Thursday, 14 January 2016

WANAPENDA MUWE HIVI KITANDANI..

Kila mwanamke huwa na ndoto za kufanikiwa maisha;
kuwa na familia, kuwa na mume ambaye atampenda maisha yake yote nk.
Ni hakika wanawake ni tofauti na wanaume, inawezekana hilo umelijua, kuna mambo ambayo wanaume hufanya kitandani na kumfanya mwanamke ajione ni mwenye furaha duniani na pia kuna wakati kuna mambo yanafanywa na wanaume kitandani na hupelekea mwanamke kujuta na kuumizwa hisia zake.

Mambo yafuatayo ni muhimu sana kuzingatiwa na mwanaume akiwa chumbani kwani wanawake wengi wanakiri kwamba mambo madogo kama haya wakati mwingine huwafanya kujisikia vibaya hasa linapokuja suala la mahaba.

1.USAFI
Kuwa msafi ni msingi wa mambo yote kitandani, ni vizuri kuoga kabla ya kulala hata kama kuna matatizo ya maji lazima uweke bajeti yako vizuri kuhakikisha unaoga kabla ya kurukia kitandani.
Usafi ni pamoja na sehemu zote za mwili wako, mikono safi na kucha zilizopunguzwa vizuri, pia kunyoa ndevu vizuri, kuna wakati kidevu kikigusa mwili wa mwanamke humkwaruza na kumuumiza, labda uwe na mke anayependa kidevu kama kile cha Osama.
Pia wapo wanaume ambao huvuta sigara na bila kuwa makini huingia chumbani na harufu ya sigara huku midomo inanuka, hapo unaharibu kila kitu.

2.KUWEPO
Ni vizuri kuwepo kwenye tendo lenyewe na mhusika mwenyewe kiroho, kimwili na kiakili, kama upo kwenye tendo la ndoa mwanamke hujisikia vizuri kwa kuwa utashirikiana na mwanamke kwa kila hatua na atajiona ni sehemu ya utendaji.
Tamka jina lake, tamka maneno mazuri na kuonekana upo na yeye isiwe kama vile wewe upo na mashine fulani ya kukupa raha.
Pia wapo ambao anaanza then anaacha (anajibrekisha), mwanamke ni tofauti na mwanaume hivyo basi kama utaacha ujue lazima ukaanze upya.
Pia wapo wanaume wanajua kabisa mwanamke ni umbo dogo na yeye mwanaume ni umbo kubwa, sasa ukimlalia na kuendelea na shughuli bila kujua hapo chini anaendeleaje si anaweza akashindwa hata kupumua, wewe kuwepo ni pamoja na kujua na kumsoma anauonaje muziki wenyewe.

3.MAANDALIZI HUANZA TANGU NGUO ZIMEVALIWA.
Mwanaume unahitaji kuanza kumuandaa mwanamke tangu mapema (kisaokolojia) tangu asubuhi mnaamka, mchana kwa kuwasiliana, jioni kwa kuwa pamoja, then chumbani ni mahali ambapo mnamalizia mission ya siku nzima tena kwa kila mmoja kumvua mwenzake nguo.
Kuna raha mtu kubaki na nguo za ndani tu, na pia kuna raha kuwa naked, kila kitu kina raha yake.

4.KUFANYA VILEVILE NA KUACHANA NA SEHEMU ZINGINE ZA MWILI WAKE
Uwe makini kuangukia kwenye utaratibu wa ratiba ya kila siku kitu kilekile wimbo uleule, mziki ule ule na mwimbaji yuleyule.
Una mbusu, unachezea matiti then penetration, huna time hadi chumbani?
Ukifanya hivi kwa kuzoea basi mwanamke atajisikia bored.
Unahitaji kuwa mbunifu na mtundu kujua sehemu zingine ambazo anaweza kusisimka na ukampa utamu mpya wa tofauti.
Even an old dog can learn new tricks.
Na kuna wengine hata kukiss hakuna kila siku yeye ni kurukia tu.

5.KUWA BUBU
Hata kama wewe ni bubu naturally linapokuja suala la mahaba unahitaji kuongea lugha unayoijua wewe ambayo itaonesha unampa appreciation kwa juhudi ambayo mke wako anafanya wakati wa tendo la ndoa.
Kama anakuuliza au anakuomba uwe unaongea ni vizuri sana ukawa unaongea wakati wa mahaba kwani kuna raha yake na utamu wake.

Kumbuka kwamba mwanamke kuathirika sana na maneno ambayo mwanaume anaongea ndiyo maana linapokuja suala la kudanganywa wanawake wengi (si wote) ni rahisi sana, hivyo basi mwanaume anayeongea wakati wa mahaba ana raha yake kwa mwanamke.
Ila uwe na kiasi usiwe unaongea tu kama radio.
Pia kuna wanawake huwa wanapenda kusikia dirty words na wengine hawapendi kabisa so uwe makini na mke wako kama anapenda mpe na kama hapendi achana kabisa.

6.KUCHEZA RAFU
Uwe mstaarabu kwani tendo la ndoa si vita.
Hakuna mwanamke anapenda matiti yake yachezewe ovyo kwa kunyumbuliwa huko na huko kama vile unataka kuyanyofoa, pia chuchu zisibonyezwe kama vile unafungua radio,so ubonyeza tu hadi radio ikome, fanya taraatibu, pia hata kama anakuruhusu upeleke mkono wako hapo chini basi fanya kila kitu kwa uangalifu ili usimuumize.
Kama unafanya vizuri utajua na kama anahitaji mgandamizo zaidi (pressure) atakwambia hata kama ni aina ya mwanamke anayependa rough sex atakwambia tu, kwani mambo ya sex ni ya ajabu sana na yana vituko vya kila aina.
Hujasikia watu wanatukana matusi mazito wakifika kileleni?
Pia wapo ambao hufanya kama vile wapo kwenye mbio za Olympic na kujaza kama vile kuna mashindano ya hydraulic mashines.
Fanya kwa taratibu na wote mtapata utamu zaidi.

7.KUMALIZA MAPEMA
Kama ni mwanaume ambaye unamaliza mapema ni muhimu kuchukua tahadhari na kujifunza jinsi ya kuchelewa kumaliza mapema kwani mara nyingi mwanaume akimaliza mapema mwanamke hukatizwa utamu na anakuwa hana jinsi.
Ni vizuri kutumia utundu wako kumfikisha kileleni yeye kwanza kabla yako.

8.KUCHELEWA KUMALIZA
Wapo wanaume ambao hubaki wamedinda masaa na wakati huohuo mke amesharidhika, kitu ambacho hupelekea mchezo mzima kuwa gwaride na mwanamke humalizwa energy na kuanza kutokuwa na hamu ya tendo kila akikumbuka urefu wa gwaride alilopewa.
Ni vizuri kuwa makini kusoma saikolojia na mwendo wa tendo lenyewe ili kujua gia unayotakiwa kuweka ili kufika pamoja katika kituo cha basi kinachotakiwa.

8.KUTOKUSHUKURU
Mwanamke anahitaji kupewa credits kwa kazi aliyofanya, unahitaji kumshukuru, sema asante kwa hudumu yake na ili uwe mwanzo wa huduma nyingine bora zaidi.
Hujasikia tendo la ndoa ni dawa, na kama ni dawa maana yake amekupa tiba ndiyo maana hata ukiwa kazini unachangamka kwa sababu unapata kitu kizuri kwa mke wako, hivyo anastahili kupewa asante.

No comments:

Post a Comment