Saturday, 11 June 2016

JE,NIKIMPA HATANIKIMBIA?


Kaka asante sana kwa mafundisho yako na tunajifunza mambo mengi sana kuhusu ndoa na mahusiano.
Mimi ni mdada ambaye kweli Natamani kuolewa hata hivyo mchumba wangu anasisitiza kwamba tufanye mapenzi kwanza (sex) ili ajue nampenda.
Je, mapenzi kabla ya ndoa si ni jambo baya?

Dada asante kwa swali zuri na swali lako si mara ya kwanza kulijibu hapa hata hivyo kila siku tunajifunza kitu kipya.
Kwa ufupi ni kwamba kawaida mtu huhitaji kile ambacho hana.
Kama mchumba wako anakutaka kimapenzi (sex) kabla ya kuoana na wewe kwa ujinga wako ukamkubalia maana yake mkishamaliza kufanya mapenzi mwenzako atakuwa hana kitu cha kuhitaji kutoka kwako ili akuoe.
Umeshajiuza kwake kwa bei rahisi kabisa.
Kumbuka na fikiria upya, ukijirusha na mchumba wako kitandani hata kama mtakuwa mmejifunika shuka gubigubi ataona kila kitu mwilini mwako na atafahamu kila kitu kuhusu wewe.
Kwa mfano ataona alama mbalimbali mwilini mwako kama vile ukubwa wa matiti, chuchu, makovu ulivyonayo, tumbo, makalio, mapaja, sehemu za siri (kipara au msitu), mgongo wako, kiuno chako.
Atafahamu jinsi na namna unavyoguna kimapenzi, unavyobusu kwa kutetemeka, atajua harufu yako ukiwa uchi, atafahamu unavyolala kama gogo au ulivyo na kiuno kizito au ulivyo na aibu au ulivyo na maji au ukavu huko chini na mengine mengi.
Yaani ameona na uchi wako, una nini tena cha kumfanya akusubiri na kukuona special?

HUNA!

Kumbuka kwa kuwa anakutaka maana yake ameshatembea na mabinti wengi hivyo mambo yote nimeandika hapo juu atakuwa analinganisha na wale alitembea nao na kuangalia wewe umekuwa mshamba kiasi gani na kama anakuacha akuache lini.
Sasa hana shida tena kufikiria kuhusu wewe bali kukumbuka tu vile ulikuwa unafanya au ameona na anachofanya analinganisha na wanawake aliotembea nao na kuona wewe hakuna jipya cha maana ni kukubwaga chini na kutafuta mwingine.
Umeshaharibu maana ya vile alikuwa anategema kupata kutoka kwako au tuseme hana chochote cha kutegemea kutoka kwako maana umeshaonesha na kumpa kila kitu.
Kumbuka hana mkataba wowote na wewe na ana uhuru wa kukuacha kwani huna jipya kwake, hana kitu kinachomfanya ajisikie kukisubiri kutoka kwako maana anakujua ulivyo na Umeshajiuza kwa bei rahisi hivyo ana hiari ya kutafuta binti mwingine.
Mapenzi kabla ya ndoa ni dhambi, ni vibaya na ni sababu kubwa ya wengi kutooana na pia ni muhuri wa kukubaliana kwamba ndoa yenu haitakuwa na uaminifu.
Mchumba anayekutaka kimapenzi kabla ya ndoa mkimbie kwa kasi ya ajabu na usigeuke tena nyuma!

INAWAHUSU SANA WANAUME.


Kama mwanamke atajiona yupo appreciated nje ya chumbani basi akifika chumbani atakuwa mwenye furaha (excited), hivyo haina maana kusubiri umpe maneno matamu akiwa kitandani badala yake mpe maneno matamu kuanzia jikoni au sebuleni.

“Never tell a woman she is beautiful when lights are off”

Mwanamke ana hamu kubwa ya ukaribu wa kimapenzi (intimacy) kutoka kwa mume wake, kujisikia yupo karibu na connected.


Kwa mwanaume sex hutokea kule downstairs chini ya mkanda ulivaa, kwa mwanamke sex ni upstairs, kwenye kichwa chake (brain).

Ndiyo maana kwao foreplay ndiyo mfumo wa maisha ya mapenzi.

Na ndiyo maana hawafiki kileleni mara zote.


Wanawake hutumia muda mwingi kuwaza ni kitu gani wanaume wanahitaji katika mahusiano na tatizo kubwa ni kwamba wanaume wachache sana huwaza kuhusu nini wanawake wanahitaji katika mahusiano, basi unahitaji kuwa mmoja ya wanaume ambao si kuwaza tu bali wanafanya kile wanawake wanahitaji.


Mwanamke anapoongea usimkatishe kwani ndiyo njia pekee ya yeye kuwa karibu na wewe.

Kumbuka anapokwambia matatizo yake wakati mwingine hana maana umpe majibu namna ya kutatua (fix the problem) bali anahitaji wewe umsikilize tu na wewe kumsikiliza maana yake unamjali.


Kwa mwanaume fedha ni status hata, hivyo kwa mwanamke fedha ni security, hivyo usiseme fedha zangu, bali sema fedha zetu.

TOFAUTI YA MAWASILIANO KTK NDOA.


Mtazamo wa mwanaume na mwanamke kuhusiana na suala la mawasiliano ni vitu viwili tofauti kabisa.

Wanaume huwa na ulimwengu wao sawa na wanawake ambao nao huwa na ulimwengu wao linapokuja suala la kuwasiliana au maongezi kati ya mke na mume.


Wanaume huwa na ulimwengu wa ngazi (hierarchical social order) kwa kujiweka nafasi ya kutawala, kuwa na amri au kuonesha mafanikio au uhuru na mamlaka aliyonayo kwa wengine. Hii ina maana kwake kuongea ni pamoja na kuhakikisha hayo yametajwa ni jambo la msingi.


Lengo kubwa la mawasiliano au kuongea katika ulimwengu wa wanaume ni kutunza uhuru wao na kuimarisha nafasi yao katika ngazi ya kijamii.


Wanawake kwa upande wao, linapokuja suala la mawasiliano au kuongea ni yeye mwanamke binafsi kujihusanisha au kujijumuisha katika ulimwengu wa wengine (networking).

Kwa mwanamke kuongea ni kuimarisha ukaribu (intimacy) kwa maana kwamba kwa mwanamke kuongea ni suala la feelings.

Mawasiliano au kuongea ni gundi ambayo huwaunganisha wanawake pamoja wao wenyewe au mwanaume na kuongea humfanya kujisikia karibu na yule anaongea naye na wakati mwingine huondoa upweke.


Tangu wanawake wakiwa na umri mdogo, akitokea binti mwingine akawa haongei basi wenzake kumlaumu kwa tabia yake ya kuwa antisocial.


Kwa kuwa wanaume huongea ili kuimarisha status zao ndiyo maana utakuta wanaume wengi huongea kwenye public.

Wanapenda kutoa reports kwenye mikutano, hutoba katika makundi ya watu na kubadilishana habari kazini na wafanyakazi wengine na huko wanang’aa lakini wakifika nyumbani wanakuwa kimya kwani wanajua nyumbani ndipo kwenye uhuru wao wa kuwa silent.


Kwa wanawake nyumbani ni mahali pa kuongea kwa uhuru na ukaribu (intimately), nyumbani ni mahali mwanamke anasubiri kwa hamu kuongea na mume wake anayempenda.


Data nyingi zinaonesha wanaume wengi huongea kwenye public kuliko wanawake na wanawake wengi huchonga sana majumbani.


“Kumsikiliza mwanamke maana yake umesema unampenda”


Kwa mwanaume kuongea ni kuwasilisha habari, kuimarisha status au njia ya kutatua tatizo, kwa mwanamke kuongea ni kuhusisha ukaribu wa ndani (sharing) na mwingine.


Wanawake huwa wanawashangaa sana wanaume kuhusiana na suala la mawasiliano.

Mwanaume A na mwanaume B wanaweza kuangalia TV bila kuongea na kesho wakasema ni marafiki, kitu ambacho kwa wanawake ni vigumu kwani urafiki kwa mwanamke ni pamoja na kuongea.

Wanaume hutumia mfumo wa kuwasiliana kwa kutumia kitu cha tatu (triangulation)

Hii ina maana mwanaume A na mwanaume B ni marafiki kwa kuwa wametumia kitu cha tatu TV kuwapa attention na kujikuta wameunganishwa.


Hii ina maana gani?

Hii ina maana kwamba kama mwanamke ana mume ambaye anachonga sana kwenye public na akifika nyumbani anakuwa bubu ili huyu mwanaume aongee inabidi mke atafute kitu cha tatu inaweza kuwa kufanya kazi yoyote kitu ambacho wote pamoja watakuwa wanafanya na katika kufanya mwanaume utajikuta anaongea.

HUWA WANAANGALIA WENYE MAFANIKIO.


Ni kama miongo mitatu sasa wanaharakati wamejitahidi kuwafanya wanaume wajisikie aibu kuvutiwa kimwili na mwanamke anayevutia katika mwonekano wake.
Ingawa ni kweli wanaume walizaliwa kuona (born to see).
Ni kweli huvutiwa na kushtuka pale mwanaume akikutana na mwanamke anayependeza na kuvutia.
Macho mwanaume yanauwezo wa kuona (scanning) mwanamke anayevutia katika kundi la mamia ya Wanawake utadhani macho yana lensi za kivita kwa ajili ya kurusha makombora kwa usahihi.
Au mwanamke anayevutia akipishana na mwanaume (si wote) lazima afanye juhudi ya ziada kuhakikisha mboni ya jicho inakaza kule alikuwa anaangalia vinginevyo anaweza kusababisha ajali.
Tukija suala la Wanawake; ingawa wao hukataa ukiwauliza ila ndani yao ukweli hujieleza kwamba mwanamke huvutiwa na mwanaume kutokana na mafanikio au uwezo alionao katika jamii.
Kuna usemi wa kingereza kwamba:

“Men are evaluated by income and professional status while women are evaluated by their looks”

Hii ina maana mwanamke na mwanaume wapo wired tofauti linapokuja suala la kumpata mwenzi au mtu wa kuishi naye pamoja.

Mwanaume hutafuta mwanamke ambaye anavutia, mwanaume huona uzuri wa mwanamke kuliko akili ya mwanamke kichwani mwake.

Mwanamke hutafuta mwanaume ambaye ana mafanikio, mwanamke huona akili ya mwanaume kuliko uzuri wake wa sura.

Ndiyo maana kuna utani kwamba mwanaume akiwa na pesa hata kama ana sura inayofanana na chimpanzee bado Wanawake watamuona ni handsome wa nguvu.

Je, ukiwachukua mabinti wanaomaliza chuo na kuwauliza kama wapo tayari kuolewa na mwanaume ambaye atakuwa na kipato cha chini kuliko wao watakubali?

Je, ukimuuliza binti yeyote ambaye ana taaluma yake na anataka kuolewa kama atakubali kuoana na mwanaume asiyevutia ila ana kazi nzuri na kipato cha uhakika?
Si rahisi kwa mwanamke kukubali kwamba anahitaji mwanaume mwenye mafanikio au akili ya maisha ili aoane naye ingawa katika ukweli mwanaume mwenye mafanikio au akili ya maisha humfanya mwanamke kujiona yupo protected, ni mwanaume ambaye anayeonekana anaweza kuwajibika au kwa lugha nyingine si pesa alizonazo bali ule uwezo wa kupata pesa alionao ndiyo humvutia mwanamke.

Ndiyo, wapo wanawake huvutiwa na wanaume walichacha (pigika) au wengine hubeba mwanaume yeyote hata hivyo mwanaume kuwa na pesa ni sexy na mwanamke anajua kuwa na mwanaume asiye na akili ya maisha au uwezo kifedha atatumia muda wake kuishi naye huku akiwa na hofu na mashaka kuhusu pesa.
Kwa wanawake wengi “money is security” najua utabisha ila ndo ukweli!

KUFIKA KILELENI KWA MWANAMKE.


Je, kufika kileleni kwa mwanamke anapofanya mapenzi ni tofauti na mwanaume?

Tafiti nyingi zimefanyika na mojawapo ni ile iliyoruhusu Wanawake na wanaume wote kuandika vile wanajisikia wanapofika kileleni na baadae wakaruhusu watu wengine wasome na wapendekeze nani ameandika kati ya mwanamke au mwanaume hata hivyo ilikuwa vigumu kwa wasomaji kufahamu maelezo yaliyoandikwa yameandikwa na mwanaume au mwanamke.
Hii ina maana kufika kileleni kwa mwanaume na mwanamke huhusisha uzoefu unaofanana.
Hata hivyo kuna tofauti ya uzoefu wa kufika kileleni kwa Wanawake na hata mwanamke mmoja na hii tofauti hutokana na aina ya kusisimuliwa ili kufika kileleni kuanzia kisimi, uke, G-spot, matiti na hata picha za kizushi (fantasy/imagery)

Je, ni kweli kwamba kinachomfikisha kileleni mwanamke huyu ni tofauti na mwanamke yule?


Ni kweli pia hata mwanamke huyo mmoja kinachomfanya asisimuliwa kufika kileleni leo ni tofauti na wiki ijayo na mwezi ujao na hata miaka matano au kumi ijayo.
Wapo wanaopenda kusisimuliwa G-spot na wengine hawataki, wapo wanaopenda kusisimuliwa kisimi wengine hakuna lolote, wapo wanaopenda kusisimuliwa uke na wengine hawataki. Wengine matiti au masikio au shingo nk kila mmoja au hata huyo mmoja uliyenaye anatofautiana kutokana na mzunguko wake wa siku kwa mwezi.
Kama tunavyopenda vyakula tofauti na nguo tofauti na usisimuliwe wapi kwa mwanamke kufika kileleni ni tofauti.
Kuamini kwamba kumsisimua mwanamke Mahali fulani ndipo huweza kumfikisha kileleni bila kuwasiliana naye wakati mwingine huweza kuwa kero.

Je, mazoezi ya Kukaza misuli ya uke huweza kuongeza uwezekano wa mwanamke kufika kileleni kirahisi?

Mazoezi ya kege



Mazoezi ya kukaza misuli ya uke ni muhimu mno. Uwezo na uimara wa misuli ya PC (puboccoccygeus) unahusiana mno na mwanamke kufika au kufurahia tendo la ndoa.
Wanawake ambao hawawezi kufika kileleni kirahisi wana misuli ya PC iliyodhaifu (loose).
Mwanamke anayeweza kufika kileleni kwa kusisimuliwa kisimi ana misuli imara hata hivyo mwenye misuli imara zaidi ni yule anayeweza kufika kileleni kirahisi kwa uke wake.

Je, ina maana kuna Wanawake huweza kufika kileleni kwa kulala na kuanza kufikiria picha za kizushi (fantasy) hata kama yupo peke yake?

Ni kweli.
Beverly Whipple, R. N. PhD katika maabara yake aliwaalika Wanawake 10 ambao walisema wana uzoefu na kufika kileleni kwa picha za kizushi (fantasy) na hao Wanawake walionesha mgandamizo wa damu, mapigo ya moyo, kubadilika kipenyo cha macho sawa na kufika kileleni kwa njia zingine kama uke na kisimi.


Wanawake huwa na tofauti za kufika kileleni kutokana na aina ya kusisimuliwa pamoja na sababu zingine kama vile anavyojisikia huo wakati, kiwango cha homoni.
Si suala la kubonyeza button na mwanamke akafika kileleni. Kufika kileleni si conditioned reflex.
Mara nyingi lengo la mume katika sex ni kuhakikisha mke anafika kileleni je kuna tatizo kuwa na mtazamo kama huo?
Kawaida tunapozungumzia maisha huwezi kukwepa kuweka malengo.
Linapokuwa suala la sex ni kweli kwamba wanaume huwa goal-directed na Wanawake huwa pleasure-directed.
Tatizo huja pale watu wameshindwa kufahamu hiyo siri na hasa wanaposhindwa kuwasiliana na wapenzi wao.
Mwanamke anaweza kufika kileleni kwa kusisimuliwa sehemu zingine za mwili kama vile masikio nk bila kuwasiliana inaweza kuleta shida kwani we are all unique.

Friday, 10 June 2016

NDOA NI KAZI..


Ndoa ni kazi.
Inayochukua muda, jitihada na commitment na wakati mwingine huhitaji professional counselling.
Kama umefika Mahali ambapo wewe na mume wako au mke wako hamuwezi hata kuwasiliana (kuongea) bila kuvurugana na umeanza kufikiria kuachana kama njia bora zaidi basi unahitaji msaada kwani kuachana bado si jibu la matatizo yote.
Katika ndoa mwanaume na mwanamke ni tofauti na kila mmoja ana mahitaji muhimu ambayo ni lazima mwenzake ayatimize na kutotimizwa hayo mahitaji husaidia kukwetua njia ya kila mmoja kutoridhika na mwenzake.
Kwa ufupi mahitaji muhimu ya mwanaume (yale anapenda mke wake amtimizie) ni kama ifuatavyo

1. HITAJI LA KURIDHISHWA KIMAPENZI (SEX).

2. HITAJI LA KUBURUDISHWA, RAHA, KUSTAREHE, KUPUMZIKA, NAFASI YA KUPUMUA, BURUDANI.

3. HITAJI LA KUWA NA MKE ANAYEVUTIA.

4. HITAJI LA KUWA NA AMANI NA UTULIVU.

5. HITAJI LA KUAMINIWA, KUHUSUDIWA NA KUHESHIMIWA.

Mahitaji ya mwanamke katika maisha ya ndoa (vile mwanamke anapenda mume amfanyie au kumtimizia) ni kama ifuatavyo:

1. HITAJI LA UPENDO, KUPENDWA, MAHABA NA HURUMA.

2. HITAJI LA MAONGEZI, MAZUNGUMZO, MISEMO, POROJO, KUSIMULIANA NA SOGA.

3. HITAJI LA UKWELI, UADILIFU, KUAMINIANA, UNYOFU, WIMA NA UWAZI.

4. HITAJI LA UHAKIKA WA KIFEDHA, AMANA KIFEDHA, UHAKIKISHO KIFEDHA, ULINZI KIFEDHA, USALAMA KIFEDHA, UTHABITI NA AMANI KIFEDHA.

5. HITAJI LA KUJITOA KWA AJILI YA FAMILIA.

Kwa ufafanuzi ni kwamba mwanamke hupenda mume akimaliza kazi jioni kwanza ajithidi kuwahi nyumbani ili ale chakula (supper/dinner) na mke na watoto, akae na mke na kuongea masuala ya familia kama watoto, matumizi ya fedha nk na hupendelea baba kutumia muda na watoto na mke na si kuangalia TV.
Mume naye hupenda anaporudi kazini mke ampe angalau dakika 15 apumue ndipo aanze kuuliza maswali na kuelezea siku ulivyokuwa na ikifika muda wa kulala mke aanzishe kwamba anahitaji tendo la ndoa.

MIMBA NA TABIA ZAKE..



Naitwa Jeffy na mke wangu anaitwa Judy, nipo nyumbani nafanya kazi zangu na mke wangu Judy ameenda kwa Daktari ili kujua inakuwaje mbona amejikuta asubuhi mambo si ndivyo kama kuchoka si kuchoka, anajisikia kichefuchefu na kuna dalili lile zoezi letu la kupata first born limewezekana.

Judy amerudi na Daktari amemwambia mke wangu ana mimba ya wiki mbili na ndani ya miezi tisa tutakuwa na mtoto.

Nipo excited ila nawaza sana namna ya kuwa baba na kuitwa baba, mikikimikiki ya nepi usiku na mchana.

Ni wiki sasa naona mke wangu iwe mchana iwe usiku iwe lunch, breakfast au supper yeye anataka ale embe na kibaya zaidi lisiwe limeiva sana wala lisiwe halijaiva sana.

Anafakamia maembe kiasi cha kunifanya nihisi anaweza kuzaa maembe badala ya mtoto.

Kinachonishangaza hata moon yake inabadilika kila wakati, dakika moja ni chakalamu na dakika inayofuata ni balaa, mkali kama nyuki na ngumu kuishi naye, alikuwa anapenda juice ya machungwa, nanasi sasa hataki hata kusikia harufu yake, cha ajabu hataki hata juice ya maembe wakati anapenda kula embe (lisilo bichi sana na ambalo halijaiva sana).

Akiniona nafakamia juice basi ananiambia kwamba kwa nini sijali hisia zake.

Kibaya zaidi sasa hata majirani hawapendi inafikia muda anataka tuhame muda huohuo na kila ninapojitahidi kumwambia haitawezekana anaiita mimi ni selfish na kwamba kila ninachojali ni mimi mwenyewe na si yeye.

Mara ananiambia anahitaji ale mishikaki na mimi naondoka kiguu na njia hadi km 4 kufuata mishikaki ili mzazi mtarajiwa ale, ile nikifika nyumbani tu na kufungua ili nimpe ile mishikaki anabadilika ghafla eti nimetumia muda mrefu mno na sasa hahitaji.

Sasa ameanza mtindo anaamka saa tisa au nane au kumi usiku na kuniomba tuongee, namuuliza na huu usiku wa manane tuongee kitu gani, majibu ananipa analalamika kwamba sijali tena kuongea na yeye na kwamba nilichokuwa napenda ni kumtia mimba.

Finally, mtoto wetu akazaliwa na kila kitu kikaanza kurudi katika hali ya kawaida..

Unaweza kujifunza kitu kama mke wako atakuwa na tabia hizo wakati akiwa mjamzito..Mvumilie kwani ni kipindi cha mpito tu.