Friday, 27 May 2016

UMUHIMU WA SALAMU KWA MWENZI WAKO.


Kwanza fahamu kwamba wanandoa wanapokaa muda mrefu baadhi ya vitu huanza kuchakaa kimapenzi. Hata hivyo upendo na wema husaidia kurudisha moto wa mapenzi na wanandoa kujiona wapya kila umri unavyozidi kuongezeka.
Matendo yanayoonesha wema kwa wanandoa ni gundi inayoshikisha wawili kujiona wapo karibu na moja ya tendo la wema ni kumsalimia mwenzako wakati mnaamka hata kama mmelala kitanda kimoja na hata kama mlikumbatiana usiku mzima au ulimuweka mwenzi wako kifuani usiku mzima.
Anayesalimiwa hujiona anapendwa, ana thamani na pia appreciated.

Tupo kwenye new millennium kiasi ambacho watu tupo busy hata kuamka tunahitaji kuweka alarm ituamshe hata hivyo badala ya kukimbia bathroom kuoga ni muhimu kumpa kwanza salamu mwenzi wako ndipo uendelee na kazi zingine au na ratiba yako.
Wanandoa ambao husalimiana asubuhi wanajiona ndoa yao ni nzuri sana na wana mahusiano yanayoridhisha.


Je, nini kinafanya maneno ya salaamu ya asubuhi kuwa muujiza katika ndoa na mahusiano?

Unapomsalimia mwenzi wako maana yake unamwambia na kumpa ujumbe kwamba ni asubuhi njema tumeamka pamoja katika upendo na furaha na kwamba unajisikia vizuri kuanza siku mpya na mtu wako na pia unaweza msingi mzuri wa mawasiliana kwa hiyo siku mpya.

Thursday, 12 May 2016

MOUTH CAN ALSO YOUR MARRIAGE BUST.



We all are friends and we talk with people around about our marriage, but we tell them what friends are very important and can bring very good results or very bad for our marriage.

Take a look at this talk secrets of your home and your husband or your wife, and one of you is going to stream in with her friends, or colleagues, or his mother or his father or his brothers around you and speaks it matters much that would exist would not dare speak.
Protect the privacy of your husband or your wife is particularly important in strengthening trust in marriage.
The coincidence is that there are a couple that they disclose the spouse to remain his friend or people is not a problem if you have a Kindle mouth.

That is only a small example fuss just a husband or wife the night, the morning wake up already father, mother, brothers, neighbors and colleagues that yesterday you disagreed when no profit is earned and thinks to tell others, then he should be very lo and ends despise.

When a spouse is secretly gave out you lost your status of being a spouse.
It's like you made the lame to your partner especially for those that tells your secrets.
Yes, there is time and it is also important to involve other marital struggles especially close person who you believe can advise you and help you, but do not shed a mystery to everyone.

The present world has changed a lot different from where the old man was out early and go seeking wife had a home to continue his work with children.

Nowadays everyone wants his leave early in the morning to go to work and at work she spends more time than at home, the greater is that the job is won by the man's wife or husband of a man or men and women who are not husband or wife or children.

Many studies show many couples now spend more time at work than to be with this family means a spouse spends a lot of work to win the man's wife or husband of someone with such a man's wife membrane has to be someone to pour his secrets for home or bedroom him and his mate is that she has date with someone's wife or the wife of a man without a trace.
For to share one secret is to be intimate with someone that is why now we have many instances of office romance than at any time in world history.
So be very careful with your mouth!

MDOMO UNAWEZA PIA KUIVUNJA NDOA YAKO.


Sisi wote huwa tunaongea na marafiki na watu wa karibu kuhusu ndoa zetu, hata hivyo mambo tunayowaambia marafiki ni muhimu sana na huweza kuleta matokeo mazuri sana au mabaya sana kwa ndoa zetu.

Tuangalie hili la kuongea siri za nyumbani kwako na mume wako au mke wako na mmoja wenu anaenda kuzimwaga kwa marafiki zake, au wafanyakazi wenzake au mama yake au baba yake au ndugu zake kwa kukuzunguka na anaongea hayo mambo kiasi kwamba ungekuwepo asingethubutu kuongea.
Kulinda siri za mume wako au mke wako ni jambo muhimu sana hasa katika kuimarisha trust katika ndoa.
Bahati mbaya ni kwamba wapo wanandoa ambao wao kutoa siri za mke au mume kwa rafiki au watu baki kwake si tatizo ni kama mdomo una washa.

Yaani kitu kidogo tu mfano kuzozana kidogo tu na mume au mke usiku, ile kuamka asubuhi tayari ameshawambia baba, mama, ndugu, majirani na wafanyakazi wenzake kwamba jana mlizozana wakati wala hakuna faida anayopata na anadhani kuwaambia wengine basi yeye anafaa sana kumbe nao huishia kumdharau.

Unapokuwa ni mwanandoa mtoa siri nje unapoteza hadhi yako ya kuwa mwanandoa.
Ni kama unatengeneza kilema kwa partner wako hasa kwa wale unaowaambia siri zenu.
Ndiyo, kuna wakati na pia ni muhimu kushirikisha wengine struggles za ndoa hasa mtu wa karibu ambaye unaamini anaweza kukushauri na kukusaidia lakini si kumwaga siri kwa kila mtu.

Ulimwengu wa sasa umebadilika sana tofauti na zamani ambapo mwanaume alikuwa anatoka asubuhi na mapema kwenda kutafuta riziki na mke alikuwa na muda nyumbani kuendelea na kazi zake na watoto.

Siku hizi kila mmoja anaaondoka asubuhi na mapema kwenda kazini na huko kazini anatumia muda mwingi kuliko nyumbani, kubwa zaidi ni kwamba kazini anashinda na mke wa mtu au mume wa mtu au wanaume na wanawake ambao si mume wala mke au watoto.

Tafiti nyingi zinaonesha wanandoa wengi sasa wanatumie muda mwingi zaidi kazini kuliko kuwa na familia hii ina maana mwanandoa anatumia muda mwingi wa kazi kushinda na mke wa mtu au mume wa mtu na kama huyo mke wa mtu ndo amekuwa mtu wa kumwagia siri zake za nyumbani au chumbani kwake na mwenzi wake anakuwa ana date na huyo mke wa mtu au mke wa mtu bila kujua.
Kwani ku-share siri ni moja ya kuwa intimate na mtu ndiyo maana sasa tunakuwa na matukio mengi ya ofisi romance kuliko wakati wowote katika historia ya dunia.
Hivyo kuwa makini sana na mdomo wako!

Wednesday, 11 May 2016

KWENU WANAUME.


Biblia ipo wazi kabisa na imetoa tamko zaidi ya mara 4 kwa mume kumpenda mke wake.
Wakati huohuo mwanamke ameariwa mara moja tu kumpenda mume wake ingawa shughuli kwake ni kumtii mume.

Kwa nini Biblia imesisitiza zaidi ya mara nne mwanaume kumpenda mke na mara moja tu mke kumpenda mume na kumtii?
Hili ni swali ambalo limekuwa linaniuumiza kichwa na katika kuchunguza naamini sababu zifuatazo ni muhimu sana.

Kwanza mwanamke anauhitaji mkubwa wa kupendwa, kuwa na mwanaume ambaye anampenda, anamjali, anamsikiliza na kujiona yupo katika mikono salama, nilikutana na mwanamke mmoja ambaye alilalamika kwamba
“Without love I have no life” wanawake wengi hujikuta katika njia panda wakiwa ndani ya ndoa na mume aliyenaye haoneshi upendo wowote na kujali.

Pili, wanaume tumekuwa na wakati mgumu sana kupenda kwa kumaanisha. Ukisikiliza mifano mbalimbali ambayo wanaume wamekuwa wanawadanganya wanawake unaweza kufika mahali ukajiuliza hivi akili za mwanamke huwa zinakuwa zimehama au ndo raha ya kupendwa!
Kiasili mwanamke amekuwa na capacity kubwa kuhusiana na mapenzi (upendo au kupendwa) kuliko mwanaume.

Mwanamke akisema amekupenda anakuwa amekupenda kwanza kwa kukuweka ndani ya moyo wake, wakati mwanaume kupenda kwake ni kwa vipande inawezekana amekupenda kwa sababu ya mguu tu basi na anaweza kukuahidi kukununulia gari na wewe ukakubali.

Na kuna wakati wanawake wamekuwa wakijiuliza hivi wanaume tuna feelings au hatuna, kwani kuna wakati tunaweza kuwa kama “animals” kwa matendo yetu na vitu tunafanya kwa hivi viumbe “wanawake”, tunajilinda kwa kusema kwamba nao wepesi mno kudanganywa!

Hata hivyo ni ngumu sana au ni mara chache sana kusikia mwanaume amejidhuru au kujiua baada ya kuachwa na mpenzi wake wa kike ingawa ni mara nyingi tunasikia mwanamke (hasa binti wa miaka 15 – 25) amejiumiza au kujiua kama si kuchanyanyikiwa kwa kumpoteza mpenzi wake wa kiume.

Ni mara chache sana kukutana au kumuona mwanamke ambaye ameamua kuachana na mwanaume anayejua kupenda na kumpa mahitaji yake yote ya emotions kwani mwanamke akipata hitaji la kupendwa au husia za kupendwa hapo ndo ugonjwa wake umepata tiba, pia ni mara chache sana kukutana na mwanamke anayeomba msaada wa ushauri kwa ajili ya mwanaume ambaye anamjali sana kwenye ndoa yake.

Tuesday, 10 May 2016

NJIA RAHISI YA KUONGEZA MAHABA KWA MKE WAKO.


Mwanaume anaweza kuongeza ladha ya mahaba kwa mke wake pale anapokuwa makini na suala la jiografia na ustadi wakati wa tendo la ndoa.
Wanawake ni viumbe ambao mara nyingi huwa distracted na mazingira waliyopo kuliko wanaume hasa linapokuja suala la faragha na usalama.

Wanawake huathirika zaidi na mazingira hasa sauti au kelele na harufu kuliko wanaume (mume) wakiwa sita kwa sita, mfano hofu ya kwamba watoto watasikia hasa kama watoto wanapiga kelele,hofu ya kusikiwa na majirani au wapiti njia, hofu ya mlango kuwa haujafungwa (komeo) nk.

Mume mmoja alisafiri kwenda nchi za mbali na aliporudi nchini kwake na kupokelewa na mkewe walienda moja kwa moja nyumbani kwao na kwa kuwa hakukuwa na watoto au mtu mwingine bali wao wenyewe tu, wakaamua kwa raha zao wapeane zawadi ya miili yao kwanza kabla ya lolote kwa kuwa walikuwa na hamu kubwa kila mmoja kwa mwenzake, hata hivyo mlango walisahau kuufunga na baada ya kumaliza kupeana zawadi mke alimuuliza mume "hivi unakumbuka mlango hatukufunga?"
Hii ni ina maana gani? ni kuthibitissha kwamba muda wote wa tendo la ndoa mke alikuwa anawaza kwamba mlango haujafungwa na alikuwa anawaza hivi watoto wakirudi na kuingia moja kwa moja itakuwaje.
Mume yeye wala hakuwa na wazo hilo na wanaume wengi wapo hivyo.
Mwingine ana enjoy sex mwingine anawaza mlango haujafungwa!

Pia sijui inakuwaje tafiti nyingi zinaonesha wanaume wala huwa hawaogopi wapi ni salama kufanya tendo la ndoa.
Kwenye gari, bafuni, jikoni, sebuleni, chumbani, store, ofisini, kiwanjani, porini, makaburini na sehemu zingine unazozijua wewe.
Kuna nchi watu walikuwa wanaulizwa maeneo ambayo wamewahi kufanyia sex, ukweli majibu yaliyokuwa yanatoka yanatisha sana.


Tatizo kubwa lingine ambalo linaweza kuwa kizuizi cha kumpa hamu mke wakati wa tendo la ndoa ni wanaume kuwa wachafu au rough, au kutozingatia usafi.
Inawezekana wewe ni mwanaume unafanya kazi ambayo baada ya kazi unakuwa na majasho au unahitaji kuoga vizuri acha suala la kupiga mswaki na kuwa na kinywa kisicho na harufu.

Kucha chafu na mikono inayotisha hata unapomshika bibie na ngozi yake laini badala ya kusisimuka wewe unamuumiza na kumpa kinyaa kama si kichefuchefu.
Bahati mbaya na huko kazini uliona picha au mwanamke mrembo basi homoni nazo zikafanya kazi basi ummemkumbuka mkeo hivyo kufika nyumbani tu unataka.


Bila kujali usafi unamrukia mkeo na kwa kuwa anauwezo wa kunusa zaidi kuliko wewe unafanya a-palalyse kwa kuishiwa hamu kabisa na wewe matokeo yake na wewe unajisikia upo rejected.
Ukweli usafi ni jambo la msingi mno.

Saturday, 7 May 2016

TIBA YA MAMA MKWE.


Hapo zamani za kale kulikuwa na Binti aitwaye Lily aliolewa, yeye na mume wake wakaenda kuishi kwa mama wa mume wake yaani mama mkwe.
Kwa muda mfupi tu walioishi Lily aligundua kwamba yeye na mama mkwe hawaendani kabisa, walitofautiana kwa kila kitu na Lily alikasirishwa sana na tabia za mama mkwe wake kwani mama mkwe alikuwa anamlaumu muda wote.

Siku zilipitia, wiki zikapita na miezi ikapita kila siku Lily na mama mkwe ni kuzozana na kushambuliana, kibaya zaidi ni kwamba kutokana na traditions ilimpasa Lily kumpigia goti kila lile ambalo mama mkwe alihitaji afanye na ukweli hali mbaya ya mahusiano kati ya Lily na mama mkwe ilimfanya hata mume wake Lily kujisikia vibaya sana.

Mwisho Lily hakuweza tena kuvumilia tabia mbaya na utawala wa mama mkwe hivyo akaamua kufanya kitu, hivyo akafunga safari kwa rafiki wa baba yake ambaye alikuwa anauza dawa za kienyeji.
Alipofika kwa huyo Mzee akamweleza yote anayokutana nayo na kwamba anaomba msaada kama anaweza kumpa sumu ili aweze kumuua yule mama mkwe na kuondokana na lile tatizo milele.

Mzee akafikiria kwa muda na mwisho akamwambia Lily atamsaidia kulimaliza tatizo lake ingawa Lily alitakiwa kusikiliza kwa makini na kutii kile ataambiwa akafanye.

Na Lily naye kwa furaha akajibu kwamba nitafanya chochote utaniambia nifanye.
Ndipo Mzee akaingia ndani na kutoka na mfuko uliosheheni dawa na akaanza kumpa maelezo Lily
"Huwezi kutumia sumu ya haraka kumuua mama mkwe wako kwani kila mmoja atakutilia mashaka wewe hivyo nimekupa kiasi cha kutosha cha dawa (herbs) ambayo itatumika kidogo kidogo na kujenga sumu ya kutosha na hatimaye kumaliza.
Hivyo kila siku tengeneza mlo safi na weka dawa kidogo kwenye hicho chakula.
Sasa, ili kila mtu asikutilie mashaka wewe hasa akifa lazima uwe makini sana kujifanya rafiki kwake, usibishane naye na kubali chochote anakwambia na umuhudumie kama vile ni malkia, si unajua ipo siku atapotea kabisa”.

Lily alikuwa na furaha ya ajabu, akamshukuru mzee na akaenda nyumbani kuanza shughuli ya kumuua mama mkwe wake.

Miezi ikapita, wiki zikapita na siku zikapita, Lily aliendelea kumpa mama mkwe chakula chenye ile sumu na alikuwa anakumbuka sana jinsi Mzee alivyokuwa amemweleza jinsi ya kuepuka kutiliwa mashaka, hivyo aliweza kujizua hasira zake na alimtii mama mkwe kwa kila kitu na alimhudumia kama mama yake mzazi (malkia)

Baada ya miezi sita, nyumba nzima ilibadilika baada ya Lily kuweza kuzishinda hasira zake kwa mama mkwe na kumtii na wakajikuta hawagombani tena na hawakuweza kuzozana au kubishana kwa miezi sita mfululizo na wakajikuta wanaelewana na kuishi vizuri.
Pia mtazamo wa mama mkwe nao ulibadilika na alianza kumpenda Lily kama binti yake mwenyewe na akawa anawasimulia rafiki zake mwenyewe kwamba Lily alikuwa ni binti mzuri mwenye tabia njema ambaye hakuna mama mkwe duniani anaweza kumpata. Lily na mama mkwe wakawa ni kama mama na binti yake.

Pia mume wa Lily alikuwa na furaha ya ajabu alipoona kile kinatokea katika familia.
Ndipo Lily akarudi kwa mzee kuomba msaada tena, akamwambia mzee,
“Tafadhari nisaidie jinsi ya kuiondoa ile sumu isimuue mama mkwe kwani amebadilika na amekuwa mwanamke mwema sana kwangu na ninampenda kama mama yangu mzazi na sitapenda afe kwa sababu ya sumu niliyompa”.

Mzee akawa anatabasamu huku anatikisa kichwa.
“Lily huna haja kuwa na mashaka au kuogopa, sikukupa sumu yoyote, dawa niliyokupa ilikuwa ni vitamins kwa ajili ya kuimarisha afya. Sumu kubwa iliyokuwepo ilikuwa kichwani mwako (mind) na mtazamo wako kuhusu mama mkwe na hiyo sumu yote imesafishwa na upendo ambayo umeutoa kwake”.

Je, mdau wangu umegundua kwamba jinsi unavyowahudumia wengine ndivyo na wao watakavyokuhudumia wewe.


Inawezekana ni kweli unasuguana sana na mama mkwe au mume wako au mke wako au mpenzi wako na tatizo kubwa ni mtazamo wako kuhusu yeye na ungeamua kumpenda na kumhudumia kama malkia au mfalme mambo yangebadilika.

Monday, 2 May 2016

SIRI YA KUWA NA NDOA NZURI.


Ukitaka kuwa na mahusiano mazuri na yule unampenda siku zote ni muhimu kujtahidi kumfahamu mwenzi wako upya kila siku kuliko kawaida yako.
Jitahidi kupata ufahamu wa kutosha kuhusu yeye jinsi anavyofikiri, na jinsi anavyotenda.
Vumbua zaidi kwa nini yeye na wewe kuna tofauti na jifunze jinsi ya kutumia hizo tofauti kufanya ndoa au mahusiano kuwa imara na wa kudumu.
Jifunze jinsi ya kufahamu yeye na pia ni namna gani unaweza kukubaliana naye katika jambo lolote, au jambo lolote kuhusu watoto, ndugu zake, mambo ya kanisani au kazini.
Pia fanya kila njia kupata ufahamu wa kutosha kuhusu yeye katika masuala muhimu ambayo mara nyingi huwa chanzo cha mifarakano na kuharibika kwa mahusiano kama vile
Pesa
Jinsi ya kulea watoto
Imani za dini
Tendo la ndoa
Na kila kitu ambacho kwenu ni muhimu sana

Sunday, 1 May 2016

NI UPENDO NA HESHIMA.


Katika ndoa si upendo tu bali kuheshimiana.
Mke huhitaji upendo na mume huhitaji heshima.

Sex kwa mwanaume na love kwa mwanamke ni two way street.
Mwanaume anapoihudumia roho yako ili akubaliwe na mwili wako wewe mwanamke (sexual release) maana yake wewe mwanamke unahitajika kumhudumia mwili wake ili na yeye akupe upendo wake.
Kuheshimiwa au heshima ni hitaji la msingi (primary need) kwa mwanaume kama ilivyo kupendwa au upendo ulivyo hitaji la msingi la mwanamke.
Hii haina maana kwamba mwanaume hahitaji upendo au mwanamke hahitaji kuheshimiwa bali ukimheshimu mwanaume hujiona unampenda na ukimpenda mwanamke hujiona unamheshimu.
Katika utafiti mmoja ambapo wanaume 100 waliulizwa swali kama wangelazimishwa kuchagua moja kati ya mambo mawili (negatives) kuishi nayo au kudumu nayo.
(A) Kuwa mwenye na bila kupendwa duniani
(B) Kuonekana hufai na kutoheshimiwa na kila mtu duniani.
Asilimia 70 walichagua A kwa maana kwamba afadhari mwanaume usipendwe na uwe mpweke kuliko kuonekana hufai na kutoheshimiwa na mtu yeyote duniani.
Hii ina maana roho ya mwanaume inajiona afadhari kutopendwa kuliko kutokuwa respected.
Mwanamke hujisikia vizuri kihisia kutokana na maongezi mazuri na mume wake na kwa kutimiziwa hitaji lake la kuwa karibu na mume wake kwa maongezi hujisikia anapendwa.
Mume akigoma kuongea na mke wake hii ina maana kwamba mke hupata signal kwamba hapendwi na mume wake na pia mume hamjali.
Na mume naye akinyimwa sex na mke wake hupata signal kwamba mke hamjali na hamheshimu katika kumtimizia mahitaji yake.
Ni kama mume analalamika kwamba mke wake hupo unfair.
Mke huonesha respect pale anapomtimizia mume wake hitaji la sex na mume huonesha upendo pale anapomtimizia mke wake hitaji ya emotions zake.
Kuna mambo mawili ambayo mke anahitaji kufahamu kuhusu mume wake linapokuja suala la sex.

1.Linapokuja suala la sex kuna tofauti kubwa kati ya mke na mume.
Mwanaume ni visually oriented, hamu ya mapenzi hupanda kwa kuona.
Akimuona mwanamke mrembo sura na umbo anakuwa stimulated.
Mwanamke hasisimki kimapenzi kwa kuona kama mwanaume.

2.Anahitaji tendo la ndoa (sexual release) kama wewe unavyohitaji upendo (emotional release)
Bila sex anajiona mke hamheshimu na anaanza kuonesha tabia zisizo za kiupendo.

Kama ni mwanaume umefika Mahali mke analia kwa sababu ya kukosa upendo unahitaji kujitazama upya na kama ni mwanamke imefika Mahali unamsema mumeo hadi anajiona si lolote au hana tofauti na watoto basi jitazame namna unavyomkose heshima.
Kumbuka maandiko yananena wazi kwamba
Hata hivyo, kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda NAFSI yake mwenyewe, naye mke LAZIMA amheshimu mumewe.