Saturday, 30 April 2016

MAHABA HAYA..!


Kwa mwanaume hakuna kitu kinakuwa sexy kama mwanamke ambaye anakuwa loud kitandani na si kuwa na vikelele tu bali kujihusisha moja kwa moja kwa mwanamke katika kuongea maneno matamu
(wengine huita dirty words hata hivyo hakuna dirty words hapa isipokuwa sweet words)

Mwanaume akiwa kwenye game anapenda sana kujua mke wake anajisikia vizuri kwa kile anafanya na kwamba mwanamke anaonesha total participation, pia vile mke unatamka jina la mume wako kwa manung'uniko ya kimahaba huleta raha sana pamoja na vikelele vingine kama vile ooooh! aaah! mmmh! nk humpa uwezo zaidi mume kuendelea kukurusha kwa namna ya ajabu na kuweza kukurishidha inavyotakiwa.

Kawaida mume huanza kukuuliza kama kile anafanya unakipenda na kwa njia ni vizuri wewe mwanamke kumweleza vile unajisikia na unaweza kuji-express kwa uwezo wako wote na hapa ndipo unaweza kuongea sweet word zote (ulizojufunza au kadri feelings zako zinavyokupa taarifa kwenye kiungo kile kinapata raha au kinaguswa kwa mguso mtamu zaidi) si unajua mapenzi ni sana na msanii mzuri anajua nini aongee na aongee namna gani na mwanamke umejaliwa kuwa na sauti ambayo kwa miguno na kulalamika kimahaba mnaweza kuwa na sherehe nzuri sana ya kuwa mwili mmoja.

Kuwa kitandani ni opportunity kubwa sana mke kuweza kuonesha umaridadi wake haina haja kushona mdomo au kubaki kimya kama vile mume amelala na gogo badala jitume kwa maneno na matendo, huu ni uwanjawako, mume wako, jipe raha na enjoy raha ya mwili.
Piga kelele kwa raha zako na unaweza kutamka kitu kizima kizima bila woga maana huyo ni mume wa ujana wako.

Wanaume nao wakati mwingine huwa insecure kama wanawake wakiwa kitandani hivyo kumtia moyo kwa miguno na vikelele vya kimahaba huweza kumpa ushahidi kwamba una-enjoy kile anafanya na kwamba skills zake na utaalamu wake mke unampa credit naye atajisikia vizuri na kufanya zaidi na hata kujifunza siku nyingine afanye kwa ufundi zaidi.
Hivyo usiogope kuwa mbunifu, lazima uwe mshangiliaji mzuri kwenye mechi na mumeo na hiyo itakuhakikishia furaha zaidi wakati wa kuwa mwili mmoja.
Utakuwa rated 5 stars woman au kama ni shule basi maksi zako ni zaidi ya 95%

MAMBO YA KUZINGATIA..
Hata kama wanaume huwa tunafurahia sana mke kuwa noise kitandani ni muhimu kuwa makini na sauti kwani kupiga kelele kama unapigwa na majambazi si ustaarabu kwani mtaa mzima unaweza kuhamaki na kuja kutoa msaada kumbe watu mnapeana raha zenu au mnaweza ku-attract mijitu inayopenda kupiga chabo bure.
Ni vizuri hakikisha chumba kina Mfumo mzuri wa kuchuja sauti kwani mnaweza kushtakiwa kwa kuzingatia kifungu cha sheria cha Antisocial behaviour order kwani mnaweza kuishia jela au mkajenge nyumba yenu huko shamba mpigiane mikelele yenu.

Wanasayansi wanasemaje kuhusu mwanamke kupiga kelele kitandani?

Wanasayansi wa kijerumani katika utafiti wao wamegundua kwamba mwanamke anapokuwa na kelele kitandani wakati wa kuwa mwili mmoja mwanaume huwa na asilimia 59 za kukojoa (siyo mkojo) tofauti na asilimia 2 kwa mwanamke kuwa kimya na pia mwanamke huwa na kilele zaidi kitandani akiwa fertile na kwa mwanamke kuwa na kilele speed ya mwanaume na uwezo wa kusugua huongezekana maradufu wakati wa kuwa mwili mmoja.
Nakutakia weekend Njema!

Friday, 29 April 2016

NINI MWANAUME ANAHITAJI KUTOKA KWAKO MWANAMKE?


Ndoa ni tamko takatifu ambalo mamilioni ya watu tumeji-commit wenyewe kwa hiari.
Hii ina maana kwamba umepata mtu wa kuishi na wewe katika raha na shida zote hadi kifo.
Unakuwa imeingia katika kifungo cha Kupendana, kuheshimiana na urafiki, hata hivyo jinsi miaka inavyoenda unaweza kujikuta unapoteza umuhimu wa huu uhusiano na mbaya zaidi unaweza kujikutana unajisahau nini unahitaji kutoka kwa mwenzako.
Kuna mambo ya msingi ambayo mwanaume yeyote huhitaji kupata kutoka kwa mke wake mpenzi na kinachotakiwa kwa mwanamke ni yeye kufahamu nini mwanaume anahitaji na kuwekeza kidogokidogo kwa kuongeza jitihada na muda ili haya mahitaji kuwa kitu halisi.

Je ni Vitu gani mwanaume huhitaji sana kutoka kwa mke wake?

1.WANAUME HUPENDA KILE KILICHOKO AKILINI MWA MWANAMKE.

Wanawake ni viumbe tofauti sana (complex) wao ni walezi kwa asili, waumbaji wa vitu, wasimamizi wazuri na wabunifu sana.
Wanaweza kwa urahisi sana kuelezea kitu kilichopo kwenye akili zao likija suala la deal lolote la biashara kama kununua au kuuza.
Wanaweza sana kwenye mambo ya design na hata mawasiliano.
Ila likija suala mwanaume hapo ndiyo kuna tofauti.
Wanaume kawaida tunapenda kujua kwamba tumetimiza mahitaji ya wake zetu na itakuwa vizuri sana kama mwanamke atawezesha mwanaume kujua kwamba mahitaji yake kama mwanamke mume anayatimiza.
Kwa hiyo mwanamke ongea nini unahitaji, au nini unapenda kwa maneno au kwa matendo kwani kununa si jawabu au kubaki kimya si jawabu.
Jawabu ni kuelezana tena kwa upole na upendo jambo lolote unahitaji mwanaume afanye.

2.WANAUME UHITAJI MWANAMKE ANAEJUA KUKUBALIANA/KUAFIKIANA.

Je kama mume wako anapenda kuangalia au kucheza soccer siku za weekend kwa ajili ya kujiliwaza huwezi kuwa naye?
Kuna ubaya gani wewe kushangalia kile mume wako anapenda (hobbies)
Kumbuka maisha ndivyo yalivyo msipofurahi pamoja na kuwa na fun pamoja usitegemee siku mambo yabadilike yenyewe tu kuna kitu unahitaji kufanya sasa ili kesho iwezekane.
Penda kufanya pamoja kile kitu mume wako anakipenda katika maisha inaweza kuwa ni kuimba, jogging, kwenda kutembea sehemu yoyote ili pamoja au matamasha na michezo mbalimbali.
Kumbuka unaweza kuwa wewe hupendi kwenda naye huko yeye anapenda kwenda, lakini kuna wanawake wanafurahi kuwa naye huko wewe umekataa kwenda na hana njia kwani ni kitu anakipenda na ni sehemu ya maisha yake (kama hatendi dhambi).

3.WANAUME UHITAJI MWANAMKE ANAEJUA MAMBO.

Huwezi kutenganisha habari za siasa, michezo, biashara, current news, sayansi na mambo ya kimataifa na mwanaume, hivyo usijiweke nyuma sana unahitaji kuwa mtu wa karibu kupiga naye story za mambo kama hayo, jitahidi na wewe kuwa wamo.
Inawezekana jioni kabla ya kulala mkawa na glass ya juice mnakunywa wawili huku watoto wamelala, wewe mwanamke kwa ujasiri shusha story za michezo mambo ya Chelsea, Manchester united, Liverpool au hata Yanga na Simba just for fun, au hata habari za mafisadi au hata habari za mfalme Suleiman au Daudi au business ambazo umezitafiti hapo mwanaume atajua nina mke ndani ya nyumba.
Wapo wanawake mume akianza kuongea habari za siasa, michezo au business anaondoka zake na kumwacha naamini wanaume hapo huwa hawafurahii kabisa.
Nakwambia ukijua kuongea na mumeo mambo ambayo wanaume wote wanayapenda utafahamu mambo mengi sana kuhusu ulimwengu, watu na ninyi wenyewe.
Pia unaweza kubadilisha akili katika kufahamu mambo.
Hii huimarisha sana ukaribu na hamasa ya kila mmoja kutaka kusikia kwa mwenzake na matokeo yake ndoa inakuwa tamu maana huo usiku mkimaliza story lazima chumbani kuwake moto.

4.MWANAUME ANAHITAJI MWANAMKE AMBAE KWA MAPENZI NI MOTO.

Huwa kuna kawaida kwamba mwanaume katika jamii zetu za kiafrika ndiyo anakuwa mwamuzi wa mambo mengi kiasi kwamba hata wanawake wenyewe hutambiana kwamba jana mume wangu alinipeleka dinner sehemu.
Je, itakuwaje kama na wewe mwanamke siku ukamwambia mume wako leo pamoja na watoto tunaenda lunch sehemu au dinner sehemu kula, au kula kitimoto na nk pamoja na watoto wenu kwa hela yako au bajeti yako au maamuzi yako.
Wakati huo huo umetinga kiwalo chako cha nguvu (sexy) hadi unamkumbushia zile ezni zenu ambazo zilifanya avutiwe na wewe hadi kukuoa.
Wanaume wanahitaji wanawake wa aina hiyo ambao siku zingine wanafanya vitu romantic au sexy angalau hata kwa mwaka mara moja siyo mwaka mzima hujafanya jambo lolote la kuimarisha mapenzi.
Wanaume wanahitaji mwenzi siyo mtu wa kuishi naye chumba kimoja
Kuagana asubuhi na kuja kukutana jioni bila kuongea chochote mchana mzima ni dalili ya uhusiano usio na afya kabisa.
Jaribu kufikiri mwenyewe hivi ukiondoka asubuhi unawasiliana na mumeo mara ngapi?
Siku hizi karibu kila mtu ana simu ya mkononi, unaweza kutuma sms, au kumpigia just to say hi honey! Mbona wakati wachumba sms zilikuwa zinatumwa hadi vidole vikaota sugu, leo kunani?
Hamu na msukumo alionao mmoja kwa mwenzake ni msingi wa kuonesha afya na mahusuano yenye furaha.
Wakati mwingine mahusiano huenda bila mawasiliana ya mara kwa mara lakini hiyo ni sumu kubwa sana kwani inaweza kufikia kipindi hakuna hata kutakana, hamu ya kila mtu kwa mwenzake hupotea na hapo ndipo watu sasa huanza kuishi kama vile watu tofauti walioamu kuishi nyumba moja na chumba kimoja lakini ule moto umetoweka.
Kwa hiyo kama wewe ni mwanamke hakikisha unakuwepo katika mahusiano kwa maana kwamba unahitaji kumtia moyo mumeo, kumuinua pale anapokata tamaa uliza nini kinaendelea asubuhi, mchana, jioni na usiku, pia akifanya kitu kizuri mpe sifa na hongera.
Jifunze kwa busara na hekima kujua nini kinaendelea katika maisha ya mume wako na pia onesha kwamba unamjali sana (care) na kwa njia hiyo automatically atakupenda zaidi na ndoa yenu itakuwa imara zadi.

5.MWANAUME ANAHITAJI MWANAMKE HURU.

Ni kweli kila mmoja anamuhitaji mwenzake ili maisha yakamilike lakini kuna wakati mwanaume anahitaji kuona ana mke ambaye anaweza kuendesha mambo mwenyewe bila kushikwa mkono kwa kila kitu.
Pia wewe mwanamke usije mwambia mume wako sikuhitaji kwa sababu naweza kufanya mambo yote mwenywe hapo litakuwa zogo la ajabu.
Hapa nazungumzia ule uwezo wa mwanamke kuweza kuendesha mambo au familia hata kama mume hayupo. Tunajua sana wanawake mnaweza mambo mengi hata kuliko sisi wanaume ila kuna wanawake ambao bila mwanaume hawezi kufanya jambo lolote kiasi ambacho mume naye akajisikia kweli nina mke anayeweza.
Pia mwanamke hahitaji kuwa mtu wa kulaumu kila kitu, mtu wa kulalamika kila kitu, leo ukilalamika hiki kesho unaanza kingine na wakati mwingine unasingizia kwamba unaumwa wakati huumwi lengo kuuchanganya mwanume, hapo ujue unaipeleka ndoa yake eneo hatari wanaume hawaipendi hiyo, wanapenda mwanamke asiye na malalamiko au lawama au msumbufu.

6.MWANAUME ANAHITAJI MWANAMKE ANAYEAMINIKA.

Bila kuaminiana, lazi kutuhumiana kunafuata na bila kuaminiana mahusiano hayawezi kuwa imara.
Mwanaume anahitaji mwanamke anayemwamini hasa pale anapokuwa hayupo.
Mwanaume anahitaji mwanamke mwaminifu huko kazini, mwanamke mwaminifu sokoni anakoenda, mwanamke mwaminifu mahali popote akiwa peke yake.
Kuwa mkweli ndiyo njia nzuri ya kujenga uaminifu, kiwe kitu kidogo au kikubwa ni muhimu kuwa mkweli na mwaminifu kwa mume wako.
Kumbuka ukidanganya kitu kimoja unahitaji kudanganya mara kumi na tano zaidi ili kufunika huo wongo kuwa ukweli hata hivyo ipo siku mambo yatagoma na mambo yakigoma utakuwa umepoteza uaminifu, na ukipoteza uaminifu ni kama kuyeyuka kwa barafu huwezi kurudisha.
Wakati mwingine kuwa mkweli na mwaminifu huonekana ngumu lakini ndiyo dawa halisi ya kuimarisha mahusiano ya ndoa yako, hata kama umenunua kitu kwa gharama sana huko dukani au sokoni mwambie ukweli bei halisi usiseme bei tofauti na ile umenunulia.
Kitu cha msingi, jaribu kufikiria kile unafanya je na wewe ungefanyiwa ungekubali? Au ungeridhilka?
Kazi kwako.

7.MWANAUME ANAHITAJI KUONA UNAVYOFANYA KTK MALEZI.

Wakati mwanamke anapochukua jukumu la kuwa mlezi katika familia mwanaume hujisikia raha sana.
Kile kitendo cha kuwasaidia watoto kama vile kufanya nao homework walizopewa shuleni, au kucheza pamoja kama vile soccer na mtoto wa miaka 4 au 5, mwanaume hujisikia raha sana kwa namna ambayo mwanamke anajibidiha kulea kile ambacho kwa pamoja mmekileta duniani.
Kama una watoto au bado kitu cha msingi lazima ujue kwamba mwanaume hujisikia vizuri sana pale unapohusika bega kwa bega kusimamia malezi ya hawa viumbe ambao mmepewa zawadi hapa duniani.
Kwa jamii zetu za kiafrika hili halina shida sana ingawa kwa huku Marekani na Canada ni kitu cha kawaida mwanaume kuachiwa kazi zote za malezi ya watoto na mwanamke akawa anakuangalia tu.

8.MWANAUME ANAHITAJI UWE RAFIKI YAKE MKUU DUNIANI.

Kama umewakuta mume na mke wakitembea wameshikana mikono naamini huwa unapata ujumbe kwamba na wewe unapenda kuwa na mume wa uhusiano wa aina hii.
(Sizungumzii wale wanafiki ambao chumbani wanazipiga na barabarani wameshikana mikono)
Binadamu ameumbwa kuwa muhitaji kwa kupendwa, muhitaji wa kuwa na rafiki kuwa na mwezi (companion) kuondoa upweke
(duniani wawili wawili mume na mke)
Mnahitaji kuwa mke na mume, lakini mnahitaji pia kuwa marafiki wakubwa siku zote.
Tunatumia muda mwingi sana kuwa na mke au mume hivyo ili kunogesha zaidi inabidi kuwa marafiki na kupeana story, michapo, kuchezezeana, kutaniana, kutembea sehemu pamoja, kucheka pamoja, kucheza michezo tunapenda pamoja, kujaribu vitu vipya pamoja.
Pia ni muhimu kuwa na marafiki wengine ila urafiki lazima uanze na ninyi wawili.

9.MWANAUME ANAHITAJI MWANAMKE MALAIKA WAKIWA SEBULENI NA MWANAMKE MTUNDU WAKIWA CHUMBANI.

Wanaume wanahitaji hot sex, tendo la ndoa ambalo linaleta msisimko, linalofurahisha na kutia hamasa mpya kila siku.
Jaribu vitu vipya, mikao, miguso, busu, na michezo ya kitandani au chochote umejifunza, acha woga kwamba atakuuliza nani kakufundisha, dunia ya leo tunaishi dunia ambayo wanaaiita information society, hivyo watu tunapashana habari na kufundishana kupitia magazeti, radio, TV, movie, internet nk.
Usiache kufanya kitu kipya huko chumbani eti kuogopa atakuuliza umejifunza wapi.
Kazi kubwa kwako ni kuhakikisha kitanda kinakuwa moto siku zote na pia kumpa vitu vya uhakika ili asitembeze macho nje kutokana na kuwa bored na mapishi ya aina hiyohiyo miaka nenda tudi.
Ni kweli kama umri umekwenda sana hamwezi kufanya kama ile miaka ya nyuma lakini isiwe sababu ya kutokuwa na sex yenye kuridhisha na mwanamke kuwa moto kitandani.
Miili yetu ni hekalu la Mungu la ajabu na la aina yake hapa duniani.
Mwili ni laini, una harufu nzuri, ukiguswa unapata raha ya ajabu, hivyo kama mwanamke unahitaji kujiweka safi na sexy muda wote bila kujali umri.
Kitu cha msingi ni kwamba mume wako anakuhitaji wewe, anahitaji ladha mpya na utamu kila siku kutoka kwako iwe ni kukugusa kwa mikono yake, au kukuangalia kwa macho yake au kukunusua mwili wako kwa pua yake au kukusikia unaongea maneno matamu kwa masikio yake na kukuonja mwili wako kwa ulimi wake.
Ni kweli anakuhitaji wewe na si mwingine na kwa kuwa anakuhitaji wewe basi
Mpe raha
Keep it hot,
steam it up
and you both will come back wanting more time and time again.
Mwisho
Kuna mambo ya msingi ambayo mwanaume anahitaji kwako na kuna kitu anataka kwako, kuna mambo mengi sana mwanaume anahitaji kwako kitu cha msingi timiza hizi ndoto kwa kuzifanyia kazi.
Kama utakuwa ni mtu unayekuwa mbunifu na mwenye kufanya mambo tofauti bila mazoea basi uhusiano wako na umpendaye utakuwa imara na mzuri kila iitwapo leo.

Tuesday, 26 April 2016

MAHITAJI MUHIMU KWA MUME.


Wanawake wengi leo wapo independent na inafika mahali wanajisahau kuwajali waume zao, ni muhimu sana kwa mwanamke kuwa na taaluma yake na pia ni muhimu sana kwa mke kukumbuka kwamba mume akifurahi nyumbani kunakuwa na furaha.
Mume akifurahi nyumbani kunakuwa na furaha, mke akifurahi maisha yanakuwa ya furaha na watoto wakifurahi nyumba inakuwa na furaha pia.
Kuna mahitaji matatu ya msingi ambayo mume akiyapata basi atafurahi na nyumbani patakuwa mahali pa furaha kwa mke na watoto.
Kumbuka mwanandoa akisema ndoa yake ina furaha na inaridhisha maana yake anatimiziwa mahitaji yake ya msingi katika ndoa au mahusiano na kama haridhiki na hana furaha maana yake hatimiziwi mahitaji yake muhimu.
Je, mahitaji ya msingi ya mwanaume kutoka kwamke wake ni yapi?
Kuna mahitaji 3 ya msingi ambayo mwanaume huhitaji kutoka kwa mke wake nayo ni
1. MWENZA.
Baada ya Adamu kuumbwa na Mungu alionekana ni mpweke hata baada ya kujichanganya na wanyama wengine; Mungu akaona haipendezi, akamuumba Hawa kwa ajili ya Adamu na akasema inapendeza.
Kwa nini mume anakuhitaji wewe mke kama mwenzi wake?
Ili uwe mtu wa kuwa naye, unayemfaa, mtu wa kucheza naye, kumbuka Adam alicheza sana na monkeys, samba, mbuni, Ng’ombe, kuku nk na vyote havikuweza kufanya ajisikia vizuri hadi Mungu alipomuumba mwanamke.

Ni muhimu sana Wake kufahamu kwamba waume zenu wanapenda kucheza na kwamba mume wako anapenda sana kucheza na wewe, kuwa na wewe, hivyo tafuta kitu chochote ambacho mume wako anakipenda, then fanya naye.
Kama humpi muda wa kuwa na wewe, kucheza na wewe basi atampata mwingine wa kuwa naye au kucheza naye, ndipo kilio huja.......

Pia jiulize kama mume wako hayupo kazini, au mahali unakofahamu yupo; je, atakuwa na nani? Wewe uliumbwa kwa ajili yake ili kuwa naye, kucheza naye na si kuwa vuvuzela!

2. TENDO LA NDOA
Sex ni neno zuri ambalo si chafu kama wengine wanavyoamini na kulitumia hata kama litatajwa kanisani; kwani Mungu aliumba sex kwa ajili ya mke na mume kufurahia uumbaji wake.
Hata hivyo linapokuja suala la sex wanaume wengi ni hitaji la pili katika mahusiano ya ndoa wakati wanawake ni hitaji namba 13 kwa kufuata umuhimu.
Mwanaume yeyote katika ndoa, hitaji la sex kwake ni msingi na bahati mbaya ni kwamba asipopata sex kwa mke wake dunia inaweza kumuuzia.
Hata hivyo nasisitiza kwamba sex nje ya ndoa huweza kumuongoza mtu kwenye kifo
Mungu aliumba hivyo:

3. HESHIMA (Respect)
Ukweli ni kwamba jambo la msingi kwa mume wako si kile unaongea kwake bali ni namna unavyongea kwake.
Inawezekana mume wako anao uwezo (potential) mkubwa sana kufanikisha maisha hata hivyo kutokana na ulivyo critical, blaming, kosa heshima na adabu kwa mumeo imekuwa ngumu sana yeye kupiga hatua.
Hitaji la kwanza la msingi kwa mwanaume yeyote ni heshima.
Kila maamuzi yanayofanyika katika ndoa yanahitaji kufanyika kwa ushirikiano wa mke na mume.
Kutoa sifa kwa mume wako ni njia ya maisha ya ndoa.
Behind every successful and great husband, there is an honouring and praising wife.
Kumbuka Baba akifurahi, nyumbani kunakuwa na upendo, furaha na amani na pia nyumbani kunakuwa mahali salama kwa kukimbilia.
Waefeso 5:21 – 24, 33

Wednesday, 20 April 2016

KUPOTEZA HISIA.


“Nimepoteza hisia za kumpenda, zimepotea na zimepotea kabisa.
Simpendi kabisa mke wangu na hata sifahamu kama kweli niliwahi kumpenda; nashangaa na sihitaji kuwa naye tena, sijisikii chochote linapokuja suala na hisia zangu kwake naamini ndoa imefika mwisho” Jerry aliongea kwa mshangao mbele ya mkewe.

Mkewe naye akajibu kwa kusema “hata sielewi tumefikia vipi hatua hii.
Tunaongea mara chache sana na hata tukiongea hatuongei jema lolote, (machozi yanaanza kumiminika kwenye mashavu) ni kulaumiana, kudharauliana, kusutana, kila mmoja anampuuza mwenzake, ndoto zimeyeyuka na hakuna ladha ya maisha.
Hapa nina maumivu makali.
Hivi inawezekana mtu ukashindwa kabisa kumpenda mtu ambaye alikuwa bila yeye maisha hayana maana?

Hali kama hii huwakuta wanandoa wengi na watu wengi walio katika mahusiano; haijalishi ni miaka mingapi au mlikuwa mnapendana kiasi gani na bila kujifahamu vizuri na kutumia busara na hekima kumaliza hili tatizo ndoa au mahusiano huweza kujikuta yameangukia kwenye shimo lefu mno.

Kila ndoa ina positive na negative moments, mwanandoa mmoja akiwa anamwangalia mwenzake kwa negatives tu itafika mahali ataanza kuji – withdraw na kujiweka mbali na automatically ataanza kujisahau kuwa caring. Wakati mmoja anajiweka mbali na mwenzake huyu mwingine huanza ku-panic na kuanza kutoa lawama kwamba hupendwi. Wanavyozidi kusuguana ndivyo wanazidi kusababisha mafuriko ya lawama emotionally na matokeo ni kuwa disconnected katika emotions na feelings.


Kuna utafiti kuhusiana na positives na negatives kwenye suala la ndoa na mahusiano na kutoa jumuisho kwamba quality ya emotions ilizonazo kwa mwenzi wako ni muhimu sana.
Ni simple lakini muhimu sana katika mahusiano.

Kama positives zitakuwa nyingi kuliko negatives unavyomchukulia mwenzi wako basi mahusiano yatakuwa bora sana, haleluya Kubwa!
Na kama negatives zitakuwa nyingi kuliko positives katika hisia kwa mwenzi wako basi shughuli nzito inakuja mbele yenu!

Ukweli ni kwamba negatives moja huhitaji positive tano ili kufanya balance ya ndoa au mahusiano kuwa katika hali nzuri (feelings).
Hii ina maana ukimbomoa mwenzi wako mara moja basi inabidi umjenge mara tano zaidi ili ku- balance ule uharibifu umefanya mara moja.
Kila negative moja unahitaji positive tano ili emotions na feelings za mapenzi yenu kurudi kuwa katika hali ya kawaida.
SIRI MUHIMU UNAPOTAFUTA MCHUMBA.

Unapotafuta mchumba "tumia kichwa chako kwanza" na tumia moyo wako ukisharidhika naye.

Katika ndoa kuna namna tofauti ya kupambana na

matatizo au kutoelewana au kubishana au kutokubaliana na jambo au shida yoyote na kila wanandoa wana namna yao, hii ina maana kwamba tatizo lilelile ambalo wengine wanavurugana na kuachana kwa wengine ni opportunity ya kujenga ndoa yao.
Inaweza kutokea kwamba mke anapenda kuwa karibu na mume wake kimapenzi (intimacy) na mume akawa anapenda kuwa mwenyewe (privacy), inaweza kuwa mke hupenda kuchelewa kulala na mume ni mtu wa kuwahi kulala na kuamka mapema, inaweza kuwa mume anapenda kuhakikisha anapata milo 3 ya uhakika kwa siku, wakati mke anapenda milo miwili tu na imetoka. Inawezakena mke anapenda sana kuongea na mume ni mtu wa kuwa silent.
Hata hivyo bila wanandoa kuwa na aina ya kuchukuliana (flexibility/adaptivity) itakuwa ngumu sana kwa wanandoa kuridhika na ndoa yao.
Kwa kijana mgeni na masuala ya mapenzi anashauriwa kutumia kichwa na si moyo ili kuweza kumfahamu binti au kaka anayempenda awe mke wake kwa maisha ya baadae.
Kwani ukishampenda (fall in love) unaweza kupoteza mwelekeo kwa kupelekeshwa na emotions hadi kupoteza lengo la mke au mume uliyekuwa unategemea uoane naye.
Kwa wastani inachukua hadi miaka 2 tangu umemuweka kichwani (mke/au mume mtarajiwa) hadi kuoana.
Kwani bila kuchunguza kwa makini unaweza kujikuta unaingia kwenye jehanamu ndogo.
Kumbuka mwanaume ambaye anakupelekesha na kukukalia wakati wa uchumba akikuoa hiyo tabia yake itakuwa maradufu.
Kama binti hajiamini wakati wa uchumba, akiolewa ndo hatajiamini zaidi.
Utakuwa unajidanganya sana ukiamini kwamba kuoa au kuolewa kunaweza kuondoa au kutatua matatizo kama wivu, hasira, uchoyo, ukali, kukosa uaminifu, ubabe, kutojiamini nk
Ukweli ni kwamba kama Unaona tabia mbaya kwa mchumba wako basi tegemea hali mbaya zaidi baada ya kuona.
Pia, wapo watu ambao huamua kuoana baada ya kujuana au kufahamiana kwa muda mdogo sana kama vile mwezi mmoja au miezi miwili.
Kama unaamini ndoa ni hadi kifo kitakapowatenganisha, kwa nini uchukue uamuzi ambao utalazimika kuishi naye maisha yote huku unateseka kwa kuwa ulifanya mambo haraka haraka.

Pia siri kubwa ambayo wengi hawaijui ni kwamba kati ya asilimia 80 hadi 90 ya wanaume au wanawake unaowaona si wazuri kiasi cha kutosha kuoana na wewe.
Hii ina maana kwamba ni asilimia 80 hadi 90 ya watu hao wanakupenda lakini wanatamani sana wakubadilishe kwanza ndipo wakupende na mapenzi ya kweli ni kumpenda mtu na kumchukua kama alivyo.

Kumtafuta mke au mume wa kudumu katika maisha siyo “kids play” ukienda kizembe kama mtoto utaoana na mtu mwenye akili za kitoto.
Ukweli ni kwamba unamtafuta mtu asiye wa kawaida, ambaye ana sifa maalumu unazohitaji na hakuna mchezo wa kukisi bali lazima uwe na uhakika.
Pia lazima ufahamu maeneo ambayo unaweza kumpata mwanamke mwenye sifa au mwanaume mwenye sifa

SIRI MUHIMU UNAPOTAFUTA MCHUMBA


Unapotafuta mchumba "tumia kichwa chako kwanza" na tumia moyo wako ukisharidhika naye.

Katika ndoa kuna namna tofauti ya kupambana na matatizo au kutoelewana au kubishana au kutokubaliana na jambo au shida yoyote na kila wanandoa wana namna yao, hii ina maana kwamba tatizo lilelile ambalo wengine wanavurugana na kuachana kwa wengine ni opportunity ya kujenga ndoa yao.
Inaweza kutokea kwamba mke anapenda kuwa karibu na mume wake kimapenzi (intimacy) na mume akawa anapenda kuwa mwenyewe (privacy), inaweza kuwa mke hupenda kuchelewa kulala na mume ni mtu wa kuwahi kulala na kuamka mapema, inaweza kuwa mume anapenda kuhakikisha anapata milo 3 ya uhakika kwa siku, wakati mke anapenda milo miwili tu na imetoka. Inawezakena mke anapenda sana kuongea na mume ni mtu wa kuwa silent.
Hata hivyo bila wanandoa kuwa na aina ya kuchukuliana (flexibility/adaptivity) itakuwa ngumu sana kwa wanandoa kuridhika na ndoa yao.
Kwa kijana mgeni na masuala ya mapenzi anashauriwa kutumia kichwa na si moyo ili kuweza kumfahamu binti au kaka anayempenda awe mke wake kwa maisha ya baadae.
Kwani ukishampenda (fall in love) unaweza kupoteza mwelekeo kwa kupelekeshwa na emotions hadi kupoteza lengo la mke au mume uliyekuwa unategemea uoane naye.
Kwa wastani inachukua hadi miaka 2 tangu umemuweka kichwani (mke/au mume mtarajiwa) hadi kuoana.
Kwani bila kuchunguza kwa makini unaweza kujikuta unaingia kwenye jehanamu ndogo.
Kumbuka mwanaume ambaye anakupelekesha na kukukalia wakati wa uchumba akikuoa hiyo tabia yake itakuwa maradufu.
Kama binti hajiamini wakati wa uchumba, akiolewa ndo hatajiamini zaidi.
Utakuwa unajidanganya sana ukiamini kwamba kuoa au kuolewa kunaweza kuondoa au kutatua matatizo kama wivu, hasira, uchoyo, ukali, kukosa uaminifu, ubabe, kutojiamini nk
Ukweli ni kwamba kama Unaona tabia mbaya kwa mchumba wako basi tegemea hali mbaya zaidi baada ya kuona.
Pia, wapo watu ambao huamua kuoana baada ya kujuana au kufahamiana kwa muda mdogo sana kama vile mwezi mmoja au miezi miwili.
Kama unaamini ndoa ni hadi kifo kitakapowatenganisha, kwa nini uchukue uamuzi ambao utalazimika kuishi naye maisha yote huku unateseka kwa kuwa ulifanya mambo haraka haraka.

Pia siri kubwa ambayo wengi hawaijui ni kwamba kati ya asilimia 80 hadi 90 ya wanaume au wanawake unaowaona si wazuri kiasi cha kutosha kuoana na wewe.
Hii ina maana kwamba ni asilimia 80 hadi 90 ya watu hao wanakupenda lakini wanatamani sana wakubadilishe kwanza ndipo wakupende na mapenzi ya kweli ni kumpenda mtu na kumchukua kama alivyo.

Kumtafuta mke au mume wa kudumu katika maisha siyo “kids play” ukienda kizembe kama mtoto utaoana na mtu mwenye akili za kitoto.
Ukweli ni kwamba unamtafuta mtu asiye wa kawaida, ambaye ana sifa maalumu unazohitaji na hakuna mchezo wa kukisi bali lazima uwe na uhakika.
Pia lazima ufahamu maeneo ambayo unaweza kumpata mwanamke mwenye sifa au mwanaume mwenye sifa.

SIRI MUHIMU UNAPOTAFUTA MCHUMBA.

Unapotafuta mchumba "tumia kichwa chako kwanza" na tumia moyo wako ukisharidhika naye.

Katika ndoa kuna namna tofauti ya kupambana na matatizo au kutoelewana au kubishana au kutokubaliana na jambo au shida yoyote na kila wanandoa wana namna yao, hii ina maana kwamba tatizo lilelile ambalo wengine wanavurugana na kuachana kwa wengine ni opportunity ya kujenga ndoa yao.
Inaweza kutokea kwamba mke anapenda kuwa karibu na mume wake kimapenzi (intimacy) na mume akawa anapenda kuwa mwenyewe (privacy), inaweza kuwa mke hupenda kuchelewa kulala na mume ni mtu wa kuwahi kulala na kuamka mapema, inaweza kuwa mume anapenda kuhakikisha anapata milo 3 ya uhakika kwa siku, wakati mke anapenda milo miwili tu na imetoka. Inawezakena mke anapenda sana kuongea na mume ni mtu wa kuwa silent.
Hata hivyo bila wanandoa kuwa na aina ya kuchukuliana (flexibility/adaptivity) itakuwa ngumu sana kwa wanandoa kuridhika na ndoa yao.
Kwa kijana mgeni na masuala ya mapenzi anashauriwa kutumia kichwa na si moyo ili kuweza kumfahamu binti au kaka anayempenda awe mke wake kwa maisha ya baadae.
Kwani ukishampenda (fall in love) unaweza kupoteza mwelekeo kwa kupelekeshwa na emotions hadi kupoteza lengo la mke au mume uliyekuwa unategemea uoane naye.
Kwa wastani inachukua hadi miaka 2 tangu umemuweka kichwani (mke/au mume mtarajiwa) hadi kuoana.
Kwani bila kuchunguza kwa makini unaweza kujikuta unaingia kwenye jehanamu ndogo.
Kumbuka mwanaume ambaye anakupelekesha na kukukalia wakati wa uchumba akikuoa hiyo tabia yake itakuwa maradufu.
Kama binti hajiamini wakati wa uchumba, akiolewa ndo hatajiamini zaidi.
Utakuwa unajidanganya sana ukiamini kwamba kuoa au kuolewa kunaweza kuondoa au kutatua matatizo kama wivu, hasira, uchoyo, ukali, kukosa uaminifu, ubabe, kutojiamini nk
Ukweli ni kwamba kama Unaona tabia mbaya kwa mchumba wako basi tegemea hali mbaya zaidi baada ya kuona.
Pia, wapo watu ambao huamua kuoana baada ya kujuana au kufahamiana kwa muda mdogo sana kama vile mwezi mmoja au miezi miwili.
Kama unaamini ndoa ni hadi kifo kitakapowatenganisha, kwa nini uchukue uamuzi ambao utalazimika kuishi naye maisha yote huku unateseka kwa kuwa ulifanya mambo haraka haraka.

Pia siri kubwa ambayo wengi hawaijui ni kwamba kati ya asilimia 80 hadi 90 ya wanaume au wanawake unaowaona si wazuri kiasi cha kutosha kuoana na wewe.
Hii ina maana kwamba ni asilimia 80 hadi 90 ya watu hao wanakupenda lakini wanatamani sana wakubadilishe kwanza ndipo wakupende na mapenzi ya kweli ni kumpenda mtu na kumchukua kama alivyo.

Kumtafuta mke au mume wa kudumu katika maisha siyo “kids play” ukienda kizembe kama mtoto utaoana na mtu mwenye akili za kitoto.
Ukweli ni kwamba unamtafuta mtu asiye wa kawaida, ambaye ana sifa maalumu unazohitaji na hakuna mchezo wa kukisi bali lazima uwe na uhakika.
Pia lazima ufahamu maeneo ambayo unaweza kumpata mwanamke mwenye sifa au mwanaume mwenye sifa.

Saturday, 16 April 2016

KUHUSU NDOA..

Tafiti nyingi zinafanana na zinakubali kwamba ndoa nyingi imara ni zile ambazo mke na mume huwa na sifa nyingi zinazofanana.
Kundi la watafiti lilikusanya ndoa 35 ambazo ziliwekwa katika makundi matatu kundi la kwanza lilikuwa la wale ambao ndoa zako zilikuwa za furaha, kundi la pili zile zilikuwa ni zile wanandoa walikuwa na wakati mgumu kuishi pamoja na kundi la tatu la wale walikuwa njiani kuachana.

Majibu yalikuwa ni kwamba wale walioishi kwa furaha walifanana sana katika mambo mengi (general activities), walikuwa marafiki na walifanana katika kujihusisha binafsi na mwenzake.
Wale ambao hawakuwa na furaha kuishi pamoja hawakufanana katika utendaji wa mambo yao kila siku, pia hawakufanana linapokuja suala la mwitikio wa hisia zao.
Wale waliokuwa wanataka kuachana kila mmoja alikuwa na sifa nyingi zisizofanana kabisa.

Kiwango cha furaha katika ndoa huweza kujieleza kutokana na kufanana kwa wanandoa katika sifa binafsi walizonazo.
Hii ina maana wanandoa wakifanana kiuchumi, tabia, mazingira, tamaduni, matumizi ya pesa, kiwango cha energy, uwezo wa kuongea na kusikiliza, kiimani, kihisia nk inakuwa rahisi kila mmoja kutegemea nini kutoka kwa mwenzake.

Hivyo ukitaka kuwa na ndoa imara ni muhimu kuwa na balance account ambayo kufanana ni zaidi ya tofauti kwa sababu kila tofauti iliyopo inahitaji kupatanisha na kuweka kuikubali hata kwa maumivu.

Saturday, 9 April 2016

USHAWAHI KUSIKIA HII MWANANDOA?

Binadamu akifikia miaka 9 – 14 mwili huanza kubadilika. Hiki ni kipindi ambacho msichana au mvulana hubadilika kutoka utoto na kuwa mtu mzima na hiki kitendo huitwa balehe na moja ya dalili ni kuota kwa nywele kwenye makwapa, sehemu za siri nk.

Leo tuzungumzie nywele za sehemu za siri yaani mavuzi.
Hizi nywele kawaida huwa na rangi tofauti na nywele za sehemu zingine kama kichwani, zingine huwa na rangi nzito zaidi, zingine huwa ngumu zaidi, zingine hunyoka, zingine hujisokota (curl)

Linapokuja suala kunyoa hizi nywele ni preference ya mtu, pia jambo la kushangaza ni kwamba wanawake ndio huzungumziwa zaidi kuliko wanaume ni kama vile wanaume hawana hizi nywele.
Imefika wanaume hujiuliza wenyewe je, mwenzangu unapenda mke kuwa na forest au kuwa na jangwa la sahara?
Kila mwanaume au mwanamke ana jibu lake.

Baadhi ya wanawake hujisikia more attractive wakiwa wamenyoa wakati wengine hujisikia raha wakiwa na thick forest.

Hata hivyo kama lilivyo suala la matiti au makalio wapo wanaume hufurahia na kujisikia excited zaidi kwa mwenzi wake kuwa na msitu wa asili wa uhakika wakati huohuo wapo wanaume ambao kwa mwanamke kuwa na msitu mnene kwake huona ni mwanamke mchafu na asiyejitunza kama anshindwa kujinyoa sehemu muhimu kama hiyo basi yupo careless na hajipendi.

Kunyoa au kutokunyoa ni suala la hiari yako na mpenzi wako hakuna sababu ya Kujiona upo sahihi au hupo sahihi pia wapo ambao hunyoana na nyakati kama hizo kwao ni faragha na kujuana.

Kutokupata information zinazotakiwa wakati mwingine huweza kusababisha mtu kuchukua hatua ambazo zinaweza kushangaza hata mpenzi wake.

FAIDA ZA KUACHA KUNYOA

Hizi nywele huwa zinashika homoni za pheromones ambazo zikisambaa huweza kuvutia mtu wa jinsi tofauti

Huweza kuzuia msuguano wakati wa tendo la ndoa, Kumbuka viungo vya uzazi vipo delicate sana.
Husaidia kufanya maeneo ya sehemu za siri kuwa jotojoto (warm)
Huzuia na Kulinda sehemu za siri hasa vitu vidogo kama mavumbi Kuingia sehemu nyeti hasa wanawake kama zilivyo nywele za kawaida zinavyolinda kichwa.
Huonesha kukua kwa mtu (sexual maturity)

FAIDA ZA KUNYOA

Huboresha tendo la ndoa hasa kwa wale wanaopenda Kipara.
Huboresha usafi; hizi nywele hushika harufu na kuweza kupelekea kutoridhishana kimapenzi, au kama muhusika hajaoga vizuri anaweza kukufukuza kwa harufu.
Kujisikia vizuri, kujiamini na kujisikia safi.

KUNYOA AU KUTOKUNYOA KATIKA NDOA
Kuwa na maeneo ambayo yanatunzwa ni moja ya njia ambayo mke na mume huweza kujisikia vizuri kwa mwenzake.
Wengine hujisikia vizuri zaidi kwa kila mmoja kuwa kipara na kufanya degree of intimacy kuwa juu zaidi (ngozi kwa ngozi hunoga zaidi)
Wanandoa wengi hukubaliana kunyoa au kunyoana kuliko kuacha msitu, sababu kubwa zikiwa
Kunyoa huleta ukaribu (intimacy)
Kuwa kipara (mwanamke) ni zaidi ya kuwa uchi kwani unakuwa kama umeondoa kile kinaficha uke hivyo mume huweza kuona kwa macho na kwa kugusa uzuri na jinsi Mungu alivyokuumba.
Pia wanandoa ambao hunyoana kuanzia honeymoon huwafanya kuwa karibu zaidi kwa kujuana zaidi.
Kunyoa ni usafi.
Agano la kale ilikuwa ni ishara ya kujitakasa.
Kunyoa mwanamke huonesha amejitoa kwa mumewe.


JE, KUNA STYLE ZA KUNYOA?
Wengine wanaponyoa huweka style mbalimbali,
Wengine hupunguza na si kunyoa Kipara kabisa.
Wengine hunyoa pembetatu ili wakivaa bikini nywele zisionekane.
Wengine hutengeneza mstatili ambao huitwa “Chaplin Moustache” kwa raha zao mke na mume.
Wengine hupaka rangi nyekundu na kuchora umbo la moyo kama zawadi kwa mwenzi wake.

JE,WEWE UNAPENDA VIPI??

Monday, 4 April 2016

TOFAUTI HIZI CHUMBANI..

Tofauti ya kiumbo kati ya mke na mume ni asilimia ndogo sana ya tofauti kati ya mwanamke na mwanaume kwa ujumla.
Bila kufahamu tofauti zilizopo tunaweza kujikuta katika shida na matatizo au confusion ya uhakika chumbani.
Ukiacha tofauti zingine zote zilizopo kati ya mke na mume linapokuja suala la sex mwanaume sex ni hitaji la kimwili kwanza (physical) na baadae emotions wakati mwanamke ni hitaji la emotions kwanza then kimwili.
Hii ina maana kwa mwanamke sex ni upendo kwanza, kujisikia vizuri kwanza, kupata caring kwanza kwa mwanamume ni kuwasha tu na bus linaondoka.

Linapokuja suala la kile anakiona mwanaume anavutiwa kwa nguvu ya ajabu (hasa anapomuona mwanamke, wakati huohuo mwanamke naye anauwezo na nguvu ya ajabu ya hamu ya upendo, ukaribu, mapenzi na kusikilizwa na mwanaume.

Mwanaume huwaza ni mara ngapi anahitaji sex wakati mwanamke anawaza ni namna gani sex itakuwa.

Sunday, 3 April 2016

WAKATI WA MIGOGORO.

Kukiwa na mgogoro kati ya mume na mke, kawaida mke hujitahidi kufanya bonding na mumewe kwa kuongea na kuhakikisha emotions zinakuwa wazi kwa kuwa hajui tofauti ya mwanaume huamini na mume wake naye atakuwa mwepesi kuongelea kama yeye na matokeo yake mwanamke huishia kuwa na hasira na frustrated.
Jambo la msingi ni kwamba mume anatakiwa kufahamu kwamba kunapotokea mgogoro au kupishana lugha ni jambo la maana sana kumsikiliza mke au kuhakikisha mnaongea na unampa mke muda na wakati wa kutosha kuongea yote aliyonayo (kutoa emotions zake hata kama atalia machozi ila hakikisha analia akiwa mwilini mwako) na kwa njia hiyo anajiona unamjali kuliko kumwambia tusiongee sasa au tutaongea baadae au kukwepa au ku-ignore maana hapo ataumia zaidi na kuona humjali, hapendwi na upo harsh.
Pia mke naye asikasirike pale anapoona mume anakwepa kuongelea tatizo au mgogoro uliopo kwani wanaume ndivyo walivyo (tofauti zilizopo kwani wanaume huamini kwa kuacha kuongelea ndiyo njia nzuri ya kumaliza mgogoro) hivyo wewe mke mpe muda na akitulia mnaweza kuongea zaidi.

KUOMBA MSAMAHA.

Wanawake wengi akisema samahani ni njia mojawapo ya kujiunganisha (connect) na Mume au mtu mwingine kama kuna mgogoro au tatizo au kitu chochote anaona hakipo sawa, anaweza kusema samahani hata upande mwingine unavyijisikia vibaya.

Kwa mwanaume kusema samahani ina maana anakubali kwamba amekosa na anatakiwa kuomba msamaha.
Mwanaume anaamini kwamba kwa kusema hivyo inamuweka chini zaidi na hujiona si mwanaume wa uhakika na kwake haikubaliki haikubaliki kabisa.
Kama mume wako huwa anatoa samahani waziwazi basi umebarikiwa kwani mwingine badala ya kusema samahani yupo tayari akanunue zawadi kubwa ujue anaomba msamaha, hata hivyo kama wewe ni mwanaume kumbuka kwamba ni muhimu sana kutamka neno samahani nimekosa kwa mkeo bila kuzunguka wala kuzungusha sentensi.

Na kukitokea conflict yoyote wanawake hujisikia wana wajibu wa kuhakikisha wanafanya kitu kuondoa hiyo conflict ndiyo maana wanawake wengi wapo tayari kwenda hata kwa mtu mwingine anayemwamini kuomba ushauri.
Wakati wanaume hukwepa na anaweza kutumia muda mwingine kufanya vitu na rafiki zake na kukwepa familia ambayo huko mke wake anamsuguano naye.
Kama ni mwanaume ni vizuri kufikiri na kujiuliza upya kipi muhimu?
Familia au rafiki zako?
Familia ilikuwepo hata kabla ya kanisa na familia ni mahali ambapo kanisa huanzia hivyo ni muhimu sana kuhakikisha unamaliza conflict yoyote na kurudi nyumbani kuwa na familia.
Ukipoteza familia umepoteza vyote!

WAKUFANANA NAE KTK MAWASILIANO.

Uwezo wa kuwasiliana kati ya mke na mume ni moja ya precious commodities muhimu sana katika ndoa au mahusiano yoyote.

Wanandoa wenye uwezo mzuri wa kuwasiliana huwa na ndoa/mahusiano bora na zaidi huweza kuwa na watoto ambao nao huwa wazuri katika kuwasiliana na hatimaye kuwa candidates wazuri wa ndoa baadae.
Pia kuwa na mawasiliano mazuri husaidia mtu kuwasiliana na watu wengine na kuwa na mvuto zaidi.

Kuna usemi wa kingereza usemao
"Great communicators are people who change their approach based upon the person they are talking to"

Hii ina maana kwamba kama wewe ni mwanaume huwezi ongea the same style kwa mwanaume mwenzako na mwanamke.
Kuongea na mwanamke au mke ni tofauti na mwanaume au mume.
Hivyo kujua au kufahamu jinsi ya kuongea au kuwasiliana na mke wako au mume wako ni jambo la msingi sana ili kuwa na mahusiano mazuri.


Kumbuka mwanaume na mwanamke wapo tofauti sana kwani;
Huwaza na kufikiri tofauti,
Huongea tofauti,
Huamua tofauti na zaidi
linapokuja suala la hisia kuna tofauti kubwa sana.


Inawezekana wewe ukiwa na mume wako au mke wako huwa mnajikuta ni bubu, au ni kubishana tu au kila mmoja hamwelewi mwenzake au mwenzako akiongea unahisi haeleweki kwani anazunguka wakati anatakiwa kuwa direct to the point.

NI HISIA.

katika mji fulani mwanamke analalamika kwa kuwa mume wake anatembea na mwanamke nje (sex) hata hivyo mwanamke anashangazwa sana kwani mume wake anatembea na mwanamke ambaye ni ugly idara zote kuliko yeye mwenye mume.
"Hilo limwanamke kwanza ni overweight na sura ndo hivyo tena" analalama huyo mwanamke.
Mume akiulizwa kulikoni kutembea na mwanamke kama huyo jibu sahihi na mkato eti
“she has time for me!

Je, hujashuhudia mwanaume anaacha mke mzuri nyumbani na kwenda kutembea na mwanamke ambaye ni garbage?
Je, uzuri wa mwanamke ni sura au elimu yake au kiwango cha hisia na muda anaokupa mwanaume katika ndoa?
Naamini jibu unalijua!

Hata hivyo katika mji mwingine mwanaume (professional/mtaalamu fulani shule imakubali) analia kwani mkewe mrembo wa uhakika anatembea na kijana ambaye ni kibarua wao (sijajua ni house boy au shamba boy maana jamaa analia hata hasemi nilihisi kama ana kizunguzungu vile)
Huyu mwanamke akiulizwa vipi mbona unatembea na kibarua wenu, anajibu
“Ananifanya nijisikie vizuri na tena ananifanya nijisikia mimi ni mwanamke muhimu na wa maana”

Kwa ujumla hawa watu wanaweza kuwa na matatizo gani? na inawezekana mimi na wewe yakatufika tusipokuwa makini.


1..Hawa watu wamewaacha wapenzi wao si kwa sababu ya ubaya wa sura au uzuri wa sura bali ni zaidi ya hapo.


2..Inaonesha kuna hisia ambazo hawa wanandoa hukosa kwa mwenzake na kuamua kwenda kutafuta sehemu zingine au wamekuwa wakizipata kwa hawa watu wamekuwa na affairs nao.


3..Watu wanaotembea (sex) nao wanaonekana wapo smart sana kujua hawa wenzetu (wanandoa) wanakosa kitu gani kwenye ndoa zao.


4..Hawa wanaotembea nao wanajua jinsi ya kuwahudumia hawa wanandoa kitu wanakosa katika ndoa zao na kitu wanachokosa ni hisia na mapenzi yanayopelekea kila mmoja kuguswa na mwenzake.


5..Unaweza ku- fall in love na hisia za mtu na si mtu mwenyewe, kwa maana kwamba mtu kama ni mwanaume unakosa hisia maalumu kutoka kwa mke wake na kazini kukawa na mwanamke ambaye anajua kile anakosa na akaamua kumpa basi unaweza kufall in love naye hata kama yeye kama mwanamke huna haja naye ila feelings zina nguvu za kuweza kufanya kuwe na affair.
Mfano mume hapati muda wa kukaa na mke wake na mke kila siku yeye ni semina na kusafiri tu na huko ofisini mzee anakaa na secretary wake na wanakuwa na muda (intimate) hadi kuanza kupeana siri za maisha.
Mwanaume au mwanamke ambaye ametumbukia kwenye tatizo kama hili huweza kurudi haraka kwenye mstari kama mke wake au mume wake akaamua kubadirika kwani ukweli hakumpenda mtu nje bali alizipenda hisia za mtu wa nje.

Suala la kumpa mpenzi wako muda wa pamoja ili aridhike ni muhimu sana kumbuka wewe usipo mpa muda mwingine atampa.

Tumeona wasichana wa kazi, vijana wa kazi, mabosi na kila aina za watu wakifanya vitu vya ajabu na wale tunaowapenda hata hivyo je, sisi tumefanya jitihada gani kutosababisha wao kukosa kile ambacho tungewapa hadi wapewe na wengine?
Hili dudu linaitwa hisia achana nalo kabisa na usifanye mchezo hasa likivaa nguo zinazoitwa mapenzi, halishikiki na linaweza kuleta maafa katika jamii.

Saturday, 2 April 2016

KUPATA MCHUMBA SAHIHI...2

Haijalishi mtu unayetaka kuoana mmekutana wapi;
hata kama ni kanisani, shuleni, kwenye mkesha wa maombi, kijijini, mjini, hotelini, sokoni, kwenye daladala, barabarani, ofisini, kazini, safarini, kwenye semina au hata kama ni kwenye internet au njia yoyote ile ambayo Mungu anaweza kuitumia maana Mungu hafungwi na njia za kukutanisha watu.
Au Haijalishi ni mzungu, mwarabu, mchina, mwafrika, au awe mnene, mwembamba, mrefu kama Ngongoti, mfupi kama Zakayo,
Awe amesoma au hajasoma, awe mbena au mchaga au mhaya au mgogo au mzigua, au awe anatoka Canada, Kenya, Uganda, Nigeria au Tanzania. Pia haijalisha ktk kukutana naye umeunganishiwa na rafiki yako, au mchungaji wako, au wazazi wako au mtu wako wa karibu.
Kitu cha msingi ni wewe kuwa makini kujiuliza haya maswali matano muhimu.


1. JE, TUNAFANANA?

Ndoa ni kama jengo la nyumba na nyumba ni sharti iwe na msingi. Msingi imara huwezesha nyumba kuhimili kila aina ya janga linalotokea kama vile mvua, upepo, mafuriko, dhoruba, tetemeko la ardhi nk. Na kuna aina ya material zinazotumika kujengea msingi na hizi aina za material ndizo huelezea aina ya msingi na uimara wake.

Unaweza kujenga ndoa kwa kuvutiwa na umbo la mtu (mvuto wa nje) au urembo tu. Pia sasa hivi kuna uzuri mwingi tu na unauzwa dukani (body shops)
Unavutiwa na kipande kimoja tu cha mwili wake kama vile shingo, matiti, matako, unene, au wembamba, nywele, smile, anavyotembea, miguu, au kifua nk.
this is just physical attraction kuna siku anaweza kubadilika kuna kuugua, kuna ajali, kuna kubadilika mwili nk kwa hiyo ku-base kwenye mwonekano wa nje peke yake lisiwe jibu kwako kuona huyu mtu ananifaa.
Hapo utakuwa umejenga msingi wa nyumba kwa kutumia mabua au miti hakika nyumba ikishika moto hata majivu tunaweza tusipate.

Ndoa hujengwa ktk misingi 3 muhimu ambayo lazima mfanane au kuwa kitu kimoja. Ni muhimu kusiwe na gap kubwa sana katika mambo haya matatu,
Nayo ni Kimwili,
Kiakili na
Kiroho
(Mind, Body and Soul).
Mara ya kwanza mnapokutana wote mmoja anapata kuvutwa na mwingine kwa njia ya tofauti na huko kuvutwa kuna base kwenye mwonekano wa tabia kama vile anavyoongea, anavyotabasamu, anavyopenda na kwa hayo tu huwezi kusema biashara imeisha ananipenda au nimempenda na kukubaliana kuoana.

Unapotumia muda zaidi kuwa naye na kumjua zaidi, uhusiano unakua na unamfahamu zaidi ya ile physical attraction ambayo uliipata kwa mara ya kwanza sasa unaweza kutambua mambo anayopenda,
mawazo yake katika mambo mbalimbali ya kiroho,
kimwili na kiakili,
unaweza kujua talents zake na hobbies zake
hapa ndo inabidi uwe makini kufanya assessment kwani hapo ndo biashara yenyewe kwani ukimpenda na ku fall in love unakuwa blind halafu utaona kila kitu shwari hata watu wakikwambia kuna tatizo utakataa na kuwambia yupo sawa kabisa na bila yeye wewe maisha hayana maana, kumbuka huyo ni mchumba si mke/mume.
Unahitaji kuwa mchunguzi zaidi kuliko kupendwa. Kumbuka hapa unatafuta mchumba hajawa mke so ukiona kuna dalili au tabia ambayo ni hatari inabidi uwe makini.

Upendo wa kweli hauwezi kuwepo bila bonding ya kiroho.
Kutofautiana kiroho na kiimani ni moja ya sababu ya ndoa kuvurugika na hatimaye kuvunjika. Hivyo ni vizuri kupata data kamili kwa kuthibitisha imani yako na yake.

2. JE, UNAKUBALIANA NAYE KTK MAMBO YAKE?
Mtu ambaye kwake pesa na kazi ni namba moja yaani ni kitu cha kwanza, kwake bila hivyo hakuna maisha, yaani muda wake na akili yake ni pesa na kazi kwanza,
Then mambo ya michezo kama soka, au kushabikia tu michezo ni kitu cha pili, familia (mke au mume na watoto) ni kitu cha tatu kwake,
Na mwisho Mungu, yaani Mungu ni kitu cha ziada kwake, akiwa hana cha kufanya ndo anakumbuka mambo ya Mungu, Kama wewe ni dada ukapata kijana wa kiume wa aina hii kuendelea naye fikiria mara mbili.

Au mwanamke ambaye kwake kujiremba, kujisifia au kusifiwa na kuhudhuria sherehe (mama wa shughuli) kwake namba moja, then familia na Mungu baadae.
Kama ni kijana wa kiume binti wa aina hii fikiria mara mbili kabla hujaamua.

Kama ninyi ni Christians kitu cha kwanza ni kila mmoja kuwa na uhusiano na Mungu wake kwanza then familia yaani mke/mume na mtoto then kazi hii ni pamoja na kazi ya Mungu.
Hivi unaweza kwenda kuimba kwaya wakati mke au mume yupo kitandani anaumwa na hakuna mtu mwingine? Mlio kwenye ndoa tusaidie hapo!.....

ITAENDELEA....

KUPATA MCHUMBA SAHIHI.

"Apataye Mke Apata Kitu Chema; Naye Ajipatia Kibali Kwa Bwana"
(Mithali 18:22)

Moja ya mambo ya msingi ambayo kila kijana anahitaji ni Ndoa ya Kudumu ukiacha ongezeko la kufeli kwa ndoa nyingi.

Wakati huohuo moja ya uamuzi (wa maana sana katika maisha ya binadamu ni kuamua nani atakuwa mume wako au mke wako na huu uamuzi ndiyo utakufanya uweze kuishi maisha ya namna gani katika ndoa yako na pia kuathiri kabisa mfumo wa maisha yako kuwa raha au kuwa karaha

Watu wengi katika maisha wamekuwa wakilaumu upande mwingine iwe mke wake au mume wake kwamba ndiye sababu ya kuvunjika kwa uhusiano au ndoa yao.
Huu ni ujinga muhusika mara nyingi ni wewe kwani asilimia 99 ni jinsi ulivyompata huyo mtu ambaye amesababisha ndoa yako au uhusiano kuvunjika.

Mtu anayestahili kupewa lawama zote ni wewe.

Kama hujaolewa au ndio upo kwenye process za kuolewa au kuoa,Fahamu kwamba hakuna jambo muhimu maishani mwako kama huo uamuzi unaotaka kufanya, unaweza kukupa furaha ya maisha au uchungu wa maisha hapa duniani.

Unahitaji kutumia
akili zako zote,
maombi yako yote,
uwezo wako wote na
kila resource ulizonazo
kwani hapa makosa hayana nafasi kabisa

Wala usikubali kumuoa huyo binti au kuolewa na huyo kaka eti kwa sababu:

Watu wanasema Mbona hujaolewa au kuoa!
Au ndugu zako, au mchungaji, au wazazi wako au rafiki zako wamekwambia!
Au kwa sababu umeona muda unakwenda!

Amua mwenyewe na jichunguze kama upo tayari na kama mtu unayetaka kuwa naye anakupa uhakika unaoridhika nao wewe mwenyewe.

Kumbuka it is easy to reshape the mountain siyo mtu, kwa hiyo kama kuna tabia fulani ambayo unaiona kwa mtu unayetaka kuoana naye na hujaridhika nayo Please fikiri zaidi ya mara mbili.
Na kama unaweza give time au fikiri mara nyingi zaidi.

Mara nyingi wanaosema watawabadilisha matokeo yake wao ndo wamebadishwa

Hapa huhitaji kuwa blind kwa sababu ya fall in loves, bado unahitaji kuwa na akili timamu kumfahamu zaidi huyo unataka kuoana naye kabla love haijawafanya kuwa blind au otherwise muwe blind maisha yenu yote.

Kuna maswali matano (5) ya msingi sana kujiuliza kabla hujajikamatisha vizuri kwenye hii kamba ya ndoa.

ITAENDELEA..

Friday, 1 April 2016

UKILITAJA JINA LAKE ATAJISIKIA RAHA ZAIDI.

Tendo la ndoa ni sanaa kama sanaa zingine na hakuna mtu anaweza kukufundisha kwamba unapotaka kuwa mwili mmoja na mke wako au mume wako kitu cha kufanya ni hivi na hivi kwani kila mwanamke ni tofauti na hata huyo mwanamke mmoja anatofautiana kwa siku kadhaa katika mwezi mmoja kutokana na mzunguko wake.
Hivyo jambo la msingi ni mwanaume kuwa na skills za kutosha kuhakikisha unamsoma vizuri mke wako na kujua mambo ya msingi kuzingatia wakati wa tendo hili takatifu na lililobarikiwa.
Kwa mfano:
Kwanza kabla ya mambo yote ni jambo la msingi sana wewe mwanaume kuwa clean na umeoga vizuri na unanukia version nzuri inayovutia, hii itasaidia yeye kuwa na focus zaidi kwa sex kuliko harufu ya ajabu ambayo inatoka kwako, hapa haijalishi una sexual skills au sexual techniques za juu kiasi gani kwani kuwa mchafu na harufu chafu ya mwili ni total turn off.
Pia ni muhimu sana kuwa na mouthwash ambayo inaweza kuua wadudu ambao wanaweza kusababisha ukawa na harufu mbaya sana mdomoni kwani kuwa na clean and fresh breath ni muhimu sana hasa suala la kubusiana.

jambo lingine muhimu ambalo kila mmoja hufahamu na kulipenda ingawa wakati wa foreplay au sexual act husahauliwa ni kukumbuka kumnong’oneza jina lake ukirudiarudia ikiendana sambamba na unavyopumua na huku ukimbusu shingo yake na sehemu zingine ambazo zinamsisimua.
Utafiti unaonesha kwamba kila mtu (binadamu) hupenda kusikia jina lake na wanawake hawana exception kwenye hili.
Unapomnong’oneza jina lake huonesha kwamba upo focused kwake na unamfikiria kuhusu yeye na kile mnafanya na inaweza kuwapa connection (emotionally) na matokeo yeye atajifungua zaidi sexually kiasi ambacho wewe mwenyewe utashangazwa.

TAHADHALI.
Ole wako utaje jina ambalo si lake!

Jambo lingine la msingi ni kwamba foreplay ambayo haihusishi kuchezea matiti na kuchezea sehemu ya siri hujenga njaa na kutamani kuchezewa hayo maeneo kitu ambacho kitamfanya baadae ukigusa huko apate raha zaidi.
Hivyo focus sehemu zingine kwanza na matiti na uke viwe ni sehemu ya mwisho kwa foreplay.

Mwisho haijalishi anafurahia kiasi gani utaalamu wako na ufundi wako jambo lingine muhimu ni kuhakikisha kunakuwa hakuna routine na inabidi ubadilishe mambo mara kwa mara, chumba kilekile, kitanda kilekile, mwelekeo uleule, saa ile ile, mwanga au giza lilelile, muziki uleule, mlalo uleule huwa inasumbua baada ya muda na inaweza kuzima kabisa moto wake kitandani.