Monday, 10 August 2015

NI KUENDELEA KUJIFUNZA TU.

Tendo la ndoa au kufanya mapenzi (sex) kwa watu wawili wanaopendana (Ndoa) ni moja ya vitu vya asili duniani vinavyowapa wahusika raha ya ajabu ambayo bado lugha za kawaida tunazotumia binadamu hazitoshelezi kuelezea.
Ingawa ni kweli mwanamke na mwanaume wapo tofauti linapokuja suala la sex bado kujifunza na kuwa equipped kwa ajili ya sex ni muhimu.
Miili yetu ni complex machines ambazo zinahitaji kutumia Owners Manual kusoma mara kwa mara ili kuelewa na kuwa wazuri kuitumia.
Wakati wanaume hujisikia vizuri baada ya sex wanawake mara nyingi hupenda kujisikia vizuri ili wajishughulishe na sex.
Pia mwanaume akiwa amesisimka kimwili ndipo hujisikia kusisimka kisaikolojia mwanamke akisisimka kisaikolojia ndipo hujisikia kusisimka kimwili.
Sex yenye utamu wa kweli hutokana na kujiachia katika fahamu zetu na kutojiachia fahamu huweza kufanya blocking ambayo huweza kuiba hamu ya kufanya mapenzi.
Ni kweli kwamba ubongo wako ni most important sex organ na kwa ubongo tunaweza kuhusanisha mwili, nafsi na roho kuumba raha ya mapenzi ambayo haiwezi kusaulika katika maisha yote tunayoishi.
Hakuna binadamu anazaliwa anajua kila kitu, hivyo basi kujifunza ndiyo silaha ya kwanza kabisa ya kufahamu mwili wako na wa Yule umpendae una react vipi linapokuja suala la kufanya mapenzi.
Wala huhitaji kununua libido meter ili kuhakikisha kitanda chenu kinakuwa na moto mambo ya msingi ni kwamba:
Hakikisha kufanya mapenzi ni moja ya priority kati yako na mume/mke
Jifahamu mwenyewe kama vile unapenda kitu gani na wapi katika mwili wako
Mfahamu vizuri partner wako
Fahamu aina mbali mbali za style za kufanya mapenzi (sex position) hiyo hiyo kila siku inakuwa mazoea, muwe wabunifu.
Hakikisha mnapata suluhisho kwa matatizo kabla ya kwenda chumbani ( wakati mwingine jifunze kukubaliana kutokubaliana.
Hakuna kitu muhimu kama romance.
Afterplay ni muhimu kama foreplay- huwezi kumaliza mazungumzo bila kutoa hitimisho.
Hakikisha unaimarisha mawasiliano.
Pia kubali mabadiliko au kutafuta kitu kipya.

KWENU WANAWAKE.!

Kumfanya mume wako aridhike kimapenzi maana yake ni kufanya akuangukie kimapenzi zaidi.
Kufanya mapenzi kwa wanandoa ni njia nzuri ya kuwaunganisha kinafsi na kujipa raha na ukaribu.

Ukijifunza sanaa ya kumkaribisha na kuwa tender kwa mwenzako basi mnaweza kutengeneza bond ambayo ni strong na mume au mke atakufurahia siku zote za maisha yenu.
Kumfanya mwanaume awe na furaha kwa mke wake huonesha jinsi unavyompenda na pia inampa msukumo wa kuhakikisha anakuwa karibu na wewe kimahaba na kuwa na muda na wewe kama wapenzi.
Kuna vitu vingi ambavyo mwanamke huhitaji kufanya kwa mume wake hata hivyo kila mwanaume ana tofauti na mwingine na kila mwanaume ana ladha yake linapokuja suala la mapenzi au tendo la ndoa.

Hivyo ni jukumu la wewe mwanamke kujifunza na zaidi kufanya utafiti wa kutosha kujua mume wako anapenda kitu gani kwako na pia mwili wako upo sensitive wapi na zaidi jiografia yake.
usiniulize jiografia ya mume ni nini, sugua ubongo!

Kila mwanaume hupenda kuona mke wake akionekana sexy na nguo amevaa, inawezekana mpo wawili tu yeye na wewe, kwa nini usimtanie mzee na kinguo cha uhakika then pima libido meter yake itasoma vipi?
Kuna vinguo vya kuogea, kuna vinguo vya chumbani, kuna nguo za kuvaa ofisini au kazini nk kila nguo huvaliwa mahali pake.
Huwezi kuvaa nguo ya kazini chumbani!

Unajua kuchezesha sauti kuna raha yake kumfanya mwanaume joka litoke pangoni, siyo kila siku kulalamika tu, lawama tu, manung’uniko tu, acha hizo jaribu siku hata kama anakosea kila siku anza kumsifia hata kwa vitu vidogo tu, mpe asante, mkumbatie na kumpa romantic touch, uwe mbunifu.
Siamini kama kuna mwanaume ameoa mke ambaye siku zote ni kelele au kununa tu, au kulalamika tu au kuongea tu makosa na kusahihisha, kwa nini asikukwepe, hata kama anakosa siku zingine geuza udhaifu wake kuwa kitu kizuri au uwe na mtazamo positive.

Hata siku moja hujamchezea kifua au kidevu chake, mfanye ajisikie yeye ni mwanaume special.
Mwanamke anatakiwa kumlinda mumewe na maadui wote kiroho na kimwili lakini wakati mwingine mke hujisahau na kuzoea ndoa hadi mume ana fall in love kihisia na mwanamke mwingine (nyumba ndogo).

Hata hivyo inawezekana mume huwa haja fall In love na yule mwanamke bali ame-fall in love na hisia zile wewe humpi na akikutana na huyo mwanamke anajisikia raha na kupata kile love tank yake ndani ya moyo wake huhitaji hata kama mwanamke mwenyewe hampendi ila emotionally ameoza kwa huyo mwanamke na anajikuta anavutwa na yeye badala ya wewe kumvutia.

Saturday, 8 August 2015

HII PIA NI MUHIMU MNAPOKUWA "FARAGHA"

Ili kuwa mwanandoa mzuri kimapenzi unahitaji kufahamu kwanza tofauti zilizopo kati ya mwanamke na mwanaume.
Kile wewe unapenda kufanyiwa ukiwa chumbani na mwanandoa mwenzako wakati mwingine ni tofauti sana na yeye anapenda wewe umfanyie.
Wanaume siku zote tupo tayari kwa sex any time anywhere, ni kama wote ni ma-genius kwenye eneo la sex.
Bahati mbaya ni kwamba wanaume wengi akishaambiwa sasa ni wakati wa faragha; moja kwa moja full speed kwenye genitals za mke wake na baada ya dakika moja akishapima maji na kuona kuna umande haijalishi ni kiasi gani anaingia bila hata maandalizi ya kutosha eti kwa kuwa yeye umeme umeshawaka.
Je, kwa nini maandalizi ya tendo la ndoa ni muhimu sana kwa mwanamke?
Kuna logic ya kisayansi kwa nini mwanamke huchukua muda mrefu sana ili kusisimka kimapenzi ukilinganisha na mwenzake mwanaume.
Mwanaume ambaye akisisimka uume wake ambao ni kama tube yenye wastani wa inches 6 tu huweza kusimama (dinda) baada ya damu kujaa. Kwa mwanaume rijari au mwenye afya njema kawaida huchukua dakika 2 tu tangu amesisimka na kuweza kufika kileleni.
Kwa upande wa mwanamke eneo ambalo huhitaji kujaa damu ili asisimke ni kubwa zaidi kwani huchukua muda mrefu damu kujaa katika genitals na matiti au tuseme mwili mzima wa mwanamke ni one single sex organ hivyo huhitaji muda mrefu zaidi ili kusisimka.
Kama mwanamke ana mood nzuri ya sex au tuseme ubongo upo wired vizuri kwa sex basi humchukua kati ya dakika 10 hadi 15 kusisimka na kuwa tayari kwa sex.
Cha kushangaza ni kwamba tafiti nyingi zinaonesha kwamba wanandoa wengi huchukua dakika kati ya 10 hadi 15 kwa tendo zima la sex.
Hii ina maana mwanamke anapokuwa amesisimka mume huwa anakuwa alishamaliza na anakoroma na matokeo yake mke huachwa akiugulia kwa hamu ya kutaka zaidi na matokeo yake mwanamke hujikuta hajatosheka na hajafikishwa pale anahitaji kufika.

NDOA SI YA MAJARIBIO.

Kuna ushauri mmoja tu muhimu sana kwa yule anaetafuta mchumba ili awe mke au mume nao ni kwamba usikimbilie au kuingia haraka bila kuchunguza kwamba huyo unaetaka kuingia naye kwani ukiingia hakuna haraka ya kutoka kwani ni shimo ambalo kutoka ni hadi kifo.
Kama wewe ni binti au msichana au mwanamke ambaye unatamani kuolewa jambo la msingi ni kuhakikisha umejua tabia kabla ya kuamua kuoana naye.
Na kama wewe ni mvulana au mwanaume ambaye unatamani kuoa jambo la msingi ni kuhakikisha unajua fika tabia ya huyo binti au mwanamke unateaka kumuoa.
Kuna mambo muhimu sana ambayo binadamu hufanya uamuzi na uamuzi wake huweza kuathiri maisha yake hapa duniani na maisha yake baada ya kufa, moja ya jambo ilo ni ndoa.
Ndoa si safari ya majaribio kwamba nikiingia haraka haraka basi hata kutoka nitatoka haraka haraka, usijidanganye!
Adhabu ya kuingia kizembezembe kwenye ndoa ni kuvumilia maisha ya huzuni na maumivu maisha yako yote yaliyobaki duniani na huyo utakaye oana naye.
Kabla ya kuoa au kuolewa tumia muda wa kutosha kutafakari majaribu, matatizo, shida na magumu yote ambayo hutokea kwa wanandoa na kwamba una uhakika mwanaume au mwanamke unayetaka kuingia naye kwenye ndoa ana hizo sifa ya kusaidiana na wewe kuhakikisha ndoa inakuwa kitu cha Baraka kwako.
Jiulize mwenyewe kama mwanamke au binti je, nina uwezo wa kimwanamke, stamina na tabia ya kuweza kubeba majukumu ya ndoa kwa uangalifu maisha yako yote ya ndoa?
Na kama ni mvulana au mwanaume jiulize je, ninao uwezo na tabia ya kuweza kuwa baba wa watoto na kichwa cha nyumba au familia na kuwa mwanaume bora kwa mke wangu maisha yangu yote yaliyobaki duniani na mwanamke naenda kumuoa?
Unaweza kuingia harakaharaka kwenye ndoa kwa kuwa unatamani kuolewa; kumbuka ukiingia kwenye ndoa hakuna kutoka wala hakuna haraka ya kutoka ni hadi kifo kitakapowatenganisha.

NI MUHIMU SANA HII KWENU WANANDOA..

Kwanza lazima nikiri kwamba wanaume wengi hujikuta wanasisimka pale mke wake akiwa hali ya utupu.
Mungu alituumba sisi wanaume kuitikia kwa kusisimka kwa mwili wa mwanamke akiwa hivyo, na wakati mwingine tunasisimka hata kama sex halikuwa wazo kichwani mwetu yaani mwili huamua kufanya kile ambacho hatujautuma.
Hivyo wanawake wote mlio kwenye ndoa ni vizuri kufahamu kwamba ukiona dalili za kusisimka usifanye conclunsion kwamba lengo la mume wako kuwa hivyo ilikuwa ni kutaka sex.

Pia ni vizuri kama mume kufahamu kwamba wenzetu wanawake hawawezi kusisimka kwa kuona mwanaume upo mtupu kama sisi wanaume tunavyosisimka kuona wake zetu wapo uchi.
Ukweli ni kwamba ni muhimu sana na vizuri sana kwa wanandoa kujifunza kufurahishana (mume na mke) kwa njia ya kuwa uchi kwani ni raha kwa mwili na afya ya ubongo.

Kwa nini mke na mume kuwa uchi ni suala muhimu?

Kwanza kuwa uchi ni mke na mume tu, hivyo kuwa uchi hujenga aina ya bonding kwani hakuna mtu unaweza kuwa uchi isipokuwa mke na mume,vinginevyo utakuwa kichaa!
Pia kama lengo ni skin contact huleta raha; basi jinsi ngozi inavyozidi kuwa kubwa kugusana na raha huongezeka maradufu kama mke na mume watakuwa uchi.

Je ni nyakati zipi wanandoa huweza kuwa uchi na kila mmoja kumfurahia mwenzake?

Wakati wa kulala
Wakati wa kuoga
Wakati ambao si kuoga wala kulala bali wawili chumbani (kucheza, kupeana joto nk)

KULALA PAMOJA
Kulala pamoja kama mume na mke ni jambo ambalo lipo kwenye mind zetu na ni jambo muhimu sana.
Suala si kulala kitanda kimoja na kuamka pamoja tu bali kulala pamoja uchi na kuwa na maongezi, kukumbatiana na kujenga ukaribu zaidi.
Utafiti wa karibuni unaonesha kwamba kulala pamoja (uchi) husaidia wanandoa kupeana homoni za pheromones (ambazo hufanya kazi ya kuimarisha bond kati ya mke na mume) hivyo kuwa uchi ni kujipa exposure kubwa ya kupeana pheromones na matokeo yake ni kujisikia mpo closer na more secure kama mume na mke na pia hizi homoni husaidia kujisikia una afya njema kimwili na kiakili.
Kama unajisikia aibu au mwoga kuwa uchi kwa mke wako au mume wako basi kuna tatizo kubwa.

KUOGA PAMOJA
Je, Unakumbuka ni lini ulioga na mume wako au mke wako pamoja?
Je, umeshakumbatiwa wakati wa kuoga?
Umeshawahi kumuogesha mwenzako au wewe kuogeshwa?
Wakati mwingine ukiona mke wako au mume wako anaenda kuoga mpe surprise kwa wewe kuomba muwe wote kwani kuna raha yake.

WAKATI AMBAO SI KUOGA WALA SI KULALA
Hii inaweza kuwa ni wakati kabla ya kulala usiku au asubuhi wakati unataka kuamka au kuondoka kitandani, unaweza kumkumbatia mume au mke kwa dakika kadhaa bila kuongea maneno yoyote, muhimu ni mwili kuwa na mawasiliano na kuwa one flesh.

Wanawake wengi huogopa sana hii kwa kuhofia kwamba hii inaweza kuwa janja ya mwanaume kutaka sex usiku kabla ya kulala au asubuhi kabla ya kuamka na wanaume huogopa sana hii kwa kuhofia kwamba mwanamke anaweza akagoma sex baada ya mwanaume kujikuta amesisimka na anahitaji sex.

Suala ambalo husumbua kwa mwanamke na mwanaume ni kwamba mke na mume wakiwa uchi akili ya mwanaume hufikiria sex na akili ya mwanamke hufikiria romance/intimacy na kila mmoja akiona haja yake haijatimizwa hujiona hajaridhika.

Jambo la msingi kwa mwanaume ni kukumbuka kwamba mke wako huhitaji kuguswa mwili wake mara kwa mara na si lazima iwe sex na hii hupelekea yeye kuwa na afya njema katika mwili na emotions zake na kukosa kupokea mguso wa kimwili husababisha asiwe na hamu ya sex.
Mwanamke kukosa ukaribu wa kimapenzi huathiri utendaji wa ubongo wake.

Pia jambo la msingi kwa mwanamke ni kukumbuka kwamba mume wako ana hamu kubwa sana ya sex na ingawa anaweza kuzuia kile angefanya hiyo haiwezi kumsaidia kuzuia anavyojisikia. Anapokuwa amepitiliza muda mrefu bila kutoa nguvu zake kupitia sex, ubongo wake huathirika pia kama wewe mwanamke unapokosa physical touch na ukaribu kutoka kwa mume wako. Hisia zake za kutaka sex si ubinafsi bali ni response ya ubongo wake kutokana na kitendo cha kukosa sex.

Jambo la kukumbuka kwa wote ni kwamba ni muhimu sana kila mmoja kujitoa kwa mwenzake na kumfahamu vizuri mwenzi wako na weka lengo kuhakikisha unatimiza mahitaji yake hata wewe usipotimiziwa mahitaji yako.
Wewe kutokuwa selffish ni baraka kwa mumeo au mkeo na wewe kutimiza mahitaji yake kutafanya na yeye atimize mahitaji yako.

Tukumbuke kwamba kuwa comfortable kuwa uchi kwa mume wako au mke wako ni faida kwako ndani na nje ya kuta za chumba chenu cha kulala.


Friday, 7 August 2015

LUGHA MUHIMU KWENYE NDOA.

Ndoa ni kama Kambai nayounganisha (kuwafunga) wawili kuwa mmoja. Kamba ya ndoa imetengenezwa kwa kuunganisha nyuzinyuzi za upendo wa ahadi nne yaani mawasiliano, kujitoa, kumwelewa mwenzako na kumsamehe.

Wakati mwenzi wako anajisikia kuridhishwa kimapenzi hujiona salama kihisia na hujiona ulimwengu unampa vyote na atajitoa zaidi kuhakikisha anajitoa katika kiwango cha juu kwao kuimarisha upendo na mahusiano.

Na anapojisikia kutoridhishwa kabisa kimapenzi, hujisikia ni kama vile anatumika au unamtumia tu kufanikisha hitaji lako la mapenzi bila kupendwa na kwake ulimwengu unageuka kuwa mahali hatari kwake na husababisha hata vitu vingine ulivyompa kama nyumba, gari, fedha nk kuwa havina maana katika uhalisia wa maisha.

Mapenzi yana lugha kama zilivyo lugha za mawasiliano, utamu wa lugha ni pale unapoifahamu kuisikia na kuiongea, pia utamu wa mapenzi katika ndoa ni pale unapofahamu lugha ya mapenzi kusikia na kuongea.

Raha ya Kiswahili ni pale unapoongea Kiswahili na mswahili mwenzako, na kuongea vile vimaneno vitamu vinavyofanya ufurahi na kucheka na kujiona kweli Kiswahili kitamu. Je inakuwaje unapoongea Kiswahili na mtu anayeongea kihindi?

Kuna watalamu na washauri ya mambo ya ndoa na mapenzi wameandika sababu nyingi sana zinazoelezea lugha halisi za mapenzi, wengine wanasema zipo 5, wengine 10, wengine 50, wengine 100 Mimi naona zipo sita ila moja (ile ya sita) ni muhimu kwa wote na ni msingi halisi wa ndoa na ni asili yake na kuizembea hiyo naamini inaharibu mtiririko wa lugha zote za hisia za mapenzi. Kuzijua hizi lugha sita na kufahamu ni zipi (ipi) mke wako au mume wako yupo basi ndoa inakuwa tamu kwelikweli, utamu halisi usio na hila, na utakiri kwamba kweli ndoa ni tamu.

Lugha za msingi za kuelewana katika ndoa kwa hisia za mapenzi ni kama ifuatavyo:-
1. Kuwa na muda na mwenzi wako
2. Kupeana zawadi
3. Kusaidia kazi/huduma
4. kumpa maneno ya kumsifia, kushukuru na kumtia moyo kwa kile anafanya
5. Mguso wa kimwili (wale wa mabusu na ma-hug kazi kwenu)
6. Mungu. Muhimu kuliko zote

Leo tutaongelea namba Moja

1. KUWA NA MUDA NA MWENZI WAKO.
Msingi wa kuwa na muda na mwenzi wako ni upamoja pamoja na kuwa kimawazo, kimwili na kiakili.

Kuwa na muda na mwenzi wako hatumaanishi kukaa pamoja kwenye sofa au makochi kuangalia TV; au movie hapo mnaipa time au muda wa pamoja TV au movie mnayoitazama siyo mwenzi wako.
Kuwa na muda na mwenzi wako ni kukaa pamoja na kumpa attention yote, anaongea na wewe unamsikiliza tena ninyi wawili tu, kutembea pamoja yaani mmeamua kwenda kutembea kwa ajili ya kwenda kutembea wewe na yeye tu si kwa sababu mnaenda kanisani au mnaenda kazini, kupeana muda wa pamoja ni kama vile kwenda kula pamoja (outing) ninyi wawili na mkifika hapo kwenye hoteli mnaongea kwa kuangaliana ninyi romantically.

Ukienda kwenye hoteli au sehemu yoyote watu wanaenda unaweza kula chakula au huduma zingine (outing) utajua tu wapenzi walio kwenye ndoa na wale ambao bado wachumba au dating couples, Guess what? Wachumba utakuta wanaongea kwa kuangaliana tena kwa karibu na vikolombwezo kibao na wanatamani wabaki hapo, tuje walio kwenye ndoa wanakula na kunywa kila mtu anaangalia kwake, wanaangalia kuta na watu na unajua wameenda kula na si kuwa na muda pamoja, halafu wana haraka sana, kidogo tu waaondoka kama vile wamelazimishwa kwenda outing.
Tuwe romantic jamani, tutaendelea kujadili zaidi huko mbele safari ya somo letu.

Ni kweli kila mtu anahitaji muda na mwenzi wake, lakini maajabu ni kwamba si kila mwanandoa ukimpa muda au kuwa naye kwake ndo anajisikia na kujiona unampenda kwani kwake kuwa na muda naye hakumgusi kama ukiwa unamletea zawadi, au unapo mpa maneno ya kumsifu kwa kitu amefanya, au kumshukuru na kumpa affirmation kwa kila anachofanya.

Kitu cha msingi ni wewe kuchunguza je mpenzi wangu anajisikiaje kwa kila mambo 5 ni lipi linamgusa sana na kujiona kwake ndo la msingi kuliko yote. Kama ni Kumpa muda ndo anajisia unampenda basi fanya makeke your baby ajipe raha.

Mbona tunapo date tunakuwa na muda pamoja huko tumepanga kukutana? Kwa nini baada ya kuoana watupeani time hata kama tunalala pamoja issue hapa ni kumpa muda ambayo katika masaa 24 hata kama ni dakika 20 tu mpe mpenzi wako na kama lugha yake ya mapenzi ni kuwa na muda na wewe basi utampatia sana na kama hufanyi ndo yale yale unampa zawadi ya gharama lakini bado anasema humpendi na love tank inazidi kuwa empty Hebu jaribu kufanya kweli uone kama mwenzi wako hajakwambia baba Fulani au mama Fulani siku hizi unanipenda sana, yaani umebadilika, acha kusema upo busy, gharama ya kusuruhisha ndoa unayoenda ICU ni mbaya sana kuliko huo ubusy.

Fanya yafuatayo katika suala zima la kumpa mwenzi wako muda wa pamoja hasa kama kwake kumpa muda ndo anajisikia unampenda
(a) Mwangalie usoni wakati anaongea atajua unamsikiliza
(b) Usimsikilize huku unafanya kazi nyingine, kama huwezi muombe akupe muda kidogo then utamsikiliza anachosema kuliko kuendelea kufanya kile unafanya huku unamsikiliza, utamuumiza sana
(c) Onyesha hisia kwa kile anakwambia, kama unahisia amekatishwa tamaa mwambia ukweli kwamba nahisi unajisikia umeumizwa au kukata tamaa, basi nitafanya hivi na hivi, changia kupata solution
(d) Hakikisha unajua anaongelea nini na anajisikiaje (body language)
(e) Usimkatishe anapoongea, sikiliza maana wengi huwa tunadhani tunajua hata alichokuwa anataka kusema hata kabla hajasema, eti nilikuwa najua utasema hicho tu

UMUHIMU WA MAWASILIANO KTK NDOA.

Mawasiliano katika Ndoa ni kama barabara ya njia mbili inayoruhusu magari kuingia na kutoka; yaani wanandoa wawili ambao mmoja akiongea mwingine anasikiliza na mwisho wanapata jibu la kudumu la tatizo lililokuwepo.
Mawasiliano mabovu husababisha kutokuelewana ktk ndoa na mahusiano ya aina yoyote.

Ni kitu cha kawaida kwa sasa kuona mabishano ambayo yanaanza asubuhi jua linaochomoza na kuendelea hadi jua linapozama jioni bila ufumbuzi.


Mabishano kama hayo yasiyo na ufumbuzi ni kama Bomu linalosubiri muda ili lilipuke.


Baadhi ya wanandoa hudhani kwamba kuacha tatizo bila kulizungumzia ni kutatua, hiyo si kweli na hali kama hiyo haileti afya ya ndoa bali ugonjwa na matokeo yake ndoto ambazo mtu alikuwa nayo kuhusu ndoa huyeyuka kama barafu lililokutana na jua la mchana.

Kanuni muhimu katika kuhakikisha ndoa inakuwa imara ni pamoja na kila muhusika kujitoa na kuelekeza jitihada za kuhakikisha kila siku anawekeza ili ndoa kustawi.

jambo la msingi ni kuwekeza katika mawasiliano bora

Mawasilinao katika ndoa au mahusiano yoyote ni kama gundi inayounganisha ndoa.


Na ikitokea hiyo gundi ikaacha kufanya kazi basi mahusiano au ndoa huanza kukatika vipande vipande, na ndoa bila kuwasiliano lazima itakufa.

Katika jamii nyingi za kiafrika watu hawapo wazi sana kujieleza kile anahitaji kutoka kwa mwenzake

Sema kile unataka bila kuzunguka.

Kama hujaridhika na style za sex za mpenzi wako sema ili ajue unataka kitu kipya, kama hujaridhika na chakula anachopika sema ili msaidiane na kuona inakuwaje, watoto, huduma kanisani maana wengine ni kanisani tu na mambo ya nyumba hana mpango, ndugu, kama hujaridhika na jinsi anavyotumia pesa sema ili ajue.

Kubaki kimya na kudhani atajua mwenyewe hata kama utahuzunika hatakuelewa eleza wazi ili kujenga ndoa yako.

hakuna njia nyingine zaidi ya ninyi wawili kuelewana na kukaa pamoja kupata jibu.

Kama unahitaji kitu Fulani kutoka kwa mwenzi wako sema nahitaji kitu Fulani, na kama kuna kitu Fulani anafanya wewe unaona kinakuletea shida mwambie kwa upole na moyo wa upendo na pia mwambie kwa nini unaona kinakuumiza kubaki kimya ni kama bomu ambalo linasubili muda na muda ukifika litalipuka.


Kama unahitaji muda wa kujibakia mwenyewe tu kufikiria mambo fulani fulani sema ili mwenzako ajue ila si kuwa mkali na kufukuza watu bila kusema kulikoni;

kuna wakati binadamu huhitaji awe yeye mwenyewe na Mungu wake, muhimu mawasiliano.


Huishi na malaika kwamba atajua kila kitu ambacho wewe unapenda au hupendi

Ndoa ni kujengana kila iitwapo leo


Na kama mwenzi wako anakasirika kwa kile umemwambia inawezekana hajakulewa so unahitaji kurudia kumwelekeza vizuri hadi aelewe kwa upendo na hekima.

Jinsi tunavyowasiliana tunatiofautiana kijinsia na kimalezi na ni muhimu sana kuwa makini kusoma lugha ya mawasiliano ya mpenzi wako.


Wanaume mawasiliano yetu ni ya moja kwa moja na wanawake mawasilino yao yanabebwa na hisia na wao ndo wanaoumizwa sana

Pia si busara kuongea na mpenzi wako kwa hasira kwani hasira wakati mwingine husababisha

Kulia machozi,

Kupiga au kupigana,

Kutupa vitu hata kama ni vya thamani kama simu za mikononi, vyombo nk,

na wengine hubaki mabubu na kushindwa kuongea.


Ndoa zote imara zina kitu kimoja kinachofanana nacho ni

Mawasiliano mazuri.

Na bila kupinga ndoa zenye matatizo nyingi matatizo huanzia kwenye

Mawasiliano mabaya.

Mawasiliano ni pamoja na

Kuwepo wakati wa maongezi,

Kumsikiliza mwenzi wako anapoongea,

na kusema kila unachohitaji kwa mwenzako.


Msingi Hasa wa Mawasiliano Katika Mahusiano Yoyote ni Katika Mambo Makuu Matatu

(a) Uwepo katika maongezi kwa mpenzi wako, upatikanaji wako pale mwenzi wako anataka kuongea kitu.

Wote mnahitajika kuwepo katika maongezi tena kwa kuhusika vizuri kwa lile linalozungumzwa.

Pia wewe unayetaka kuongea hakikisha mwenzi wako yupo tayari kukusikiliza siyo kulazimisha akusikilize wakati unajua anafanya kitu kingine muhimu tafuta muda muafaka.


(b) Msikilize kwa makini mwenzi wako na kama huna muda wa kusikiliza mwambie ni wakati gani utakuwa tayari na utasikiliza kwa makini kuliko kusikiliza huku unafanya kitu kingine.


(c) Husika katika mazungumzo au maongezi, hakikisha mwenzi wako anapata hisia kwamba unasikiliza na unajali pia unachangia kile anaongea na ongea kwa upendo, ukaribu kwani anayeongea ni mtu muhimu sana kwako hapa duniani.

Pia uwe wazi kueleza hisia zako na mawazo yako halisi kuhusiana na lile mnaongea


Mambo ya kufanya na kutokufanya wakati mnawasiliana
Lenga katika kutatua tatizo siyo kushinda mjadala au mabishano

Hakikisha unamsikiliza mwenzi wako vizuri na unaelewa ana maanisha kitu gani

kwani wanaume wengi hata kabla mke hajamaliza kuongea tayari tunadakia “nilikuwa najua unataka kusema hivyo”

Jieleze vizuri kama hujaelewa kuliko kujidai umeelewa then ukafanye sivyo

Heshimu mawazo ya mwenzako hata kama huwezi kupata jibu sasa kwa tatizo alilokwambia; kuliko kutoa majibu ambayo huishia kumkatisha tamaa mwenzako

Tumia muda mwingi kufanya maongezi kujadilia mambo unayodhani ni ya msingi kuliko kutumia muda mwingi kuongea kile ambacho si muhimu na kuacha kile ambacho ni muhimu

Kuwa mwepesi kusamehe na mwepesi kusahau pia, hakuna nafasi ya kitu kinaitwa "Nimekusamehe ila sitasahau."

Uwe mwangalifu lugha yako au maneno yako na body language kwani unaweza kuwa unaongea kitu kingine na mwonekano wako ni kitu kingine;

Ongea kile unamaanisha; wengi hupenda kulalamika badala ya kuongea kile anataka.

Usiende kulala kabla ya kutatua tatizo, Usilale na gubu au donge moyoni hakikisha umeliyeyusha kabla hujalala.

Usiongee na mpenzi wako kijeuri au kihuni au bila heshimu au kibabe hasa wanaume.

Usimlaumu mwenzi wako mbele za watu.

Unapotoa maamuzi yoyote usitoe kwa hasira

Usianze mjadala kwa kukumbushia mambo yaliyopita zamani hasa wanawake


Usidhani mwenzi wako anakuumiza kwa sababu hakubaliani na wewe inawezekana yupo sahihi hivyo mpe muda.