Thursday, 16 June 2016

NDOA IMARA NA ZINAZODUMU.


Ukiona kosa moja kwa mke wako au mume wako, hutakiwa kuliangalia na kuliwekea sura kamili au hutakiwi kulipa uhai badala yake lipe jina na liweke kando kwa kujaribu kulinganisha na uzuri wake au mambo matano mazuri kuhusu yeye(positive traits).


Kwa mfano unajikuta mume wako au mke wako amewaka hasira kwa jambo dogo tu hadi unahisi dunia umebadili mwelekeo, hata hivyo badala ya kuanza kufikiria hizo hasira zake Unachotakiwa kufanya ni kujiambia mwenyewe kwamba:

“ Ni kweli ana hasira hata hivyo ni mwanamke/mwanaume anayenijali, anayenipenda, anayewajibika, ni mbunifu na anajua kuniridhisha chumbani”.

Kumbuka strongest relationships ni zile ambazo partners wanaweza kujenga picha ya uzuri wa mwenzake (idealized/illusioned) kuhusu uwezo wake na si udhaifu.


Kwa kuufuta udhaifu au kuondoa mawazo kuhusu udhaifu wake na kuweka uwezo wake au uimara wake unahusanisha information muhimu za kufanya mke wako au mume wako awe mzuri zaidi na ukampenda zaidi.

Kwa miaka zaidi ya 100 hekima na busara iliyodumu na ambayo hata wengine wanaamini ni ile kwamba kinyume cha uzuri ni ubaya.

Hii ina maana kwamba Ukitaka kujua uzuri wa kitu basi unatafuta ubaya wake kwanza.

Ukitaka kujua furaha ni kitu gani au ina thamani kiasi gani unajaribu kumchunguza mtu mwenye huzuni kwanza.

Watoto ambao wanatumia madawa ya kulevya hutumika kujua namna ya kuwalinda watoto wasiotumia madawa ya kulevya wasijiingize kwenye hivyo vitendo.


Watoto ambao ni watoro shuleni hutumika kujifunza kuwafanya watoto wengine wawe na mahudhurio mazuri.


Linapokuja suala la ndoa si kweli kwamba ili kujifunza ndoa kuwa nzuri au kusiwe na talaka basi ni vizuri kujifunza ndoa ovyo au ndoa ambazo zimeishia kwenye talaka.

“Bad is not always the opposite of good”

Ukweli ni kwamba linapokuja suala la ndoa Ukitaka kujenga ndoa nzuri au imara unahitaji kujifunza kutoka ndoa imara na si ndoa ovyo au zile zimeishia kwenye talaka.

Vitu vinavyopatikana kwenye ndoa imara havina uhusiano na vitu vilivyosababisha ndoa ovyo kuwa ovyo kwani ndoa imara zina siri yake ambayo si kinyume cha ndoa ovyo.


Ndoa imara ni zile ambazo mwanandoa mmoja au wote huwa na picha kamili ya mwenzi wake, huwa na sifa ambazo amezijenga kwa mwenzi wake ambazo ukweli ni kwamba inawezekana kwamba mwenzi wake hana ila yeye huamini anazo na ni kuwa positive kwamba anamfaa.

Ndoa imara na zinazodumu ni zile ambazo mwanandoa huamini katika uimara au uwezo wa mke wake au mume wake hata kama huo uwezo hana.

Unaweza kuona kama ni utani au contradiction hata hivyo ndio ukweli.

Nina amini mke wangu ni caring, nina amini mke wangu ni sweetie, nina amini mke wangu ananifaa, nina amini mke wangu ni mzuri, nina amini mke wangu ni mchapa kazi, nina amini mke wangu ni mrembo, nina amini mke wangu ananifaa hata kama hizo sifa hana kwa kuwa naamini basi ninavyoamini ndivyo itakuwa na nitakuwa na furaha kuliko kuwaza vinginevyo.

NI VIZURI KUWA WAZI.


Kawaida linapokuja suala la mapenzi opposite attract na the same repel kwa maana kwamba mara nyingi huwa tunavutiwa na strength za mwingine kwa kuwa hufanana na weakness zetu.
Watu ambao hutuvutia sana ni wale ambao huonesha strength katika maeneo ambayo sisi tupo weak.

Ukikutana na mtu wa jinsia tofauti na wewe na mkawa pamoja kwa muda mrefu pamoja na ukavutwa kutokana na strength zake ambazo zinakubaliana kwenye weakness zako penzi huzaliwa na baadae inaweza kuwa ndoa

Ndoa ni kuwekana wazi.

Wakati Bwana harusi na Bibi harusi wanaposimama mbele ya Mhubiri kanisani na kutoa ahadi zao kwa Mungu na wageni wote walioalikwa huwa wanaahidiana kwamba
“Ninakuahidi kukupenda na kukunyenyekea kwa muda wote wa uhai wetu”
Hii ina maana kwamba maharusi huwa wanakazia kwamba kwa kuwa nakubali kiapo chako na unyenyekevu wako kwangu leo basi nitajifunua kwako mzimamzima kuanzia sasa si kimwili tu bali kisaikolojia pia kwani hadi hapa nimejidhihirisha/nimejifunua kwako katika upande ule wa mazuri tu (strength) kuhusu mimi.
Sasa kwa kuwa tunaoana nitajiweka wazi kwako mzimamzima na nina imani kubwa na wewe kwamba utaendelea kunipenda kama nilivyo.

Ndoa ni kuwekana wazi, ni kila mmoja kujidhihirisha kwa mwenzake kama alivyo pamoja na weaknesses zake.
Vitu vyote ambavyo vilikuwa vimejificha wakati wa uchumba hadi honeymoon basi kuanza kwa ndoa vyote huwa mezani juu kwa kila mmoja kuona.
Na hapo ndipo kwenye mtihani wa kwanza wa wanandoa wapya.
Honeymoon siyo residence ya kudumu ya ndoa, baada ya honeymoon (na wengine hata wakati wa honeymoon) wanandoa wapya hushikwa na mshangao wa partner anavyobadilika na kuwa kama mwingine kabisa.
Ukweli ni kwamba unapoona partner wako anaonekana kama mwingine tofauti na yule wa wakati wa uchumba, ukweli ni kwamba sasa matching inaanza, kufahamiana kikwelikweli kunaanza na wenye hekima na busara huwa makini katika kukabiliana na hizo tofauti na kuendelea kusherehekea hizo tofauti kwa upendo na kuvumiliana kwani huwezi kumbadilisha na kumbadilisha ni kupoteza muda wako.

LOVE MAY BE BLIND BUT MARRIAGE IS A REAL EYE-OPENER.

Wednesday, 15 June 2016

TOFAUTI HUWA HAZIKOSEKANI.


Wanandoa imara au waliofanikiwa katika ndoa yao ni wale ambao wanaweza kukaa pamoja na kujadili tofauti zao katika namna ambayo huwezesha kujenga ukaribu kimapenzi (intimacy) zaidi.

Wanafahamu jinsi ya kukubaliana na kutokukubaliana, wanafahamu namna ya kuhakikisha kutokukubaliana hakusababishi maafa kwenye maeneo mengine ya mahusiano yao.

Si kweli kwamba tunaolewa au kuona ili kuchukuliana katika migogoro hata hivyo kutofahamu namna ya kupambana na migogoro huweza kusababisha kutofanya vizuri katika mambo mengine ambayo ndo sababu za kuoana.

Kukwepa migogoro au kukwepa kuongea pamoja eti kunaweza sababisha mgogoro mzito si hekima wala busara kwani njia bora ni kuwa wazi kuongea pamoja ili kujadili tofauti au kutokuelewana kunakojitokeza ili wanandoa waweze kufahamiana zaidi.

Kwa lugha nyingine si rahisi mke kufahamu mume anapenda chakula gani bila kuongea kwanza, pia haina maana kukaa kimya kwa kuwa mke anapika chakula usichopenda basi atabadilisha na kukupikia chakula unapenda. Si rahisi mume kukupeleka outing kama hamuongei.

Wapo wanandoa ili kuepuka migogoro huacha kuongea na kuwa kimya, ni muhimu sana wanandoa kufahamu utafiti wa ndoa imara unasemaje.
Kila ndoa imara kwa wastani ina maeneo 10 ambayo wanandoa hawafanani au hawawezi kukubaliana au kwa lugha nyingine hawataweza kufikia muafaka maishani mwao.

Kwa nini hizi ndoa imara pamoja na tofauti 10 na bado zinaitwa ndoa imara?

Jambo la msingi au siri kubwa ni kwamba wanandoa wanafahamu namna ya kukabiliana na hizo tofauti na kuishi nazo, kupendana pamoja na kutofautiana na zaidi kila mmoja anamuelewa mwenzake na kukubaliana kihisia na kuchukua nafasi yake kama ni yeye.

Wanandoa imara hufurahia na kusherehekea tofauti zao na hufarijika kwa kuwa sasa anamfahamu mwenzake, anajua eneo ambalo wapo tofauti then wanaaendelea kupendana huku kila mmoja akifahamu namna ya kukabiliana na hizo tofauti.

Hawa wanandoa imara wanafahamu wazi kabisa kwamba hata kama watabadilisha partners bado watapata matatizo mapya katika maeneo ya kutokukubaliana, kuwa tofauti na kwa huzuni kubwa kazi kubwa itakuwa ni mizigo waliyotoka nayo kwenye ndoa zao za kwanza kama vile watoto nk ndiyo maana kwao talaka haina sauti wala nguvu na huwa haizungumzwi, ni neno lililofutwa katika maongezi.
Zaidi ya kukabiliana na tofauti na kutokukubaliana pia ni muhimu sana kusherehekea/kumbatia (embrace) mabadiliko.
Wakati tunaoana huwa tunaahidi kukaa pamoja hadi kifo kitakapo tutenganisha hata hivyo huwa hatuahidi kubaki vilevile bila mabadiliko yoyote, tunahitaji kukua, kuongezeka skills, kwa wabunifu na wazuri zaidi kila siku zinavyozidi kwenda.
Kuna mambo mengi tunaweza kujifunza kadri ziku zinavyozidi kwenda kama vile kusema asante, kuomba msamaha.
Hivyo inawezekana kujifunza tabia njema ambazo zinaweza kujenga ndoa na kuziacha tabia mbaya ambazo zinaweza kuharibu ndoa.

MTAZAMO WAKO UKOJE?


Huwezi kuongelewa mapenzi bila kutaja suala la pesa. Wapo watu ambao wanaamini kuwa na pesa nyingi, nyingi kabisa za kutosha husaidia pesa kuwa imara na linaloridhisha.
Hata hivyo tumeona penzi la uhakika hata wakati pesa zikiwa hazipo au tumeona penzi la kweli hata katikati ya umaskini uliokithiri.
Hii haina maana kwamba pesa siyo muhimu, pesa ni muhimu sana. Na pesa ina umuhimu kwa kila mahusiano hata, hivyo inabidi ujiulize mwenyewe je, upo kwa ajili ya pesa au kwa ajili ya penzi la kweli.
Utakuwa mtu wa maana sana kama utakuwa unatazama na kuwekeza kwenye penzi la kweli na si pesa.
Pia ni vizuri kuwa makini na mtazamo wa mpenzi wako je yupo kwako kwa ajili ya pesa au kwa ajili ya penzi la kweli.
Mtazamo wake kuhusu pesa ni muhimu sana.

Saturday, 11 June 2016

TABIA HIZI WAKATI MWINGINE ZINAKERA KTK NDOA.


Kuna wakati mwanandoa mmoja anajikuta yupo ndani ya ganda la yai kwa maana kwamba anajikuta anakabiliana na mke au mume ambaye anadhibiti, anayeamulisha, anapenda ufyate ulimi, anakukalia kooni, huna hiari yako na anakusimamia kila kitu.


Judy ni mmoja ya wanawake ambao wanatabia ya kufanya auditing hadi chumbani.

Kwanza mumewe huambiwa asahau tendo la ndoa siku za wiki (weekdays), labda Ijumaa usiku au Jumamosi usiku, pia watoto lazima wawe wamelala dakika 90 zilizopita na wawe kweli wamelala fofofo kwa kukaguliwa zaidi ya mara tatu na kuthibitisha kwamba kweli wamelala folilo kabla ya wao kuingia kwenye sita kwa sita.


Mume wake lazima ahakikishe ameoga kwa dakika 30, ahakikishe ametumia sabuni, kitamba (washcloth) na kupiga mswaki, akitumia dakika pungufu ya hizo lazima ataambiwa hajaoga akawa safi (amelipua) hivyo hawezi kupata unyumba (kama una hasira hapa nyumba haitoshi).

Pia mume anatakiwa ahakikishe anatandika taulo sehemu ambayo yeye Judy atalala wakati wa tendo la ndoa kitu kinachofanya eneo la kufanyia mapenzi kuwa dogo.


Anatakiwa kuhakikisha taa zimezimwa wakati wa tendo la ndoa na wanaenda kulala kabla ya saa nne usiku siku ya kupeana unyumba.

Pia kunatakiwa kusiwe na sauti ya binadamu au kitu chochote ndani ya mita 500 vinginevyo hakuna unyumba.

Ni kweli ni muhimu sana binadamu kuwa na taratibu lakini taratibu zingine badala ya kuwajenga wanandoa huwabomoa na kuwa vipande vipanda ambavyo kuvirudisha inakuwa ngumu maradufu.


Mume wa Judy itafika siku atasema “enough is enough”


Jeffy ni mwanaume ambaye kwake kila kitu ni utaratibu, akikwambia anapiga simu saa mbili kamili ni kweli atakupigia saa mbili kamili. Akikwambia atakuwa mahali fulani saa fulani, count him there. Jumamosi anakata majani kuzunguka nyumba yake na Jumapili jioni anaosha gari lake, kwa ufupi shughuli zake zinafanywa kwa mtindo wa saa.


Likija suala la tendo la ndoa na mke wake basi utaratibu wake ni kila baada ya siku tano, penda usipende mwanamke awe anataka au hataki period.

Kutokana na tabia za controlling wapo wanaume wamefanya wanawake kujisikia baridi kali mwilini kila mlango ukigongwa mume anapofika nyumbani kutoka kazini na kumfanya mwanamke kuwa turned off ile jioni na usiku mzima.


Hapa haijalishi umesoma au hujasoma, upo smart au ovyo, tajiri au maskini, kumbuka skills zinazokufanya ufanikiwe kazini kwako wakati mwingine ndo skills zinazofanya ushindwe masuala la chumbani kwako na mke wako au mume wako.

Tabia za kudhibiti na kutaka kila kitu kufanyika kwa umakini wa kupindukia (Control & Perfection) wakati mwingine huharibu mapenzi na ndoa badala ya kujenga.

ANA MTAZAMO GANI KUHUSU PESA?


Watu tunatofautiana katika mitazamo kuhusu fedha, baadhi huiangalia fedha kwa jicho la kutoa (giving) na wengine kwa jicho la kuitunza (saving) na wengine kutumia (spending)

Kama wewe ni kijana wa kiume au kike ambaye upo katika harakati za kusaka mwenzi wa maisha basi ni muhimu sana kuwa na makubaliano au kufahamu mtazamo wa huyo mtarajiwa kuhusu fedha.


Judy ni mwanamke ambaye mume wake Jeffy akipata mshahara huamuriwa akabidhiwe na anachofanya ni kugawa zile pesa na kuziweka kwenye bahasha tofauti tofauti, bahasha moja kwa ajili ya kununua chakula, bahasha nyingine usafiri, nyingine pango la nyumba, nyingine kununua nguo na nyingine sadaka kanisani na nyingine kwa ajili ya dharura.


Mume akitumia pesa kutoka moja ya bahasha lazima aeleze ni bahasha ipi alichukua pesa, na amefanyia kitu gani, na risiti ziko wapi na change zipo wapi na duka gani alienda kununua na alikuwa na nani na ametumia usafiri gani na amelipa kiasi gani.

Jeffy hujikuta oppressed, frustrated na hawezi kuvumilia tena!


Je, unadhani hiyo ndoa itadumu kwa muda gani?


Kumbuka wengine hutumia pesa kama emotional agenda, kama kwenye huo mfano bahasha za Judy si bahasha tu bali ni mfuko anaotumia ku-mcontrol Jeffy.

Kuna watu walitembelea ndoa moja na ilikuwa ni summer time na joto lilikuwa limepanda nyuzi 40 centigrade.

Ikafika mahali watu wakawa wana sweat utadhani wapo ndani ya sauna wakati huohuo nyumba ilikuwa na viyoyozi vya uhakika ila vimezimwa kwa utaratibu kwamba hadi ifike tarehe iliyowekwa ndipo huwashwa.

Wanandoa walipoulizwa kwa nini kuzima wakati joto linatuua, wakawajibu tarehe tuliyoweka kuwasha viyoyozi haijafika bado na kuwasha sasa ni matumizi mabaya ya pesa.

Hawa wanandoa wanafurahia ndoa yao kwa kuwa wanamtazamo sawa kuhusu fedha na hakuna kulemba!

Kuna wanawake ambao kwao fedha za mume ni za familia, na pesa zake ni zake.

Hii ilitokea kwa Suzy na Simon wakati fulani ambapo Suzy alikuwa anafanya kazi na Simon naye alikuwa anafanya kazi.

Simon akipata mshahara, Suzy humkomalia na kupanga bajeti namna ya kutumia hizo fedha kwani anachojua ni kwamba mshahara wa mume ni wa familia na mshahara wake ni kwa ajili yake tu.

Hata Simon alipotaka kununua kitu kutokana na ule mshahara basi Suzy huja juu kwa kuanza kutoa lecture kwa Simon namna watoto wanavyohitaji nguo na vifaa vingine wakati huohuo yeye Suzy pesa anayopata kazini kwake anaila kisirisiri.

Mitazamo kama hii huweza kuharibu ndoa kwa kasi ya ajabu kama dhoruba.

Angalia kwa makini yule unategemea kuwa mke au mume anazielewaje fedha kama unaona mtazamo wake ni wa ajabu ajabu ushauri wangu ni kwamba fikiria kwa makini kabla ya kuchukua uamuzi wa kuwa naye.

NI KUJIDANGANYA.


Kuna usemi mmoja wa kingereza unaosema:

“Someone is better than no one”

Kwa maana kwamba wapo watu ambao (hasa wanawake wale ambao wanaona muda unaenda bila kuwa na mchumba au mpenzi wa kuwa naye katika maisha) huamua kushikana na bora mwanaume kwa imani kwamba ni heri kuwa na huyo mmoja (unfaithful, untrustworthy) kuliko kutokuwa na mwanaume yeyote.


Subiri kidogo nikwambie!

Kujiingiza kwa mwanaume ambaye moyo wako hauko radhi eti kwa sababu unataka na wewe uonekane una mpenzi au una mchumba au una mume ni kuumiza hisia zako.

Hata kama unaamini utafanikisha matakwa yako bila kuunganishwa emotionally, intellectually au affectionally utaishia kuumizwa.


Pia huyo someone ambaye unaona ni afadhari kuliko kuwa mwenyewe ni looser ambaye anakuzuia wewe kumpata anayefaa, kwa lugha nyingine huwezi kumpata mwanaume mwenye sifa njema kama utaendelea kukaa au kushikamana na huyo someone wako ambaye hata hivyo ana sifa ovyo.

Wengi wanajuta kwa sababu ya kuamini kwamba "someone is better than no one, hata hivyo waliokiri kwamba "no one is better than a relationship that lack respect" wanapeta.