Saturday, 30 January 2016

KABLA NA BAADA YA NDOA.

Inawezekana baada ya kuishi katika mahusiano ya uchumba sasa umeoa au kuolewa, Karibu sana kwenye chama kubwa, chama la ndoa, ulimwengu mpya kabisa, ambako mapenzi huchukua sura mpya ya uhalisia.
Sasa kila kile uliona si tatizo kwa mchumba wako unajikuta kinakuudhi, namna anavyotafuna chakula sasa inaudhi, namna anaweka muziki katika sauti ya juu sasa inaudhi, namna anaacha nywele kwenye sink bafuni sasa inaudhi, namna anaacha taulo lenye maji bila kulitundika ukutani inaudhi.
Namna anaacha kitanda bila kutandika inaudhi, namna anavyokoroma akilala usiku sasa inaudhi, namna anavyoacha drawer za makabati bila kuzifunga inaudhi sana, namna anavyoacha kuweka nguo na makoti kwenye hanger sasa inaudhi mno, namna anavyoongea bila break sasa inakuudhi sana.

Kumbuka wakati wa uchumba hivi vitu uliviona vidogo sana na kwamba hakuna tatizo!

Swali la kujiuliza je, nini kimetokea kwa ule upendo?

Ilikuwa ni illusions kukusababisha ujipeleke mwenyewe hadi kusaini mkataba wa ndoa na kukiri kwamba hadi kifo, katika raha na shida, katika afya na ugonjwa na inawezekana wewe ni mmoja ya wale ambao wanalaani sana ndoa walizonazo kwani wale ambao kwanza waliwaambia NAKUPENDA NA NITAKUPENDA wamewadanganya na sasa unajikuta upo kwenye ndoa ambayo kila siku hali ni mbaya.
Una haki ya kukasirika kwani ni kweli ulidanganywa na tatizo lilikuwa ulipokea information ambazo hazikuwa sahihi. Na hizo information zilikuwa ni ile hali ya kupendana (fall in love) ambayo katika ukweli si upendo wa kweli bali ni illusions.
Kale kakichaa ka kuamini kwamba tutapendana milele bila kuumizana wala kukwazana kangedumu na kuwa hivyo siku zote.
Katika asili “fall in love” ni mating character ya binadamu kuhakikisha mke na mume wanavutiana ili kuhakikisha species inaendelea na si upendo wa kweli.
Ulikuwa tayari kuacha kusoma kwa ajili ya mitihani ili kuwa na mpenzi wako maana yeye alikuwa muhimu mno.
Uliacha kwenda kwa rafiki zako hata ndugu zako kwa kuwa ulimpenda sana mchumba wako.
Uliacha hata kwenda kusoma au kwenda kazini ili kuhakikisha unampa mpenzi wako kile moyo wake unakipenda.

Yaani mtu akili inahama hadi unajiona wewe ni Mama Theresa kwa maana ya kutoa kila kitu ili kuonesha upendo kumbe ni illusions.
Kumdondokea mtu (fall in love) ni hali ambayo hudanganya na kumfanya mtu ajione kweli yupo katika upendo wa kweli. Huamini kwamba hakuna tatizo linaweza kuwepo kila kitu ni shwari.
Baada ya hali ya kudondokeana (in love) kuchuja (kawaida baada ya miaka 2) ndipo mtu huanza kurudi kwenye ulimwengu halisi.
Ndipo unaanza kugundua yale unayapenda na kuona kumbe ni tofauti na yeye anayoyapenda.
Unajikuta wewe unapenda sex na yeye anajisikia kuchoka na hapendi.
Unapenda kununua gari kwanza na yeye anapenda mjenge nyumba kwanza.
Unapenda kutembelea wazazi wako yeye anasema hapendi mtumie muda mwingi kwa wazazi wako.
Unapenda kwenda kuangalia match ya mpira wa miguu, anakwambia unapenda mpira kuliko yeye.
Kidogo kidogo ule moto wa mapenzi ya kwanza (fall in love) huanza kuyeyuka na kila mmoja sasa anaanza kujikita kwenye kujipenda yeye na mambo yake, kujihisi na kuwaza kivyake na sasa mnazidi kuwa watu wawili tofauti.
Bila kufahamu namna mapenzi yanapanda na kushuka mnaweza kuishia kuachana.
Hivyo ni muhimu sana kujua ilo kuhusu kupanda na kushuka kwa mapenzi.

Thursday, 28 January 2016

SEX INAVYOSUMBUA NDOA NYINGI.

Sex ni issue inayosumbua sana wanaume na wanawake katika ndoa.

Mwanamke katika ndoa huhitaji intimacy & affection ili ajihusishe na tendo la ndoa wakati mwanaume anahitaji tendo la ndoa na hana mpango na masuala ya intimacy & affections tu.


Wapo wanawake ambao piga ua wamejipangia kwamba bila kuwa karibu na mimi kimapenzi sahau kuhusu sex kwani ni kama kuutumia mwili wangu.


Ukweli unaouma ni kwamba wanaume wengi wanaotoka nje ya ndoa (cheat, chepuka) hufanya hivyo kwa sababu wananyimwa katika ndoa zao.

Mwanaume anayetoka nje mara zote ndiye anayebeba lawama na dhambi.

Yeye ndiye victim wa tatizo zima hata kama mke wake alihusika katika kutengeneza mazingira ya mwanaume kuchepuka.


Mwanamke huhitaji love ili kujisikia vizuri emotionally na mwanaume naye huhitaji respect kwa mke kutii hitaji lake la mwili (sex) ili kujisikia yupo mke anamtii.


Wapo wanaume ambao kwa kunyimwa hitaji lao la msingi la tendo la ndoa ndani ya ndoa zao huwa hawaoni shida au tatizo kupoteza familia, uongozi, hadhi (reputation), uhusiano na Mungu wake au kuaminiwa na jamii kwa kwenda kutimiziwa na mwanamke mwingine nje ya ndoa.

Inaweza kuwa bado hujanielewa naongea kitu gani hata hivyo umeshaona wanaume wanatoka na kuacha wake zao wazuri na kwenda kutembea na wanawake ovyo ambao kila mtu hushangaa na ni wanaume wazito na wanaoheshimika kwenye jamii.

Ukweli ni kwamba hitaji la tendo la ndoa kwa mwanaume ni kubwa kuliko unavyofikiria.


Inawezekana wewe ni mwanamke ambae mume wako ni mtumishi wa Mungu au mume wako ana cheo au wadhifa au anapenda sana familia na kwa kuwa siku za karibuni umeoana hakutumizii hitaji lako la kupendwa basi na wewe umeamua kumnyima tendo la ndoa hadi abadilike ndipo na wewe umpe mwili wako kwani una amini kwa namna alivyo hawezi kutoka!

Unajidanganya!

Hujasikia watumishi wa Mungu ambao wameanguka?

Hata kama huna mood kinakushinda nini kutumia dakika tano tu kumpa hitaji lake na awe happy na wewe all the time?


Katika kushauriana na wanawake wengi ambao waume zao hutoka nje wengi huruka na kukiri kwamba wanaume zao ni tamaa na shetani ndo amewatuma kufanya vitu kama hivyo hata hivyo mwanamke mmoja alikiri kwamba ni kweli anajisikia vibaya sana kwamba alihusika katika kusababisha mume wake kutoka nje kwani yeye alikuwa anajihusisha sana na watoto wake na kazi na hakupenda kabisa kumpa sex mume wake kwa muda mrefu.


Mume mmoja alilalamika kwamba:

“Ni kweli simlaumu mke wangu kwa mimi kutoka nje ila hawezi kutoka msafi katika hili kwani alinifanya kujiona mimi ni failure wa kila kitu nyumbani mwetu na sikuruhusiwa hata kumgusa miezi na miezi.

Kama angenitii na kunipa hitaji langu la sex basi nisingetoka kwani mwanamke niliyetembea naye alinifanya nikajisikia vizuri muda wote na kila alivyozidi kuniambia mimi ni mwanaume mzuri nilizidi kuwa karibu na huyo mwanamke na sikuwa na lengo la sex ila kutokana na respect aliyonipa ilifika mahali nikaamua kutembea naye hata kama sura na umbo lake ni kama sokwe"


Mwanaume anahitaji sexual release kama mwanamke anavyohitaji emotional release.

Bila tendo la ndoa mwanaume hujiona hujamtii au kumpa respect na moja kwa moja huanza kuwa na tabia zisizo za upendo kwa mwanamke.

Wanawake wengi huwa na ndoto za kuhakikisha baada ya kuolewa mahitaji yao ya emotions yanatimizwa na waume zao hata hivyo wao wenyewe hujisahau kuwapa waume zao mahitaji yao ya tendo la ndoa na automatically inakuwa ngumu kwa mwanamke mwenyewe kutimiziwa mahitaji yake ya emotions.


Namna mwanaume aliumbwa ni tofauti na mwanamke ndiyo sababu mwanaume anapenda tendo la ndoa na linampa satisfactions ambazo humfanya kukumchangamkia na kuchakarika kuhakikisha na yeye anamtimizia aliyemtimizia.


Wewe mwanamke unapenda tendo la ndoa pale mwanaume anapokuwa karibu kimapenzi na wewe hata hivyo kwa mwanaume ni reverse gear, tendo la ndoa ndilo humfanya mwanaume kuwa karibu na mwanamke.

SECOND CHANCE..

Fikiria wewe ni mwanamke ambaye baada ya kuishi na mwanaume kwa muda unaoujua wewe na kwa sababu unazozijua wewe mwanaume hayupo tena na wewe.
Amekuacha na mtoto/watoto na baada ya kuponya majeraha ya kuondokewa au kubaki mwenyewe sasa unajiona upo katika hali ya kutafuta mwanaume anayefaa awe mume wako na ikiwezekana iwe ndoa yenye Baraka na inayokuridhisha.

Inawezakana ulifanya makosa huko nyuma ndo maana sasa upo “single mom” au inawezekana hukufanya makosa bali imetokea tu na umejikuta ni “super single mom” na unataka ujipe second chance na kwamba hupendi ufanye makosa ili kumpata mume anayefaa tena na ikiwezekana awe baba mzuri kwa watoto ambao tayari unao.

TAHADHARI.
Kumbuka hapa kuna mambo mawili wakati unaendelea na taratibu zako za kumsaka mume, kuna suala la kumpenda (fall in love) au kutimiziwa mahitaji uliyonayo (fall into needs)

Hii ina maana gani?
Inawezekana unahitaji baba mpya wa kutimiza mahitaji ya watoto wako au unahitaji mtu wa kukusaidia ili mambo ya fedha yawe sawa au unahitaji mtu wa kukupikia au unahitaji mtu wa kukufulia nguo au unahitaji mtu wa kukusaidia kulipa kodi ya nyumba au unahitaji mtu wa kukutimizia mahitaji yako ya mwili.
Kujiingiza kuolewa ukidhani ni njia bora ya kutatua matatizo uliyonayo ni kujiingiza kwenye crisis ya hali ya juu.

Kuolewa kunatakiwa kuwe na msingi wa upendo wa kweli wa kumpata mtu ambaye atakuwa mwenzi kwa upendo wa kweli ambao unavutia na kumkubali kama alivyo.

Je, ni mambo gani ya msingi kuyafuata ili kumpata mume mwema tena.

1.NENDA POLEPOLE.
Ili kumpata mwanaume anayefaa basi nenda polepole katika process zote mara tano ya ile ulifanya mara ya kwanza kwa mwanaume ulieshi naye.
Usijirushe haraka haraka kwa mwanaume wakati hujui hata jina lake la ukoo.
Pia usijiingize haraka na Kuamini yule aliekuacha atakoma kuringa kwani ndoa ni yako si yake na itachekesha sana siku ukisikia hata huyo mwanaume uliyejiingiza haraka sasa unajuta.
Nenda polepole na penda kidogokidogo, usikubali mapenzi kukufanya kuwa kipofu.

2.FUNGA KUFULI LAKO.
Ulishakuwa sexually active hadi ukawa na mtoto/watoto.
Unaweza kujikuta unaingia kupasha moto mashuka ya kulalia na usijisikie kukosa adabu au kuona ni kitu cha kawaida.
Akishakushika na kukupa kisses kwenye shavu unajiona mwili una “warm up” na unajisikia raha, usilemae utaweka rekodi mpya!
Kama ulishajua utamu wa tunda ni ngumu sana kupiga brake usilivamie tena hata hivyo kuwa na msimamo ndiyo silaha.
Mwambie wazi kabisa mchana kweupe kwamba
“Nakupenda, sitafanya sex hadi niwe nimeolewa na kama inakupa shida naomba uwe wazi maana sitabadilisha msimamo wangu hii ni kwa mwanaume yeyote anayetaka kunioa”

3.IWE SIRI.
Usiwaambie watoto/mtoto wako mapema eti umepata baba mpya au ndugu zako kwamba nimempata handsome wangu wakati hata hujui tabia yake vizuri.
Kama unaweza panga mipango yako nje ya nyumbani na huyo mtarajiwa wako na kama unaweza subiri hadi siku uone kweli una engagement ring kidoleni na matayarisho ya harusi yapo mlangoni.

4.KUBALIANA NAE WAPI MTAISHI:
Je, baada ya kuoana mtaishi kwenye nyumba yake au yako au mpya?
Je, mtakuwa mnalala kitanda kile ulikuwa unalala la jamaa yako wa zamani?
Je, mtakuwa mnalala chumba kilekile ulikuwa unalala na mzee?
Je, kama na yeye ana watoto na wewe unawatoto na watoto wa mmoja wakawa wanawaambia watoto wageni “hii siyo nyumba yenu” utajisikiaje?

5.UWE MVUMILIVU.
Kitu chochote kizuri hutumia muda zaidi na wakati mwingine husuasua hata hivyo uvumilivu hulipa.
Inaweza kuwa ngumu kuliko unavyotegemea kwani kumpata mwanaume atayaekuwa responsible kwa watoto wa mwanaume mwingine si rahisi.
Hivyo jiandae kulipa gharama na usitegemee mambo makubwa sana kwa ndoa yako mpya.

WANAUME HUKOSEA HAPA TU..

Wanaume mara nyingi hujulikana kwa kuwa wajuaji, hata kama kitu hajui basi akiwepo mwanamke huanza kuonesha anajua na ikiwezekana anaweza kuonesha kwamba yeye ni expert wa hicho kitu.

Lakini linapokuja suala la tendo la ndoa wakati mwingine mume hujikuta amekwama kwenye basic errors and omissions na kusababisha makosa makubwa kama si usumbufu kwa mke wake.

Wakati mwingine tatizo ni mazingira kwani wanaume wengi hulelewa katika mazingira ya kuhakikisha yeye anakuwa breadwinner wa familia yake na suala la mahusiano (ndoa, mapenzi) hujifunza mwenyewe.


Hebu tuangalie kwa ufupi baadhi ya makosa ambayo mara nyingi mwanaume hufanya akiwa na mke wake chumbani.


1.ANAJIFANYA ANAJUA KILE MKE WAKE ANAHITAJI CHUMBANI:

Mara nyingi mwanaume hufanya mapenzi na mke akifikiri kwamba kile anafanya basi mke atakipenda hii ni kutokana kile anajua yeye kuhusu mwanamke.

Ukweli ni kwamba kila mwanamke yupo tofauti.

Kumbuka hata mwanamke mmoja anatofautiana namna ya kusisimka kimapenzi hata kwa mwezi mmoja au miaka kadhaa katika mahusiano ya kimapenzi na mume.

Si mara zote katika mwezi au miaka yote katika ndoa basi mwanamke kila siku mkiwa chumbani ukigusa matiti yake anasisimka.


Hii ina maana kile kinachomfanya kusisimka zaidi mwanzo wa mwezi ni tofauti na katikati ya mwezi na mwisho wa mwezi hii ni kutokana na utendaji wa hormones.

Pia kile kilichokuwa kinamsisimua sana miaka 5 iliyopita kinaweza kuwa tofauti sana na mwaka huu.


2.ANAJIFANYA ANA KILA ANACHOHITAJI MKE.

Wapo wanawake ambao hataweza kufika kileleni maishani mwake, kwani ili kufika kileleni anahitaji kusuguliwa kisimi mizunguko 3,000 kwa dakika moja. Je, ni kiungo gani cha binadamu kinaweza kufanya hiyo kazi?

3.KUDHANI VILE MWANAUME UNAJISIKIA WAKATI WA TENDO LA NDOA NI SAWA NA MWANAMKE.

Anavyojisikia mwanaume na mwanamke ni tofauti kutokana na umbali wa uume kwenye uke.

Eneo linalozunguka uke huwa sensitive zaidi kuliko ndani kabisa.

Hivyo deep thrusting wakati mwingine huweza kusababisha mwanamke kusikia kizunguzungu kama si tumbo linapigwa ngumi.


4.UNADHANI UNAFAHAMU ELIMU YA MAUMBILE YA MWANAMKE.

Wanaume karibu wote wanafahamu kisimi au kinembe kipo wapo ingawa hawajui kina manufaa gani kwa mwanamke na yeye mwenye mwanaume kuhusiana na suala la tendo la ndoa.

Na bado wanaume wengi wanaamini kwamba mwanamke lazima afike kileleni kwa njia ya uke tu na si kisimi.

Kwa wanawake wengi kufika kileleni kwa njia ya kusuguliwa uke (intercourse bado ni kitendawili (utakesha).

Pia tatizo kubwa wanaume wengi hawafahamu ni namna gani kisimi kihudumiwe, namna anavyohudumiwa mwanamke mmoja inaweza kuwa si lolote kwa mwingine kwani kila mmoja ana aina yake.

Ukitaka kufahamu namna gani ahudumiwe kisimi chake, muuulize mke wako mwenyewe.


5.UNADHANI AKIWA WET MAANA YAKE AMESISIMKA.

Kuna wakati baadhi ya wanaume hujikuta kwenye mataa baada ya mke kushindwa kuwa wet.

Kuna imani potofu kwamba akiwa wet maana yake amesisimka hata hivyo wanawake hutofautiana kuna wengi huwa wet zaidi ya wengine na wengine kuwa wet si kawaida yao.

Pia kuwa wet hutofautiana kutokana na siku zake au mzunguko wake, pia stress na medication na wengine wana tatizo la hormones.

Jambo la msingi mfahamu vizuri mke wako, jambo la msingi anatakiwa kutayarishwa kabla hata hajaingia chumbani ili akiingia chumbani awe alishajiweka na kuwa tayari hapo itakuwa sahihi kwamba “wet means stimulated”


6.UNADHANI KUWA BUBU NDO KANUNI ZA MCHEZO.

Wanaume wengi hudhani kuwa kimya wakati wa tendo la ndoa ndiyo kanuni bora.

Ukweli ni kwamba unampa wakati mgumu sana mke wako kukisia kile unahitahitaji ili kuridhishwa kimapenzi.

Tuesday, 26 January 2016

KAMA UNATAKA AFURAHIE.

MWANAMKE:
Ili mwanamke afurahi tendo la ndoa:
Ni muhimu ajisikie anapendwa na mume wake, ajione yeye ni kitu cha thamani na kusifiwa na mume wake.
Ni pale anapojiona anasikilizwa na kuwa respected.
Pale kukiwa na mazingira ambayo ni romantic (ndiyo maana sex on spot au bila kuandaana na kupeana muda wa kuwa connected kimapenzi huwezekana kwenye movies na si kwenye real life) mke anahitaji kusaidiwa kazi ndogondogo kama kupika, kuosha dishes, kusafisha nyumba, watoto nk ndipo awe tayari kwa kumfanya Mr. aendeleze smile lake. Mke hupenda na hujiamini pale anapojiona ni msafi hasa kabla ya kuguswa sehemu yoyote katika mwili wake, kwake hygiene ni jambo la msingi sana ingawa wanaume wengi hujisahau as if hadi wafanyiwe sniff test.
Mwanamke ili afurahie tendo la ndoa anahitaji privacy.
Anahitaji kuhakikishiwa kwamba mlango umefungwa (locked) pia hakuna mtu anawasikiliza au kusikia heka heka za mahaba (ndiyo maana si rahisi sana mwanamke kukubali tendo la ndoa akiwa nyumbani kwa wakwe.
Mwanamke anahitaji kujiona mume anamuelewa na zaidi anapata kisses, hugs, touch, na cuddling mara kwa mara.

MWANAUME:
Mwanaume ili afurahi tendo la ndoa;
Ni pale anapojisikia kwamba mke wake anamuhitaji (needed), hiyo ni siri kubwa ambayo mwanaume hujiona anasisimka kimapenzi.
Pia mwanaume ili afurahie sex anahitaji sehemu au mahali ambapo anaweza kuhudumiwa na kwa mwanaume sehemu yoyote, eneo lolote hata tatizo kwake sex inawezekana.
Hii ina maana kama kuna mahali binadamu anaweza kwenda au kufika basi mwanaume kwake sex itawezekana.

MAMBO 3 BORA KWA MUME.

Wanawake wengi leo wapo independent na inafika mahali wanajisahau kuwajali waume zao, ni muhimu sana kwa mwanamke kuwa na taaluma yake na pia ni muhimu sana kwa mke kukumbuka kwamba mume akifurahi nyumbani kunakuwa na furaha.
Mume akifurahi nyumbani kunakuwa na furaha, mke akifurahi maisha yanakuwa ya furaha na watoto wakifurahi nyumba inakuwa na furaha pia.
Leo tuangalie mahitaji matatu ya msingi ambayo mume akiyapata basi atafurahi na nyumbani patakuwa mahali pa furaha kwa mke na watoto.
Kumbuka mwanandoa akisema ndoa yake ina furaha na inaridhisha maana yake anatimiziwa mahitaji yake ya msingi katika ndoa au mahusiano na kama haridhiki na hana furaha maana yake hatimiziwi mahitaji yake muhimu.
Je, mahitaji ya msingi ya mwanaume kwa mke wake ni yapi?
Kuna mahitaji 3 ya msingi ambayo mwanaume huhitaji kutoka kwa mke wake nayo ni

1. MWENZA.
Baada ya Adamu kuumbwa na Mungu alionekana ni mpweke hata baada ya kujichanganya na wanyama wengine; Mungu akaona haipendezi, akamuumba Hawa kwa ajili ya Adamu na akasema inapendeza.
Kwa nini mume anakuhitaji wewe mke kama mwenzi wake?
Ili uwe mtu wa kuwa naye, unayemfaa, mtu wa kucheza naye, kumbuka Adam alicheza sana na monkeys, samba, mbuni, Ng’ombe, kuku nk na vyote havikuweza kufanya ajisikia vizuri hadi Mungu alipomuumba mwanamke.

Ni muhimu sana Wake kufahamu kwamba waume zenu wanapenda kucheza na kwamba mume wako anapenda sana kucheza na wewe, kuwa na wewe, hivyo tafuta kitu chochote ambacho mume wako anakipenda, then fanya naye.
Kama humpi muda wa kuwa na wewe, kucheza na wewe basi atampata mwingine wa kuwa naye au kucheza naye, ndipo kilio huja...................
Pia jiulize kama mume wako hayupo kazini, au mahali unakofahamu yupo; je, atakuwa na nani? Wewe uliumbwa kwa ajili yake ili kuwa naye, kucheza naye na si kuwa vuvuzela!

2. TENDO LA NDOA
Sex ni neno zuri ambalo si chafu kama wengine wanavyoamini na kulitumia hata kama litatajwa kanisani; kwani Mungu aliumba sex kwa ajili ya mke na mume kufurahia uumbaji wake.
Hata hivyo linapokuja suala la sex wanaume wengi ni hitaji la pili katika mahusiano ya ndoa wakati wanawake ni hitaji namba 13 kwa kufuata umuhimu.
Mwanaume yeyote katika ndoa, hitaji la sex kwake ni msingi na bahati mbaya ni kwamba asipopata sex kwa mke wake dunia inaweza kumuuzia.
Hata hivyo nasisitiza kwamba sex nje ya ndoa huweza kumuongoza mtu kwenye kifo
Mungu aliumba hivyo:

3. HESHIMA.
Ukweli ni kwamba jambo la msingi kwa mume wako si kile unaongea kwake bali ni namna unavyongea kwake.
Inawezekana mume wako anao uwezo mkubwa sana kufanikisha maisha hata hivyo kutokana na ulivyo critical, blaming, kosa heshima na adabu kwa mumeo imekuwa ngumu sana yeye kupiga hatua.
Hitaji la kwanza la msingi kwa mwanaume yeyote ni heshima.
Kila maamuzi yanayofanyika katika ndoa yanahitaji kufanyika kwa ushirikiano wa mke na mume.
Kutoa sifa kwa mume wako ni njia ya maisha ya ndoa.
Behind every successful and great husband, there is an honouring and praising wife.
Kumbuka Baba akifurahi, nyumbani kunakuwa na upendo, furaha na amani na pia nyumbani kunakuwa mahali salama kwa kukimbilia.

MAMBO MATATU BORA KWA MKE.

Tafiti nyingi zinaonesha kwamba unapomchagua partner wa kuoana naye maana yake unachagua tatizo la kudumu nalo au raha ya kudumu nayo miaka 10, 20 au 30, 40, 50 ijayo.

Hata hivyo pamoja na hayo suala la kuwa na ndoa inayoridhisha haliji automatic ni suala la kuwekeza kujitoa na kufanyia kazi kuanzia mambo madogo madogo ambayo mwenzi wako anahitaji kutimiziwa.
Mume anapotoa maisha yake kwa mke wake maana yake ni hawi selfish na kutokuwa selfish ni jambo zuri ambalo linaweza kumfanya mke kuwa na furaha katika maisha na ndoa kwa ujumla.
Pia mume anapoishi vibaya na mke wake, hata akiomba maombi yake hayana maana, hii ina maana ili mume apate kibali cha maombi yake ni muhimu kuishi vizuri kwa kumpenda mke wake.
Je, ni mahitaji gani ya msingi kwa mke katika ndoa?

1. MAWASILIANO
Ni muhimu mno kwa mume kuamua au kuchagua kuwasiliana na mke wake, kuwasiliana na mke maana yake kumpa muda wa kuongea naye (quality time).
Pia si ustaarabu kwa mume kutumia neno “safi tu” au “fine” pale akiulizwa kuhusiana na kazi au vile anajiskia.
Fikiria mume unarudi kazini na ile kufika nyumbani mke wake anamuuliza
“vipi honey habari za kazi?”
Na mume anajibu “safi tu”
then anaendelea na ratiba zake za kusoma gazeti au kuangalia TV.
Kumbuka mwanamke hahitaji headlines au bottom lines; anahitaji full story, anahitaji habari kamili.
Ndiyo maana wanawake wengi huonekana ni the noisiest human being (vuvuzelas) kwa kuuliza maswali mengi huku wakijua mume hana hamu na kuongea, hata hivyo kwao ni kilio cha kutaka kusikilizwa, mtu wa kuwasiliana naye ambaye ni wewe mume.
Ni kweli wanaume wengi baada ya kazi na mihangaiko ya maisha kwa siku nzima anaporudi nyumbani huwa ameishiwa maneno ya kuongea hata hivyo ni muhimu sana kumpa mke angalau dakika 15 kuongea naye tu habari za kazi na maisha kwa ujumla kwani anahitaji connections kutoka kwa mume.
Mke anahitaji neno kwa neno kila kile unafikiria, mke anahitaji connections na mume wake angalau dakika thelathini kwa siku; mawasiliano kati ya mke na mume ni hitaji la msingi la mke katika ndoa.
Kuwasiliana ni feelings na wanawake wanapenda neno feelings ndiyo maana hujikuta wana-fall in love.
Kawaida wanaume wengi wakiulizwa na wake zao wanajisikiaje kutokana na kuonesha felings za kuwa kunaatizo, chakushangaza ni kwamba wanaume wengi hujibu “hawajui”. Wanaume wengi hawajui vile wanavyojisikia kwa sababu siyo watu wa hisia.

Wanaume hutoka nje ya ndoa zao, kwa sababu hao wanawake huwapa heshima hao wanaume kwa kuwapa sex.
Wanawake hutoka nje ya ndoa kwa sababu hao wanaume huwajali kwa kuwasikiliza ku-connect na hisia zao.

2. KUONGOZA
Ndoa nyingi zimeharibika kwa sababu mwanandoa mmoja anakuwa amemkalia mwenzake (dominate); kuongoza maana yake kuanzisha jambo lolote katika ndoa ili kulifanyia kazi na kuwajibika (initiate).
Wanawake katika ndoa hulalamika kwamba waume zao wanashindwa kuongoza nyumba zao matokeo yake wanawake wengi wamekuwa ni watu wa kulaumu na kulalamika.
Mke huitaji mume kuwa kiongozi katika maswala ya kiroho (maombi, kusoma neno), watoto (shule, michezo, nidhamu), mahaba (birthday, tendo la ndoa, anniversary) nk.
Pia mume anahitajika kuwa kiongozi mzuri linapokuja suala la pesa (pia ni vizuri kukumbuka kwamba maamuzi ya fedha ni mahesabu siyo hisia ambapo Mr. Bajeti hupewa kipau mbele).

3. UHAKIKA (SECURITY)
Mke anahitaji kuwa na uhakika kwamba mume wake anampenda anamjali, ni yeye peke yake na anasikilizwa.
Mke anahitaji kuwa na uhakika kwamba mume hatamuacha atakuwa na yeye siku zote.
Mke ambaye hana uhakika na upendo wa mume wake anakuwa hajiamini, anajiona hana thamani, anajiona hapendezi na anakuwa hasikii vizuri kwa kuwa kila wakati anajawa na mawazo.
Mke anahitaji kuwa na uhakika kwamba wewe mume ni mume wa mke mmoja kama alivyo yeye mke wa mume mmoja.

Monday, 25 January 2016

UNAMPENDAJE..?

Tukubaliane kwamba kuna vitu ambavyo mke au mume ukifanyiwa na mume wake au mke wake hujisikia anapendwa au kwamba mke wake au mume wake anakujali.
Wote tunapenda kupokea zawadi kutoka kwa wapenzi wetu ila kuna wengine akipokea zawadi hujisikia anapendwa zaidi na mwingine huona ni kawaida, wote tunapenda kukaa na wapenzi watu na kutumia muda pamoja (quality time) hata hivyo kuna wengine bila kukaa na kuongea na mume wake au mke wake anajisikia hapendwi hata kama amenunuliwa gari nk.

Wengine kupendwa ni kusaidiwa kazi au kufanya kazi pamoja, wengine kupendwa ni mguso (touch) bila kukumbatiwa, busu au sex kwake hajapendwa.

MFANO
Judy amezaliwa katika familia ambayo mama yake alikuwa anapika chakula kitamu sana kiasi kwamba baba yake alikuwa anamsifia mama yao kila wakati kwa huo uhodari wa kuandaa misosi ya nguvu, baada ya Judy kuolewa naye hutumia muda mwingi kuandaa chakula cha nguvu ili mume wake Jeffy afurahi kama alivyokuwa anafurahi baba yake kutokana na mapishi mazuri ya mama yake.
Hata hivyo Jeffy yeye anasema hajali sana suala la chakula kwani kwake chakula chochote sawa tu na anamshangaa sana mke wake Judy ambaye hutumia muda mwingi kupika badala ya kutumia huo muda kufanya mambo mengine.
Judy hujisikia vibaya kwa sababu pamoja na kupika chakula kitamu na cha uhakika mume wake Jeffy huwa hatoi sifa zozote wala kumtia moyo na badala yake anakatishwa tamaa na kujiona hapendwi.
Jeffy naye anaona mke wake hana heshima kwa kuwa anapenda kupika tu na hilo haligusi moyo wake na kujiona kweli ana mke anayemjali.
Tatizo ni kwamba Judy hajaolewa na baba yake bali ameolewa na Jeffy, linapokuja suala la kupendwa kwa mume wake misosi haina maana yoyote bali kukumbatiana, kupeana busu na kukaa chumbani na kufurahia raha ya kuwa mke na mume.
Jerrt anakiri kwamba mke wake anapokuwa active kimapenzi na kuwa karibu kimapenzi hujisikia anapendwa na mke wake kuliko suala la chakula kitamu.
***
Jacqueline na Jackson sasa ni miaka 35 kwenye ndoa yao; Jacqueline anajisikia afadhari kuachana na Jackson kwa kuwa hakuna jipya kwani moto wa mapenzi katika ndoa umezima kabisa.
Jacqueline anakiri wazi kwamba yeye na mume wake hawana tatizo lolote la kifedha wala hakuna siku wamejikuta wanagombana hata hivyo anajisikia hakuna upendo wowote kutoka kwa mume wake.
Jackson alipoulizwa unafanya kitu gani kuhakikisha mke wako Jacqueline anafurahi na kujisikia anapendwa.
Jackson alieleza kwa mshangao kwamba hamuelewi mke wake anataka kitu gani kwani amejitahidi kufanya kila kitu ambacho mwanaume anaweza kufanya ili mke ajisikie happy lakini mke anaendelea kulalamika kwamba anajisikia hapendwi.
Jackson anasema anajitahidi kuhakikisha anapika chakula cha usiku (dinner) mara 4 kwa wiki, siku mbili zinazobaki wanaenda out na rafiki zao, anaosha dishes hizo siku nne kwa wiki, anasafisha nyumba kila siku kwani mke wake analalamika kwamba mgongo unamatatizo, anajitahidi kusafisha mazingira nje ya nyumba na pia kufua nguo na kuzinyosha nk
Unaweza kujiuliza sasa huyu mwanamke analalamika kitu gani kama mwanaume anaweza kujishusha na kufanya hayo yote na bado mwanamke anaendelea kulalamika.
Jacqueline alipiulizwa je, ulitaka mume wako afanye kitu gani ili ujisikie unapendwa akajibu kwamba angefurahi kama ingetokea siku moja mume wake akaketi kwenye kochi na yeye na wakakaa na kuanza kuongea pamoja, kusikilizwa huku wakiongea mambo mbalimbali yanayohusu ndoa na maisha yao hapo Jacqueline angejisikia kupendwa kwani kila wakati mume wake ni kuzunguka huko na huko mara kupika mara kusafisha nyumba mara nje yaani yeye na kazi tuu na mke hana nafasi.
Jacqueline anasema anachotaka ni mume wake kukaa chini na yeye angalau dakika 20 kwa siku, waangaliane usoni, waongee mambo yanayowahusu wao na maisha kwa ujumla, huko ndo Jacqueline anaona ni kupendwa (quality time)
Hii ina maana kwamba kwa Jackson kubwa busy hata kama ni kumsaidia kazi mke wake bado hakuweza kutimiza hitaji la emotions kwa mke wake.
Bado love tank la mke wake lilikuwa empty na kujazwa ni pale wakiwa pamoja, kukaa pamoja, kuongea pamoja.
Sasa Jackson anakiri kwamba kwa miaka yote 35 alikuwa hajajua kwa nini mke wake alikuwa analalamika kwamba hawaongei, anakiri aliamini akimuuliza mke wake umeamkaje basi huko ndo kuongea, hakujua kuongea ni kukaa chini, kutazamana na kuongea na mmoja akisikiliza kwa dakika 20 au 30 na ndicho mke wake alikihitaji.
Mara nyingi wanaume tunapoona nyumbani kuna chakula, kuna fedha kuna kila kitu tunaamini basi mke atakuwa ameridhika kihisia kitu ambacho si kweli kwani kila mwanamke ana aina yake hasa ambayo kwake ni kupendwa.

ANAJUA NINI ANAFANYA

Mara nyingi siyo (mara chache) mume au mke hujikuta mwenzake ni msumbufu kwa kuuliza maswali ambayo hayana msingi kwa kuwa kinachoulizwa ni kile ambacho mume au mke huwa anafahamu namna ya kukifanya.
Nahisi bado hujanielewa naongea kitu gani labda nikupe mfano.
Siku moja Judy na mume wake Jerry waliamua kwenda kuwatembelea wazazi wa Jerry ambao wapo nje kidogo ya mji wanaoishi.
Hata hivyo baada ya kufika nyumbani kwa wazazi wao wakaambiwa kwamba wazazi wao nao walipanga kwenda kutembelea shamba.
Wote kwa pamoja yani Judy, Jerry, mama yake Jerry na baba yake Jerry wakapanda gari moja na kuanza safari ya kuelekea shamba.
Judy alikaa kiti cha mbele na baba yake Jerry (mkwe) ambaye ndo alikuwa dereva na Jerry alikaa kiti cha nyumba pamoja na mama yake.
Baada ya kusafiri kwa muda fulani Jerry akahisi baba yake anaenda au kuelekea njia ambayo si yenyewe hivyo akamnong’oneza mama yake kwamba baba yake anaenda njia ambayo si yenyewe
(aliamini kwa kumwambia mama yake basi mama yake ataropoka maneno yasiyopimika kumsema baba yake kwa kitendo cha kuendesha gari kwenda njia ambayo si sahihi).
Cha ajabu mama yake akamjibu Jerry kwamba “Baba yako anajua anachokifanya” kitu ambacho kilimfanya Jerry ajiulize kwani angekuwa ni yeye anayepotea na kuelekea mahali siko mke wake angemsema kwa fujo kama kawekewa vuvuzela mdomoni.
Ni kweli baba alipotea njia hata hivyo baada ya muda akakumbuka kwamba amekosea hivyo akageuza gari na kuelekea kule ambako ni sahihi.
(alikuwa anajua anachokifanya)
Walipofika shamba baba yake aliiweka kofia yake juu ya kiti na baada ya muda akaamua kukaa na akawa kasahau kwamba anaikalia kofia na kuikunja kunja; ndipo Jerry akamwambia mama yake
“Unamuona baba anakalia kofia na kuikunja si mwambie anakalia kofia yake?”
mama yake akamjibu Jerry kwamba
“ Baba yako anajua kile anakifanya”
jibu ambalo pia lilimfanya Jerry afikirie upya kuhusiana na mahusiano yake na mke wake hasa suala la kukosoana vitu vidogo vidogo kama hivi.
Inawezekana umemwambia mume wako anatakiwa kupaka rangi nyumba na kila siku unarudiarudia kumsema ukiamini kwa kumpigia kelele basi ataanya kile unasema, Mumeo anajua kile anakifanya ndiyo maana pamoja na kumsema nyumba bado haijapakwa rangi!
Inawezekana kila siku unamwambia mke wako anatakiwa kuhakikisha drawer za makabati zinafungwa kila akifungua hata hivyo kila siku unazikuta zipo wazi, ukweli ni kwamba mke wako anajua kile anakifanya.
Ni kweli inawezekana umeshamwambia mpenzi wako akufanyie kitu Fulani na ni muda sasa umepita na bado hajatimiza au hajafanya, umeamua kumsema kila siku ili afanye au kutimiza ahadi yake, hata hivyo ukweli ni kwamba yeye ni mtu mzima na anajua kila anakifanya.
Kumbuka kuwa kwenye ndoa ni kuwa mtu mzima na mtu mzima hapigiwi kelele kama mtoto kwani kila mtu mzima anajua anachokifanya na hakuna kitu mwanaume hapendi kama mwanamke ambaye kila wakati ni kukosoa na kusema sema tu na kumuweka kundi moja na watoto;
Ukweli ni kwamba mume wako anajua anachokifanya pia mke wako anajua anachokifanya.
Wengi tumegundua hii siri hatupigishani kelele kwani nikimwambia mke wangu leo nitaosha dishes zote au nitakusaidia kufua nguo hana haja ya kuniliuza au kunikazania utafanya saa ngapi hiyo kazi badala yake anatakiwa kurelax na kuenjoy maisha kwani mume wake ninajua ninachokifanya na ninafahamu nitafanya wakati gani.
Usiumize kichwa chako, anajua anachofanya!

UMEWAHI KUSIKIA HII?

Kuna jambo moja ambalo watu wengi hulichukulia mzaha, masihara au utani wakati wa kutafuta mwenzi wa maisha (mke au mume) nalo ni suala la mtoto wa kwanza kuzaliwa na mtoto wa mwisho kuzaliwa.

Swali la kujiuliza je, kuna matokeo yoyote au athari zozote kuoa au kuolewa na mtoto wa mwisho au kwanza kuzaliwa katika familia yao?

Jibu ni NDIYO KUBWA,
Kuna athari kubwa kama ni kweli unayeoana naye ni mtu wa kwanza au wa mwisho kuzaliwa ingawa kuna exceptions.
Kama una mchumba ambaye kwao ni mtoto wa mwisho kuzaliwa jambo la msingi ambalo naweza kukushauri ni wewe kuwa tayari for adventures, na kama ni mtoto wa kwanza kuzaliwa basi jiandae kuwa audited kila kitu au kukaliwa au kuongozwa bila kujali ni mwanaume au mwanamke period.
Mtoto wa kwanza kuzaliwa kawaida hujikuta ni kiongozi mahali popote na hupenda kuongoza, kupenda kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri na kama kilivyopangwa maana ndivyo alikuwa anaagizwa na wazazi kwake kuhakikisha wadogo zake wanatii kile ameagizwa;
“Hakikisha wadogo zako wamekula, wametandika kitanda, waosha vyombo, wamefagia uwanja, wamelala mapema nk”.
Mtoto wa mwisho kuzaliwa hujikuta ni mtoto hata akiwa mtu mzima kwa kuwa kwao bado ni mtoto na huwa hana shida na kitu chochote kwani kwake kila kitu ni rahisi na anapenda raha, sherehe na life is easy.
Kila kitu nyumbani kilikuwa ni kwa ajili yake kwa kuwa yeye ndiye mtoto hata baada ya kuwa mtu mzima bado anajiona ni mtoto Ndiyo maana huchelewa hata kuongea, kufanya vitu mwenyewe kama vile kujua muda wa kula, sehemu ya kuweka nguo, kutandika kitanda, kuoga nk, yeye hujiona ni special kid, ni mtoto wa baba na mama na amekua wakati wazazi wamezoea maisha.
Kwa ujumla tabia za watoto wa kwanza kuzaliwa huwa ni kukaliwa wenzao (controlling, bossy, leading, perfectionist, auditors, no fun, firm and rigid) wengi ni viongozi na watoto wa mwisho kuzaliwa hujiona ni special kid, hujiona mtoto miaka yote, watu wa sherehe, don’t care, easy wengi ni comedians.

Je, inakuwaje wakioana mtoto wa kwanza na mtoto wa mwisho kuzaliwa?
Kama mmoja ni wa kwanza kuzaliwa na mwingine ni wa mwisho kuzaliwa (au mmoja ana tabia ya mtoto wa kwanza kuzaliwa na mwingine tabia ya mtoto wa mwisho kuzaliwa basi ndoa itakuwa nzuri kwani tabia zitawafanya wa-balance.
Uzembe wa mtoto wa mwisho utakomeshwa na mtoto wa kwanza kuzaliwa ambaye hupenda kuongoza na kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa haijalishi ni mke au mume.
Hujasikia mwanamke analalamika kwamba mume wake hakustahili kuoa au kuishi na mke, maana yake ni mtoto wa mwisho na haijalishi amesoma au hajasoma watoto wa mwisho tabia hufanana.

Je, inakuwaje wakioana wote ni watoto wa mwisho au wote watoto wa kwanza kuzaliwa?
Ukweli ni kwamba match ya ndoa ya aina hii huwa inakera sana kwani kama wote ni watoto wa kwanza kuzaliwa kila mmoja atapenda kuwa kiongozi na sidhani kama hiyo meli haitazama. Na wakikutana wote watoto wa mwisho basi ni balaa kwani ndoa itakuwa haina kiongozi na itakuwa ni adventures.
Watoto wengi wa kwanza Ndiyo marais, wachungaji na viongozi mbalimbali na watoto wengi wa mwisho ni ma-MC na comedians.

Watoto wa kwanza kuzaliwa likija suala la sex wanachagua sana na kuwa na utaratibu ambao huchosha (routine sex), pia hufanya sex kama wakaguzi kama vile lazima kuoga kabla ya sex, taa zizimwe, kusiwe na mtu hajalala usingizi within 100m, piga mswaki, usiku tu tena baada ya saa tatu na si baada ya saa nne nk, ni usumbufu.
Bila watoto wa mwisho sherehe huwa hazinogi ingawa wao tatizo lao si kawaida yao kuwahi na kufika on time kwenye sherehe, ingawa watoto wa kwanza kwao ratiba ni muhimu.
Likija suala la siasa first born wengi ni wagombea na wanapenda kuwa viongozi wakati last born ni viongozi wa kuwasemea au kushabikia first born.
Watoto wengi wa kwanza kuzaliwa ni selfish, wachoyo, hawatoi vitu kirahisi bila maelezo ya kutosha, wakati wale wa mwisho ni easy, ni rahisi, hugawa ovyo si wachoyo ni watu wa to have fun.
Kumbuka kama unaoana na mtoto wa mwisho kuzaliwa hakikisha huweki matarajio makubwa sana kwani kwake ndoa ni jambo la kawaida tu naamini wale ambao tayari mpo kwenye ndoa mnafahamu hili kwani mmmeshakutana na maajabu ya kutosha.
Pia mimi ni mmoja ya watoto wa katikati hivyo sisi ni waasi (rebels) hatutaki tabia zenu ninyi watoto wa mwisho (don’t care) na ninyi watoto wa kwanza kuzaliwa (controlling) Ndiyo maana tunajua kiboko cha mtoto wa mwisho kuzaliwa ni mtoto wa kwanza kuzaliwa ingawa mkioana na sisi watoto wa mwisho hatuna shida ndoa inaenda tu maana tunawajua sana.
Anyway ninyi watoto wa kwanza kuzaliwa ni muhimu sana kwetu maana bila ninyi ndoa zingekuwa za kizembe sana, na ninyi watoto wa mwisho ni muhimu sana maana bila nyinyi ndoa haziwi na sherehe wala “to have fun”.

Sunday, 24 January 2016

KUISHI PAMOJA KABLA YA NDOA.

Kwa nini jamii nyingi za vijana wa leo huchukua uamuzi wa kuanza kuishi pamoja kinyumba kabla ya kuoana rasmi na ndipo kuanza maisha?
Wengi hutoa sababu nyingi mojawapo ni kuokoa fedha za kutumia kwani badala ya nyumba mbili huwa nyumba moja, kutumia muda mwingi pamoja, kuwa karibu kihisia, kuzoeana kimapenzi (sexual intimate) pia ni kitu rahisi ambacho hakina gharama.
Zaidi wengi hutoa sababu kwamba wanaishi pamoja kabla ya kuoana rasmi kwa sababu wanajitahidi kuangalia namna wanafanana na kufahamiana kwa undani zaidi na kujaribu kama itawezekana kuishi pamoja na kuridhika kwamba waoane (wanaogopa kununua mbuzi kwenye gunia) kwa kuchunguzana mazingira ya masaa 24 siku 7.

Je, ni kweli wachumba kuishi pamoja kwanza hupelekea kuoana na ndoa kuwa imara baada ya kuoana?

Ukweli ni kinyume chake, tafiti nyingi zinaonesha kwamba watu ambao huamua kuishi pamoja (Cohabitation, common law, kuvutana, kuishi katika dhambi, kuchukuana nk) kwanza huongeza uwezekano wa kuachana baada ya kuoana na mara nyingi wengi hata kuoana huwa inashindikana huku kila mmoja akiwa amejeruhiwa vibaya kwa kupoteza muda wake na mali zake.
Kubwa zaidi wapo ambao hufikia hatua hata ya kuzalishana watoto na hata kabla ya kuoana huachana huku mwanamke akipelekeshwa na maisha ya kutunza watoto wakati baba anaenda kuona mke mpya.
Hii style ya kuishi pamoja kabla ya kuoana si lolote wala chochote zaidi ya kupotezeana muda na kuharibiana maisha na kuweka rekodi ambazo huwa gharama kubwa kwa maisha yote ya mtu kwamba aliwahi kuishi na mwanaume au mwanamke a hakuoana naye, unakuwa umejiwekea kibandiko (label) kwamba wewe ni moja ya failures na itaku cost kujisafisha katika ile jamii.

Kwa nini ni muhimu sana kuoana kwanza na ndipo kuishi pamoja?

Pamoja na kwamba kuoana kwanza ndiyo utaratibu wenye Baraka wa ndoa zote, kuingia kwenye ndoa si mchezo au jambo dogo bali ni agano kati ya wawili wanaoana na Mungu kwa maana hiyo lazima kuwepo kiapo (commitment) kitu ambacho hufunga wawili wanaoana kuishi maisha yao pamoja bila kujali nini kinatokea mbele “No matter what”
Kiapo ambacho unaapa kwa mwenzi wako siku ya kuona ni kukubali kuishi naye maisha yako yote yanayobaki hapa duniani na ni msingi wa ndoa na kwamba hiki kiapo ni unconditional kwamba utaishi naye hata kama ni matajiri au maskini, afya njema au ugonjwa, katika shida au raha, kuwa na watoto au kutokuwa na watoto hadi kifo kitakapowatenganisha.
Wanaochukuana au kubebana na kuanza kuishi huwa katika risk ya kuachana muda wowote kwa kuwa hakuna kiapo, hakuna ahadi hakuna commitment, hakuna furaha ya kweli, hakuna amani ya kweli kwa kuwa si utaratibu wa ndoa na ni njia nzuri ya kuachana na kuharibiana maisha na mara nyingi anayeumizwa zaidi ni mwanamke.
Jambo la msingi na la kukumbuka ni kwamba unapofahamu kwamba mwenzako yupo fully committed kwako hii husababisha ujisikie vizuri (security) na huweza kuimarisha kujisikia kitu kimoja na wewe ni mali yake na zaidi mnaimarisha ile bond ya kuzoeana na kuwa karibu kimapenzi kwa kuwa unafahamu mwenzangu amejitoa na kunikubali maisha yake yote.
Kubebana na kuchukuana na kuanza kuishi pamoja kabla ya ndoa ni njia nzuri ya kufanyia mazoezi ya kuachana.

JE,WEWE UTAKUBALI?

Fikiria wewe ni binti (au mzazi wa binti) ambaye unataka kuolewa na mwanaume ambaye hajasoma (illiterate) utakubali?

Ni kweli elimu ni kitu kizuri hata hivyo elimu si kigezo cha upendo.
Naamini kitu cha msingi kwa mahusiano yoyote ni upendo wa kweli, kujali, kufanana na kuelewana.
Ukweli binafsi nitakubali kuolewa na mwanaume illiterate kwani inawezekana ana sababu za msingi za yeye kutokwenda shule na baada ya kuoana tunaweza kushauriana ajiendeleakimasomo.
....alisema Judy

Ukweli nitaolewa na yule nimeamua na nimempenda na angalau awe ameelimika.
Sidhani kama nitaweza kukubali ombi la mwanaume yeyote kunioa wakati hana elimu yoyote na hajaelimika, je itakuwaje kwa watoto tutakao wazaa? Je anaweza kupata kazi nzuri kwa ajili ya kuleta kipato cha familia huku hajasoma?
Pia kwa kuwa mimi mwanamke nimesoma na yeye hajasoma maana yake hatufanani na kutokuwa na gap kubwa sana katika uelewa wa mambo kitu ambacho sikipendi.
......Margaret

Nimeona mfano halisi wa dada ambaye alikuwa na elimu ya kidato cha sita na akaolewa na kaka mwendesha pikipiki ambaye alikuwa hana shule na hajaelimika kwa lolote.
Baada ya dada kuolewa kilichofuata ni kulea mtoto mmoja baada ya mwingine hadi ndoto zake za kuwa lawyer zikafutika.
Pia huyu mwanaume illiterate huwa hana shukurani kwa namna yule dada anavyojitahidi kuhakikisha anaanya kila analoweza familia iwe na mkate wa kila siku na kusomesha watoto.
Sitakubali binti yangu ajiingize kwenye ujinga kama huo hata siku moja na pia nitajitahidi kuelimisha mabinti wasije ingia katika matatizo kama hayo.
.......Mrs Betty


Kama kuna upendo na kuna kufahamiana na kuelewana na kama ni kweli huyu mwanaume ana sifa ninazohitaji Ukweli nitakubali tuoane na nitaomba Mungu aniongoze.
............Julieth

Kwangu kuwa illiterate si kizuizi hasa linapokuja suala la mahusiano pale tu kukiwa na kuelewana kati yangu mimi binti na huyo mwaname na kama ana sifa zile niahitaji. Najua kuna matatizo na watu watasema sana kwa kumkubali huyo kaka ambaye hana shule kabisa hata hivyo kama kuna kujitoa na kumuomba Mungu hakuna lisilowezekana.
...........Esther

Binafsi siwezi kujiingiza kwenye jaribu la kijinga kama hilo na kuona na mwanaume ambaye hajaenda shule.
......Anne

Na Je, wewe msomaji ungekubali? Au unasemaje

WAFANYAKAZI WA NDANI..

Nimekuwa naletewa maswali ambayo yamekuwa yakinipa picha tofauti kuhusu wafanyakazi wa ndani (house maids) hasa kwa wanawake kulalamikia waume zao au ndugu zao wa kiume kutembea na wafanyakazi wao wa ndani wa kike (house girls) na pia wanaume kulalamika kwamba wake zao hutembea na wafanyakazi wao wa ndani wa kiume (house boy)
Je, ni kweli kwamba hawa wafanyakazi ni hatari kwa ndoa zetu pia kama wanandoa wanakuwa hawapo makini?
Baada ya kupita mtaani na kuwauliza baadhi ya akina mama walikuwa na haya ya kuchangia na swali lilikuwa:-
Je, Ungependa kuwa na mfanyakazi wa nyumbani mvulana( house boy) au msichana (house girl)?

MAJIBU..
Binafsi napenda mfanyakazi wa ndani ambaye ni msichana kutokana na kazi ya kutunza mtoto na pia kwa usalama kwani ni rahisi kumthibiti msichana kuliko mvulana.
Wasichana ni wazuri zaidi kwa masuala ya ndani ingawa nitakuwa makini kumbadilisha kabla hajaanza kufanya vitu vyake
Dina – Kawe Dar es Salaam
Mimi nitapenda kuwa na mfanyakazi wa ndani mvulana tena awe na umri wa miaka 13 hadi 16 kwani mvulana wa umri huu hawezi kuleta kasheshe ukilinganisha na wasichana wa siku hizi. Pia kuwa na mfanyakazi wa ndani msichana ni kama kuweka tangazo kwamba mume wako sasa amepata mke mwingine.
Leo maadili yameshuka sana na hawa mabinti ni hatari sana na wanaweza kufanyia lolote kuhakikisha ndoa yako inaweza kuwa tofauti kukiwa na hiyo nafasi.
Nimeshuhudia msichana wa kazi wa miaka 20 akisababisha mama mwenye nyumba kuachana na mume wake na yeye kuchukua usukani hivihivi. Hii ina maaa wasichana wa kazi wa leo wanahitaji usimamizi mkali sana hasa kutokuwa na nafasi ya kuingia chumbani hasa ukiwa hupo nyumbani na mume akiwa nyumbani peke yake na huyo binti.
Mama junior – Ilala Dar es Salaam

Mimi napenda kuwa na mfanyakazi wa kiume kwani wapo imara na hakuna longolongo kazi ni kazi, mabinti sana sana itakuwa ni kukuzunguka ili mume wako anaswe na hata kukuibia mali zako na wakati mwingine kiburi na hata kuhakikisha mambo yako hapo nyumbani hayaendi na kukufanya mume akuone hufai na yeye anafaa na unajua nini kitafuata....
Jane – Kimara Dar es Salam
Naona hapa inabidi kuwa makini, binafsi kama nitakuwa na msichana wa kazi jambo la msingi ni kuhakikisha umri wake si zaidi ya miaka 14 kwani ukiwa na msichana wa kazi ambaye ameshakua (mature) hapo unacheza na ndoa yako kwani wanaume hushawishika na kile wanaoana, wapo dhaifu sana wanapoona mabinti wanaojiremba siku hizi (matiti na mwili nusu uchi) na huyo house girl anaweza kumjaribu mume wako na anaweza kufanyia kile ambacho hakuwa nacho akilini.
Ukweli usipokuwa makini na haya mambo unaweza kujuta.
Pia sidhani kuna kitu kitaweza kunizuia kuwa na mfanyakazi mvulana hata hivyo lazima awe mvulana mdogo na si mwanaume mtu mzima kwani tumesikia wengine wameishia kubaka, kuwapa mimba wanafamilia wa kike na hata kuiba mali na kuondoka nazo, Ukweli hawa wanaume wanaopewa kazi za kufanyia ndani ya nyumba zetu ni hatari zaidi kuliko mabinti.
Mama Jenifer – Magomeni Dar es Salaam


Kwa ushauri wangu nitapenda kuwa na mfanyakazi wa ndani mwanaume kwa kuwa wao ni hodari na wapo rahisi kuliko wasichana.
Pia kama ni mwanamke ukisafiri huna wasiwasi kwa kuwa wanakuwa makini na kazi zao na si sawa na mabinti ambao unaondoka huku nyumba hujui mume wako itakuwaje na hao wasichana ambao siku hizi ni homa ya jiji.
Joyce mgaya – Sinza Dar es Salaam

Kwa upande wangu nitapenda kuwa na msichana chini ya miaka 11 kwani yeye ana upendo wa mama kwa watoto wangu na pia kazi za ndani kitu kimoja ambacho lazima niweke wazi ni kwamba hataruhusiwa kufua nguo za mume wangu au kwenda chumbani Kwangu na mume wangu.
Mvulana hapa kwani nina mabinti nyumbani na anaweza kuleta shughuli nzito kwa mabinti zangu na nikajuta.
Mama Yuster Kimara Dar es Salaam

Kwa upande wangu sihitaji mfanyakazi yeyote awe msichana au mvulana kwani mabinti zangu ni wakubwa sasa na pia naziweza kazi zangu zote za hapa nyumbani na hata kama ni nyingi watoto wangu hunisaidia.
Mama James Mbezi Dar es Salaam

Mimi nitatafuta mwanamke mtu mzima ambaye anaweza kufanyia kazi na atakuwa anafanya kazi na kurudi kwake, siwezi kuchukua wasichana wadogo ambao wamekua tayari kwani napenda mume wangu abaki wangu mwenyewe na si vinginevyo.
Mama Helena – Kimara Dar es Salaam
Je, wewe unasemaje

NI MUHIMU.

KWA WANAWAKE TU:
Nini cha kutarajia kutoka kwa mpenzi wako mkiwa na faragha chumbani kwenu?


1.Haijalishi ni handsome kiasi gani au msomi kiasi gani hadi anaitwa Dr. au Professor; haijalishi ni diplomat au businessman au mbunge au tajiri linapokuja suala la sex wanaume wengi (siyo wote) ni zero wa kufahamu nini kinaweza kumfanya mwanamke asisimke na kufurahia sex.

2.Usijidanganye kwamba anajua mapenzi hata kama huko nyuma aliwahi kuwa na mpenzi.
Ukiwauliza wanaume wengi kisimi (clitoris) ni kitu gani katika mwili wa mwanamke, wanakuuliza kwa mshangao “Unasema kitu gani?”

3.Usijidanganye kwamba anajua ramani ya kupita katika kukufikisha kwenye raha ya mapenzi (kileleni) kama unavyohitaji bila wewe kumwambia; Ukweli ni kwamba unahitaji kumwambia si mara moja tu bali mara kwa mara vile unapenda akufanyie ili ufurahie sex na yeye kama vile;
“Mpenzi huwa najisikia raha sana unapofanya hivi au vile”
“Nilipenda sana na kiujisikia raha sana jana ulipoanza kwa kufanya hivi ila leo ningtependa uanze hivi”
“Huwa najisikia raha unavyochezea ………………….. namna hivi”
Baada ya hapo relax na mwache aendee kukupa raha!

KWA WANAUME TU:
Nini mpenzi wako (mke wako) anahitaji kutoka kwako mkiwa faragha!

1.Usifikirie sex ni bingo, sex ni sehemu ya mahusiano na ni kitu ambacho ni ziada baada ya kuimarisha na kutimiza mambo mengine katika mahusiano hata kama ni madogo madogo lakini kwa mke wako ni mambo muhimu kama vile kumsaidia kazi, kumwambia “nakupenda” kupiga naye story mbalimbali za maisha kwa upendo, kupeana zawadi nk.


2.Jitahidi kutimiza mahitaji ya mpenzi wako kwanza ndo yaje yako kila eneo la maisha yenu ya mahusiano.

3.Fahamu kwamba mpenzi wako anahitaji mazingira ya kimapenzi romantic, kujisikia unamjali (caring), unamwamini (trust) , kiasi cha kujisikia salama (safe/protected) na si kukimbilia sex.
Baada ya hapo hayo mengine utazidishiwa na atajituma kukupa kile unahitaji.

PESA NA NDOA.

Hakuna mtu ambaye huwa anaingia kwenye Ndoa huku anajua hiyo ndoa Haitafika mbali.

Jinsi Unavyokuwa na Ufahamu mkubwa wa nini kinaweza kutokea baada ya kuoana hiyo itakuwezesha Kuzuia na Kujiandaa kukabiliana na changamoto zitakazotokea mbele ya safari ya Ndoa.
Matatizo yanayohusiana na pesa yamekuwa chanzo kikubwa cha migogoro ya ndoa nyingi. Matatizo haya huhusika moja kwa moja na jinsi ya kusimiamia na uaminifu katika pesa.
Kama hujaoa/olewa bado unaweza kukaa partner wako mkaongea masuala ya pesa na pia ukapata ufahamu wake kuhusu suala zima la pesa ili mkiingia kwenye ndoa unajua kabisa mwenzangu ni mtu wa aina gani lipokuja suala la pesa na uchumi kwa ujumla.
Na kama upo kwenye ndoa naamini umemchunguza mwenzako na kujua ana tabia ipi likja suala la pesa.
Hapa chini kuna maswali ambayo kama mwongozo tu hasa pale ynapojibiwa kwa ukweli na uaminifu ambayo inaweza kukusaidia kujua mtazamo wa mwenzako kuhusu pesa.

1. Wakati unafanya shopping huwa unafikiria kitu gani hasa?
(a) Vitu unavyonunua.
(b) Pesa unayotumia kununua hivyo vitu

2. Ikitokea mwisho wa mwezi ukapungukiwa pesa hata kama una mahitaji muhimu?
(a) Nafikiria Kukopa
(b) Sinunue kitu chochote

3. Huna Fedha (cash) na unataka kununua vitu na upo mbali na Bank yako utatoa uamuzi gani?
a) Nitatumia ATM card niliyonayo kwenye ATM machine iliyojirani
b) Sitanunua kitu kwani sipendi kutumia ATM card kwani kuna gharama za kutumia kadi

4. Huwa unajisikia una uwezo kifedha pale ikiwa?
(a) Una nunua kile kitu umekuwa unahitaji.
(b) Unapoiweka fedha kama mali (save).

5. Kwa jinsi unvyowekeza sasa na kuweka akiba.
(a) Hujui kabisa ni kiasi gani utakuwa nacho siku ukistaafu kazi.
(b) Unajua kiwango halisi cha pesa utakuwa nayo utakapostaafu kazi.

6. Unapoweka pesa bank kwa ajili ya akiba.
(a) Unajisikia ni wajibu (inaumiza kidogo)
(b) Unajisikia ni raha sana

7. Ukiwa na rafiki zako, unapoongelea masuala ya pesa huwa hukosi kutaja kipi ?
(a) Punguzo la bei uliyopata
(b) Punguzo la mali uliyonunua

8. Kama umepandishwa cheo utasherehekea vipi?
(a) Kwa kununua kitu maalumu kwa ajili yako mwenyewe
(b) Utaruka hewani na kushangilia “waoooooo”

Kama Amejibu kwa kuchagua (a) nyingi basi ni Mtumiaji mzuri wa pesa na kama amejibu kwa kuchagua (b) nyingi basi ni mweka akiba mzuri

Kama kuna tofauti kubwa yaani mmoja ni mtumiaji na mwingine anapenda kuweka akiba basi uwezekano wa kuwa na migogoro inayotokana na fedha ni kubwa, lakini haina maana kwamba itakuwa migogoro bali changamoto kamili inayokukabili mbele ya safari na unabidi ujiweke sawa jinsi ya kushughulikia Tatizo la pesa ndani ya ndoa.

Na kama partners wote ni Watumiaji; maana yake hakuna atakayekuwa na break ya kuzuia matumizi na matokeo yake mwisho wa njia kunakuwa zogo na matatizo ya fedha kwani mnatumia bila kuwake akiba.
Madeni huumiza ndoa, uwe mwangalifu.
Na kama wote ni watu wa kuweka akiba; hiyo ni nzuri ila mnahitaji wakati mwingine kufurahi kwa kutumia pesa kwa ajili ya just for fun.
Maana mnaweza kujikuta ni mabahiri wa ajabu kiasi kwamba hata raha ya kutumia pesa hakuna.
Kitu cha msingi ni kuhakikisha kila mmoja anamsoma mwenzake kujua mwenzake ana mtazamo gani kuhusu suala la pesa.
na pia kujua ni jinsi gani mnaweza kuhakikisha mnafurahia maisha ya sasa na wakati huo huo mnawekeza fedha na miradi ambayo mbele ya safari mtakuwa na fedha kwa ajili ya kusomesha watoto na hata wakati mkiwa wazee.
Wakati ni sasa usisubiri ukiwa mzee ndo unapanga mipango mikubwa ya kuwekeza anza hata kabla hujaoa au kuolewa.
Kama umeolewa au umeoa; panga malengo, timiza ndoto zako.
Kuwa na ndoa imara yenye afya ni pamoja na kuwa na mafanikio katika Creation of Wealth kwa ajili ya maisha yenu miaka 5, 10, 20, 50 au 100 ijayo.

AINA ZA WANAUME WANAOMALIZA HARAKA NA SIFA ZAO.

AINA YA 1.
Huyu hajijui kama ni mtu wa kumaliza haraka (dakika 2), anapotaka mapenzi anamuita mke wake, then akishamvulia nguo ni kuingiza na fanya dakika 2 amemaliza, hajali lolote, hajui mwanamke ana kitu kinaitwa kufika kileleni, hajawahi kusikia na hana mpango wa kujua, anajua anachofanya ni sahihi.
Tendo la ndoa akijitahidi ni dakika 5

AINA YA 2.
Anajua sana kwamba mwanamke anatakiwa afike kileleni ila anajifanya hajui. Tofauti na (Aina 1) hapo juu, yeye akiona mwanamke anaugulia kwa kuachwa solemba yeye hujifanya ndo mwanamke amefika kileleni, na wala haulizi kwa mke wake kama hivyo ndo kufika kileleni ili apate ukweli.

AINA YA 3.
Anajua tatizo lake, hafurahii kabisa hii hali na anataka kumuona Daktari ila anaona aibu na anasema hana muda wa kwenda kumuona Daktari au mshauri yeyote wa mambo ya Ndoa. Anajitahidi kwa kumuandaa mke wake kwa kubusu na kumpa migusu ya kimahaba ya kila aina, Ila yeye akiwa tayari tu anaacha kuendelea kumwandaa mke wake na badala yake anaingiza na kumalizia then imetoka, hafurahii ile hali ila ndo hivyo maisha yanaenda.

AINA YA 4.
Huyu anajua tatizo lake na pia anajua umuhimu wa mke wake kufika kileleni;
hivyo anaanza kwa kumpa mke wake romance ya uhakika hadi anafika kileleni kabla hajamwingilia.
Akiona mke yupo katika hali inayoonesha ameridhrika na amefika kileleni kwa njia za stimulation ndipo na yeye anaanza kufanya mapenzi kisha anamaliza huku mke wake amefurahi kwani amefika kule kunatakiwa.

Hii ina maana kwamba kama mwanaume ni mjanja na ana akili ya kujua yeye ni mtu wa kuwahi kumaliza na anamwandaa mke wake hadi anaridhika, basi kwa ke kuwa mtu wa kumaliza mapema haina tatizo na anaweza kuwa na mahusiano mazuri na yenye furaha katika mapenzi na mke wake huku juhudi zingine za kumuona daktari na maombi zikiendelea.
Pia afahamu kwamba hahitaji kuwa mchoyo na mtu wa kujitanguliza yeye (selfish) na badala yake kumtanguliza mpenzi wake afike kileleni kwanza badala yake.

Kiukamilifu; kufanya mapenzi vizuri kwa mwanamke ni penis ya kawaida, kumuandaa vizuri na kwa muda wa kutosha, busu za kutosha sehemu anazopenda, kumpa mgusu wa mwili kwa mikono yako sehemu zote zinazompa raha ya mapenzi, kukaa ndani yake kwa muda mrefu huku akipata msuguano wa muda mrefu na kwa mwendo anaotaka yeye kutokana na anavyoitikia, kujua mikao yake ya mapenzi anayopenda ili kupata raha zaidi na zaidi kufahamu na kumpa kile anahitaji ili kufika kileleni.

Kumbuka kama amawahi kufika kileleni maana yake anajua vionjo muhimu vinavyoweza kumfikisha kileleni hivyo mwanaume mbunifu wa mapenzi lazima unamsikiliza yeye akuongoze kule anataka kwenda kwani kwa mwanume kufika kileleni kwako ni kitu ambacho kipo.

MWISHO.
Je mwanamke unawajibu gani katika kuleta usawa kuhakikisha utendaji wa mapenzi unakidhi haja yako?

JIBU:-
Unahitaji kuwa wazi kuongea na kuelezea kile Unahitaji kufanyiwa tena kwa uwazi na uhuru. Usibaki kimya na kulala tu usingizi wakati wa tendo ndoa ukidhani kwamba utafika kileleni, ongea kwa mumeo mwambia kwa upendo kabisa nini Unahitaji, kwani ukipoteza hamu ya mapenzi basi hii raha ya mapenzi sahau kabisa kwani unakuwa umechimba shimo ambalo huwezi kutoka.

TATIZO SI SIZE,TATIZO NI UBUNIFU WAKO.

Kwa wanaojua Mchezo wa Soccer; Kitu cha Msingi si Size ya Kiatu, Bali ni Skills za Mchezaji Mwenyewe ndiyo Zinawezesha Mchezo uwe mtamu na Kisha Magoli ya Kutosha.
Maswali ambayo huwasumbua sana Wanandoa wengi na yamefika mezani kwa madaktari wa mambo ya afya na mahusiano ni kuhusu wanawake kutofika kileleni (orgasm) na wanaume kumaliza haraka tendo la ndoa (ejaculation) na pia, je kuna uhusiano wowote kati ya mwanamke kufika kileleni na size ya kiungo nyeti (penis) cha mwanaume?

Ukiangalia haraka unaweza kusema hayo mambo mawili yanafanana; kwani kama mwanaume anaweza kumaliza haraka (kukojoa au kufika kieleleni), ina maana ni dhahiri mwanamke atakosa kufika kilele kwani mwanaume anakuwa alishamaliza zamani,
Lakini ukweli ni kwamba kama mwanaume atamuandaa mwanamke vizuri basi hata kama huwa anawahi kumaliza haraka (dakika 2) itakuwa haina shida.

Pia watu bado wanajiuliza, ni size gani na urefu gani unafaa kwa kiungo nyeti cha mwanaume kuhakikisha mwanamke anafika kileleni?
Je ni udogo kiasi gani unafaa kumwezesha mwanamke kufika kileleni?

Wapo wanaume kutokana na walivyoumbwa kuwa na umbile dogo automatically hujasikia inferior au vibaya na kujiona kama vile hawana uwezo wa kuwapa wapenzi wao mapenzi halisi na kuwafikisha kule wanataka na matokeo yake wengi huwa hawapo wazi kujiachia kwa wake zao au wanaogopa hata wake zao kuona na kuwapa uhuru kukifurahia hicho kiungo nyeti na adimu wakati wa tendo la ndoa.

Kila mwanaume ana kiungo tofauti kama ilivyo kwa alama za vidole vilivyotofauti kwa kila binadamu.
Ukubwa au kimo cha kiungo si msingi wa ufanisi wa utendaji wa tendo la ndoa bali muhusika mwenyewe ndiyo msingi wa mafanikio katika tendo la ndoa.
Huhitaji kuwa mjinga kiasi hicho kudhani kwamba urefu au ufupi, unene au wembamba wa penis ndiyo unafanikisha mke wako wako au mpenzi wako kufikia kilele; badala yake unaweza kumsababishia maumivu na kumkosesha raha ya mapenzi.

Hata mwanaume mwenye penis ndogo anaweza kuwa mtaalamu wa kumfikisha mke wake katika furaha ya kweli katika tendo la ndoa.
Njia pekee ni kijifunza jinsi ya kufanya mapenzi vizuri, jinsi ya kuwa partner mzuri.

Huo ni mwili wako upende, jifunze kuutumia, jitahidi kuutumia kwa ubunifu na kwa kimahaba zaidi.
Mbusu na kumpa mgusu wa mwili mpenzi wako kwa muda mrefu hadi unahakikisha amenyegeka vizuri kwa kumchezea sehemu zote ambazo ukimgusa anapata raha inayomuwezesha kuwa hot kwa kuwa ni partner wako; mwili wake wote ni mali yako na ni wewe, hivyo safiri kila sehemu ya kiungo cha mapenzi kwa kadri unavyoweza kuliko kukimbilia kumwingilia wakati hata hajanyegeka.

Amini, usiamini kila mwanamke anapenda mwanaume au mume ambaye ana kipaji, talent, ana ubunifu, aliyemtaalamu anayeweza kumpa romance ya uhakika na si kuwa na penis kubwa tu bila ujuzi then baada ya dakika 2 upo pembeni unapiga usingizi wakati partner wako anaugulia kwa kuachwa kwenye mataaa.
Hapo ndipo utasikia mwanamke anasema hajisikii kama unampenda anaona kama vile unamtumia tu ili kutimiza matakwa yako ya mapenzi.

Kuwa na kiungo kidogo siyo kosa wala uhalifu bali umeumbwa hivyo na kuujua mwili wako na kujua majibu sahihi ya mahitaji ya kimahaba kwa mke wako hiyo ndiyo akili na unaonekana mwanaume Smart kwani wewe ndo unajua kupenda, unajua mapenzi.

Kuhusu mwanaume kumaliza haraka, pia si kosa wala uhalifu hata kukufanya ujione si lolote, badala yake elekeza jitihada katika kukabiliana na hilo tatizo na inawezekana kwa kupata ushauri wa daktari au kufanyiwa maombi.

Kitu cha msingi unatakiwa kujua kwamba kuna tofauti kubwa sana za kijinsia kati ya mwanaume na mwanamke.
Kwa asili mwanaume hupenda mara mwanamke akiwa uchi yeye mara moja aingize na kuendelea na mchezo wakati mwanamke yeye anahitaji maandalizi, jitahidi kuwa na muda wa kutosha wa foreplay kwa mke wako zaidi ya dakika 10-15 ili awe tayari kwa tendo la kuingiliwa na wewe.

Na kila mwanamke ana namna yake ya kufikishwa kwenye raha mwingine atapenda aina fulani ya mkao na mwingine atapenda aina nyingine ya mkao, mwingine atapenda achezewe kisimi na mwingine atapenda achezewe chuchu, na mwingine atapenda sehemu nyingine hivyo mwanaume anahitaji kuwa mvumilivu na sharp kumsoma mke na kujua ni kitu gani anahitaji na wapi anahitaji kuguswa zaidi ili afike huko kunako raha yenyewe.
Pia mawasiliano wakati wa faragha yenyewe ni muhimu; kwa maneno na vitendo wengine hawasemi bali wanakuelekeza kwa mkono.

MAMBO 6 KUHUSU FEDHA KTK NDOA.

Zipo Ndoa ambazo mke na mume wanaishi tu kwa sababu ya watoto, au kuogopa kupoteza nyumba, au mali kwani utamu na raha ya Ndoa imetoweka, hata hivyo kila kitu kina chanzo na ni muhimu kujua chanzo ili uweze kutatua tatizo kabla halijakumaliza na kujikuta umechelewa.
wahenga walisema
"Heri Kinga Kuliko Kuponya".

Migogoro mingi ya wanandoa hutokana na mambo yanayohusu pesa.
Pia mfumo wetu dume katika jamii umeongeza tatizo kuwa kubwa zaidi kwani suala la pesa ameachiwa mume bila mke kuwajibika, kujua au kuchangia lolote, hata wanawake wenyewe wengi wamejiweka katika kundi la kuwaachia wanaume kuwajibika kwa kila kitu kinachohusu pesa katika na kutoa maamuzi yote yanayohusu pesa katika ndoa.
Na kuna maamuzi mengine yameangamiza familia kwa sababu ni mtu mmoja tu katika ndoa ndo hutoa maamuzi linapokuja suala la pesa yaani baba au mume.

Sasa ulimwengu umebadilika wanawake nao wana uwezo, wanafanya kazi, wanaingiza pato katika familia na ndoa.
Pia kuna familia ambazo mke ndiye mwenye kipato kikubwa kuliko mume, na kuna ndoa ambazo kila mmoja akipata pesa hutumia anavyotaka yeye bila kukaa pamoja na kupanga nini kifanyike na matokeo yake kumekuwa na migogoro ya hapa na pale na kusuguana kwa hapa na pale.

Mambo yafuatayo ni muhimu sana kuwekwa wazi kwa wanandoa kwa ajili ya kuimarisha ndoa hasa linapokuja suala la fedha.

1.KUWA NA ACCOUNT MOJA.
Kitu kikubwa ambacho wana ndoa wapya hukumbana nacho mara wakishaanza maisha pamoja ni jinsi ya kupangilia matumizi ya pesa.
Kama wote mnafanya kazi, je ni muhimu kuwa na account moja ya pesa? au kila mmoja kuwa na account yake then wote kuwa na account ya tatu ya pamoja?

Asilimia kubwa ya wanandoa wapya hufungua Account ya pamoja wakishaoana .

Kitu cha msingi ni kuhakikisha mmekuwa kitu kimoja si katika mwili mmoja tu, bali hata katika pesa.
Kuwa na account moja ni sawa, pia kuwa na account tofauti ni sawa.
Kitu cha msingi ni kuelewana juu ya mapato na matumizi ya pesa zenu na pia malengo ya kiuchumi ya muda mrefu na muda mfupi, kama kuwekeza na akiba kwa pamoja.
Pia kujua aina ya matumizi ya pesa kwa kila mmoja kwani kama mmoja ni mtumiaji na mwingine ni mtu wa kuweka akiba, mnahitaji kujuana ili kusiwe na kinyongo kwa mmoja.

Pia kama mmoja wenu ameingia kwenye ndoa huku anadaiwa na Bank ni vizuri kumjuulisha mwenzake kwani kuoana ni pamoja na hilo deni mnakuwa kitu kimoja.
Kuna wengine wanaingia kwenye ndoa huku tayari walishawekeza kwa ajili ya mke/mume na watoto aliokuwa anatarajia.
Kitu muhimu ni kuwa wazi kuhakikisha mke wako au mume wako anajua.

2.JINSI YA KUPAMBANA NA MADENI.
Katika mambo yote ya pesa katika ndoa, madeni ni jambo linaloongoza kuleta zogo mwenye ndoa na kama hamjafahamishana vizuri inaweza kuleta maafa.
Pia mara nyingi wana ndoa huwa wanatofautiana katika mtazamo kujua lipi ni deni kubwa au dogo hasa kutokana na elimu ya fedha ya kila mmoja.

Hilo ni deni lenu wote hivyo lazima muweke mikakati ya kuondokana nalo kwa pamoja.
Mara nyingi wengi hujiingiza katika deni bila upande mwingine kujua hali ikiwa mbaya ndiyo mtu anaanza kutoa taarifa kwamba ilikuwa hivi na vile huku nyumba inataka kuuzwa au kufukuzwa kazi.
Hapo ndiyo zogo huanza na ndoa huanza kuyumba kwani upande mwingine hujiona hauthaminiwi.

3.MMOJA KUWA MTUMIAJI WA PESA ZAIDI YA MWENZAKE.
Wanandoa wengi hulaumiana kwamba "wewe ni mtumiaji mbaya kuliko mimi" au kumtuhumu mwenzake kwamba anatumia pesa katika kununua vitu visivyo muhimu katika maisha.

Jinsi ya kutumia pesa huleta maneno katika ndoa nyingi, wapo wanaume akipata pesa tu ni kwenda kununua TV kubwa, Music System na vitu vingi vya starehe wakati mke anataka Pesa ya kununua kiwanja amechoka kukaa nyumba ya kupanga, au mwanamke yeye ni kununua nguo za fasheni mpya iliyoingia mjini hata kama ni gharama kubwa wakati mtoto anahitaji ada ya shule.
Kitu cha msingi ni kuwa na malengo ya muda mrefu na muda mfupi na kwamba kuwa na uelewano wa kujua nini kinunuliwe (bajeti).
Kuvaa ni muhimu na pia kuwa na vitu vya starehe ndani ya nyumba ni muhimu ila kupanga malengo na kuwa na mawasiliano mazuri hilo ndiyo jambo la kwanza.
Kaa pamoja, panga vitu vya msingi,
Tununue nini na kwa nini?
Tuwekeze wapi? na kwa nini?
Tuweke akiba kiasi gani kila mwezi na kwa nini?

Panga pamoja kila mmoja aelewe kwa nini hiki kinafanywa Badala ya hiki.

4.KUWEKEZA KWA BUSARA NA HEKIMA.
Mustakhabali wa maisha yenu ya miaka 5, 10, 20. 30, 50 ijayo ni sasa na jinsi mnavyotimia pesa na kupanga malengo.
Kuwekeza pesa katika business mara nyingi huwa na risk na risk ikitokea mara nyingi mmoja huanza kumlaumu mwenzake kwamba wewe ndo ulilazimisha tufanye hivyo.

Ni muhimu kushirikiana katika kuweka uamuzi wa pamoja mnapowekeza pesa kwenye miradi au business pamoja.
na piakukubaliana risk yoyote ikitokea pamoja kwani kama ni faida ni yenu wote na kama hasara ni yenu wote.
Katika hali ya kawaida katika ndoa inaonesha kwamba wanaume ndo wanaongoza kwa kujitosa kufanya kitu chochote (business) hata kama kuna risk kubwa baadae na wanawake huogopa sana kuwekeza katika kitu ambacho hawana uhakika.

Kitu cha msingi ukitaka kufanikiwa katika business au maisha lazima uwe risk taker kwani ukifanikiwa unaweza kubadilisha uwezo wa kifehda wa familia yako, ingawa unahitaji kufanya utafiti mkubwa kabla ya kuwekeza pesa zako na uwe na njia ya kupunguza risk inapotokea au Usibebe mayai yote kwenye kikapu kimoja kwani kikidondoka umeumia.

5.KUTUNZA SIRI ZINAZOHUSU PESA.
Wengine wanaamini siri za pesa walizonazo bila mume au mke kujua hazina ubaya sana kwenye ndoa.
Ukweli ni kwamba unahatarisha sana ndoa yako kwa kuficha siri za pesa ulizonazo au business unazofanya bila mke au mume kujua.
Wengine wameficha wake au waume fedha walizonazo katika Account walizonazo
Wengine hata wakinunua vitu hudanganya bei waliyonunulia vitu.
Na wengine hujiingiza katika business ambazo mke au mume hajui na huko ikitokea hasara au tatizo ndo hurudi kusema kwa mke au mume, hapo ndo zogo linaanza.

Wengine huwapa ndugu zao au marafiki zao pesa nyingi bila mke au mume kujua na siku mke au mume akijua kwamba mmoja alitoa pesa bila kuambiwa hapo tena moto unalipuka.
Ni muhimu kutoficha siri zozote kwa mke au mume wako kwani lolote linaweza kutokea wakati mwingine hata kifo, utatesa watoto bure kwa kuficha siri muhimu kama hizo ambazo si siri bali jambo muhimu kwa mke au mume wako.

6.KUPANGA KWA AJILI YA FEDHA YA DHARURA.
Wengi hudhani haina haja kuwa na pesa ya dharura
Na wengine hupanga fedha ya dharura kwani chochote kinaweza kutokea, anaweza mtoto kuugua au ninyi wenyewe mmoja kuugua ghafla pia kunaweza kutokea mchango wa dharura bila kujua.
Hata kama una kazi nzuri kama hujajipanga vizuri kwa ajili ya mambo ya dharura unaweza kushangaza mke au mume kwani lolote laweza kutokea.

Matatizo hayataisha hadi tuwe tumekufa, kupangilia vizuri masuala ya pesa kutawezesha ndoa yako kuwa yenye afya na imara.

Friday, 22 January 2016

WANAUME CHEATERS..

Katika asilimia 100 ya wanaume wanaotoka nje ya ndoa zao, asilimia 12 ya hao wanaume wanao cheat hufanya hivyo kwa sababu ni cheaters, wao hutoka nje ya ndoa zao No matter what! .
Hata kama wanaridhishwa na wake zao zaidi ya kawaida bado akikutana na mwanamke mwingine bila kujali ana sura inayofanana na chimpanzee kwake ni mistress na atafanya kila analoweza ili kutembea naye (sex).
Ndoa iridhishe isiridhishe wao hutoka.
Wao hutoka nje ya ndoa zao kwa sababu ni cheaters tangu mwanzo.
Kama ni mwanamke utafanya kila ambacho mwanaume duniani anatakiwa kufanyiwa na bado atatoka; hawa ni vilema, hawana hisia, hawajui kuumiza mke ni kitu gani, hawana adabu, hawana heshima, wameshindikana.
Hawajali utu wao, vyeo vyao, umuhimu wao katika familia na jamii, wanatoka nje.


JE,TUSEMEJE KWA ASILIMIA 88 INAYOBAKI?

Hapa kuna kitu cha kujifunza, nacho ni kwamba kuna matumaini makubwa kwa wanawake wengi kwamba efforts wanazofanya katika kuhakikisha ndoa zao zinakuwa na afya ni jambo zuri na la msingi sana kwani hawa wa asilimia 88 huwa na sababu kamili inayowafanya kutoka nje ya ndoa zao. Hivyo mwanamke anayejituma kuhakikisha anatengeneza mazingira mazuri kwa mume wake kuridhika nyumbani husaidia kuilinda ndoa.
Mwanamke mwenye busara huwekeza efforts nyingi katika:
1. Kumfanya mwanaume ajisikie si mpweke katika ndoa yake.

2. Kumpa heshima (appreciation & respect) katika mahitaji yake kimwili na kiroho.

NI VEMA ASUBIRI KWANZA.

Moja obstacle ya kuridhishana kimapenzi kwa wanandoa ni suala la timing.
Tunaposema timing tunamaana kwamba badala ya jambo kufanyika katika wakati sahihi,hufanyika kinyume chake.
Mke anaweza kuanza kumsisimua mume (manually & orally) na baada ya mume kusisimka sawasawa wanaendelea moja kwa moja kwenye intercourse.
Kwa kuwa mume amesisimka zaidi kuna uwezekano mkubwa kwa mume kufika kileleni haraka sana na Kumwacha mke bila kuridhishwa.
Matokeo yake mke anakuwa frustrated kwani pamoja na juhudi zake za kumsisimua mume wake haikuchukua hata dakika 3 mume kumaliza.
(Kufika kileleni wakati mke kwanza bado ndo alikuwa anaanza kufurahia).

JE,USHAURI MUHIMU NI UPI?

Jawabu rahisi ni kuwa na timing nzuri; baada ya mke kumsisimua mume kwa uhakika inatakiwa mume apumzike huku mume akiendelea kumsisimua mke kwa kiwango cha kukaribia au hata kumfikisha mke kwa mara ya kwanza kileleni (manually & orally) na ndipo mume aanze kumuingia mke (intercourse).
Kwa njia hii mwanamke huwa tayari yupo njiani au tayari kufika kileleni na mume atakuwa anaanza upya kusisimka (amezitunza risasi zake) na inamchukua muda zaidi kufika kileleni na anaweza pia kufika kileleni wakati mmoja na mke wake.
Pia ni muhimu kwa mke kuwa wazi kwa mume wakati wa intercourse kumwelekeza mume namna na kiwango cha thrusting anayohitaji kutokana na msisimko anaoupata kwa kupunguza au kuongeza speed.

NDOA ZILIZO IMARA..

Mwanandoa imara siku zote hutazama kwenye uimara wa mwanandoa mwenzake na si katika udhaifu wake.
Hii ina maana mwenzake akifanya kosa (kumrushia neno linaloumiza, kufanya kile ambacho hakukipenda nk) pamoja na kuumia bado huanza kufikiria mambo mazuri kuhusu huyu mwenzi wake ambaye amemuumiza na kujisemea moyoni kwamba “pamoja na kunirushia neno ambalo limeniumiza lakini ni mwanamke/mwanaume ambaye siku zote amekuwa akinipenda na kunijali” na huendelea kuikabili ile hasira au uchungu wa kuumizwa kwa kuendelea kufikira positives zilizopo kwa mwenzake.
Kwa upande wa mwanandoa dhaifu au ndoa zisizo imara wanandoa huweka msimamo na mtazamo unaojikita katika kuangalia au kuona udhaifu wa mwenzake tu.
Ni ukweli ulio wazi na usiofichika kwamba hata ndoa imara ambazo tunaziona ni mfano wa kuigwa hukumbana na matatizo katika kila kona ya maisha iwe matatizo ya kifedha, ugonjwa, ndugu, watoto, kazi, mapenzi, nk hata hivyo system wanayotumia kupambana na hayo matatizo ni tofauti sana (model) na ndipo kwenye siri ya kufanikiwa kwa ndoa na kuzorota kwa ndoa.

NI KWAMBA:-

1. Ikitokea mwenzi wako amekuudhi kwa kitu fulani, fikiria (au tafuta) mambo mazuri 3 ambayo Anafanya katika ndoa yenu. (inaweza kuwa amekupa watoto/mtoto mzuri, anakujali kwa kukutimizia mahitahitaji mengine kama chakula, mavazi na malazi, anakuridhisha kimapenzi, amekufanyan uonekane wa maana hata kwa ndugu zako nk)

2. Badala ya kumshambulia mke wako au mume wako shambulia lile tatizo kwani lile tatizo ambalo limekufanya uumie ni vitu viwili tofauti na yeye.

3. Jiulize; “Hivi kwa namna nilivyo mtu mwenye akili timamu nitakasirika na kukaa na hii stupid issue moyoni hadi lini?” watu wote wenye busara huhakikisha jua halizami bila kumaliza hasira zao.!

MAPENZI BAADA YA KUOANA?

"Nilidhani tunapendana sana lakini baada ya honeymoon ndoa imekuwa maafa"


Tume Date kwa miezi sita na tulijiona duniani ni sisi tu kwa moto wa mapenzi/mahaba, lakini baada ya kuoana nyumba yetu imekuwa uwanja wa vita kwa kutokuelewana, Why?


Hili swali na mengine mengi yanayofanana na hilo huulizwa na maelfu ya watu ambao wameoa haijalishi mmeishi miaka mingapi, na wengine wamepeana talaka na kuoa na kuolewa mara nyingi zaidi na bado maswali kama hayo yapo.

Wengine wamewauliza wazazi wao, viongozi wao wa dini na pia washauri wao, lakini wakirudi nyumbani baada ya kupewa ushauri na majibu bado hali ni ile ile ni kama vile kutibu cancer kwa kutumia Asprini.

Inakuwa raha sana kabla ya kuoana/uchumba na baada ya kuoana hali inakuwa tofauti kabisa na wengine wanajuta kwa nini waliolewa na kuoa.

Pamoja na kuwa na TV, radio, magazeti, vitabu vyenye topic nzuri za kuimarisha ndoa zetu na semina mbali mbali, lakini bado mapenzi baada ya ndoa yanazidi kuwa kitendawili.

Ni ndoa chache kwa sasa ambazo zimebarikiwa kufahamu siri hii kubwa ya mapenzi baada ya kuoana na kutokana na kufahamu siri hiyo hao wanandoa wanaweza kukuthibitishia kwamba hakuna kitu kizuri duniani kama kuwa na mke au mume. Ndoa ni tamu, ndoa ni mpango wa Mungu kumkamilisha binadamu, ndoa ni msingi wa familia na taifa.

JE,SIRI NI NINI?

Tuanze kwa kuangalia msingi kabisa wa mambo ya mahusiano ya kimapenzi hatua kwa hatua na leo napenda kukuletea utangulizi wakati tunaelekea kuchambua hili suala.


Mapenzi yana lugha kama zilivyo lugha za kawaida yaani Kiswahili, Kingereza au Kichina. Wengi tumezaliwa tunaongea lugha tulizafundishwa na wazazi wetu au ndugu zetu na kutokana na kuzifahamu vizuri zimekuwa lugha mama yaani Primary. Tunajisikia raha kutumia hizo lugha na pia tunajisikia raha kusikia kwani tunaelewa kuliko lugha zingine.


Katika mapenzi kuna lugha pia (emotional love languages) kwa hiyo mwanaume anaweza kuwa ana lugha yake na mwanamke ana lugha yake katika kuitikia mapenzi au kujisikia kwamba anapendwa. Kutokujua lugha ya mwenzake ni sawa na watu wawili (wanandoa) kuishi pamoja na kuwasiliana kwa kutumia kichina na kiswahili na kudhani wataelewana. Haitawezekana kamwe!

Hujasikia mwanaume analalamika kwamba "Mke wangu nimepa kila kitu, nimemjengea nyumba nzuri, nimemnunulia gari zuri, fedha za matumizi nampa nk, lakini analalamika kwamba simpendi, hiyo ni kudhihirisha kwamba huyo mwanaume kwa kumpa nyumba nzuri na gari zuri mke wake kwake ni lugha ya kuonesha anampenda mwanamke, wakati mwanamke kupewa gari na nyumba kwake bado si kupendwa yawezekana kusikilizwa na kuwa na muda pamoja (quality time) kwani ni lugha inayoeleweka kuonesha anapendwa.

...Je,lugha hizo ni zipi na zinafanyika vipi??


ITAENDELEA.....

Monday, 18 January 2016

KUSHIKA UJAUZITO..

Wengi hasa wanawake wamekuwa wakitaka kujua kuhusuana na jinsi ya mwanamke kupata mimba au kuzuia kutopata mimba.
Naamini maelezo yafuatayo ukisoma kwa makini unaweza kupata ufahamu na kujibiwa maswali yako yote ambayo yamekuwa yanakutatiza.
Pia ni vizuri kuzingatia na kutochanganya Kalenda ya menstrual cycle tunayoongelea hapa na ile 'kalenda ya mwaka' inayohusu tarehe za miezi 12 ya mwaka ambayo huwa tunaitundika ukutani huko nyumbani na maofisini kwetu!

Wanawake wamegawanyika katika makundi makubwa 4 linapokuja suala la siku za hedhi.
Kuna wale wa Mzunguko mfupi yaani siku 22.

Mzunguko wa kati yaani siku 28

Mzunguko mrefu yaani siku 35.

Na mzunguko abnormal siku 15

Kama mwanamke ana menstruation cycle ya siku 22 inabidi afanye kama ifuatavo:
Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstruation cycle kama hapa chini:
1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, *8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, 21st, 22nd.
Kisha ahesabu kuanzia ile 22nd day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15.
Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 8th day ya kalenda yake.
Hivyo 8th day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 22.
Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!

Kama mwanamke ana menstruation cycle ya siku 28 inabidi afanye kama ifuatavo:
Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa chini:
1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, *14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th.
Kisha ahesabu kuanzia ile 28th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15.
Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 14th day.
Inamaana kwamba 14th day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstruation cycle ya siku 28.
Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!

Kama mwanamke ana menstruation cycle ya siku 35 inabidi afanye kama ifuatavo:
Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstruation cycle kama hapa chini:
1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, *21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th, 29th, 30th, 31st, 32nd, 33rd, 34th, 35th.
Kisha ahesabu kuanzia ile 35th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15.
Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 21st day.
Inamaana kwamba 21st day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstruation cycle ya siku 35.
Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!

Kama mwanamke ana abnormal menstruation cycle ya siku 15
BASI KUNAUWEZEKANO WA KUTOPATA MIMBA KABISA KAMA INAVYOONEKANA HAPA CHINI:
Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstruation cycle kama kawaida:
1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th.
Kisha ahesabu kuanzia ile 15th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15.
Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 1st day.
Inamaana kwamba, the 1st day of her bleeding ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstruation cycle ya siku 15.
Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed, na ndiyo hiyo hiyo siku ambayo mwanamke wa kundi hili anaweza kupata mimba!
Hii inamaana kwamba, siku ambayo linaharibika lile yai la upande mmoja ndiyo siku hiyo hiyo ambayo yai la upande wa pili linapevuka tayari kwa kurutubishwa.
Mwanamke wa aina hii anaweza kupata mimba tu kama atakutana na mwanaume siku ile anayoanza kubleed, kwani siku ambayo yai moja linaanza kuharibika ndio siku hiyo hiyo ambayo yai la upande wa pili linakuwa tayari kurutubishwa
Na wanawake wa kundi hili la nne ukiwauliza vizuri watakiri kwamba hawajawahi kuona au ku-feel ule ute mweupe ambao wenzao huwa wanaupata siku ile yai linapokuwa tayari kwa kurutubishwa, kwani ute wa wanawake wa kundi hili la nne huwa unachanganyikana na damu kwa vile unatoka siku ile ile wanapoanza ku-bleed.Pia wanawake wa kundi hili huwa wanatokwa na kiasi kidogo sana cha damu na bleed hukatika ndani ya siku moja au mbili tu!

NB:
Mwenye uwezo wa kuhakikisha mwanamke anapata mimba ni Mungu mwenyewe, unaweza kutumia njia zote na kila uwezo wa kibinadamu nab ado mimba isitokee au unaweza kuzuia kwa njia zote na mimba bado ikapatikana.
MASWALIJe, nifanye nini ili nizae mtoto wa KIUME:
Ili mwanamke aweze kuzaa mtoto wa KIUME, inabidi alale na mwanaume siku ile ya mimba (fertile day), ambayo ni siku ya 15.
Je, nifanye nini ili nizae mtoto wa KIKE:
Ili mwanamke aweze kuzaa mtoto wa KIKE, inabidi alale na mwanaume siku 3 kabla ya ile siku ya mimba (yaani siku 3 kabla ya ile fertile day)
Hii inaondoa uwezekano wa mbegu za kiume kulirutubisha yai, kwani mbegu zote za kiume zitakuwa zimeshakufa ndani ya siku mbili za mwanzo na kuziacha zile za kike zikidunda kwa siku moja zaidi zikilisubili yai lifike!
Je, Kama menstruation cycle yangu Ni siku 15, nifanye nini ili nipate mtoto wa kike?
Ili mwanamke mwenye menstruation cycle ya siku 15 aweze kuzaa mtoto wa KIKE, inabidi alale na mwanaume siku 3 kabla ya siku ile ya bleed (yaani siku 3 kabla ya ile siku anayoanza kutokwa damu ya hedhi)!
Kwa mwanamke wa kundi hili inabidi tukumbuke kwamba, siku yake ya mimba ndiyo siku hiyo hiyo anayoanza ku-bleed!

KUMALIZA SHUGHULI HARAKA..(2)

Kawaida baada ya mwanaume kuwa na tabia ya kumaliza haraka kinachofuata ni kuanza kukwepa sex kitu ambacho inakuwa ngumu zaidi kudhibiti tatizo, mwanaume akiwa anauwezo wa kudhibiti kumaliza mapema pia huweza kuwa na hamu zaidi ya kufanya mapenzi.

Wengine hutumia njia ya kuondoa mawazo kujihusisha na tendo lenyewe kwa kuwaza vitu vingine hata hivyo hapo ni kujinyima raha na huweza kupelekea vitu kuwa ovyo zaidi.
Si vema kuhamisha mawazo yako kutoka kwenye akili zako wakati wa tendo la ndoa kwani ni sex muunganiko wa roho, mwili na nafsi.
Jambo la msingi ni kuwa na ufahamu wa viwango tofauti vya msisimko wa kimapenzi kuhusiana na kiungo chako (uume).
Unatakiwa kujua ni namna gani unajisikia unapokaribia kufikia hatua ambayo hakuna kurudi nyuma.

Ukishakuwa umefahamu unavyojisikia kuelekea point of No return hapo haitakuwa vigumu kufanya marekebisho ambayo yatakuruhusu kubaki umesisimka lakini bila kumaliza (kukojoa).

Kusisimka kimapenzi huwa ni mzunguka wa hatua 4 muhimu ambazo ni:-

KUPANDA KWA MDADI.
Huu ni wakati ambao kupumua huongezeka, uume husimama (hudinda). hatua ya pili ni:-

KILIMANI- hii ni hatua ambayo uume huwa umebaki umesisimka kwa kiwango cha juu.
Hatua inayofuata ni hatua ya tatu ambayo ni:-

KUMALIZA au KUKOJOA na hatua ya mwisho ambayo kupumua hurudi kama kawaida na uume hurudi na kuwa kawaida.
Ufunguo muhimu katika kudhibiti kumaliza mapema ni ku-maintain hatua ya pili yaani kubaki hapo kilimani bila kupiga risasi hata kama umelenga vizuri na unajisikia kuachia, hapa ndipo panahitaji imani na kujikana maana huwa ni kuelekea kwenye raha kamili ya sex kwa mwanaume, ila kumbuka uliye naye anahitaji uendelee zaidi.

NINI KIFANYIKE KUDHIBITI HALI HII?
Usitumie drugs au kilevi eti ndo unaweza kudhibiti hii hali, vitu kama hivi huweza kukupa interference na kupunguza uwezo wa kuelewa wakati muhimu wa wewe kuthibiti kumaliza mapema.
Kwanza jikubali, wanaume wengi huamini kwamba sex ni kwenye uume tu na pia kufanya mapenzi ni pale uume ukiingia kwenye uke tu.
Kufikiria hivyo ni tiketi ya moja kwa moja ya mwanaume kuwahi kukojoa au kumaliza.

Kufanya mapenzi kunakoridhisha (best sex) ni pamoja na kupeana mahaba, romance kuanzia juu kichwani kwenye nywele hadi kwenye kucha za vidole miguuni.
Mwanaume anayejifunza kujipa raha kimapenzi kupitia sehemu zote zinazompa raha (chuchu, lips, shingo, midomo, ulimi, nk) huweza kurelease tension kupitia hizo sehemu na kutosubiri sehemu moja tu yaani uume ndo iwe sehemu ya kupata raha ndo maana huweza kukojoa mapema.
Ni kwamba mwanaume anakuwa amefunga outlet zingine na kubaki na uume tu hivyo ni rahisi kufikia point ya no return tena kwa haraka mno.
Ukishajifunza kupata raha ya mapenzi kuanzia nywele kichwani hadi kucha miguuni maana yake mwili mzima unachukua raha ya mapenzi badala ya uume peke yake na matokeo yake utabaki ndani ya mke wako kwa muda mrefu.

Kujipa raha ya mapenzi ya mwili mzima ni njia ya ku-relax na kurelax ni moja ya njia muhimu za kujipa good sex.
Kwa mfano kuoga pamoja kwanza au kufanyiana massage kwanza kabla ya kuanza kwa tendo la ndoa husaidia mwanaume kurelax na zaidi kuupa mwili mzima sexual pleassure matokeo yake ni kufanya mapenzi kwa muda unaotosha na bibie kuridhika.

Kuwa na uwezo wa kupumua vizuri (deep breath) hii haina maana kwamba wakati unafanya mapenzi huwa hupumui, la hasha bali upumuaji wako inawezekana si ule usiotakiwa kwani wanaume wengi huzuia kupumua wakiwa kwenye sex.
Wengine huogopa kusikika wanapumua tofauti, sex ni kazi kama kazi zingine sasa usipopumua unadhani kitatokea nini, ikiwezekana pumua huku unatoa visauti, achia kupumua usijivunge kwani unapoficha kupumua maana yake unakaribisha uume ukusaidie kupumua na njia sahihi kwa uume kupumua ni kukojoa mapema.
Wengi baada ya kujifunza kupumua kwa kujiachia wamefanya mabadiliko makubwa sana katika muda wa kuwa ndani bila kumimina risasi.
· .
Ukishajua kuutumia mwili mzima kuhusika na raha ya mapenzi pamoja na kupumua sasa inakuja technic nyingine ya kujipiga stop.
Unaweza kuwasiliana na partner wako jinsi ya kupeana signal kwamba nakaribia kile kituo ambacho nikifika sitarudi tena, hakuna break.
Unaweza kutoa uume nje huku ukiendelea kupumua na ukiona unapata zile feelings kwamba huwezi kukojoa basi unaweza kurudi na kuendelea tena, kiasi cha kujipiga stop na kuendelea ni uamuzi wa ninyi wawili mnaohusika hasa baada ya mke kuridhika.

Kwa wale ambao kufanya mapenzi kupo katika level nyingine (oral sex) wanaweza kutumia oral sex kuthibiti mwanaume kumaliza mapema kwa mwanaume kujipa stop akiona anakaribia kumaliza kwa oral sex hii ni baada ya kupata mafanikio hasa baada ya kuona sasa mwanaume anaweza kwenda mbali zaidi ya kawaida yake.

Pia aina ya milalo wakati wa mapenzi huchangia mwanaume kumaliza mapema, kwa mfano missionary position (mwanaume juu mwanamke chini) huu huwezesha mwanaume kumaliza haraka kuliko mwanamke kuwa juu na mwanaume chini, otherwise mwanaume ni vizuri ukafanya utafiti wako kujua ni mlalo gani huwa unajisikia kuchelewa kumaliza na mke wako kuwahi kufika kileleni.

Pia ni vizuri kufanya mapenzi bila kuwa mabubu,kufanya mapenzi huku mnaongea husaidia mwanaume kurelax (na mwanamke pia) na husaidia mwanaume kuchukua muda mrefu kumaliza
Kujifunza kuthibiti kumaliza mapema kunaweza kuchukua muda mrefu na mazoezi ya kutosha, unaweza kujisikia kusumbuka tu wakati unajitahidi kuthibiti hata hivyo kwenye nia njia ipo na wewe utaweza tu nakuamini.

Mwisho, kujifunza mwanaume kumaliza mapema kutampa mpenzi wako raha kubwa sana kimapenzi. Wanawake hupenda good sex ambayo ni leisure, playful, whole body, massage kwa wingi.
Na wanawake wengi hulalamika kwamba wanaume huwa na haraka tukiwa kwenye miili yao, tupo too much mechanical, tunakimbilia kule chini tuingize tumalize na tuishie zetu kwa usingizi, tuna focus matiti na maeneo ya uke tu.
Wanawake hujisikia mwili mzima ni uwanja wa kucheza kimapenzi na hushangazwa na wanaume kugundua visehemu kidogo tu katika uwanja mzima na kuvipenda.
Hata uume pia umeumbwa kwa ajili ya leisure, kuchezewa, mapenzi ya mwili mzima, massage ya mwili mazima ndipo sex, kuwa focused kwenye uume peke yake huweza kuupa uume mgandamizo ambao hupelekea kutoa risasi mapema.

Kimsingi kama wanaume wangekuwa wanafanya mapenzi kwa namna ambayo wanawake wanapenda basi kusingekuwa na malalamiko na wanaume wangekuwa na matatizo kidogo yanayohusiana na tendo la ndoa.