Friday, 29 April 2016

NINI MWANAUME ANAHITAJI KUTOKA KWAKO MWANAMKE?


Ndoa ni tamko takatifu ambalo mamilioni ya watu tumeji-commit wenyewe kwa hiari.
Hii ina maana kwamba umepata mtu wa kuishi na wewe katika raha na shida zote hadi kifo.
Unakuwa imeingia katika kifungo cha Kupendana, kuheshimiana na urafiki, hata hivyo jinsi miaka inavyoenda unaweza kujikuta unapoteza umuhimu wa huu uhusiano na mbaya zaidi unaweza kujikutana unajisahau nini unahitaji kutoka kwa mwenzako.
Kuna mambo ya msingi ambayo mwanaume yeyote huhitaji kupata kutoka kwa mke wake mpenzi na kinachotakiwa kwa mwanamke ni yeye kufahamu nini mwanaume anahitaji na kuwekeza kidogokidogo kwa kuongeza jitihada na muda ili haya mahitaji kuwa kitu halisi.

Je ni Vitu gani mwanaume huhitaji sana kutoka kwa mke wake?

1.WANAUME HUPENDA KILE KILICHOKO AKILINI MWA MWANAMKE.

Wanawake ni viumbe tofauti sana (complex) wao ni walezi kwa asili, waumbaji wa vitu, wasimamizi wazuri na wabunifu sana.
Wanaweza kwa urahisi sana kuelezea kitu kilichopo kwenye akili zao likija suala la deal lolote la biashara kama kununua au kuuza.
Wanaweza sana kwenye mambo ya design na hata mawasiliano.
Ila likija suala mwanaume hapo ndiyo kuna tofauti.
Wanaume kawaida tunapenda kujua kwamba tumetimiza mahitaji ya wake zetu na itakuwa vizuri sana kama mwanamke atawezesha mwanaume kujua kwamba mahitaji yake kama mwanamke mume anayatimiza.
Kwa hiyo mwanamke ongea nini unahitaji, au nini unapenda kwa maneno au kwa matendo kwani kununa si jawabu au kubaki kimya si jawabu.
Jawabu ni kuelezana tena kwa upole na upendo jambo lolote unahitaji mwanaume afanye.

2.WANAUME UHITAJI MWANAMKE ANAEJUA KUKUBALIANA/KUAFIKIANA.

Je kama mume wako anapenda kuangalia au kucheza soccer siku za weekend kwa ajili ya kujiliwaza huwezi kuwa naye?
Kuna ubaya gani wewe kushangalia kile mume wako anapenda (hobbies)
Kumbuka maisha ndivyo yalivyo msipofurahi pamoja na kuwa na fun pamoja usitegemee siku mambo yabadilike yenyewe tu kuna kitu unahitaji kufanya sasa ili kesho iwezekane.
Penda kufanya pamoja kile kitu mume wako anakipenda katika maisha inaweza kuwa ni kuimba, jogging, kwenda kutembea sehemu yoyote ili pamoja au matamasha na michezo mbalimbali.
Kumbuka unaweza kuwa wewe hupendi kwenda naye huko yeye anapenda kwenda, lakini kuna wanawake wanafurahi kuwa naye huko wewe umekataa kwenda na hana njia kwani ni kitu anakipenda na ni sehemu ya maisha yake (kama hatendi dhambi).

3.WANAUME UHITAJI MWANAMKE ANAEJUA MAMBO.

Huwezi kutenganisha habari za siasa, michezo, biashara, current news, sayansi na mambo ya kimataifa na mwanaume, hivyo usijiweke nyuma sana unahitaji kuwa mtu wa karibu kupiga naye story za mambo kama hayo, jitahidi na wewe kuwa wamo.
Inawezekana jioni kabla ya kulala mkawa na glass ya juice mnakunywa wawili huku watoto wamelala, wewe mwanamke kwa ujasiri shusha story za michezo mambo ya Chelsea, Manchester united, Liverpool au hata Yanga na Simba just for fun, au hata habari za mafisadi au hata habari za mfalme Suleiman au Daudi au business ambazo umezitafiti hapo mwanaume atajua nina mke ndani ya nyumba.
Wapo wanawake mume akianza kuongea habari za siasa, michezo au business anaondoka zake na kumwacha naamini wanaume hapo huwa hawafurahii kabisa.
Nakwambia ukijua kuongea na mumeo mambo ambayo wanaume wote wanayapenda utafahamu mambo mengi sana kuhusu ulimwengu, watu na ninyi wenyewe.
Pia unaweza kubadilisha akili katika kufahamu mambo.
Hii huimarisha sana ukaribu na hamasa ya kila mmoja kutaka kusikia kwa mwenzake na matokeo yake ndoa inakuwa tamu maana huo usiku mkimaliza story lazima chumbani kuwake moto.

4.MWANAUME ANAHITAJI MWANAMKE AMBAE KWA MAPENZI NI MOTO.

Huwa kuna kawaida kwamba mwanaume katika jamii zetu za kiafrika ndiyo anakuwa mwamuzi wa mambo mengi kiasi kwamba hata wanawake wenyewe hutambiana kwamba jana mume wangu alinipeleka dinner sehemu.
Je, itakuwaje kama na wewe mwanamke siku ukamwambia mume wako leo pamoja na watoto tunaenda lunch sehemu au dinner sehemu kula, au kula kitimoto na nk pamoja na watoto wenu kwa hela yako au bajeti yako au maamuzi yako.
Wakati huo huo umetinga kiwalo chako cha nguvu (sexy) hadi unamkumbushia zile ezni zenu ambazo zilifanya avutiwe na wewe hadi kukuoa.
Wanaume wanahitaji wanawake wa aina hiyo ambao siku zingine wanafanya vitu romantic au sexy angalau hata kwa mwaka mara moja siyo mwaka mzima hujafanya jambo lolote la kuimarisha mapenzi.
Wanaume wanahitaji mwenzi siyo mtu wa kuishi naye chumba kimoja
Kuagana asubuhi na kuja kukutana jioni bila kuongea chochote mchana mzima ni dalili ya uhusiano usio na afya kabisa.
Jaribu kufikiri mwenyewe hivi ukiondoka asubuhi unawasiliana na mumeo mara ngapi?
Siku hizi karibu kila mtu ana simu ya mkononi, unaweza kutuma sms, au kumpigia just to say hi honey! Mbona wakati wachumba sms zilikuwa zinatumwa hadi vidole vikaota sugu, leo kunani?
Hamu na msukumo alionao mmoja kwa mwenzake ni msingi wa kuonesha afya na mahusuano yenye furaha.
Wakati mwingine mahusiano huenda bila mawasiliana ya mara kwa mara lakini hiyo ni sumu kubwa sana kwani inaweza kufikia kipindi hakuna hata kutakana, hamu ya kila mtu kwa mwenzake hupotea na hapo ndipo watu sasa huanza kuishi kama vile watu tofauti walioamu kuishi nyumba moja na chumba kimoja lakini ule moto umetoweka.
Kwa hiyo kama wewe ni mwanamke hakikisha unakuwepo katika mahusiano kwa maana kwamba unahitaji kumtia moyo mumeo, kumuinua pale anapokata tamaa uliza nini kinaendelea asubuhi, mchana, jioni na usiku, pia akifanya kitu kizuri mpe sifa na hongera.
Jifunze kwa busara na hekima kujua nini kinaendelea katika maisha ya mume wako na pia onesha kwamba unamjali sana (care) na kwa njia hiyo automatically atakupenda zaidi na ndoa yenu itakuwa imara zadi.

5.MWANAUME ANAHITAJI MWANAMKE HURU.

Ni kweli kila mmoja anamuhitaji mwenzake ili maisha yakamilike lakini kuna wakati mwanaume anahitaji kuona ana mke ambaye anaweza kuendesha mambo mwenyewe bila kushikwa mkono kwa kila kitu.
Pia wewe mwanamke usije mwambia mume wako sikuhitaji kwa sababu naweza kufanya mambo yote mwenywe hapo litakuwa zogo la ajabu.
Hapa nazungumzia ule uwezo wa mwanamke kuweza kuendesha mambo au familia hata kama mume hayupo. Tunajua sana wanawake mnaweza mambo mengi hata kuliko sisi wanaume ila kuna wanawake ambao bila mwanaume hawezi kufanya jambo lolote kiasi ambacho mume naye akajisikia kweli nina mke anayeweza.
Pia mwanamke hahitaji kuwa mtu wa kulaumu kila kitu, mtu wa kulalamika kila kitu, leo ukilalamika hiki kesho unaanza kingine na wakati mwingine unasingizia kwamba unaumwa wakati huumwi lengo kuuchanganya mwanume, hapo ujue unaipeleka ndoa yake eneo hatari wanaume hawaipendi hiyo, wanapenda mwanamke asiye na malalamiko au lawama au msumbufu.

6.MWANAUME ANAHITAJI MWANAMKE ANAYEAMINIKA.

Bila kuaminiana, lazi kutuhumiana kunafuata na bila kuaminiana mahusiano hayawezi kuwa imara.
Mwanaume anahitaji mwanamke anayemwamini hasa pale anapokuwa hayupo.
Mwanaume anahitaji mwanamke mwaminifu huko kazini, mwanamke mwaminifu sokoni anakoenda, mwanamke mwaminifu mahali popote akiwa peke yake.
Kuwa mkweli ndiyo njia nzuri ya kujenga uaminifu, kiwe kitu kidogo au kikubwa ni muhimu kuwa mkweli na mwaminifu kwa mume wako.
Kumbuka ukidanganya kitu kimoja unahitaji kudanganya mara kumi na tano zaidi ili kufunika huo wongo kuwa ukweli hata hivyo ipo siku mambo yatagoma na mambo yakigoma utakuwa umepoteza uaminifu, na ukipoteza uaminifu ni kama kuyeyuka kwa barafu huwezi kurudisha.
Wakati mwingine kuwa mkweli na mwaminifu huonekana ngumu lakini ndiyo dawa halisi ya kuimarisha mahusiano ya ndoa yako, hata kama umenunua kitu kwa gharama sana huko dukani au sokoni mwambie ukweli bei halisi usiseme bei tofauti na ile umenunulia.
Kitu cha msingi, jaribu kufikiria kile unafanya je na wewe ungefanyiwa ungekubali? Au ungeridhilka?
Kazi kwako.

7.MWANAUME ANAHITAJI KUONA UNAVYOFANYA KTK MALEZI.

Wakati mwanamke anapochukua jukumu la kuwa mlezi katika familia mwanaume hujisikia raha sana.
Kile kitendo cha kuwasaidia watoto kama vile kufanya nao homework walizopewa shuleni, au kucheza pamoja kama vile soccer na mtoto wa miaka 4 au 5, mwanaume hujisikia raha sana kwa namna ambayo mwanamke anajibidiha kulea kile ambacho kwa pamoja mmekileta duniani.
Kama una watoto au bado kitu cha msingi lazima ujue kwamba mwanaume hujisikia vizuri sana pale unapohusika bega kwa bega kusimamia malezi ya hawa viumbe ambao mmepewa zawadi hapa duniani.
Kwa jamii zetu za kiafrika hili halina shida sana ingawa kwa huku Marekani na Canada ni kitu cha kawaida mwanaume kuachiwa kazi zote za malezi ya watoto na mwanamke akawa anakuangalia tu.

8.MWANAUME ANAHITAJI UWE RAFIKI YAKE MKUU DUNIANI.

Kama umewakuta mume na mke wakitembea wameshikana mikono naamini huwa unapata ujumbe kwamba na wewe unapenda kuwa na mume wa uhusiano wa aina hii.
(Sizungumzii wale wanafiki ambao chumbani wanazipiga na barabarani wameshikana mikono)
Binadamu ameumbwa kuwa muhitaji kwa kupendwa, muhitaji wa kuwa na rafiki kuwa na mwezi (companion) kuondoa upweke
(duniani wawili wawili mume na mke)
Mnahitaji kuwa mke na mume, lakini mnahitaji pia kuwa marafiki wakubwa siku zote.
Tunatumia muda mwingi sana kuwa na mke au mume hivyo ili kunogesha zaidi inabidi kuwa marafiki na kupeana story, michapo, kuchezezeana, kutaniana, kutembea sehemu pamoja, kucheka pamoja, kucheza michezo tunapenda pamoja, kujaribu vitu vipya pamoja.
Pia ni muhimu kuwa na marafiki wengine ila urafiki lazima uanze na ninyi wawili.

9.MWANAUME ANAHITAJI MWANAMKE MALAIKA WAKIWA SEBULENI NA MWANAMKE MTUNDU WAKIWA CHUMBANI.

Wanaume wanahitaji hot sex, tendo la ndoa ambalo linaleta msisimko, linalofurahisha na kutia hamasa mpya kila siku.
Jaribu vitu vipya, mikao, miguso, busu, na michezo ya kitandani au chochote umejifunza, acha woga kwamba atakuuliza nani kakufundisha, dunia ya leo tunaishi dunia ambayo wanaaiita information society, hivyo watu tunapashana habari na kufundishana kupitia magazeti, radio, TV, movie, internet nk.
Usiache kufanya kitu kipya huko chumbani eti kuogopa atakuuliza umejifunza wapi.
Kazi kubwa kwako ni kuhakikisha kitanda kinakuwa moto siku zote na pia kumpa vitu vya uhakika ili asitembeze macho nje kutokana na kuwa bored na mapishi ya aina hiyohiyo miaka nenda tudi.
Ni kweli kama umri umekwenda sana hamwezi kufanya kama ile miaka ya nyuma lakini isiwe sababu ya kutokuwa na sex yenye kuridhisha na mwanamke kuwa moto kitandani.
Miili yetu ni hekalu la Mungu la ajabu na la aina yake hapa duniani.
Mwili ni laini, una harufu nzuri, ukiguswa unapata raha ya ajabu, hivyo kama mwanamke unahitaji kujiweka safi na sexy muda wote bila kujali umri.
Kitu cha msingi ni kwamba mume wako anakuhitaji wewe, anahitaji ladha mpya na utamu kila siku kutoka kwako iwe ni kukugusa kwa mikono yake, au kukuangalia kwa macho yake au kukunusua mwili wako kwa pua yake au kukusikia unaongea maneno matamu kwa masikio yake na kukuonja mwili wako kwa ulimi wake.
Ni kweli anakuhitaji wewe na si mwingine na kwa kuwa anakuhitaji wewe basi
Mpe raha
Keep it hot,
steam it up
and you both will come back wanting more time and time again.
Mwisho
Kuna mambo ya msingi ambayo mwanaume anahitaji kwako na kuna kitu anataka kwako, kuna mambo mengi sana mwanaume anahitaji kwako kitu cha msingi timiza hizi ndoto kwa kuzifanyia kazi.
Kama utakuwa ni mtu unayekuwa mbunifu na mwenye kufanya mambo tofauti bila mazoea basi uhusiano wako na umpendaye utakuwa imara na mzuri kila iitwapo leo.

No comments:

Post a Comment