Thursday, 23 June 2016

MAHUSIANO BAADA YA USALITI.


Baada ya affair kutokea au kugundulika huwa ni wakati mgumu kwa wanandoa; jambo la msingi ni kwamba kuaminiana kulikoyeyuka huweza kurudi hasa baada ya hasira kwisha na wanandoa kuanza kuwa karibu kihisia tena.
Hii hutokea tu na pale tu kama wahusika wameelezana na kufahamu sababu za kwa nini affair ilitokea.
Ukweli ni kwamba kuelezea sababu za kwa nini affair ilitokea ni moja ya jambo gumu sana na pia ni moja ya jambo muhimu sana katika kuiponya ndoa.
Ni muhimu kujua sababu za affair kwa kuwa kama wewe ni uliyesalitiwa na mwenzako utatakiwa kujifunza kwa mapana yote kwa nini mwenzako alichepuka (affair) ili kuweza kurudisha ukaribu wa kimapenzi na kuaminiana upya.
Kama wewe ndiye umesaliti ni vizuri kuelezea sababu za kuchepuka kwako kwa sababu ndicho mwenzako anapenda kufahamu.
Kujua sababu za affair ni kuchambua au kuweka wazi sababu zilizofanya mwingine achepuke.
Ili kufahamu vizuri maana ya kwa nini affair ilitokea hebu tujaribu kuweka suala la affair katika ndoa kama vile nyumba inavyoingiliwa na majambazi usiku.

Baada ya nyumba kuvunjwa ni muhimu kuchunguza nini kilifanya majambazi kuvunja na kuingia kuiba kirahisi, ni mianya ipi ilisababisha hao wezi kuvunja na kuingia kirahisi?
Je, tatizo ni majirani hatari?
Na je, ulichukua hatua gani kujilinda na hao majirani ambao wamesaidia kuwapa majambazi data au siri na namna ya kuvunja na kuingia katika nyumba yako?
Je, uliwaona watu wageni ambao walikuwa wanapita karibu na nyumba na hukutilia maanani na ukaona ni jambo la kawaida?
Je, nyumba yako haikuwa na milango ya uhakika?

Kuingiliwa na majambazi na kuibiwa haina maana kwamba unawajibika na tabia mbaya za wale majambazi.
Hata hivyo ukihamia nyumba nyingine utajisikia secured kama utafahamu sababu zilizofanya majambazi kupata mwanya wa kuvunja na kuingia kukuibia nyumba yako ya kwanza.
Hutakuwa na uhakika wa usalama wako kuibiwa na majambazi kama hutafahamu sababu zilizofanya uibiwe mara ya kwanza.
Trust na usalama wa kuwa karibu kimapenzi katika ndoa umeharibiwa na mwenzako ambaye amekusaliti, kama majambazi walivyoingia na kuvunja nyumba na kuiba, hutakuwa salama hadi ujue sababu zilizochangia.
Au inawezekana mmoja wenu alikuwa na urafiki na mtu wa nje ambaye alikuwa hana heshima na ndoa yenu.
Pia inawezekana kulikuwa na dalili za mwenzako kutoka nje na wewe ukapuuzia. Inawezekana hakukuwa na ukaribu wa kimapenzi kati yenu na hiyo ikatoa mwanya kwa yeye kuvutiwa kihisia na mtu wa nje.
Inawezekana kuzozana kwenu kila siku kumefanya muwe mbali kimapenzi na kihisia hivyo kutoa mwanya kwa mwingine kutoka nje.
Inawezekana mmoja alikuwa hamheshimu mwenzake na alipopata anayemheshimu nje akaishia kuchepuka.
Inawezekana kulikuwa na ukame wa tendo la ndoa ndani ya ndoa yenu na mwingine akajikuta anapenda kutuliza kiu nje.
Au inawezekana ni shetani tu.............................
Ukishajua sababu basi inakuwa rahisi kubadilisha mambo na si wanandoa wote huwa tayari kukubaliana na hizi changamoto.

Wednesday, 22 June 2016

NI VIZURI KUZINGATIA KWANZA..


Inakuwaje watu wawili waliopendana deep idara zote inafika siku wanakuwa baridi na wanajiona ni watu wawili tofauti kabisa kwenye ndoa yao?

Kuna mambo mengi sana husababisha kuanzia na yale yaliyo ndani ya ndoa yao na yale yaliyo nje ya ndoa yao hata hivyo ukweli love is so terrible and is so important, kuna wakati mwingine mpenzi (mke au mume) anaweza kukupa au kukunulia gari au kukujengea nyumba ya uhakika lakini bado ikawa haina maana kama hatatimiza mambo ya msingi kuhusiana na upendo wake kwako.

Ndiyo unakuja ule usemi
“Buying very expensive gifts doesn’t make woman happy but real love and affections”

Kuna aina tofauti za migogoro na jinsi ya kukabiliana nayo, wengine mgogoro ukizuka hata majirani wanajua leo kuna vita kati ya Mr na Mrs wake na baada ya muda wanarudi kwenye mstari. Wengine vita vyao huwa slow, kimya kimya, hakuna kelele ni cold war na kila mmoja huanza mbali na mwenzake kihisia, kiroho na kimwili polepole ila matokeo yake ni hatari tupu.

Kama ni mwanandoa mpya ni vizuri kuwa makini katika maamuzi mbalimbali mnayofanya na kufikiria kwa makini huku ukiangalia zaidi ya miaka 5 ijayo, kwa mfano;

Jerry na Judy wameamua baada ya kuoana tu wanazaa mtoto haraka iwezekanavyo kwa kuwa kila mmoja ana kazi hivyo shida ipo wapi kama pesa zipo. (Ingawa ukweli pesa huwa hazitatui matatizo yote)

Hata hivyo uamuzi wa kuwa na mtoto haraka kabla hawajajuana vizuri na kufikia mahali wakawa wanafahamiana tofauti na uchumba ni jambo la msingi. (siyo lazima ukubali huu ushauri kwani inatokana mmejuana kiasi gani na mchumba wako)

Kuna watoto wakizaliwa huja na package ambayo mzazi hulali kama vile kulia (cry) muda wote na mke kumtumikia huyo mtoto all the time (acha ile ya kumaliza madaktari wote kujua kwa nini mtoto analia usiku mzima na wanakwambia hakuna tatizo) na kufikia mahali mume akawekwa pembeni kwani mtoto kwanza na wakati huohuo ndoa bado changa.

Mke hujikuta mtoto anamuhitaji na mume anamuhitaji na hawawezi kubalance kwani bado ni mgeni na hii institution.


Watoto wengine huwa na matatizo ya kula, kiasi kwamba mama hujikuta hawezi hata kumwachia mtu yeyote amtunzie mtoto na matokeo yake mama hujikuta muda wote anatumikia mtoto na wakati mwingine kuacha kazi (ajira) na pia mume kuwekwa pembeni.

Matokeo yake wanandoa hujikuta wanakuwa mbali na feelings kufa na kila mmoja anaanza kuona ndoa hairidhishi wakati hata miaka 2 haijamaliza.

Jambo la msingi ni mwanamke kufahamu vizuri aina ya mume uliyenaye kwani kuna wanaume ambao wanaweza kuwa baba na kuna wengine ni kazi, wanaendana na usemi kwamba:

“Men don’t become fathers overnight, where as women have strong maternal instinct in them”

Suala la kule mtoto linahitaji mke na mume wote kushirikiana kuhakikisha si mmoja ndiye anakuwa na mzigo zaidi.

Tuesday, 21 June 2016

KUPENDELEA MTOTO MMOJA ZAIDI YA WENGINE.


Tabia ya kumpendelea mtoto mmoja au kila mzazi kuwa na mtoto wake ambaye anagusa zaidi moyo wake ipo sana katika familia zetu.Wengi huwa hawataki kulitaja au kuliongelea kwa undani ingawa ni kweli familia nyingi zitakiri kwamba hili ni tatizo sugu na pia inawezekana wewe ni mmoja ya watoto waliopendwa au ambao hawakupendwa na moja ya wazazi wenu.

1.Kwa nini upendeleo hutokea kwa mtoto mmoja?

Inawezekana tabia ya huyo mtoto ni njema zaidi kuliko wengine, wakipewa kazi mmoja anafanya na mwingine hafanyi mara zote, anayetii hujikuta anapendwa zaidi.
Inawezekana tabia ya huyo mtoto ni rahisi na mwenzake au wenzake ni ngumu.
Inawezekana mtoto anafanana na mzazi zaidi kuliko wengine (tabia na mwonekano).
Inawezekana huyo mtoto anafanikisha matarajio ya wazazi wake au mzazi mmoja.

Inawezekana kwa sababu ni mvulana peke yake au msichana peke yake mzazi hujikuta anampenda zaidi.
Pia inawezekana talents zake au vipaji vyake vinafanana na vile mzazi anataka mtoto awe au inawezekana ndiyo values za familia.
Pia inawezekana mtoto asiyependwa ni mtoto ambaye ni mbishi au ni mtoa hamasa (challenge authority) kuliko mwenzake au wenzake. Mtoto ana njia zake au mitazamo yake kuhusu maisha na vitu hivyo wazazi au mzazi hujikutana wanabishana kila kitu.

Pia kuna mazingira ya kuzaliwa ambayo hufanya mtoto kupendelewa zaidi ya wenzake kama vile mtoto kuzaliwa siku au wakati (huohuo) ambao mzazi wa baba au mama (babu au bibi) yake anafariki, ingawa haina ushahidi wa kisayansi ila matukio mengi huonesha kwamba mtoto wa aina hii huonekana wa thamani kuliko wengine na ni kama vile roho ya babu au bibi huenda kwa mtoto anayezaliwa na wazazi kujikuta wanampenda kuliko kawaida.
Au inaweza kuwa ngumu sana mzazi kuweka bond na huyo mtoto kutokana na huzuni, stress na depression mzazi alipata wakati anazaa na wakati huohuo mzazi wake mwenyewe (baba au mama) naye anafariki.

Mtoto kuzaliwa bila kutegemea hasa baada ya wazazi kudhani wamemaliza kuzaa.
Mtoto kuwa na matatizo ya afya hivyo wazazi kutumia muda mwingi kwake na wengine kujiona mwenzao anapendelewa.
Wakati mwingine inatokea tu mzazi hujikuta anampenda mtoto fulani katika familia kuliko wengine.

2. Nini mojawapo ya Dalili za mtoto kupendelewa?

Kununuliwa zawadi zaidi ya wenzake.
Kutoa adhabu rahisi kuliko wenzake kwa kosa moja, wenzake wanakula fimbo yeye anaonywa tu.
Sherehe au sikukuu zake kuwa tofauti na wenzake kwa jinsi zinavyoandaliwa nk.
Wenzake wakiomba kitu hichohicho wanakataliwa lakini yeye anapewa au kuruhusiwa.
Mzazi kutumia jina lake kumaanisha watoto wake wote kama vile baba anarudi kazini na watoto hawapo na mtoto anayempenda anaitwa Ben na badala ya kuuliza watoto wapo wapi yeye anauliza “akina Ben wako wapi?”

Tumia muda mwingi na mtoto mmoja.
Kuonesha upendo wa dhahiri kwa mtoto mmoja nk nk nk.

3.Je, mtoto ambaye anajisikia hapendelewi na mzazi au wazazi hujisikiaje?

Mtoto anakuwa na wakati mgumu sana kujikubali na kujipenda mwenyewe kwa kuwa anaamini mzazi/wazazi hawampendi na anaweza kuwa na tatizo sugu la kutojiamini (chronic low self-esteem)
Mtoto hujiona duniani hakuna haki na kwa kuwa hatendewi haki na yeye anaweza kuanza kutowatendea haki wengine.

4.Je, mtoto anayependwa anaweza kupata madhara yoyote?

Ukweli ni kwamba hata mtoto ambaye anajiona anapendwa pia anaweza kupata tatizo la kukosa kujiamini kwani anakuwa too much spoiled.
Kwa kuwa anapendwa basi atajitahidi kufanya zaidi kwani anaamini asipofanya kila kitu juu anaweza kupoteza kuendelea kupata upendeleo hivyo kama ni shule atajitahidi kupata grades za juu, kama ni tabia atajitahidi asikasirike nk na matokeo yake atakuwa hajiamini na anaweza kupota msongo mawazo.

Mtoto anayependelewa anaweza kuwa si mzuri sana linapokuja suala la wenzake wa rika moja au walimu au watu wengine kwenye maisha kwani kile kitendo cha kujiona anapendelewa na wazazi au mzazi humpa kakiburi Fulani.

Mtoto anayependwa hujiona yeye ndo mzuri na huwa hakosei hata hivyo maisha hayako hivyo na matokeo yake atakuwa na wakati mgumu mbele ya maisha hasa llikija suala la kupambana na matatizo.

Hasara ya kumpendelea mtoto mmoja huendelea hadi kwa wajukuu na inaweza kuleta matatizo na migogoro kwa kuwa wajukuu wa watoto wote huanza kuzozana kwa kuwa mmoja wa wazazi wao alikuwa anapendwa zaidi na babu au bibi.


5.Je, kwa mume na mke ni tatizo?

Ndiyo kunaweza kutokea mgogoro kati ya mke na mume hasa kwa mtoto mmoja kupendelewa na mzazi mmoja, kwa mfano baba anampa fedha nyingi zaidi mtoto mmoja anayempenda bila kujali ni mdogo kuliko wenzake, mama akiona au kusikia naye huja juuu kitendo ambacho kitafanya ndoa iwe katika mzozo.

6.Je, unaweza kuepuka vipi kumpendelea mtoto mmoja?

Kwanza wewe mzazi jikubali kwamba wewe ni binadamu na kwamba katika watoto wako mmoja anakubalika kwako zaidi kuliko wengine.
Wasikilize watoto wengine ambao wanakwambia unampendelea mwenzao na usijilinde, wasikilize na anza kufanyia kazi yale wanasema (kuacha kumpendelea mmoja)

Gundua utofauti wa kila mtoto na kile anapenda kufanya (characteristics, skills, interest) na mhudumie kutokana na vile anavipenda.

Usiwalinganishe au kumsema mmoja kwa sababu ya mwingine kwani kila mtoto yupo tofauti, sentensi kama “mwenzako Ben akirudi shule anafanya homework yake vizuri na anamaliza wewe hadi ulazimishwe!”
Ni kweli amekosea hata hivyo kila mtoto yupo tofauti na kila mtoto anatakiwa kuambiwa kama yeye na si mwingine.
Kama unanunua zawadi ni vizuri kununua zawadi zinazolingana siyo mmoja unanunua zawadi ya Tsh. 100,000 na mwingine Tsh. 20,000
Tumia muda vizuri na sawa kwa watoto wote.

Kumbuka jinsi unavyozidi kuwa na watoto wengi ndivyo utakuwa na kibarua kigumu zaidi, kwani unahitaji kutafuta muda maalumu kwa kila mtoto na kugundua kipaji chake na kuhakikisha unakiendeleza sawa na watoto wengine.

Jambo la msingi ni kila mzazi kumpa (treat) kila mtoto sawa katika hali zote na juhudi za ziada zinahitaji katika mazingira ya nyumbani kuhakikisha watoto wote wanalelewa sawa na kila mmoja kujiona ana thamani sawa kwa wazazi mmoja mmoja na kwa pamoja.

Thursday, 16 June 2016

NDOA IMARA NA ZINAZODUMU.


Ukiona kosa moja kwa mke wako au mume wako, hutakiwa kuliangalia na kuliwekea sura kamili au hutakiwi kulipa uhai badala yake lipe jina na liweke kando kwa kujaribu kulinganisha na uzuri wake au mambo matano mazuri kuhusu yeye(positive traits).


Kwa mfano unajikuta mume wako au mke wako amewaka hasira kwa jambo dogo tu hadi unahisi dunia umebadili mwelekeo, hata hivyo badala ya kuanza kufikiria hizo hasira zake Unachotakiwa kufanya ni kujiambia mwenyewe kwamba:

“ Ni kweli ana hasira hata hivyo ni mwanamke/mwanaume anayenijali, anayenipenda, anayewajibika, ni mbunifu na anajua kuniridhisha chumbani”.

Kumbuka strongest relationships ni zile ambazo partners wanaweza kujenga picha ya uzuri wa mwenzake (idealized/illusioned) kuhusu uwezo wake na si udhaifu.


Kwa kuufuta udhaifu au kuondoa mawazo kuhusu udhaifu wake na kuweka uwezo wake au uimara wake unahusanisha information muhimu za kufanya mke wako au mume wako awe mzuri zaidi na ukampenda zaidi.

Kwa miaka zaidi ya 100 hekima na busara iliyodumu na ambayo hata wengine wanaamini ni ile kwamba kinyume cha uzuri ni ubaya.

Hii ina maana kwamba Ukitaka kujua uzuri wa kitu basi unatafuta ubaya wake kwanza.

Ukitaka kujua furaha ni kitu gani au ina thamani kiasi gani unajaribu kumchunguza mtu mwenye huzuni kwanza.

Watoto ambao wanatumia madawa ya kulevya hutumika kujua namna ya kuwalinda watoto wasiotumia madawa ya kulevya wasijiingize kwenye hivyo vitendo.


Watoto ambao ni watoro shuleni hutumika kujifunza kuwafanya watoto wengine wawe na mahudhurio mazuri.


Linapokuja suala la ndoa si kweli kwamba ili kujifunza ndoa kuwa nzuri au kusiwe na talaka basi ni vizuri kujifunza ndoa ovyo au ndoa ambazo zimeishia kwenye talaka.

“Bad is not always the opposite of good”

Ukweli ni kwamba linapokuja suala la ndoa Ukitaka kujenga ndoa nzuri au imara unahitaji kujifunza kutoka ndoa imara na si ndoa ovyo au zile zimeishia kwenye talaka.

Vitu vinavyopatikana kwenye ndoa imara havina uhusiano na vitu vilivyosababisha ndoa ovyo kuwa ovyo kwani ndoa imara zina siri yake ambayo si kinyume cha ndoa ovyo.


Ndoa imara ni zile ambazo mwanandoa mmoja au wote huwa na picha kamili ya mwenzi wake, huwa na sifa ambazo amezijenga kwa mwenzi wake ambazo ukweli ni kwamba inawezekana kwamba mwenzi wake hana ila yeye huamini anazo na ni kuwa positive kwamba anamfaa.

Ndoa imara na zinazodumu ni zile ambazo mwanandoa huamini katika uimara au uwezo wa mke wake au mume wake hata kama huo uwezo hana.

Unaweza kuona kama ni utani au contradiction hata hivyo ndio ukweli.

Nina amini mke wangu ni caring, nina amini mke wangu ni sweetie, nina amini mke wangu ananifaa, nina amini mke wangu ni mzuri, nina amini mke wangu ni mchapa kazi, nina amini mke wangu ni mrembo, nina amini mke wangu ananifaa hata kama hizo sifa hana kwa kuwa naamini basi ninavyoamini ndivyo itakuwa na nitakuwa na furaha kuliko kuwaza vinginevyo.

NI VIZURI KUWA WAZI.


Kawaida linapokuja suala la mapenzi opposite attract na the same repel kwa maana kwamba mara nyingi huwa tunavutiwa na strength za mwingine kwa kuwa hufanana na weakness zetu.
Watu ambao hutuvutia sana ni wale ambao huonesha strength katika maeneo ambayo sisi tupo weak.

Ukikutana na mtu wa jinsia tofauti na wewe na mkawa pamoja kwa muda mrefu pamoja na ukavutwa kutokana na strength zake ambazo zinakubaliana kwenye weakness zako penzi huzaliwa na baadae inaweza kuwa ndoa

Ndoa ni kuwekana wazi.

Wakati Bwana harusi na Bibi harusi wanaposimama mbele ya Mhubiri kanisani na kutoa ahadi zao kwa Mungu na wageni wote walioalikwa huwa wanaahidiana kwamba
“Ninakuahidi kukupenda na kukunyenyekea kwa muda wote wa uhai wetu”
Hii ina maana kwamba maharusi huwa wanakazia kwamba kwa kuwa nakubali kiapo chako na unyenyekevu wako kwangu leo basi nitajifunua kwako mzimamzima kuanzia sasa si kimwili tu bali kisaikolojia pia kwani hadi hapa nimejidhihirisha/nimejifunua kwako katika upande ule wa mazuri tu (strength) kuhusu mimi.
Sasa kwa kuwa tunaoana nitajiweka wazi kwako mzimamzima na nina imani kubwa na wewe kwamba utaendelea kunipenda kama nilivyo.

Ndoa ni kuwekana wazi, ni kila mmoja kujidhihirisha kwa mwenzake kama alivyo pamoja na weaknesses zake.
Vitu vyote ambavyo vilikuwa vimejificha wakati wa uchumba hadi honeymoon basi kuanza kwa ndoa vyote huwa mezani juu kwa kila mmoja kuona.
Na hapo ndipo kwenye mtihani wa kwanza wa wanandoa wapya.
Honeymoon siyo residence ya kudumu ya ndoa, baada ya honeymoon (na wengine hata wakati wa honeymoon) wanandoa wapya hushikwa na mshangao wa partner anavyobadilika na kuwa kama mwingine kabisa.
Ukweli ni kwamba unapoona partner wako anaonekana kama mwingine tofauti na yule wa wakati wa uchumba, ukweli ni kwamba sasa matching inaanza, kufahamiana kikwelikweli kunaanza na wenye hekima na busara huwa makini katika kukabiliana na hizo tofauti na kuendelea kusherehekea hizo tofauti kwa upendo na kuvumiliana kwani huwezi kumbadilisha na kumbadilisha ni kupoteza muda wako.

LOVE MAY BE BLIND BUT MARRIAGE IS A REAL EYE-OPENER.

Wednesday, 15 June 2016

TOFAUTI HUWA HAZIKOSEKANI.


Wanandoa imara au waliofanikiwa katika ndoa yao ni wale ambao wanaweza kukaa pamoja na kujadili tofauti zao katika namna ambayo huwezesha kujenga ukaribu kimapenzi (intimacy) zaidi.

Wanafahamu jinsi ya kukubaliana na kutokukubaliana, wanafahamu namna ya kuhakikisha kutokukubaliana hakusababishi maafa kwenye maeneo mengine ya mahusiano yao.

Si kweli kwamba tunaolewa au kuona ili kuchukuliana katika migogoro hata hivyo kutofahamu namna ya kupambana na migogoro huweza kusababisha kutofanya vizuri katika mambo mengine ambayo ndo sababu za kuoana.

Kukwepa migogoro au kukwepa kuongea pamoja eti kunaweza sababisha mgogoro mzito si hekima wala busara kwani njia bora ni kuwa wazi kuongea pamoja ili kujadili tofauti au kutokuelewana kunakojitokeza ili wanandoa waweze kufahamiana zaidi.

Kwa lugha nyingine si rahisi mke kufahamu mume anapenda chakula gani bila kuongea kwanza, pia haina maana kukaa kimya kwa kuwa mke anapika chakula usichopenda basi atabadilisha na kukupikia chakula unapenda. Si rahisi mume kukupeleka outing kama hamuongei.

Wapo wanandoa ili kuepuka migogoro huacha kuongea na kuwa kimya, ni muhimu sana wanandoa kufahamu utafiti wa ndoa imara unasemaje.
Kila ndoa imara kwa wastani ina maeneo 10 ambayo wanandoa hawafanani au hawawezi kukubaliana au kwa lugha nyingine hawataweza kufikia muafaka maishani mwao.

Kwa nini hizi ndoa imara pamoja na tofauti 10 na bado zinaitwa ndoa imara?

Jambo la msingi au siri kubwa ni kwamba wanandoa wanafahamu namna ya kukabiliana na hizo tofauti na kuishi nazo, kupendana pamoja na kutofautiana na zaidi kila mmoja anamuelewa mwenzake na kukubaliana kihisia na kuchukua nafasi yake kama ni yeye.

Wanandoa imara hufurahia na kusherehekea tofauti zao na hufarijika kwa kuwa sasa anamfahamu mwenzake, anajua eneo ambalo wapo tofauti then wanaaendelea kupendana huku kila mmoja akifahamu namna ya kukabiliana na hizo tofauti.

Hawa wanandoa imara wanafahamu wazi kabisa kwamba hata kama watabadilisha partners bado watapata matatizo mapya katika maeneo ya kutokukubaliana, kuwa tofauti na kwa huzuni kubwa kazi kubwa itakuwa ni mizigo waliyotoka nayo kwenye ndoa zao za kwanza kama vile watoto nk ndiyo maana kwao talaka haina sauti wala nguvu na huwa haizungumzwi, ni neno lililofutwa katika maongezi.
Zaidi ya kukabiliana na tofauti na kutokukubaliana pia ni muhimu sana kusherehekea/kumbatia (embrace) mabadiliko.
Wakati tunaoana huwa tunaahidi kukaa pamoja hadi kifo kitakapo tutenganisha hata hivyo huwa hatuahidi kubaki vilevile bila mabadiliko yoyote, tunahitaji kukua, kuongezeka skills, kwa wabunifu na wazuri zaidi kila siku zinavyozidi kwenda.
Kuna mambo mengi tunaweza kujifunza kadri ziku zinavyozidi kwenda kama vile kusema asante, kuomba msamaha.
Hivyo inawezekana kujifunza tabia njema ambazo zinaweza kujenga ndoa na kuziacha tabia mbaya ambazo zinaweza kuharibu ndoa.

MTAZAMO WAKO UKOJE?


Huwezi kuongelewa mapenzi bila kutaja suala la pesa. Wapo watu ambao wanaamini kuwa na pesa nyingi, nyingi kabisa za kutosha husaidia pesa kuwa imara na linaloridhisha.
Hata hivyo tumeona penzi la uhakika hata wakati pesa zikiwa hazipo au tumeona penzi la kweli hata katikati ya umaskini uliokithiri.
Hii haina maana kwamba pesa siyo muhimu, pesa ni muhimu sana. Na pesa ina umuhimu kwa kila mahusiano hata, hivyo inabidi ujiulize mwenyewe je, upo kwa ajili ya pesa au kwa ajili ya penzi la kweli.
Utakuwa mtu wa maana sana kama utakuwa unatazama na kuwekeza kwenye penzi la kweli na si pesa.
Pia ni vizuri kuwa makini na mtazamo wa mpenzi wako je yupo kwako kwa ajili ya pesa au kwa ajili ya penzi la kweli.
Mtazamo wake kuhusu pesa ni muhimu sana.