Wednesday, 11 May 2016

KWENU WANAUME.


Biblia ipo wazi kabisa na imetoa tamko zaidi ya mara 4 kwa mume kumpenda mke wake.
Wakati huohuo mwanamke ameariwa mara moja tu kumpenda mume wake ingawa shughuli kwake ni kumtii mume.

Kwa nini Biblia imesisitiza zaidi ya mara nne mwanaume kumpenda mke na mara moja tu mke kumpenda mume na kumtii?
Hili ni swali ambalo limekuwa linaniuumiza kichwa na katika kuchunguza naamini sababu zifuatazo ni muhimu sana.

Kwanza mwanamke anauhitaji mkubwa wa kupendwa, kuwa na mwanaume ambaye anampenda, anamjali, anamsikiliza na kujiona yupo katika mikono salama, nilikutana na mwanamke mmoja ambaye alilalamika kwamba
“Without love I have no life” wanawake wengi hujikuta katika njia panda wakiwa ndani ya ndoa na mume aliyenaye haoneshi upendo wowote na kujali.

Pili, wanaume tumekuwa na wakati mgumu sana kupenda kwa kumaanisha. Ukisikiliza mifano mbalimbali ambayo wanaume wamekuwa wanawadanganya wanawake unaweza kufika mahali ukajiuliza hivi akili za mwanamke huwa zinakuwa zimehama au ndo raha ya kupendwa!
Kiasili mwanamke amekuwa na capacity kubwa kuhusiana na mapenzi (upendo au kupendwa) kuliko mwanaume.

Mwanamke akisema amekupenda anakuwa amekupenda kwanza kwa kukuweka ndani ya moyo wake, wakati mwanaume kupenda kwake ni kwa vipande inawezekana amekupenda kwa sababu ya mguu tu basi na anaweza kukuahidi kukununulia gari na wewe ukakubali.

Na kuna wakati wanawake wamekuwa wakijiuliza hivi wanaume tuna feelings au hatuna, kwani kuna wakati tunaweza kuwa kama “animals” kwa matendo yetu na vitu tunafanya kwa hivi viumbe “wanawake”, tunajilinda kwa kusema kwamba nao wepesi mno kudanganywa!

Hata hivyo ni ngumu sana au ni mara chache sana kusikia mwanaume amejidhuru au kujiua baada ya kuachwa na mpenzi wake wa kike ingawa ni mara nyingi tunasikia mwanamke (hasa binti wa miaka 15 – 25) amejiumiza au kujiua kama si kuchanyanyikiwa kwa kumpoteza mpenzi wake wa kiume.

Ni mara chache sana kukutana au kumuona mwanamke ambaye ameamua kuachana na mwanaume anayejua kupenda na kumpa mahitaji yake yote ya emotions kwani mwanamke akipata hitaji la kupendwa au husia za kupendwa hapo ndo ugonjwa wake umepata tiba, pia ni mara chache sana kukutana na mwanamke anayeomba msaada wa ushauri kwa ajili ya mwanaume ambaye anamjali sana kwenye ndoa yake.

No comments:

Post a Comment