mungu na kumtegemea yeye (kitu ambacho wengi huona kigumu) huweza kupata maana halisi ya upendo wa kweli (intimacy, love and affections) kati ya mke na mume.

Mungu ameweka hamu ya kupendwa ndani yetu kwa sababu maalumu na Mungu hana mpango wa kutufanya tuishi katika ndoa ambazo zinatufanya kuwa frustrated na disappointed bali furaha na kicheko katika familia ingawa siri kubwa ya kwanza ni kumpenda Mungu kwanza.

Hii ina maana unapompenda Mungu kwanza ndipo utampenda mke au mume pia kwani upendo wa Mungu kwetu hufanya reflection kuwapenda wale wanaotuzunguka akiwepo partner wako.

Mpango wa Mungu ni kwamba ule upendo unaowafikisha wanandoa wapya madhabahuni kufunga ndoa huwa ni upendo kichanga kabisa siyo upendo uliokomaa kwani upendo wa kweli (real love) kati ya mke na mume huweza kuzaliwa baada ya mke na mume kuishi pamoja kwa muda mrefu kwa kupitia shida, majaribu, conflicts, storms, tofauti, furaha, amani na kila mmoja kuwa commited kwa mwenzake kwa kuzikubali tofauti na kila mmoja kuondoa uchoyo binafsi na kujenga kitu kimoja kinachofanana.

Bahati mbaya kubwa ni kwamba wanandoa wapya wengi baada ya kukutana na disappointments au frustrations huhisi ni dalili kwamba ndoa imefika mwisho kumbe huo ndiyo mwanzo wa kujenga upendo mpya.

Ndoa huhitaji kazi na jitihada ya wawili walioamua kuishi pamoja haitokei naturally kama watu wawili wanapopendana kwa mara ya kwanza na kwamba inakuwa tambalale kila iitwapo leo.

Ndoa ni kuvumiliana na kujitoa ili kujenga upendo wa kweli kwa muda na si wa usiku mmoja tu. Unahitaji kuwekeza jitihada zako, uaminifu, imani na matumaini.

Mke kuwa na hitaji la upendo wa ndani (intimacy) kutoka kwa mume wake tofauti na mwanaume ni hitaji ambalo hufanya kazi kama injini kwa wanandoa kuhitaji kuridhishana hata hivyo mke akiamua kuchukua njia nyingine ya kuwa mkali na mchungu kwa mume anaweza kuifanya ndoa ijae uchungu na upweke na hatimaye kusambaratika.

Mungu ameweka siri kubwa sana kwa watu wawili imperfect kutengeneza kitu kimoja (mwili mmoja) hii ni kazi inayohitaji kazi ili kuwe na bond strong.

Tukumbuke kwamba wanandoa wapya wawili ambao hukubaliana kwenda mbele za Mungu kutoa viapo vya kuishi pamoja kama mke na mume ni binadamu wa kawaida ambao ni dhaifu haijalishi wanajitahidi kiasi gani kuficha mapungufu yao kila mmoja kwa mwenzake hata hivyo baada ya kuoana na kuanza maisha kila mmoja hujifunza kwamba ni kitu kisichokwepeka kuficha mapungufu na kwamba upungufu ni sehemu ya binadamua na jambo la msingi ni kila mmoja kumkubali mwenzake kama alivyo.

Ukiwaona wachumba ambao wanategemea kuoana macho yao huwa hayaoni chochote isipokuwa uimara na ahadi kamili ya upendo uliondani ya mioyo yao.
Ikitokea ukamuuliza binti (wachumba) je, unaona kasoro yoyote kwa mchumba wako (kijana wa kiume) bila shaka atakwambia Mungu amenibariki sana kunipa mume mtarajiwa ambaye hana kasoro wala tatizo lolote.

Hata hivyo hizo ni illusions, ni maluweluwe ni fantasy ni kitu ambacho hakitadumu kwa muda mrefu kwani akishaolewa tu hatahitaji kufikiri sana kuorodhesha kasoro za mume wake na wakati mwingine atalalamika kwamba nilikuwa sijui kwamba tupo tofauti kiasi hiki.
"Wachumba huishi kwenye ikulu na wanandoa huishi kwenye nyumba halisi"

Kabla ya kuolewa mwanamke huona matumaini yanayong’aa kwa mume wake mtarajiwa, anaona ulinzi, uimara, matumaini na upendo usio mfano na mwingine huringa na kutembea kwa madaha hata hivyo baada ya kuolewa anaanza kuona udhaifu na ndoto zote zinaanza kuyeyuka na kusinyaa kama au maridadi kwenye jua kali la ikweta, hukatishwa tamaa na yote huja ghafla kama kimbunga na anaanza kuumia na kujuta kwa kuwa mahitaji yake hayajatimizwa kama alivyokuwa anaona mwanzoni.
Haamini jinsi mume asivyomjali na kumsikiliza na kumpenda.

Hadi hapo mke anaweza kuamua kuitikia kwa:-
(i) Kwa hasira kutokana na hayo mume wake amemuonesha]
(ii) Kwa Kuwekeza kwa upendo, imani katika uwezo/uimara (strength zile anaziona kwa mume wake na kuanza kuijenga ndoa upya

Ili mambo yaenda vizuri au upendo wa kweli uzaliwa mke anatakiwa kuamini uwezo wa ndani wa mume wake alionao ( streghth siyo weakness).
Anaweza kuwekeza kwa mume halisi aliyejificha kwa mume wa nje mwenye kutojali kutimiza ndoto zake za uchumba na honeymoon.

Mungu amempa kila mwanamke uwezo wa ajabu wa kumsaidia mume wake kukua na baada ya muda mume kuwa mcha Mungu sawa na anavyotakiwa.
Bahati mbaya ni kwamba wanawake wengi wamekatishwa tamaa sana kiasi kwamba huyu mwanaume aliyenaye leo hawezi kuwekeza chochote kwa ajili ya mume huyu atakavyokuwa kesho.

Wednesday, 8 June 2016

NI UPENDO TU UNAOHITAJIKA.


Kinachoshangaza ni kwamba wanandoa wanapokutana na matatizo katika ndoa yao, wazo la kwanza kuja ni “kwa sababu nilioana na mtu ambaye si sahihi” inaweza kuwa kwa nyakati fulani au kwa mtu fulani ni sahihi na si sahihi kwa kila mmoja hasa katika karne hii mpya.
Tatizo unawaza kwamba ungekuwa umeoana na mwingine basi tatizo kama hilo lisingekuwepo, huku ni kuota mchana kweupe , Unajidanganya, halafu mbaya zaidi unamjua hata yule ambaye unaamini ungeoana naye usingepata matatizo haya unayopitia, ni upuuzi !
Unapoanza mahusiano na mtu yeyote mwanzoni huonekana ni kila kitu safi, sasa zoeana, mfahamu, ishi naye ndipo utajua kuwa kuishi na binadamu yeyote unahitaji upendo na kwamba huyo uliyemchagua ni wewe tu duniani unaweza kuvumilia vituko vyake au udhaifu wake tena kwa upendo na furaha na kumpokea kama alivyo.

Thursday, 2 June 2016

NI MUHIMU KWA WANANDOA.


Uumbaji wa Mungu ni wa ajabu sana hasa linapokuja suala la mahusiano Kati ya mwanamke na mwanaume katika ndoa.
Ili kuridhishana kimwili kati ya mwanamke na mwanaume jambo la msingi ni kufahamu vizuri hatua kamili ambazo ili tendo la ndoa likamilike lazima zifuatwe na hasara zake.

Hata hivyo wakati mwingine wanandoa hujikuta katika mgogoro katika eneo lingine la ndoa na matokeo yake masuala ya kitandani pia huwa ovyo na zaidi kuanza kulalamikiana kila mmoja akimlaumu mwenzake.
Kawaida tendo la ndoa hupitia hatua tatu muhimu ambazo ni vizuri kila mwanandoa kufahamu na pia ni muhimu kufahamu kwamba kila hatua huwa na vikwazo vyake na hili lisipozingatiwa unaweza kujisikia wewe tu ndiye unayepunjwa kwenye ndoa.

Hizi hatua tatu muhimu kila moja ina uwezo wake na mzunguko wake binafsi na pia vikwazo vyake.
Hatua ya kwanza ni:-

HAMU YA TENDO LA NDOA.

ili kupata hamu ya tendo la ndoa lazima ubongo uhusike kwani kwenye ubongo kuna mfumo maalumu wa fahamu (neural) ambao kutokana na hali iliyopo mtu hujisikia hamu.

Hatua ya pili ni :-

KUSISIMKA.

hii ni hatua ambayo baada ya kuwa na hamu damu huweza kusambaa sehemu muhimu kama vile matiti, uke au uume kwa ajili ya kuhakikisha sex inafanyika.

Hatua ya mwisho ni:-

KUFIKA KILELENI.

hii hutokana na kukaza kwa misuli ya uke au uume na kutoa raha isiyoelezeka na baada ya hapo ni kama mwisho wa furaha ya tendo lenyewe.

NINI VIKWAZO VYA HATUA HIZI MUHIMU?

Wasiwasi, hofu, mashaka, woga, kuogopa na uadui hupelekea mtu kukosa hamu ya tendo la ndoa.
Fadhaa zozote kuhusu sex hupelekea kukosa kusisimka na kuwa tayari kwa mapenzi pia ku-concentrate kwenye skills na techniques au style za sex kuliko kufurahia tendo lenyewe hupelekea kushindwa kufika kileleni.

Kumbuka utendaji wa sex katika ndoa huonesha hali ya ndoa nzima katika mambo yote kwani mara nyingi ndoa ikiwa na mgogoro hata tendo la ndoa huwa ni bora liende, si kuridhishana bali wajibu na ukweli unabaki kwamba sex katika ndoa huelezea ndoa ipoje.

Kama kuna mgogoro ambao haujapata jibu au kutokuelewana katika ndoa basi mfumo mzima wa sex hubadilika.

Je, unajisikia raha na hamu kubwa na kusisimka kwa ajabu kama zile siku za kwamba wakati mnaoana?
Je, jinsi unavyoridhika na tendo la ndoa ni sawa na ulivyokuwa unategemea? Au ni kama wajibu na si kupeana raha?
Ukweli unao mwenyewe.

Uzoefu unaonesha jinsi wanandoa wanavyozidi kuishi pamoja; tendo la ndoa huwa zuri zaidi na la kuridhisha zaidi kuliko mwanzo au miaka ya mwanzo.

Wednesday, 1 June 2016

MAKOSA YA KUEPUKWA KTK NDOA.


1. KUTOKUHESHIMIANA.

Si vizuri kumtamkia maneno mabaya mwenzi wako mbele za watu.
Mke au mume anahitaji kuheshimiwa, kupewa asante kuwa appreciated na zaidi kumsifia mbele za watu na sivinginevyo.
Kuongea mambo mazuri kwa mke au mume wako mbele za watu ni muhimu sana.
Wapo wanaume hutukana wake zao mbele za watu na wapo wanawake hujibu mbovu waume zao hata mbele za watu au wageni. Kama kuna kitu amekuudhi kwa nini usisubiri mkaongee chumbani mkiwa wawili?

2. KUTOSIKILIZA MMOJA AKIONGEA.

Hii inajumuisha kuwa na mawazo ya mbali wakati mume au mke anaongea, yeye anaongea wewe unaendelea kuangalia TV, Unaendelea kusoma gazeti, unaendelea kusoma kitabu, Unaisikiliza laptop kuliko mume wako au mke wako.
Pia hii inajumuisha kuwa mbali kimwili (body language) wakati mwenzako anaongea, wapo wanandoa ambao hata mwenzake hajamaliza kuongea tayari anadakiwa kwamba najua ulichokuwa unataka kusema, pia wapo ambao hata ukiuliza swali yupo kimywa, mbaya zaidi ni pale unapoona na kuhisi mwenzako ana tatizo lakini ukimuuliza anabaki kimya au anakwambia hakuna tatizo, Inaumiza sana hasa kwa wenzetu wanawake ambao asilimia kubwa ya wanaishi kwa hisia, na kuumiza hisia zao ni kitendo kibaya sana, ni vitu vidogo lakini ni muhimu kuliko unavyodhani.

3. KUKOSA MAHABA.

Ukiacha mke wako au mume wako anahangaika na kutoridhishwa kimapenzi maana yake unachimba shimo ambalo ukijifukia utatokea jehanam, na kama unaona umepoteza interest na sex fanya kila njia kupata ushauri na msaada ili urudi kwenye mstari.
Matatizo mengi ya ndoa zinazokufa huanza kwa ugonjwa wa kutoridhishwa kimahaba na mume au mke.
Kumbuka ndoto za watu wengi kuoana ni kupata mtu atakayemtosheleza kimapenzi.

4. KUJIONA SAHIHI MARA ZOTE.

Hii inajumuisha wewe kuwa ndo msemaji na muelimishaji wa mke wako au mume wako, yaani wewe ndo unajua kila kitu, upo sahihi siku zote, au bila neno lako la mwisho basi information haijakamilika.
Siku zingine kubali kwamba umekosea au huna jibu, hakuna mtu anaweza kufurahia kuwa na mtu ambaye siku zote yeye ndo yupo sahihi labda kama unaishi na mtu mwenye mtindio wa akili.

5. KUTOKUFANYA KILE UNASEMA.

Siku zote Imani bila matendo imekufa na Imani ni matendo, “Actions do speak louder than words”. Ukisema utafanya kitu Fulani, fanya.
Wanawake ni viumbe ambao hutunza sana ahadi tunazowapa, hivyo usiahidi kitu ambacho huwezi kufanya, kwani mwenzio anaandika kwenye ubongo wake siku akija kukutolea mahesabu ya ahadi hewa umefanya utaipata fresh, pia na wanaume (si wote) kwa ahadi hewa hatujambo, tujifunze kufanya kila tunachosema.
Tusitoe ahadi tamu kumbe hewa, inaumiza sana.

6. UTANI UNAOUMIZA.

Kama mwenzio anakwambia utani wako unamuumiza achana nao, kuna utani mzuri lakini kuna wakati mnaweza kufikishana pabaya na lazima uwe makini kusoma saikolojia za mwenzi wako, kuna wengine anaweza kukutania wewe usikwazike, na utani huohuo ukimrudishia yeye anakwazika so be very careful usimuumize mwenzako.

7. KUTOKUWA MWAMINIFU.

Kudanganya na kuwa na siri zako binafsi katika mahusiano huweza kujenga wawili kuwa mbali na kutokuaminiana.

8. KUWA MTU UNAYEUDHI KILA WAKATI.

Inaweza kuwa ni mzembe, mchafu, mtu wa kuchelewa kila mahali, mtu wa kusahihisha kila kitu mwenzio anafanya, mtu wa kulalamika tu kila wakati kila kitu, kuwa kimya tu mwenzio akitaka muongee masuala ya ndoa au familia. Unajua unaudhi lakini unaendelea kuudhi.

9. KUWA MCHOYO.

Yaani unatumia pesa nyingi sana kwa mambo yako na mume wako au mke wako akitumia pesa kidogo tu kelele na zogo hadi nyumba inakuwa moto.
Hadi nyumba yako haipo friendly maana hata kuburudika kwa soda tu kwako ni issue wakati ukiwa mwenyewe unajichana ile mbaya na kuku kwa chips na kitimoto na watu ambao ni nje na familia yako, hiyo ni aibu!

10. UKALI ULIOPITILIZA.

Kila mwanandoa anahitaji kuwa mstaarabu linapokuja suala la kutatua mgogoro wowote, wapo ambao tatizo likitokea mke au mume na watoto wanatamani kuhama nyumba maana hapakaliki, Ni kweli kwa kelele zako na mihasira yako unaweza kuwin huo mgogoro lakini mbele ya safari bado utajikuta ni wewe ndo umeharibu zaidi.
Sidhani kama kuna mtu anapenda kukaripiwa kama mbwa ndani ya ndoa