Tuesday, 18 August 2015

ZINGATIA HAYA ILI UWE NA NDOA IMARA

FUNGUO ZA KUJENGA NDOA IMARA NA MAHUSIANO YA KUDUMU


USIKAE NA DONGE MOYONI

Kitu kizito kuliko vyote kukibena duniani ni DONGE MOYONI.

Pia unaweza kuathirika zaidi na kile umeweka moyoni kwani mwenzako anaweza kuwa hajui.

Kuweka vitu moyoni bila kuvitoa au kuzungumza na mwenzi wako huweza kuathiri afya na amani.


Kawaida kama una hasira hakikisha unazimaliza mapema na kuelewana na mwenzi wako kabla jua halijazama na kama ni usiku hakikisha unaenda kulala huku umeshalitoa donge lako.

FAHAMU KWAMBA HONEYMOON SIYO MAISHA YA NDOA

Kuna tofauti kubwa kati uchumba, Honeymoon na maisha ya ndoa, uchumba na Honeymoon hupewa moto kemikali ambazo zimo ndani yetu. Hatua ya pili ambayo ni ndoa yenyewe hapa tairi linakutana na barabara ili kuweka wazi uimara na udhaifu. Katika ndoa ni majukumu na kuwajibika na familia iliyoanzishwa, wakati uchumba na Honeymoon ni kuburudishana.

MUNGU KWANZA
Kumweka Mungu kwanza katika ndoa, huleta furaha ya kweli (joy) faraja na ulinzi. Kumweka Mungu kwanza maana yake mume na mke wanaishi kwa utii na amri za Mungu mwanzilishi wa ndoa wanaomba pamoja na kuwa na mahusiano yanayoongozwa na Mungu. Kwa vipimo vya kibinadamu huwezi kuwa na furaha siku zote kwa safari ndefu kama ya ndoa furaha ya kweli hupatikana kwa kumuweka Mungu namba moja.



MFAHAMU MWENZI WAKO NA KUJIFAHAMU WEWE MWENYEWE

Baada ya mapenzi ya Honeymoon kwisha wanandoa huwa na mgodi wa kuanza kuchunguzana na kufahamiana. Wakiwa Honeymoon wanandoa huona kila kitu shwari, wakianza maisha ya ndoa kila mmoja huanza kuona makosa kwa mwenzake hata Kirusiyo hiyo ni nafasi ya wanandoa kufahamiana ni nafasi nzuri ya wanandoa kusifiana, kutumia muda pamoja, kupeana zawadi, kusaidiana kazi ndogo ndogo za nyumbani, kubusiana na kukumbatiana (touch)


KUWA MSIKILIZAJI MZURI

Binadamu ana asili ya kupenda kuongea zaidi kuliko kusikiliza, kusikiliza kuna maana zaidi kuliko kuongea, wanaume Huongea ili kitu kifanyike na mwanamke Huongea kuchangia wazo na hisia zake. Kuna wakati kila mwanandoa anahitaji kusikilizwa wanaume ni vizuri kuwasikiliza wake zao wanapotoa mawazo yao na hisia zao. Mwanamke huongea maneno 45 elfu kwa siku, na mwanaume 15 elfu, ni nani anahitaji kusikilizwa zaidi?


KICHEKO

Wanandoa wanahitaji kuwa na kicheko siyo kuwa serious kila wakati kutaniana kusikopitilizwa huongeza furaha katika ndoa pia ni zawadi kutoka kwa Mungu. Wanandoa ni muhimu kuwa na wakati ambapo wanaweza kukaa pamoja na kuwa na kicheko iwe ni kuangalia TV na kusimuliana hadithi ambazo zinawafanya mcheke ni vizuri wanandoa kucheka wakiwa wao wenyewe au wakiwa pamoja na watu wengine. Kicheko huleta raha katika ndoa.


JIFUNZE KUKUBALI KWAMBA UMEKOSA NA KUOMBA MSAMAHA

Binadamu wote tunafanya makosa na wakati mwingine hayo makosa huumiza tunaowapenda. Lazima tukumbuke wakati tumekosa tunahitaji tuombe msamaha. Usizunguke (indirect way) bali be straight sema “Nisamehe au I am sorry”. Pia usibadili topic au kuanza kusifia ili usiombe msamaha.


Pia tunahitaji kufahamu kwamba wenzi wetu si mara zote wapo perfect kama ulivyo wewe (imperfect).

Pia ni vizuri kufahamu kwamba ndoa ni kazi inayoendelea na siyo mwisho wa safari.


MHESHIMU, USIMDHARAU

Kumdharau mwenzi wako wakati mwingine huwa kitu rahisi sana. Mwanzo wa mapenzi hata kama kuna hitilafu mara nyingi huitilii maanani, una minimize, lakini baada ya honeymoon kwisha utaona na kukumbuka/ Tambua mambo mengi ambayo huyapendi na unaweza kuanza kupambana nayo na kumdharau mwenzi wako.

Kumdharau mwenzi wako ni kama mmomonyoko ambao ni sumu kwenye mahusiano.

Mwanandoa mwenye busara hawezi kumuaibisha mwenzi wake bali ataongea kwa hekima na kumaliza tofauti zozote kwa upendo.

Kawaida angalia uwezo wake na si udhaifu wake.


USICHUJE (filtering)

Usimchekeche na kumbandika jina la kudumu kwamba mara zote yupo vile:

Sentensi zinazoanza na haya maneno uwe makini sana
Kila siku unafanya KirusiiKirusii…………………..

Mara zote nakwambia lakini………………

You never……………………

You always……………………

Mara nyingi Ukitokea msuguano wengi huanza kulalama kwa kutumia hayo maneno huwa na maana kwamba unafanya the same mistake over and over na anakupa hicho kibandiko kama jina la mkosaji wa kila siku.

Si kweli kwamba unaweza kufanya makosa yaleyale kila siku, muda wote miaka yote.


WEKA MKAZO KWENYE UWEZO NA SI UDHAIFU

Mwanamke na mwanaume wapo tofauti siku zote na ni mpango wa Mungu kuwa tofauti ili kwa tofauti tuweze kusherehekea uumbaji wa Mungu na ili mke na mume waweze kila mmoja kumridhisha mwenzake.

Huwezi kuwa na mwenzi ambaye ana udhaifu mwingi kuliko uwezo na ukiona ana udhaifu mwingi kuliko uwezo basi tatizo ni wewe si yeye.

SEMA NAE..!!

Kuongea suala la tendo la ndoa (sex) katika ndoa au kwa mume wako au kwa mke wako ni moja ya topic ngumu sana chini ya jua au katika uso wa dunia.
Kama utakuwa na maongezi au mawasiliano kuhusiana na suala la sex katika ndoa yako maana yake mtakuwa wazuri katika hiyo department.
Wanandoa wengi ambao wamekuwa na tabia ya kuongea kuhusu maisha yao ya sex kwa uhuru na ukweli wamekuwa na maisha mazuri chumbani kwako kwani si rahisi kufahamu mwenzako anahitaji kitu gani hadi umwambie.
Kuwa wakimya kuhusiana na kuongea kuhusu sex na mke wako au mume wako husaidia kuwa wajinga zaidi na wakati mwingine kutoridhishana sawa na uhitaji wa mwili wako au feelings zako.
Hatari kubwa zaidi ni pale wanandoa wanaposhindwa kuongea wenyewe na matokeo yake kutoridhika na kutoridhika ndiko husaidia kukwetua njia ya mmoja au wote kuanza kuangalia nje (kuchepuka)
Firikia wewe ni mwanamke una vitu mume wako akifanya basi huwa unajisikia kusisimka na mwili kuanza kutoa kuwa juicy na kutamani sana sex na mume wako.
Kwa nini usiwe huru ukamwambia kwamba unapenda iwe hivi:
Mwambie!

WAKATI NIMESISIMKA
Natamani mume wangu uwe na wewe unatoa sauti au na wewe uwe unaongea,
Napenda uwe unaongea maneno matamu ya kimapenzi,
Napenda mume wangu nini unakipenda kwenye mwili wangu,
Napenda uniguse (touch) na kunichezea namna hii (onesha),
Napenda ufanye hivi kwenye chuchu na matiti yangu,
Napenda unitazame usoni,
Napenda unichezee kisimi namna hii (mwambie unapenda afanye kwa kutumia nini na namna gani)
Napenda ufanye hivi kwenye G- spot,
Napenda kuchezea uume wako hivi nk

WAKATI WA SEX
Napenda na wewe uwe unaguna na kutoa sauti za kimahaba au uongee maneno matamu na elezea namna unafurahia au unajisikia kuwa ndani yangu,
Napenda uendelee kunibusu namna hii,
Endelea kusisimua kisimi changu namna hii (eleza kwa kutumia nini)
Natamani tunapoanza tuanze kwa mlalo huu na baadae tumalize kwa mlalo (love making position) hii,
Natamani uanze kwa kasi au msuguano wa polepole na baadae haraka zaidi namna hii,
Nioneshe kama na wewe unafurahia,
Nk

UNAPOFIKA KILELENI
Napenda upunguze kasi na kuniacha au napenda uongeze kasi unapoona nakaribia kufika kileleni,
Napenda unikumbatie na kunibusu nk

BAADA YA KUMALIZA SEX
Napenda sana uendelee kubaki ndani yangu hadi tulale usingizi nk,
Napenda unikumbatie huku tunalala,
Napenda angalau mkono wako au mikono yako ibaki mwili mwangu huku tunalala,
Natamani tuendelee kupiga story,
Natamani uendelee kunibusu.
Kumbuka huu ni mwongozo tu kwani kila mwanamke ana mahitaji yake kutoka kwa mume wake jambo la msingi ni kwamba jisikia huru kuongea na mume wako nini unahitaji kabla, wakati na baada ya sex.
Usisubiri eti utafaidi sana sex baada ya kumaliza kusomesha watoto au hadi mfanikiwe maisha au hadi umalize miradi Unafanya kwani itafika Mahali utakuwa na pesa na muda ila energy huna.

NI KUWEKANA WAZI TU.

Kawaida linapokuja suala la mapenzi opposite attract na the same repel kwa maana kwamba mara nyingi huwa tunavutiwa na strength za mwingine kwa kuwa hufanana na weakness zetu.
Watu ambao hutuvutia sana ni wale ambao huonesha strength katika maeneo ambayo sisi tupo weak.
Ukikutana na mtu wa jinsia tofauti na wewe na mkawa pamoja kwa muda mrefu pamoja na ukavutwa kutokana na strength zake ambazo zinakubaliana kwenye weakness zako penzi huzaliwa na baadae inaweza kuwa ndoa.

Ndoa ni kuwekana wazi.
Wakati Bwana harusi na Bibi harusi wanaposimama mbele ya Mhubiri kanisani na kutoa ahadi zao kwa Mungu na wageni wote walioalikwa huwa wanaahidiana kwamba
“Ninakuahidi kukupenda na kukunyenyekea kwa muda wote wa uhai wetu”

Hii ina maana kwamba maharusi huwa wanakazia kwamba kwa kuwa nakubali kiapo chako na unyenyekevu wako kwangu leo basi nitajifunua kwako mzimamzima kuanzia sasa si kimwili tu bali kisaikolojia pia kwani hadi hapa nimejidhihirisha/nimejifunua kwako katika upande ule wa mazuri tu (strength) kuhusu mimi.
Sasa kwa kuwa tunaoana nitajiweka wazi kwako mzimamzima na nina imani kubwa na wewe kwamba utaendelea kunipenda kama nilivyo.
Ndoa ni kuwekana wazi, ni kila mmoja kujidhihirisha kwa mwenzake kama alivyo pamoja na weaknesses zake.
Vitu vyote ambavyo vilikuwa vimejificha wakati wa uchumba hadi honeymoon basi kuanza kwa ndoa vyote huwa mezani juu kwa kila mmoja kuona.
Na hapo ndipo kwenye mtihani wa kwanza wa wanandoa wapya.
Honeymoon siyo residence ya kudumu ya ndoa, baada ya honeymoon (na wengine hata wakati wa honeymoon) wanandoa wapya hushikwa na mshangao wa partner anavyobadilika na kuwa kama mwingine kabisa.
Ukweli ni kwamba unapoona partner wako anaonekana kama mwingine tofauti na yule wa wakati wa uchumba, ukweli ni kwamba sasa matching inaanza, kufahamiana kikwelikweli kunaanza na wenye hekima na busara huwa makini katika kukabiliana na hizo tofauti na kuendelea kusherehekea hizo tofauti kwa upendo na kuvumiliana kwani huwezi kumbadilisha na kumbadilisha ni kupoteza muda wako.

JE,STYLE IPI NI NZURI?

Linapokuja suala la mwanamke kupata mimba (ujauzito) kuna mijadala mingi ipo kuhusiana na mlalo upi unafaa kwa ajili ya kutengeneza mtoto.
Hata hivyo hakuna mlalo ambao unajulikana au kushauriwa kwamba ndio unafaa duniani hata hivyo kuna maswali mengi ambayo huhusiana na suala zima la tendo la ndoa na kupata mimba.

Je, Baadhi ya milalo ni bora zaidi ya mingine linapokuja suala la kupata mimba?

ingawa kumekuwa na utafiti mdogo kuhusiana na hili suala bado utafiti umekuwa unaonesha kile hutokea wakati wa tendo la ndoa.
Katika zote missionary position (Mwanaume juu mwanamke chini huku wakiangaliana) inaonekana ndiyo inatoa uwezekano mkubwa zaidi kwa kuwa husaidia kuwa na deep penetration kuzihakikishia sperms zaidi ya mlango wa uzazi (womb).
Pia mwanamke kuingiliwa kwa nyuma (rear entry) huwezesha positioning ya sperms vizuri kama missionary position.

Je, kama mwanamke natakiwa kulala na si vinginevyo ili kupata mimba?

Wanasayansi wanasema ili kuondoa uwezekano wa sperms kushindwa kuogelea kutokana na gravity hasa mwanamke anapokuwa amekaa au simama juu ya mwanaume. Kama sperms zina afya hakuna tatizo ingawa kama sperms hazina afya mwanamke anashauriwa kulala wakati wa tendo la ndoa au hata baada ya tendo la ndoa ili sperms kufikia target.

Je kuna muhimu wowote kufika kileleni ili kupata mimba?

Ni dhahiri kwamba mwanaume ni vizuri afike kileleni (mshindo) katika process ya “baby making” ili kuhakikisha anazipa sperms speed inayotakiwa kufika kwenye target. Utafiti wa karibuni unaonesha pia mwanamke ni vizuri afike kileleni ikiwezekana wakati mmoja na mume wake kwani contractions zinapotokea husaidia sperms kufikia mji wa uzazi.

Je, kama ninataka mtoto wa kike au kiume mlalo gani unafaa?

Suala la milalo halina uhusiano na jinsia ya mtoto bali timing na frequency ndiyo muhimu kwa kusababisha jinsia ya mtoto.

KUNA TOFAUTI...!!

Wanandoa imara au waliofanikiwa katika ndoa yao ni wale ambao wanaweza kukaa pamoja na kujadili tofauti zao katika namna ambayo huwezesha kujenga ukaribu kimapenzi (intimacy) zaidi.

Wanafahamu jinsi ya kukubaliana na kutokukubaliana (disagreements), wanafahamu namna ya kuhakikisha kutokukubaliana hakusababishi maafa kwenye maeneo mengine ya mahusiano yao.
Si kweli kwamba tunaolewa au kuona ili kuchukuliana katika migogoro hata hivyo kutofahamu namna ya kupambana na migogoro huweza kusababisha kutofanya vizuri katika mambo mengine ambayo ndo sababu za kuoana.

Kukwepa migogoro au kukwepa kuongea pamoja eti kunaweza sababisha mgogoro mzito si hekima wala busara kwani njia bora ni kuwa wazi kuongea pamoja ili kujadili tofauti au kutokuelewana kunakojitokeza ili wanandoa waweze kufahamiana zaidi.

Kwa lugha nyingine si rahisi mke kufahamu mume anapenda chakula gani bila kuongea kwanza, pia haina maana kukaa kimya kwa kuwa mke anapika chakula usichopenda basi atabadilisha na kukupikia chakula unapenda. Si rahisi mume kukupeleka outing kama hamuongei.

Wapo wanandoa ili kuepuka migogoro huacha kuongea na kuwa kimya, ni muhimu sana wanandoa kufahamu utafiti wa ndoa imara unasemaje.
Kila ndoa imara kwa wastani ina maeneo 10 ambayo wanandoa hawafanani au hawawezi kukubaliana au kwa lugha nyingine hawataweza kufikia muafaka maishani mwao.

Kwa nini hizi ndoa imara pamoja na tofauti 10 na bado zinaitwa ndoa imara?
Jambo la msingi au siri kubwa ni kwamba wanandoa wanafahamu namna ya kukabiliana na hizo tofauti na kuishi nazo, kupendana pamoja na kutofautiana na zaidi kila mmoja anamuelewa mwenzake na kukubaliana kihisia na kuchukua nafasi yake kama ni yeye.

Wanandoa imara hufurahia na kusherehekea tofauti zao na hufarijika kwa kuwa sasa anamfahamu mwenzake, anajua eneo ambalo wapo tofauti then wanaaendelea kupendana huku kila mmoja akifahamu namna ya kukabiliana na hizo tofauti.

Hawa wanandoa imara wanafahamu wazi kabisa kwamba hata kama watabadilisha partners bado watapata matatizo mapya katika maeneo ya kutokukubaliana, kuwa tofauti na kwa huzuni kubwa kazi kubwa itakuwa ni mizigo waliyotoka nayo kwenye ndoa zao za kwanza kama vile watoto nk ndiyo maana kwao talaka haina sauti wala nguvu na huwa haizungumzwi, ni neno lililofutwa katika maongezi.
Zaidi ya kukabiliana na tofauti na kutokukubaliana pia ni muhimu sana kusherehekea/kumbatia mabadiliko.
Wakati tunaoana huwa tunaahidi kukaa pamoja hadi kifo kitakapo tutenganisha hata hivyo huwa hatuahidi kubaki vilevile bila mabadiliko yoyote, tunahitaji kukua, kuongezeka skills, kwa wabunifu na wazuri zaidi kila siku zinavyozidi kwenda.
Kuna mambo mengi tunaweza kujifunza kadri ziku zinavyozidi kwenda kama vile kusema asante, kuomba msamaha.
Hivyo inawezekana kujifunza tabia njema ambazo zinaweza kujenga ndoa na kuziacha tabia mbaya ambazo zinaweza kuharibu ndoa.

MTIMIZIE HITAJI LAKE..

Kazi si kuoana kazi ni kutimiziana mahitaji bila kuchoka!

Ndoa ni kazi.
Inayochukua muda, jitihada na commitment na wakati mwingine huhitaji professional counselling.
Kama umefika Mahali ambapo wewe na mume wako au mke wako hamuwezi hata kuwasiliana bila kuvurugana na umeanza kufikiria kuachana kama njia bora zaidi basi unahitaji msaada kwani kuachana bado si jibu la matatizo yote.
Katika ndoa mwanaume na mwanamke ni tofauti na kila mmoja ana mahitaji muhimu ambayo ni lazima mwenzake ayatimize na kutotimizwa hayo mahitaji husaidia kukwetua njia ya kila mmoja kutoridhika na mwenzake.
Kwa ufupi mahitaji muhimu ya mwanaume (yale anapenda mke wake amtimizie) ni kama ifuatavyo

HITAJI LA KURIDHISHWA KIMAPENZI (SEX).

HITAJI LA KUBURUDISHWA, RAHA, KUSTAREHE, KUPUMZIKA, NAFASI YA KUPUMUA, BURUDANI.
HITAJI LA KUWA NA MKE ANAYEVUTIA.
HITAJI LA KUWA NA AMANI NA UTULIVU.
HITAJI LA KUAMINIWA, KUHUSUDIWA NA KUHESHIMIWA.

Mahitaji ya mwanamke katika maisha ya ndoa (vile mwanamke anapenda mume amfanyie au kumtimizia) ni kama ifuatavyo:
HITAJI LA UPENDO, KUPENDWA, MAHABA NA HURUMA.
HITAJI LA MAONGEZI, MAZUNGUMZO, MISEMO, POROJO, KUSIMULIANA NA SOGA.
HITAJI LA UKWELI, UADILIFU, KUAMINIANA, UNYOFU, WIMA NA UWAZI.
HITAJI LA UHAKIKA WA KIFEDHA, AMANA KIFEDHA, UHAKIKISHO KIFEDHA, ULINZI KIFEDHA, USALAMA KIFEDHA, UTHABITI NA AMANI KIFEDHA.
HITAJI LA KUJITOA KWA AJILI YA FAMILIA.

Kwa ufafanuzi ni kwamba mwanamke hupenda mume akimaliza kazi jioni kwanza ajithidi kuwahi nyumbani ili ale chakula (supper/dinner) na mke na watoto, akae na mke na kuongea masuala ya familia kama watoto, matumizi ya fedha nk na hupendelea baba kutumia muda na watoto na mke na si kuangalia TV.
Mume naye hupenda anaporudi kazini mke ampe angalau dakika 15 apumue ndipo aanze kuuliza maswali na kuelezea siku ulivyokuwa na ikifika muda wa kulala mke aanzishe kwamba anahitaji tendo la ndoa.

NI PENZI AU PESA?

Huwezi kuongelea mapenzi bila kutaja suala la pesa. Wapo watu ambao wanaamini kuwa na pesa nyingi, nyingi kabisa za kutosha husaidia penzi kuwa imara na linaloridhisha.
Hata hivyo tumeona penzi la uhakika hata wakati pesa zikiwa hazipo au tumeona penzi la kweli hata katikati ya umaskini uliokithiri.
Hii haina maana kwamba pesa siyo muhimu, pesa ni muhimu sana. Na pesa ina umuhimu kwa kila mahusiano hata, hivyo inabidi ujiulize mwenyewe je, upo kwa ajili ya pesa au kwa ajili ya penzi la kweli.
Utakuwa mtu wa maana sana kama utakuwa unatazama na kuwekeza kwenye penzi la kweli na si pesa.
Pia ni vizuri kuwa makini na mtazamo wa mpenzi wako je yupo kwako kwa ajili ya pesa au kwa ajili ya penzi la kweli.
Mtazamo wake kuhusu pesa ni muhimu sana.