Thursday, 31 March 2016

KUPOTEZA HISIA..

“Nimepoteza hisia za kumpenda, zimepotea na zimepotea kabisa.
Simpendi kabisa mke wangu na hata sifahamu kama kweli niliwahi kumpenda; nashangaa na sihitaji kuwa naye tena, sijisikii chochote linapokuja suala na hisia zangu kwake naamini ndoa imefika mwisho” Jerry aliongea kwa mshangao mbele ya mkewe.

Mkewe naye akajibu kwa kusema “hata sielewi tumefikia vipi hatua hii.
Tunaongea mara chache sana na hata tukiongea hatuongei jema lolote, (machozi yanaanza kumiminika kwenye mashavu) ni kulaumiana, kudharauliana, kusutana, kila mmoja anampuuza mwenzake, ndoto zimeyeyuka na hakuna ladha ya maisha.
Hapa nina maumivu makali.
Hivi inawezekana mtu ukashindwa kabisa kumpenda mtu ambaye alikuwa bila yeye maisha hayana maana?

Hali kama hii huwakuta wanandoa wengi na watu wengi walio katika mahusiano; haijalishi ni miaka mingapi au mlikuwa mnapendana kiasi gani na bila kujifahamu vizuri na kutumia busara na hekima kumaliza hili tatizo ndoa au mahusiano huweza kujikuta yameangukia kwenye shimo lefu mno.

Kila ndoa ina positive na negative moments, mwanandoa mmoja akiwa anamwangalia mwenzake kwa negatives tu itafika mahali ataanza kuji – withdraw na kujiweka mbali na automatically ataanza kujisahau kuwa caring. Wakati mmoja anajiweka mbali na mwenzake huyu mwingine huanza ku-panic na kuanza kutoa lawama kwamba hupendwi. Wanavyozidi kusuguana ndivyo wanazidi kusababisha mafuriko ya lawama emotionally na matokeo ni kuwa disconnected katika emotions na feelings.


Kuna utafiti kuhusiana na positives na negatives kwenye suala la ndoa na mahusiano na kutoa jumuisho kwamba quality ya emotions ilizonazo kwa mwenzi wako ni muhimu sana.
Ni simple lakini muhimu sana katika mahusiano.

Kama positives zitakuwa nyingi kuliko negatives unavyomchukulia mwenzi wako basi mahusiano yatakuwa bora sana, haleluya Kubwa!
Na kama negatives zitakuwa nyingi kuliko positives katika hisia kwa mwenzi wako basi shughuli nzito inakuja mbele yenu!

Ukweli ni kwamba negatives moja huhitaji positive tano ili kufanya balance ya ndoa au mahusiano kuwa katika hali nzuri (feelings).
Hii ina maana ukimbomoa mwenzi wako mara moja basi inabidi umjenge mara tano zaidi ili ku- balance ule uharibifu umefanya mara moja.
Kila negative moja unahitaji positive tano ili emotions na feelings za mapenzi yenu kurudi kuwa katika hali ya kawaida.


Wednesday, 30 March 2016

NI MUHIMU PIA..

Ulipooa au kuolewa kulikuwa na sababu na pia ulifanya commitment kuhakikisha unatumia muda wako wote wa maisha yako na yeye milele na milele au hadi kifo kitakapowatenganisha.


Kama unataka kuwa na mume mzuri anayehakikisha anakutunza wewe na watoto wako na ana ku-treat vizuri au kama unataka kuwa na mke ambaye siku zote mambo ni safi kila siku, basi unahitaji ku-invest vilivyo kwenye ndoa yako.
Jitahidi kumpa romantic life kila iitwapo leo, kufanya juhudi kukitunza kile ulichaonacho, kwani usione vinaelea vimeundwa na wewe pia unaweza kukiunda chako kikaelea, uwezo unao na muda ni sasa.
Ili ndoa iwe imara unahitaji kutumia muda wako na nguvu zako ili maisha yawe safi wewe na mpenzi wako.

Kuna vitu tunaviita vidogo sana ambayo ni muhimu sana katika kila ndoa yenye furaha na afya, hivi vitu havilengi kufanya mapenzi (tendo la ndoa) moja kwa moja



Hivi ni vitu muhimu na havitakiwi kuachwa kwa kila ndoa imara na yenye afya na ndoa imara na yenye afya huleta raha si kwa wahusika tu bali kwa familia nzima kwa jamii inayowazunguka na taifa pia.

Ni vitu gani hivyo vidogo Muhimu?

Kumpa mgusu wa kimwili mwenzako,

Kumshika kwa mikono yote (holding),

Kumkumbatia.

Kuongea pamoja au kumsikiliza mwenzanko dakika 10 au 15 kila siku.

Kuongea na mwingine kumsikiliza mwenzake kila siku kunajenga ukaribu na kuaminiana, na kupeana mguso wa kimwili kila usiku na asubuhi husaidia kila mmoja kujiona ni wa thamani kwa mwenzako.

Inakuwaje hapo?
Je, umewahi kusikia kitu kinaitwa "Njaa ya ngozi"

Basi, njaa ya ngozi ni mwitikio wa kihisia kutokana na kukosa kuguswa kimwili.
Binadamu huhitaji kiwango fulani cha kugusana ngozi kwa ngozi kila siku ili kuishi na kukosa hicho kitendo basi ngozi hupata njaa na matokeo yake mtu hudhoofika.

Njaa ya ngozi ndiyo inayosababisha sana wapenzi kutaka kufanya tendo la ndoa
Katika milango mitano ya fahamu, kugusa ndiyo mlango pekee wa fahamu unaojulikana kuwa ni muhimu kuliko yote, kitaalamu umuhimu wa kuguswa (touch) huzidi ule wa chakula.
Kuguswa ni mlango wa kwanza wa fahamu kujitokeza wakati wa mtu anazaliwa na huwa mlango wa mwisho wa fahamu wakati mtu anakufa.
Na kuna wana ndoa wengi sana wanapata njaa ya ngozi bila wao kujijua hapa hatuzungumzii kufanya mapenzi bali tunazungumzia nonsexual touching kama vile kukumbatia, Mguso wa mtekenyo.

Kuguswa (touch) ni moja ya muhitaji muhimu ya Binadamu hivyo Hakikisha kila siku unampa mpenzi wako Mguso wa kimahaba iwe kumpa busu huku umemshika au umemkumbatia.


Kitu kingine kidogo muhimu ni nini?
Kitu kingine muhimu ni kwa mwanamke kuwa na vivazi vinavyoacha mwili wazi ukiwa chumbani.

Tafuta chupi ambazo zinavutia kwa mume wako kukuangalia mkiwa wawili tu hata kama hamjapanga kufanya mapenzi hiyo inampa hamu na kujiona anakuhitaji zaidi kila siku.
Kuna wanandoa ambao kwao kuwa mikao ya hasara hasara na uchi chumbani ni mwiko, hapo mnajinyima raha mwenyewe.

Friday, 25 March 2016

JIAMINI..

Fikiria wewe ni mwanamke na upo uchi mbele ya kioo chumbani,
Je, unapenda vile unajiona nywele, pua, matiti, tumbo, hips, mapaja, sehemu za siri?
Kama unajiona upo beautiful hongera mikono juu kabisa, na kama huridhiki pole hujiamini.Mwanaume huweza kusimamisha uume kila dakika 15 akiwa amelala usiku na mwanamke huweza kutoa majimaji (lubrication) kwenye uke wake kila dakika 15 akiwa amelala.

Binadamu ni wanyama pekee ambao hamu ya kufanya mapenzi au kufanya mapenzi (sex) si kwa ajili ya kuzaliana tu bali kupena raha ya kimahaba (sexual pleasure)

Pia Clitoris (kisimi) ni kiungo pekee katika mwili wa mwanamke kipo kwa ajili ya kumpa raha ya mapenzi, hakuna kazi nyingine ni hiyo tu.

Raha ya sex kwa mwanamke si katika uke tu kama alivyo mwanaume kwa uume wake bali ni zaidi ya hapo yaani mwili mzima.

Data zinaonesha kwamba wanawake ambao wamepatwa na matatizo ya ut wa mgongo (spinal cord injuries) na hawawezi kuhisi kitu chochote kuanzia kwenye kiuno kushuka chini bado wana uwezo wa kufika kileleni
Sababu kubwa ni kwamba ubongo hupokea hisia (feelings) za kusisimuliwa kimapenzi kupitia njia zingine nje ya uti wa mgongo hasa mwanamke anapochezewa matiti au kissing nk.
Hii ina maana mwanamke mwili mzima ni single sex organ tofauti na wanaume wanaowaza kwamba ili mwanamke afurahie mapenzi ni lazima uhakikishe unachimba vizuri Gold kule bondeni.

Quality ya mapenzi katika ndoa si mara ngapi mnafanya kwa siku au kwa wiki au kwa mwezi au kwa mwaka bali ni kuridhishana au kuridhika kwa wahusika kutokana tendo lenyewe.

Jamii inawadanganya wanawake kwamba wakiwa na sura fulani, au uzito fulani watakuwa wazuri katika mapenzi.
Thubutu, Mwanamke yeyote akiwa uchi mwanaume yeyote humuona ni mrembo na huchanganyikiwa kabisa.
Haina haja kuzima taa au kutaka giza eti kwa kuwa matiti yako ni makubwa mno au madogo sana, au mwili umenenepa sana au mwembamba sana, au ngozi upo tofauti na unavyodhani.
Ukiwa uchi tu mwanaume hukuona bonge na beautiful woman.

Pia jamii inapotoshwa kwamba kitendo cha mwanaume kusugua uke kwa uume wake kwa kila aina za style ni tendo linalompa mwanamke raha ya mapenzi.

Ukweli si wanawake wote hufikishwa kileleni kwa uume kuwa ndani ya uke tu (clitoral and viginal stimulation) bali kwa mwili mzima kama single sex organ na pia kuandaliwa kwa muda unaotakiwa.

Jamii imezungukwa na tamaduni zinazofanya mwanamke kujiona akiwa na shape Fulani au size Fulani ndipo atafurahia sex kitu ambacho ni kweli kwani ili mwanamke afurahie sex kwanza lazima ajifahamu mwenyewe na kuufurahia mwili wake kama ulivyo kujiamini kuhusu self esteem na body image yake.

Kuna asilimia zaidi ya 50 ya wanawake huwadanganya waume zako kwamba wamefika kileleni kitu ambacho si kweli ili mambo yaishe.
Kwa nini wanadanganya?
kwa sababu wanaume wengi huwa hawawaandai vizuri so anaona afahadhari aone amefikishwa maana lengo la wanaume wengi huwa kumfikisha mwanamke kileleni na si kumpa raha ya mapenzi.

MIGOGORO YA NDOA,HUATHIRI AFYA.

Kuolewa au kuoa ni kitu kingine na kujenga ndoa ni kitu kingine.
Ndoa yenye furaha huwa haijengwi siku ya ndoa au siku ya harusi au siku ya kuvalishana pete tu bali hujengwa kila iitwapo leo.

Ndoa inapokuwa na mgogoro mara nyingi (si zote) wanandoa huathirika zaidi na mara nyingi mwanamke huonekana ni makini na kuelekeza juhudi nyingi ili mahusiano yaendelee na kuwa yenye afya njema

Migogro mingi ya mahusiano (Ndoa au uchumba) mara nyingi mwanamke ndiye huathirika zaidi.
Wanaume hata kama ndoa ina mgogoro bado huonekana wapo physically fit na mentally fit kabisa nakuendelea kujichanganya na wenzao kama vile hakuna linaloendelea ktk ndoa zao wakati wanawake ndoa ikiwa na tatizo basi kwa kumwangalia tu unaweza kupata ujumbe kamili achilia kukoswakoswa kugongwa na magari.

Why?
Wanawake na wanaume hutofautiana sana jinsi ya kukabiliana au kuchimbua (ku-process) hisia (feelings), tukuto (emotions) zinazotokana na mgogoro uliopo.
Wanaume huweza kuvumilia tukuto na hisia zao bila kutegemea mwanamke au kuegemea kwa mwanamke, hii ina maana kwamba mwanaume hujikana, hujiondoa, huwa hajali, hu-withdraw hisia zake au kujisikia kwamba ana mgogoro na matokeo yake haathiriki sana.

Wakati huohuo mwanamke yeye kwanza ni mtu wahisia na tukuto (feelings & emotions ) tatizo likitokea hujihusisha zaidi, huji-engage, hujitoa (dedicate), huji-commit kupata solution, hujiuliza maswali wengine watasemaje? huwaza zaidi kuhusu yeye na mpenzi wake na jinsi ya kusaidia mgogoro uishe, matokeo yake huathirika zaidi na hudhoofisha afya yake na kuweza kukumbwa na magonjwa kama shinikizo la damu, stress, depression, stroke, magonjwa ya moyo nk.

MWANAMKE AFANYEJE?
Jambo la msingi ambalo mwanamke anaweza kufanya ndoa inapokuwa katika mgogoro ni kumuomba Mungu ampe hekima, busara na ushindi ili ndoa iwe katika mstari kwani ni jaribu na lazima ushinde, kila ndoa bora imejaribiwa na kuonekana imara, usione vinaelea vimeundwa.

Pia mwanamke anahitaji kuwa positive, kwamba anaweza na kwamba bado ndoa ipo, mume ni wake na aendelee kumpenda na kutamkia mambo mazuri mume wake kuliko kuwa na mtazamo negative.
Pia mwanamke anahitaji kujiamini kwamba chanzo cha furaha yake ni Mungu hivyo hakuna binadamu anaweza kuondoa furaha yake hadi aamue mwenyewe.

WANAWAKE HUJISAHAU.

Tatizo kubwa la wanawake wakiwa kwenye mahusiano (ndoa au uchumba) ni kwamba huwa wanasahau mahitaji yao na kujikuta wanavutwa na kuhusika zaidi na mahitasji ya wengine au wapenzi wao kihisia na kisaikolojia.

Challenge kubwa inaowakabili wanawake wote duniani wakishaiingia kwenye mahusiano ni uwezo wa kuimarisha sense of self, kujitambua, kujiamini, na kuanza na wao kwanza kabla ya mpenzi hasa linapotokea suala la mgogoro.
Wakati mwanamke hu-expand mwanaume hu-contract.
Kama ilivyo nguvu ya centripetal amabyo huhusika kuvuta kitu katikati (mwanaume) na nguvu ya centrifugal ambayo huhusika kuvuta kitu pembeni (mwanamke) kutoka katikati ndiyo ilivyo kwa mwanamke na mwanaume kwani mwanaume mara zote hurudi kwenye centerpoint hupungua, husinyaa, huongea kidogo, huongea kwenye point, wakati mwanamke yeye hupanuka kutoka katikati kwenda pembeni, huongea sana hata kama si point, huvutika kuongeza maongezi.

Ndiyo maana wanaume hulaumiwa sana linapokuja suala la mawasiliano kwani mwanamke na mwanaume wanapoongea mwanamke hu-expand maongezi na mwanaume hui-contract na kuongea kwenye point.

Kawaida mwanaume hufikiria kwanza (kwa ndani) kile anataka kuongea ili kujua kama ni point, wakati mwenzake mwanamke huendelea kuongea tu na anapoongea inamsaidia kuijua point,
Hii ina maana mwanamke huongea iliajue point na mwanaume hujua point ili aongee.

Bila kujua hii tofauti basi mwanaume asiyejali anaweza kusikitika sana kumsikiliza mpenzi wake na kuona alikuwa anaongea pumba au pointless na amempotezea muda wake au kuendelea kubishana kwamba mwanamke haongei point au kumkatisha kwa kuwa anachoongea hakielewiki.

Mwanaume anayejali husikiliza kwanza hata kama mwanamke anaongea kitu ambacho anahisi hakieleweki hata hivyo baadae ataelewa na mwanamke anajisikia mwanaume anamjali na kumsikiliza na maisha yanaenda

UMUHIMU WA KUPEANA ZAWADI KTK NDOA.

Mwanamke anahitaji alama za upendo kutoka kwa mwanaume.
Mwanaume anapompelekea mwanamke (mkewe) zawadi hii hudhihirisha kwamba mwanamke ana thamani na anamjali, mfano zawadi ya maua huonesha kwamba mwanamke ni mrembo na ana uzuri ambao mwanaume anaukubali.

Iwe zawadi kubwa au ndogo zote hutoa maana halisi ya mapenzi, humsaidia mwanamke kufahamu kwamba yeye ni mwanamke special, na kumpa zawadi mwanamke ni njia ya kumpa heshima na thamani ambayo mwanamke huhitaji kutoka kwa mume wake.

Kuna alama nyingi ambazo huonesha kwamba unampenda mke wako moja ni kumpa zawadi mbalimbali kama maua au kadi yenye ujumbe unaoelezea hisia zako kwake nk.
Ni muhimu mwanaume kuwa creative na innovative katika kuhakikisha penzi linazidi kunawiri kila iitwapo leo katika ndoa yako na unajitahidi kutoa hisia zako original pale unampa zawadi au kumwandikia text message (sms) yoyote, kitu cha msingi afahamu kwamba kuna mwanaume anayemjali.

Wanaume wengi huwa wanakuwa wataalamu na wajuzi sana wa kuwapelekea wapenzi wao zawadi motomoto na kadi zenye maneno matamu matamu mwanzo wa mahusiano (uchumba au ndoa) na baada ya muda wanaachana kabisa na hiyo tabia, hili ni kosa kubwa sana ktk masuala ya ndoa, kutoa zawadi hakuzeeki wala ku-expire hudumu na kudumu na kudumu, ni njia muhimu sana ya Kuonesha unamjali mke wako.

Kama ni mwanamke unakumbuka lini mpenzi wako amekuletea zawadi?
Na kama ni mwanaume je, unakumbuka ni lini umempelekea mke wako zawadi?
Eti haya mambo yamepitwa na wakati!
Shauri yako!
Usione vinaelea vimeundwa!

Wanawake wengi kwenye ndoa au mahusiano hujisikia na kujiona hawapendwi na waume zao, hujisikia wanaume hawawajali, ukiangalia kwa undani moja ya sababu ni mwanaume ameacha kumpa zawadi hata ndogondogo, au maneno mazuri (notes) au kadi kama alivyokuwa anafanya mwanzo na kwa sababu ulikuwa unampa na umeacha anajiona humpendi tena, si ulikuwa unampa? sasa imekuwaje? unampelekea nani tena? maana ulikuwa na tabia ya kutoa zawadi.

Kiwango cha attention unayompa mke wako ni alama muhimu ya Kuonesha upendo wako kwake.

Mwanamke hujisikia anapendwa na kwamba unamjali pale mwanaume:-
Unampompa zawadi iwe ndogo au kubwa,
Unapompa zawadi ya kadi yenye maneno mazuri yanayoelezea hisia zako kwake,
Unapomhudumia kwa kumjali,
Unapomsikiliza yeye na kujiona anasikilizwa,
Unapojitolea kumsaidia kazi ndgondogo na mambo ambayo anajisikia upo na yeye,
Unapompa plan za mambo mbalimbali mnayotaka kufanya pamoja kama familia iwe "outing", likizo, business n.k,

Pale unapomuuliza anavyojisikia hasa baada ya kazi au unapohisi emotions zake hazipo sawa,
Unapochukua muda wa ziada kuwa naye na kuwa kwa ajili yake,
Unaposhirikiana naye ktk huzuni au tatizo huku ukimfariji na kumkumbatia,
Unapompa nafasi ya kujisikia huru kwako hata kudeka (si wote)
Unapogundua kwamba amevaa amependeza mavazi na nywele na kumpa sifa anazostahili.
Unapom-surprise na zawadi au notes na
Unapompigia simu ukiwa umesafiri na kumuulizia anaendeleaje na jinsi gani utakuwa unaongea naye na kuwasiliana naye.

Thursday, 24 March 2016

HAMU YA MAPENZI KUPUNGUA KTK NDOA.

Unapoona au kuhisi hali hii kutokea,
Jambo la msingi napenda kukukumbusha tu kwamba unatakiwa kufanya yale ulikuwa unafanya pale mwanzo kama vile:-

Je, unakumbuka namna mlikuwa mnapeana kisses na hugs pale mwanzo?

Tafuta muda na uwe na muda wa kumfurahia mwenzako kwa kumpa ladha za mabusu kwenye lips zake.

Maandalizi ya moto wa mapenzi huanzia nje ya chumbani hivyo ni busara kuhakikisha unakuwa connected na mke wako kwa kuwa na mawasiliano mazuri kimwili, kiroho na kimoyo.

Je, mnapomaliza sex huwa inakuwaje?

Kama huwa unazama kwenye usingizi na kumwacha mke wako bila kuendelea kuwa mwilini mwake na kumweleza namna unajisikia na raha unayopata na namna unavyompenda, Kumbuka wakati kama huu ni muhimu kuwa karibu zaidi kuliko mwanzo wa maandalizi ya kufanya mapenzi.

Je, unaendelea kuwa mwanafunzi wa kujifunza na kuwa mbunifu chumbani kwako?

Je, unajua mke wako anasisimka zaidi kwa kumfanyia vitu gani?
Vumbua maeneo yote anayoweza kusisimka kwani huwezi kufanya kile kile kila siku na akajisikia kusisimka na excited kwani si vibaya sana mke wako kufahamu kwamba mkiingia chumbani anajua utafanya 1, 2, 3, 4 kama kawaida yako.
Pia fahamu anaposema nimeridhika kwake ina maana gani.
Zaidi kumbuka unavyoendelea na ndoa mambo hubadilika, kuna masuala ya kazi, majukumu, maisha nk na kuna wakati mke huchoka, huwa na nguvu, hukasirika, huweza kutokea huzuni na misiba nk hii ina maana kuna aina mbali mbali za sex tofauti na siku ya honeymoon wakati ule wote lengo na mitazamo ulikuwa kupeana raha na kila mmoja alikuwa na matarajio makubwa sana.
Kuna wakati mke wako atajisikia hamu kubwa ya kufanya mapenzi na kutamani kila kinachotembea akirukie, hapa inabidi ujue upepo umevuma ili apewe perfect sex, fireworks na jitahidi kuwa connected na yeye then atafurahia hata kufika kileleni mara mbilimbili, hapo kazi kwako!
Kuna wakati mmoja atakuwa anahitaji kubwa la sex na mwingine hana hiyo hamu na Jifunze kwamba mnaweza kupeana sex ya chapuchapu (quickie) na mwingine kuridhika na mwingine kuendelea na ratiba zake.
Inawezekana pia wewe ukawa huna mood ya sex lakini mke wako anakuhitaji.
Hapa huhitaji kung’ang’ania iwe kama ile ya jana.
Pia kuna wakati mke wako au wewe mmoja atakutana na shida au huzuni na mmoja atahitaji kumfariji mwenzake na hakuna kitu muhimu na kizuri kama mmoja aliyehuzunishwa kujikuta yupo kifuani na kuzungukwa na mikono ya mwenzi wake huku akipata maneno ya faraja na hata kushirikiana mwili hata katika huzuni (comfort sex).
Utakuwa hatua moja mbele kama utafahamu aina za sex katika ndoa na sababu zake na pia kufahamu kwamba lengo la sex wakati mwingine si kufika kileleni bali kuwa connected.
Pia uwe mwepesi kuweka wazi matarajio yako kwani mke huhitaji kuandaliwa kiakili kabla ya kuingia chumbani hivyo kama kuna migongano, mvurugano au jambo ambalo lipo pending bila kupewa ufumbuzi basi linapewa ufumbuzi kabla ya kuingia chumbani.
Kwa hapo Naamini unaweza kuwasha upya moto wa mahaba chumbani kwako na mwenzi wako kama mwanzo.