Wednesday, 18 November 2015

NI SEX TU?

Kila unaporudi nyumbani unakutana na mkeo anatabasamu namna hii mlangoni?????

Sex si sababu ya msingi au motivator kwa ajili ya mwanaume kutoka nje ya ndoa yake bali ni kukosa emotions, feelings katika ndoa yake.
Yapo magazeti, TV, Movies, blogs, radio na media zingine zinapiga kelele kwa sauti kwamba kukosekana kwa great sex ndiko kunawafanya wanaume kutoka nje ya ndoa zao hata hivyo tafiti ambazo zinakubaliana na Biblia na sayansi pia zinaonesha si sex bali emotions.
Ni kweli kwamba sexual skills, au ufundi wa kufanya sex huleta ladha na utofauti chumbani hata hivyo linapokuja suala la ndoa mambo ni tofauti.
Hitaji kubwa la mwanaume ni kuheshimiwa (respect, appreciation) kutoka kwa mke wake.
Mwanaume yupo wired kujiona ni winner na kitendo cha kukosa respect au appreciation nyumbani humfanya kujiona ni loser, failure na matokeo yake hujiona hapendwi na hujiweka mbali na mke.
Hii ina maana mwanamke anapoona mambo hayaendi sawa ndani ya nyumba kubadilisha sexual style si move nzuri ukilinganisha na kubadilisha namna unavyompa respect na appreciation.
Ili kumlinda mume asitoke nje jambo la msingi ni mara ngapi mume anapata sex na si ufundi au umaridadi ulionao katika kumzungusha kitandani.
Kabla ya kujikanyaga ili kupunguza uzito, dieting au kufahamu style mbalimbali za love makini ni muhimu sana wewe mwanamke kujua unakuwa available kwake mara ngapi kwa wiki au mwezi.
Hujasikia huu msemo:
Mume akipewa sex anakuwa so nice kwa mke wake na asipopata sex anakuwa jeuri.
Mwanaume akiwa appreciated na respected anajiona ni winner na moja ya sababu ya kumpa appreciation ni kumpa sex mara nyingi achana na suala la skills kwanza.
Je, anapokuwa nyumbani unaongea naye vipi?
Hasira, kukefyakefya au kunung’unika na kulalamika tu kwa kila jambo?
Je, unamshukuru na kumpa appreciation kwa kazi zile Anafanya hata kama ulitegemea uwe wajibu wake?
Je, unamsukuma kwa kila jambo unalotaka wewe afanye na hakuna tofauti kati ya mtoto na yeye?
Je, anapofika mlangoni jioni anaoporudi kazini unaonesha sura ya huzuni, hasira, kukata tamaa hadi anajisikia vibaya na kujiona hapo nyumbani yeye ni failure.
Kumbuka wewe mwanaume usipomfanya ajisikia vizuri basi mwanamke mwingine anaweza kufanya ajisikia vizuri na ikawa hatua moja kuelekea kuzamisha ndoa yako.

DALILI KWAMBA ANA "NYUMBA NDOGO"

Dalili za mwanaume anayechepuka

1. ANATUMIA MUDA MWINGI NJE NA NYUMBANI
Huwezi kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja na kila mmoja ukampa muda sawa.
Wengi huanza kubadilika na kukwepa kuwepo nyumbani na mke wake hata kabla ya affair.
Mwanaume kutumia muda mwingine nje ya nyumbani haina maana kwamba ana-cheat bali inaweza kuwa dalili kwamba ana cheat hasa kukiwa na dalili zingine.
Hata hivyo ukigundua mapema unaweza kuzuia na kuepuka maumivu ya cheating.
Wakati mwingine hawa wanaume huwafunga kamba wake zao kwamba
“Nikitaka kutoka nje, naweza hata muda wa kawaida hivyo nikichelewa haina maana na-cheat”
uwe makini na huo usemi kwani ukweli ni kwamba wanaume wengi hutumia muda wa ziada na si muda wa kazi kufanya cheating zao.
Ukiona mume ana dalili za kukwepa kuwepo nyumbani kama ilivyokuwa kawaida, basi inabidi uwe makini na kuchunguza kujua nini kinaendelea.

NINI CHA KUFANYA:
Ni vizuri kukaa pamoja na kujadili pamoja kuangalia kama kuna issues ambazo haridhiki nazo zirekebishwe haraka ili arudi kwenye mstari.
Pia jiulize:
Je, hapo nyumbani kuna amani, heshima, upendo, na utulivu?
Na je, namna unaongea na mume wako kuna respect? Au ni kulalamika, hasira, huzuni na yeye anajiona ni failure na loser?
Inawezekana huko anaenda kunampa kile anakikosa hapo nyumbani au kwako wewe mke.

2. TENDO LA NDOA MARA CHACHE
Kupunguza kwa kiwango cha sex kati ya mke na mume ni dalili mojawapo kwamba kuna kitu hakipo sahihi na mojawapo inaweza kuwa mume anachepuka kwa “yule mwanamke”.
Pia unaweza kuijua hii dalili mapema na ukazuia huzuni kutokea katika ndoa yako kwa kupiga gia ya reverse kwa kuongeza frequency za sex kati yako na mumeo.
Wapo ambao ni wajanja zaidi ambao huendelea na sex kama kawaida ili wasishtukiwe hata hivyo kutokana na kuwekeza kwa “yule mwanamke” automatically akiwa na mke wake hamu hupungua na matokeo ni kupungua kwa uhitaji na kiwango cha sex hushuka.

NINI CHA KUFANYA:
Kwanza jiulize swali hili:
Je, kiwango cha sex ni mara chache kuliko kawaida? Kama ni chini ya kiwango ni vizuri wewe mwanamke pia kulianzisha uone nini kinatokea.
Kama mwanamke Jitahidi kutengeneza mazingira ambayo yatakufanya usijisikie kuchoka sana na kama inawezekana unaweza kumuomba mume wako kukusaidia kazi ndogondogo za pale nyumbani.
Pia fikiria ni kitu gani unaweza kuongeza (kipya) ili kuimarisha sex na kama inawezekana mnaweza kwenda nje ya hapo nyumbani kwa ajili ya kuwa na intimacy zaidi.

3. ANAANZA KUKUKWEPA WEWE MWENYEWE MKE WAKE
Anaweza kukukwepa kwa njia zile mnatumia kuwasiliana iwe mchana au usiku huanza kupunguza.
Unaweza kujikuta simu hazijibiwi, sms hazipewi majibu na mara simu imefungwa.
Kama ana simu ya mkononi anaanza kutembea nayo hadi anapenda kuoga, anapoi-charge kama ni nyumbani basi ataisimamia kama FBI wanaomsimamia terrorist aliyekamatwa kabla ya kujilipua.
Na kuna simu akiipokea No matter what ataenda kuongelea nje au kwenye uchochoro wowote.
Kama upo makini utajua tu something is not right!
Kikubwa zaidi hapendi kuwa na wewe “closer” kitendo hiki hufanya muwe mbali kihisia.

NINI CHA KUFANYA:
Jaribu kuchunguza kama simu unazompigia sinamsumbua kazini au ni jeuri yake tu na ukorofi kwa sababu ya “yule mwanamke”
Ongea naye namna ya kuwa na muda pamoja kwa kila wiki.
Wakati mwingine mpigie simu ya kumpa appreciation kwa ajili ya kitu chochote amefanya badala ya simu za kulalamika na kumfanya ajione failure na loser.
Kama una hints chunguza simu yake ya mkononi na kama huna hints achana nayo kwani hakuna mwanaume anapenda kutembea huku amefugwa video camera usoni kuchunguzwa kila kona anayopita.

4. ANAKUWA CRITICAL
Alikuwa anapenda mapishi yako, unavyoonekana (sura na maumbile), mapenzi yako, namna unapenda bajeti; ghafla from nowhere anaanza kulalamika na kukulaumu kwa kila unachofanya.
Inawezekana tatizo ni yule mwanamke!
Kiti kidogo kikikosewa inakuwa kama kapatia sababu ya kuanzisha mgogoro au vita ya tatu ya dunia.
Wakati mwingine anaweza kuwa mwonezi (harassing)

NINI KIFANYIKE:
Jadili kwa nini mume wako anakuwa critical na wewe muulize kwa upendo bila wewe kuwa critical pia.
Pia jadili kujua tatizo lipo wapi ili lirekebishwe huku wote mkiwa positive.

UMUHIMU WA SALAAMU KWA WANANDOA.

Je, ni muhimu wanandoa kusalimiana mnapoamka asubuhi?

Kwanza fahamu kwamba wanandoa wanapokaa muda mrefu baadhi ya vitu huanza kuchakaa kimapenzi. Hata hivyo upendo na wema husaidia kurudisha moto wa mapenzi na wanandoa kujiona wapya kila umri unavyozidi kuongezeka.
Matendo yanayoonesha wema kwa wanandoa ni gundi inayoshikisha wawili kujiona wapo karibu na moja ya tendo la wema ni kumsalimia mwenzako wakati mnaamka hata kama mmelala kitandani kimoja na hata kama mlikumbatiana usiku mzima au ulimuweka mwenzi wako kifuani usiku mzima.
Anayesalimiwa hujiona anapendwa, ana thamani na pia appreciated.

Tupo kwenye new millennium kiasi ambacho watu tupo busy hata kuamka tunahitaji kuweka alarm ituamshe hata hivyo badala ya kukimbia bathroom kuoga ni muhimu kumpa kwanza salamu mwenzi wako ndipo uendelee na kazi zingine au na ratiba yako.
Tafiti zinaonesha wanandoa ambao husalimiana asubuhi wanajiona ndoa yao ni nzuri sana na wana mahusiano yanayoridhisha.


Je, nini kinafanya maneno ya salaamu ya asubuhi kuwa muujiza katika ndoa na mahusiano?

Unapomsalimia mwenzi wako maana yake unamwambia na kumpa ujumbe kwamba ni asubuhi njema tumeamka pamoja katika upendo na furaha na kwamba unajisikia vizuri kuanza siku mpya na mtu wako na pia unaweka msingi mzuri wa mawasiliano kwa hiyo siku mpya.

EPUKA KUFANYA HAYA.

Unapokuwa kitandani na mpenzi wako kitu ambacho hupendi kitokee ni kumfanya ajisikie vibaya na kukosa hamu ya kuendelea na raha ya kufanya mapenzi.  Hata hivyo kuna watu si wastaarabu au ujinga tu hufanya mambo yafuatayo kwa makosa. 
Ni muhimu ukayafahamu na kutofanya ili partner wako afurahie huo muda wa faragha yenu.

1.KUTOKUBUSU:
Amini usiamini wapo ambao hufanya mapenzi bila kubusiana (iwe katika maandalizi au wakati wa tendo lenyewe).
Unashauriwa kumbusu mpenzi wako na kama hujui namna ya kubusu ni vizuri kufundishana kwani mapenzi ni sanaa na kujifunza ni jambo la msingi

2.KUPIGA KABLA YA KUSISIMKA
Wapo watu ambao hupenda vionjo vya ajabu kama vile kufinya, kupiga kofi iwe mashavuni au matakoni, kumkaba kooni nk hata hivyo hivi vitu vinafanywa kabla ya muziki kukolea au kusisimka huwa ni usumbufu kwa anyefanyiwa kwani kwa kuwa mwili haujasisimka huwa anapata maumivu badala ya raha hakikisha mpenzi wako ammesisimka na yupo katika ulimwengu wa raha ya mapenzi ndipo umuume hilo sikio au shingo au bega nk.

3.KUACHA SEHEMU ZINGINE
Wapo watu hasa wanaume, anapomuandaa mpenzi wake anachojua ni matiti na bondeni kujua  kama kumelowa then kumuingiza na kumaliza kazi. Jambo la msingi ni kwamba mwili wote wa mwanamke ni kiungo cha mapenzi. Kuanzia nywele kichwani hadi kucha na unyayo mguuni huhitaji kusisimuliwa na utaratibu wa kweli matiti na uke ni vitu vya mwisho katika safari ya kumuandaa

4.UZITO WAKO
Wapo watu wamebarikiwa uzito na linapokuja suala la kufanya mapenzi sijui makusudi au mazoea huamua kuegesha uzito wao kwa mpenzi wake.
Please, fahamu kwamba unapo kuwa juu yake kama wewe ni mzito uwe mwangalifu unaweza kumfanya akakosa hata hewa au akapunguza uwezo wake wa kupumuana ukaharibu good time yafaragha

5.KUMALIZA HARAKA AU KUCHELEWA MNO
Hii inahusu sana wanaume
Mwanaume unahitaji kujizuia ili umalize katika wakati mwafaka sawa na uhitaji wakuridhishwa kwa mpenzi wako ukimaliza haraka utamwacha bibie hajaridhika, na kuchelewa sana bibie atajikuta amebebeshwa chuma.
Kuepukana na hili ni muhimu mwaume kutumia mda mwingi katika maandalizi (foreplay) hii itawasaidia wote wawili kujisikia raha

6.KUTOKUSEMA UNAKALIBIA KILELENI
Kutomwambia mpenzi wako kwamba unakaribia kileleni siyo ustaarabu ni vizuri kumwambia ili ajue mpenzi wako anastahili kufahamu kwamba unakaribia kufika kileleni.

7.KUKAA KIMYA
Je, unapenda kusikia mpenzi wako anapata kitu kizuri toka kwako?
Kama unapenda basi naye anapenda mwambie kama anafurahia sio lazima iwe maneno bali hata kelele za kimahaba, hiyo itamtia moyo  na kuelimika zaidi katka suala la kelele za mahaba

NI MUHIMU KUWA NA UJUZI KTK NDOA.

Kama wewe ni kizazi cha Adam na Hawa basi suala la ndoa linakuhusu sana na ndoa ni kitu beautiful, Kwani huleta mahusiano ya kutosheleza yanayowaunganisha watu wawili mke na mume.
Inapendeza kwamba Mungu amemuumba mtu maalumu kwa ajili yako.

10. UJUZI WA KUTATUA MATATIZO
Kama wanandoa hawana ujuzi wa kutatua matatizo inaweza kusababisha ndoa kuwa ngumu sana hasa miaka 2 ya kwanza katika ndoa.
Kuwa na ujuzi namna ya kutatua matatizo katika ndoa ni kufahamu namna ya kuzozana kwa kuelezana ukweli kwa upendo, kufahamu ni wakati gani wa kukaa kimya au kuzungumza.

9. UJUZI WA KUMWEKA MWENZI WAKO NAMBA MOJA
Kumbuka katika ndoa kuna wewe, mwenzi wako na Mungu.
Jambo la msingi ni uhusiano wako na Mungu wako (siyo kazi ya Mungu, au kwenda kanisani bali uhusiano wako na Mungu, then mwenzi wako (mume au mke) ndipo wanakuja watoto na mwisho kazi.
Kama mke wako anafuata baada ya watoto, mama yako au baba yako au ndugu zako au rafiki zako au TV au Manchester United au chochote kile basi ndoa yako haina jipya na ipo siku mwenzi wako ataona hana maana katika ndoa yenu.

8. UJUZI WA KIMAISHA
Ni muhimu sana kila mwanandoa kufanya vitu ambacho vitakuwa msingi wa maisha ya baadae pia kila mwanandoa analo jukumu la kujiuliza ni namna gani anaweza kuwa mwanandoa mwema miaka 10 au 20 ijayo.
Kila mwanandoa analojukumu la kujiuliza nifanye vitu gani ili niwe mwenye mvuto hata miaka 10 ijayo.
Je, niende shule?
Je, nianzishe biashara?
Je, nifanyeje kumpa support mwenzi wangu katika kazi zake au taaluma yake?

7. UJUZI WA KUSAMEHEANA
Unapokuwa kwenye uchumba, mchumba akifanya kitu cha ajabu unaweza ukaachana naye na kumsahau kabisa, hata hivyo kwenye ndoa unatakiwa kusamehe na kusahau sasa hivi.
Mwenzi wako anapofanya kitu na kujiona amekosea, atakuomba msamaha Kwani ni kweli yeye ni binadamu na ana mapungufu na hayupo sahihi mara zote.
Muda ule ambao unakuwa hutaki kusamehe mahusiano huacha kukua na hudumaa.
Kama huna uwezo/moyo wa kusamehe basi kwenye ndoa usiingie; jibakie single milele.

6. UJUZI WA KUWA MBUNIFU
Kwenye ndoa tunaishi pamoja na kuonana kila siku, tunalala pamoja, kula pamoja, oga pamoja nk.
Bila kuwa mbunifu kuwa na “fun stuff” ndoa huzoeleka na kuchosha.
Tafuta vitu ambavyo mkifanya pamoja vitawafanya kuwa na kitu kipya.
Wapo wanandoa ambao akioa au kuolewa basi Hakuna jipya, Hakuna ubunifu kila mwaka vitu ni vilevile, badilika fanya vitu Tofauti kama hujawahi kwenda sehemu fulani nenda na mkeo au mumeo, have fun!

5. UJUZI WA MTAZAMO CHANYA
Jifunze kuwa na mitazamo chanya kwenye tabia za mwenzi wako. Ni kweli kuna vitu unavipenda kuhusu yeye na kuna vitu ambavyo unavichukia kuhusu yeye, hata hivyo ukweli ni kwamba vitu vizuri unavyovipenda kuhusu yeye ndivyo vimekufanya uoane naye na kwamba vina nguvu kuliko vile ambavyo huvipendi kuhusu yeye.
Weka mtazamo (focus) kwenye vile vitu ambavyo vinawafanya ninyi wawili kuwa kitu kimoja.
Ukimnyoshea kidole kimoja mwenzi wako, basi unatakiwa kujinyoshea vidole 5 wewe mwenyewe.

4. UJUZI WA KUJIAMINI
Lazima uamini kwamba ndoa yenu itadumu na Hakuna kitu kinaitwa talaka na talaka haitakubalika.
Ni muhimu sana ujiamini kwamba mwenzi wako ( mume wako au mke wako) anakipenda sana kama wewe unavyompenda yeye hata kama haoneshi kwamba anakipenda.
Fahamu hivyo na amini hivyo.
Kwa njia hii huwezi kuyumbishwa na upepo wa mashaka na hofu wakati kunajitokeza kutoelewana.
Kwa njia hii itakuwa rahisi kuirudisha ndoa kwenye mstari.

3. UJUZI WA KUJIFUNZA
Wakati mwingine katika ndoa huwa tunajidanganya sana kwamba tunawafahamu vizuri wenzi wetu hata hivyo baada ya muda tunaanza kushangaa na kujiona tumeoana na mtu ambaye amebadilika sana na Tofauti na wakati ule mnaoana.
Hata hivyo kujisikia mume wako au mke wako amebadilia na kuwa binadamua mwingine si Sababu ya kuachana au kupeana talaka.
Kama huna ujuzi wa kumsoma au kujifunza kuhusu mwenzi wako basi hukutakiwa kuoa au kuolewa au hukustahili kuoa au kuolewa naye.

2. UJUZI WA KUJUA NAMNA WENGINE WANAWAONA/WANAJIFUNZA
Kama umeoa au kuolewa na unajifanya hujaoa au kuolewa ni kweli dunia na viumbe wake wanakuona ni kweli hujaoa au kuolewa pamoja na umri wako kwenda.
Unatakiwa kuonekana wewe na mwenzi wako ni watu wenye furaha na amani na kweli iwe furaha na amani ya kweli siyo fake.
Mnatakiwa kuwa na smile la kweli na liwe na kweli si fake.
Lazima uwe makini na kufahamu wengine wanawaonaje kama wanandoa na hiyo itakusaidia kujiweka sawa kuhakikisha kunakuwa na kicheko katika ndoa yenu.

1. UJUZI WA NAMNA YA KUGOMBANA
Hakuna ndoa ambayo wanandoa hawajawahi kupishana au kupingana au kutoelewana au kutokukubaliana katika jambo fulani au tabia fulani.
Pia ni muhimu sana kufahamu kila mnagombana au Sababu ya kitu kinafanya kuwe na msuguano.
Unatakiwa kuwa na ujuzi wa kufahamu kwamba kugombana kokote kusiwe kwa masaa kadhaa, au siku kadhaa au miezi kadhaa.
Pia ni muhimu sana kuangalia namna unabishana au unaongea wakati wa kutokukubaliana na jambo lolote.
Pia focus katika kulishambulia Tatizo lenyewe na siyo mwenzi wako.

MAZOEZI HUONGEZA HAMU.

Tafiti nyingi zinaonesha kwamba kufanya mazoezi ya kawaida huongeza kiwango cha homoni za endorphins ambazo huhusika na kuongeza intensity ya kusisimka kimapenzi.
Ile kujisikia upo fit kimwili hukusaidia kujisikia mzuri zaidi na pia husaidia kukupa mood ukiwa chumbani.
Hata hivyo kuna limit ya mazoezi kwani ukifanya mazoezi magumu zaidi yanayopitiliza kiwango kama vile mkimbiaji wa marathon au kuendesha bicycle kwa muda mrefu (kwa mwanamke husababisha kuwa na clitoral dumbness –kisimi kupoteza uwezo wa kusisimka tena), kwa pamoja haya mazoezi huweza kukufanya uchoke na kushindwa kuwa na hamu ya tendo la ndoa.

Hivyo mazoezi ni muhimu lakini yasiwe ya kuzidisha!

Monday, 9 November 2015

NI RAHISI SANA KUIMARISHA NDOA YAKO.

ILI uwe na ndoa yenye furaha ni lazima utenge muda wa kutafakari namna ya kuiboresha na
kutafuta furaha ya ndoa hiyo. Ndugu zangu, kila kitu kinatengenezwa.

Waswahili wanasema, ukiona vyaelea, ujue vimeundwa. Huwezi kuacha mambo yakajiendesha hovyo ukategemea kuwa na ndoa bora. Uhusiano imara unakutegemea wewe.
Kila mmoja ana wajibu wa kuangalia furaha ya mwenzake. Yapo mambo mengi muhimu ambayo kama
wanandoa wakiyafanya huboresha uhusiano wao, lakini hapa nitakutajia yale muhimu zaidi.

ISHI KIRAFIKI.

Kuna baadhi ya wanandoa wakishaingia kwenye muunganiko huo, ule urafiki uliokuwa zamani wakati wa uchumba, hilo ni tatizo. Ukitaka kuwa na ndoa yenye furaha lazima umfanye mwenzi wako kama rafiki yako.Baadhi ya wanaume wana tatizo la ubabe na kujiona kuwa wao ni wanaume hivyo hawapaswi kuguswa kwa lolote.

Ndoa inageuka jeshini. Hilo ni tatizo.
Mshirikishe mwenzako kwenye mambo yako. Kuwa na kauli njema muda wote. Sikiliza shida za
mwenzako na namna ya kuzitatua.

Sikiliza pia hisia zake.Usipoishi naye kirafiki, maana yake ataogopa hata kukueleza mambo fulani ya msingi ambayo labda havutiki nayo. Ukimsogeza kama rafiki atakueleza mambo ambayo hayamfurahishi.
Mkiishi kama marafiki ni rahisi kusameheana. Ndoa nzuri ni ile yenye kusameheana ndani yake.
Kukaa na mambo moyoni husababisha mikwaruzano ya kudumu.
Kama marafiki, mtapata muda wa kushughulikia kero zenu haraka kabla hazijakua.

MIPANGO YA KIFEDHA.

Kama kuna jambo linalosabisha migongano na kupunguza uaminifu ndani ya ndoa ni suala la
fedha. Kwa bahati mbaya sana wanaume wengi ni wasiri sana kuhusu mapato yao.
Huna sababu ya kumficha mke wako kuhusu kipato chako. Mshirikishe, ajue unapata kiasi gani kwa mwezi. Labda una biashara nyingine au vyanzo mbalimbali vya mapato nje ya ajira yako ya kudumu, zungumza na mwenzako.

Ziko faida nyingi, kwanza ataona unavyomwamini na kumthamini na kumfanya sehemu ya mafanikio
ya familia, lakini pia anaweza kukushauri mambo ya msingi ambayo yatasaidia kukuza kipato
chenu.

Kubwa zaidi ni kwamba, utamfundisha namna ya kuendesha biashara zako, hata siku ikitokea
umeugua atasaidia kuimarisha biashara.

MATATIZO YA FAMILIA
Kuangalia matatizo ya pande zote mbili za familia mlizotoka, inasaidia kuimarisha mapenzi.
Mwenzako akikuambia kuhusu tatizo labda la mtoto wa dada yake, usipuuze.
Hata kama hamna fedha, unaweza kumshauri jambo zuri ambalo litamuweka vizuri kihisia.

Wengine huwa na majibu mabaya: “Kwani nimekuoa wewe au ukoo mzima?” kauli hii siyo sahihi na
hubomoa nyumba.

Kujua na kuthamini matatizo ya mwenzako ni kati ya mambo muhimu sana yanayoleta furaha kwenye ndoa. Kuwa na kauli nzuri. Kweli, inawezekana huna fedha au mipango yenu imeingiliana, isiwe tatizo.

Mjulishe mwenzako kwa lugha laini na ikiwezekana mawazo yako yanaweza kumfanya akajua mahali
pa kuanzia. Kuchukulia tatizo la mwenzako kama lako, inaongeza amani, maana anajiona sehemu
kamilifu ya muunganiko wenu wa ndoa.

Wengi hawajui hili na hata kama wanajua, hawatoi umuhimu mkubwa kwa wenzi wao. Ndoa ni tunu
rafiki zangu. Tujitahidi kuheshimu na kuzilinda kwa nguvu zetu zote.