Monday, 2 May 2016

SIRI YA KUWA NA NDOA NZURI.


Ukitaka kuwa na mahusiano mazuri na yule unampenda siku zote ni muhimu kujtahidi kumfahamu mwenzi wako upya kila siku kuliko kawaida yako.
Jitahidi kupata ufahamu wa kutosha kuhusu yeye jinsi anavyofikiri, na jinsi anavyotenda.
Vumbua zaidi kwa nini yeye na wewe kuna tofauti na jifunze jinsi ya kutumia hizo tofauti kufanya ndoa au mahusiano kuwa imara na wa kudumu.
Jifunze jinsi ya kufahamu yeye na pia ni namna gani unaweza kukubaliana naye katika jambo lolote, au jambo lolote kuhusu watoto, ndugu zake, mambo ya kanisani au kazini.
Pia fanya kila njia kupata ufahamu wa kutosha kuhusu yeye katika masuala muhimu ambayo mara nyingi huwa chanzo cha mifarakano na kuharibika kwa mahusiano kama vile
Pesa
Jinsi ya kulea watoto
Imani za dini
Tendo la ndoa
Na kila kitu ambacho kwenu ni muhimu sana

No comments:

Post a Comment