Sunday, 3 April 2016

WAKATI WA MIGOGORO.

Kukiwa na mgogoro kati ya mume na mke, kawaida mke hujitahidi kufanya bonding na mumewe kwa kuongea na kuhakikisha emotions zinakuwa wazi kwa kuwa hajui tofauti ya mwanaume huamini na mume wake naye atakuwa mwepesi kuongelea kama yeye na matokeo yake mwanamke huishia kuwa na hasira na frustrated.
Jambo la msingi ni kwamba mume anatakiwa kufahamu kwamba kunapotokea mgogoro au kupishana lugha ni jambo la maana sana kumsikiliza mke au kuhakikisha mnaongea na unampa mke muda na wakati wa kutosha kuongea yote aliyonayo (kutoa emotions zake hata kama atalia machozi ila hakikisha analia akiwa mwilini mwako) na kwa njia hiyo anajiona unamjali kuliko kumwambia tusiongee sasa au tutaongea baadae au kukwepa au ku-ignore maana hapo ataumia zaidi na kuona humjali, hapendwi na upo harsh.
Pia mke naye asikasirike pale anapoona mume anakwepa kuongelea tatizo au mgogoro uliopo kwani wanaume ndivyo walivyo (tofauti zilizopo kwani wanaume huamini kwa kuacha kuongelea ndiyo njia nzuri ya kumaliza mgogoro) hivyo wewe mke mpe muda na akitulia mnaweza kuongea zaidi.

KUOMBA MSAMAHA.

Wanawake wengi akisema samahani ni njia mojawapo ya kujiunganisha (connect) na Mume au mtu mwingine kama kuna mgogoro au tatizo au kitu chochote anaona hakipo sawa, anaweza kusema samahani hata upande mwingine unavyijisikia vibaya.

Kwa mwanaume kusema samahani ina maana anakubali kwamba amekosa na anatakiwa kuomba msamaha.
Mwanaume anaamini kwamba kwa kusema hivyo inamuweka chini zaidi na hujiona si mwanaume wa uhakika na kwake haikubaliki haikubaliki kabisa.
Kama mume wako huwa anatoa samahani waziwazi basi umebarikiwa kwani mwingine badala ya kusema samahani yupo tayari akanunue zawadi kubwa ujue anaomba msamaha, hata hivyo kama wewe ni mwanaume kumbuka kwamba ni muhimu sana kutamka neno samahani nimekosa kwa mkeo bila kuzunguka wala kuzungusha sentensi.

Na kukitokea conflict yoyote wanawake hujisikia wana wajibu wa kuhakikisha wanafanya kitu kuondoa hiyo conflict ndiyo maana wanawake wengi wapo tayari kwenda hata kwa mtu mwingine anayemwamini kuomba ushauri.
Wakati wanaume hukwepa na anaweza kutumia muda mwingine kufanya vitu na rafiki zake na kukwepa familia ambayo huko mke wake anamsuguano naye.
Kama ni mwanaume ni vizuri kufikiri na kujiuliza upya kipi muhimu?
Familia au rafiki zako?
Familia ilikuwepo hata kabla ya kanisa na familia ni mahali ambapo kanisa huanzia hivyo ni muhimu sana kuhakikisha unamaliza conflict yoyote na kurudi nyumbani kuwa na familia.
Ukipoteza familia umepoteza vyote!

WAKUFANANA NAE KTK MAWASILIANO.

Uwezo wa kuwasiliana kati ya mke na mume ni moja ya precious commodities muhimu sana katika ndoa au mahusiano yoyote.

Wanandoa wenye uwezo mzuri wa kuwasiliana huwa na ndoa/mahusiano bora na zaidi huweza kuwa na watoto ambao nao huwa wazuri katika kuwasiliana na hatimaye kuwa candidates wazuri wa ndoa baadae.
Pia kuwa na mawasiliano mazuri husaidia mtu kuwasiliana na watu wengine na kuwa na mvuto zaidi.

Kuna usemi wa kingereza usemao
"Great communicators are people who change their approach based upon the person they are talking to"

Hii ina maana kwamba kama wewe ni mwanaume huwezi ongea the same style kwa mwanaume mwenzako na mwanamke.
Kuongea na mwanamke au mke ni tofauti na mwanaume au mume.
Hivyo kujua au kufahamu jinsi ya kuongea au kuwasiliana na mke wako au mume wako ni jambo la msingi sana ili kuwa na mahusiano mazuri.


Kumbuka mwanaume na mwanamke wapo tofauti sana kwani;
Huwaza na kufikiri tofauti,
Huongea tofauti,
Huamua tofauti na zaidi
linapokuja suala la hisia kuna tofauti kubwa sana.


Inawezekana wewe ukiwa na mume wako au mke wako huwa mnajikuta ni bubu, au ni kubishana tu au kila mmoja hamwelewi mwenzake au mwenzako akiongea unahisi haeleweki kwani anazunguka wakati anatakiwa kuwa direct to the point.

NI HISIA.

katika mji fulani mwanamke analalamika kwa kuwa mume wake anatembea na mwanamke nje (sex) hata hivyo mwanamke anashangazwa sana kwani mume wake anatembea na mwanamke ambaye ni ugly idara zote kuliko yeye mwenye mume.
"Hilo limwanamke kwanza ni overweight na sura ndo hivyo tena" analalama huyo mwanamke.
Mume akiulizwa kulikoni kutembea na mwanamke kama huyo jibu sahihi na mkato eti
“she has time for me!

Je, hujashuhudia mwanaume anaacha mke mzuri nyumbani na kwenda kutembea na mwanamke ambaye ni garbage?
Je, uzuri wa mwanamke ni sura au elimu yake au kiwango cha hisia na muda anaokupa mwanaume katika ndoa?
Naamini jibu unalijua!

Hata hivyo katika mji mwingine mwanaume (professional/mtaalamu fulani shule imakubali) analia kwani mkewe mrembo wa uhakika anatembea na kijana ambaye ni kibarua wao (sijajua ni house boy au shamba boy maana jamaa analia hata hasemi nilihisi kama ana kizunguzungu vile)
Huyu mwanamke akiulizwa vipi mbona unatembea na kibarua wenu, anajibu
“Ananifanya nijisikie vizuri na tena ananifanya nijisikia mimi ni mwanamke muhimu na wa maana”

Kwa ujumla hawa watu wanaweza kuwa na matatizo gani? na inawezekana mimi na wewe yakatufika tusipokuwa makini.


1..Hawa watu wamewaacha wapenzi wao si kwa sababu ya ubaya wa sura au uzuri wa sura bali ni zaidi ya hapo.


2..Inaonesha kuna hisia ambazo hawa wanandoa hukosa kwa mwenzake na kuamua kwenda kutafuta sehemu zingine au wamekuwa wakizipata kwa hawa watu wamekuwa na affairs nao.


3..Watu wanaotembea (sex) nao wanaonekana wapo smart sana kujua hawa wenzetu (wanandoa) wanakosa kitu gani kwenye ndoa zao.


4..Hawa wanaotembea nao wanajua jinsi ya kuwahudumia hawa wanandoa kitu wanakosa katika ndoa zao na kitu wanachokosa ni hisia na mapenzi yanayopelekea kila mmoja kuguswa na mwenzake.


5..Unaweza ku- fall in love na hisia za mtu na si mtu mwenyewe, kwa maana kwamba mtu kama ni mwanaume unakosa hisia maalumu kutoka kwa mke wake na kazini kukawa na mwanamke ambaye anajua kile anakosa na akaamua kumpa basi unaweza kufall in love naye hata kama yeye kama mwanamke huna haja naye ila feelings zina nguvu za kuweza kufanya kuwe na affair.
Mfano mume hapati muda wa kukaa na mke wake na mke kila siku yeye ni semina na kusafiri tu na huko ofisini mzee anakaa na secretary wake na wanakuwa na muda (intimate) hadi kuanza kupeana siri za maisha.
Mwanaume au mwanamke ambaye ametumbukia kwenye tatizo kama hili huweza kurudi haraka kwenye mstari kama mke wake au mume wake akaamua kubadirika kwani ukweli hakumpenda mtu nje bali alizipenda hisia za mtu wa nje.

Suala la kumpa mpenzi wako muda wa pamoja ili aridhike ni muhimu sana kumbuka wewe usipo mpa muda mwingine atampa.

Tumeona wasichana wa kazi, vijana wa kazi, mabosi na kila aina za watu wakifanya vitu vya ajabu na wale tunaowapenda hata hivyo je, sisi tumefanya jitihada gani kutosababisha wao kukosa kile ambacho tungewapa hadi wapewe na wengine?
Hili dudu linaitwa hisia achana nalo kabisa na usifanye mchezo hasa likivaa nguo zinazoitwa mapenzi, halishikiki na linaweza kuleta maafa katika jamii.

Saturday, 2 April 2016

KUPATA MCHUMBA SAHIHI...2

Haijalishi mtu unayetaka kuoana mmekutana wapi;
hata kama ni kanisani, shuleni, kwenye mkesha wa maombi, kijijini, mjini, hotelini, sokoni, kwenye daladala, barabarani, ofisini, kazini, safarini, kwenye semina au hata kama ni kwenye internet au njia yoyote ile ambayo Mungu anaweza kuitumia maana Mungu hafungwi na njia za kukutanisha watu.
Au Haijalishi ni mzungu, mwarabu, mchina, mwafrika, au awe mnene, mwembamba, mrefu kama Ngongoti, mfupi kama Zakayo,
Awe amesoma au hajasoma, awe mbena au mchaga au mhaya au mgogo au mzigua, au awe anatoka Canada, Kenya, Uganda, Nigeria au Tanzania. Pia haijalisha ktk kukutana naye umeunganishiwa na rafiki yako, au mchungaji wako, au wazazi wako au mtu wako wa karibu.
Kitu cha msingi ni wewe kuwa makini kujiuliza haya maswali matano muhimu.


1. JE, TUNAFANANA?

Ndoa ni kama jengo la nyumba na nyumba ni sharti iwe na msingi. Msingi imara huwezesha nyumba kuhimili kila aina ya janga linalotokea kama vile mvua, upepo, mafuriko, dhoruba, tetemeko la ardhi nk. Na kuna aina ya material zinazotumika kujengea msingi na hizi aina za material ndizo huelezea aina ya msingi na uimara wake.

Unaweza kujenga ndoa kwa kuvutiwa na umbo la mtu (mvuto wa nje) au urembo tu. Pia sasa hivi kuna uzuri mwingi tu na unauzwa dukani (body shops)
Unavutiwa na kipande kimoja tu cha mwili wake kama vile shingo, matiti, matako, unene, au wembamba, nywele, smile, anavyotembea, miguu, au kifua nk.
this is just physical attraction kuna siku anaweza kubadilika kuna kuugua, kuna ajali, kuna kubadilika mwili nk kwa hiyo ku-base kwenye mwonekano wa nje peke yake lisiwe jibu kwako kuona huyu mtu ananifaa.
Hapo utakuwa umejenga msingi wa nyumba kwa kutumia mabua au miti hakika nyumba ikishika moto hata majivu tunaweza tusipate.

Ndoa hujengwa ktk misingi 3 muhimu ambayo lazima mfanane au kuwa kitu kimoja. Ni muhimu kusiwe na gap kubwa sana katika mambo haya matatu,
Nayo ni Kimwili,
Kiakili na
Kiroho
(Mind, Body and Soul).
Mara ya kwanza mnapokutana wote mmoja anapata kuvutwa na mwingine kwa njia ya tofauti na huko kuvutwa kuna base kwenye mwonekano wa tabia kama vile anavyoongea, anavyotabasamu, anavyopenda na kwa hayo tu huwezi kusema biashara imeisha ananipenda au nimempenda na kukubaliana kuoana.

Unapotumia muda zaidi kuwa naye na kumjua zaidi, uhusiano unakua na unamfahamu zaidi ya ile physical attraction ambayo uliipata kwa mara ya kwanza sasa unaweza kutambua mambo anayopenda,
mawazo yake katika mambo mbalimbali ya kiroho,
kimwili na kiakili,
unaweza kujua talents zake na hobbies zake
hapa ndo inabidi uwe makini kufanya assessment kwani hapo ndo biashara yenyewe kwani ukimpenda na ku fall in love unakuwa blind halafu utaona kila kitu shwari hata watu wakikwambia kuna tatizo utakataa na kuwambia yupo sawa kabisa na bila yeye wewe maisha hayana maana, kumbuka huyo ni mchumba si mke/mume.
Unahitaji kuwa mchunguzi zaidi kuliko kupendwa. Kumbuka hapa unatafuta mchumba hajawa mke so ukiona kuna dalili au tabia ambayo ni hatari inabidi uwe makini.

Upendo wa kweli hauwezi kuwepo bila bonding ya kiroho.
Kutofautiana kiroho na kiimani ni moja ya sababu ya ndoa kuvurugika na hatimaye kuvunjika. Hivyo ni vizuri kupata data kamili kwa kuthibitisha imani yako na yake.

2. JE, UNAKUBALIANA NAYE KTK MAMBO YAKE?
Mtu ambaye kwake pesa na kazi ni namba moja yaani ni kitu cha kwanza, kwake bila hivyo hakuna maisha, yaani muda wake na akili yake ni pesa na kazi kwanza,
Then mambo ya michezo kama soka, au kushabikia tu michezo ni kitu cha pili, familia (mke au mume na watoto) ni kitu cha tatu kwake,
Na mwisho Mungu, yaani Mungu ni kitu cha ziada kwake, akiwa hana cha kufanya ndo anakumbuka mambo ya Mungu, Kama wewe ni dada ukapata kijana wa kiume wa aina hii kuendelea naye fikiria mara mbili.

Au mwanamke ambaye kwake kujiremba, kujisifia au kusifiwa na kuhudhuria sherehe (mama wa shughuli) kwake namba moja, then familia na Mungu baadae.
Kama ni kijana wa kiume binti wa aina hii fikiria mara mbili kabla hujaamua.

Kama ninyi ni Christians kitu cha kwanza ni kila mmoja kuwa na uhusiano na Mungu wake kwanza then familia yaani mke/mume na mtoto then kazi hii ni pamoja na kazi ya Mungu.
Hivi unaweza kwenda kuimba kwaya wakati mke au mume yupo kitandani anaumwa na hakuna mtu mwingine? Mlio kwenye ndoa tusaidie hapo!.....

ITAENDELEA....

KUPATA MCHUMBA SAHIHI.

"Apataye Mke Apata Kitu Chema; Naye Ajipatia Kibali Kwa Bwana"
(Mithali 18:22)

Moja ya mambo ya msingi ambayo kila kijana anahitaji ni Ndoa ya Kudumu ukiacha ongezeko la kufeli kwa ndoa nyingi.

Wakati huohuo moja ya uamuzi (wa maana sana katika maisha ya binadamu ni kuamua nani atakuwa mume wako au mke wako na huu uamuzi ndiyo utakufanya uweze kuishi maisha ya namna gani katika ndoa yako na pia kuathiri kabisa mfumo wa maisha yako kuwa raha au kuwa karaha

Watu wengi katika maisha wamekuwa wakilaumu upande mwingine iwe mke wake au mume wake kwamba ndiye sababu ya kuvunjika kwa uhusiano au ndoa yao.
Huu ni ujinga muhusika mara nyingi ni wewe kwani asilimia 99 ni jinsi ulivyompata huyo mtu ambaye amesababisha ndoa yako au uhusiano kuvunjika.

Mtu anayestahili kupewa lawama zote ni wewe.

Kama hujaolewa au ndio upo kwenye process za kuolewa au kuoa,Fahamu kwamba hakuna jambo muhimu maishani mwako kama huo uamuzi unaotaka kufanya, unaweza kukupa furaha ya maisha au uchungu wa maisha hapa duniani.

Unahitaji kutumia
akili zako zote,
maombi yako yote,
uwezo wako wote na
kila resource ulizonazo
kwani hapa makosa hayana nafasi kabisa

Wala usikubali kumuoa huyo binti au kuolewa na huyo kaka eti kwa sababu:

Watu wanasema Mbona hujaolewa au kuoa!
Au ndugu zako, au mchungaji, au wazazi wako au rafiki zako wamekwambia!
Au kwa sababu umeona muda unakwenda!

Amua mwenyewe na jichunguze kama upo tayari na kama mtu unayetaka kuwa naye anakupa uhakika unaoridhika nao wewe mwenyewe.

Kumbuka it is easy to reshape the mountain siyo mtu, kwa hiyo kama kuna tabia fulani ambayo unaiona kwa mtu unayetaka kuoana naye na hujaridhika nayo Please fikiri zaidi ya mara mbili.
Na kama unaweza give time au fikiri mara nyingi zaidi.

Mara nyingi wanaosema watawabadilisha matokeo yake wao ndo wamebadishwa

Hapa huhitaji kuwa blind kwa sababu ya fall in loves, bado unahitaji kuwa na akili timamu kumfahamu zaidi huyo unataka kuoana naye kabla love haijawafanya kuwa blind au otherwise muwe blind maisha yenu yote.

Kuna maswali matano (5) ya msingi sana kujiuliza kabla hujajikamatisha vizuri kwenye hii kamba ya ndoa.

ITAENDELEA..

Friday, 1 April 2016

UKILITAJA JINA LAKE ATAJISIKIA RAHA ZAIDI.

Tendo la ndoa ni sanaa kama sanaa zingine na hakuna mtu anaweza kukufundisha kwamba unapotaka kuwa mwili mmoja na mke wako au mume wako kitu cha kufanya ni hivi na hivi kwani kila mwanamke ni tofauti na hata huyo mwanamke mmoja anatofautiana kwa siku kadhaa katika mwezi mmoja kutokana na mzunguko wake.
Hivyo jambo la msingi ni mwanaume kuwa na skills za kutosha kuhakikisha unamsoma vizuri mke wako na kujua mambo ya msingi kuzingatia wakati wa tendo hili takatifu na lililobarikiwa.
Kwa mfano:
Kwanza kabla ya mambo yote ni jambo la msingi sana wewe mwanaume kuwa clean na umeoga vizuri na unanukia version nzuri inayovutia, hii itasaidia yeye kuwa na focus zaidi kwa sex kuliko harufu ya ajabu ambayo inatoka kwako, hapa haijalishi una sexual skills au sexual techniques za juu kiasi gani kwani kuwa mchafu na harufu chafu ya mwili ni total turn off.
Pia ni muhimu sana kuwa na mouthwash ambayo inaweza kuua wadudu ambao wanaweza kusababisha ukawa na harufu mbaya sana mdomoni kwani kuwa na clean and fresh breath ni muhimu sana hasa suala la kubusiana.

jambo lingine muhimu ambalo kila mmoja hufahamu na kulipenda ingawa wakati wa foreplay au sexual act husahauliwa ni kukumbuka kumnong’oneza jina lake ukirudiarudia ikiendana sambamba na unavyopumua na huku ukimbusu shingo yake na sehemu zingine ambazo zinamsisimua.
Utafiti unaonesha kwamba kila mtu (binadamu) hupenda kusikia jina lake na wanawake hawana exception kwenye hili.
Unapomnong’oneza jina lake huonesha kwamba upo focused kwake na unamfikiria kuhusu yeye na kile mnafanya na inaweza kuwapa connection (emotionally) na matokeo yeye atajifungua zaidi sexually kiasi ambacho wewe mwenyewe utashangazwa.

TAHADHALI.
Ole wako utaje jina ambalo si lake!

Jambo lingine la msingi ni kwamba foreplay ambayo haihusishi kuchezea matiti na kuchezea sehemu ya siri hujenga njaa na kutamani kuchezewa hayo maeneo kitu ambacho kitamfanya baadae ukigusa huko apate raha zaidi.
Hivyo focus sehemu zingine kwanza na matiti na uke viwe ni sehemu ya mwisho kwa foreplay.

Mwisho haijalishi anafurahia kiasi gani utaalamu wako na ufundi wako jambo lingine muhimu ni kuhakikisha kunakuwa hakuna routine na inabidi ubadilishe mambo mara kwa mara, chumba kilekile, kitanda kilekile, mwelekeo uleule, saa ile ile, mwanga au giza lilelile, muziki uleule, mlalo uleule huwa inasumbua baada ya muda na inaweza kuzima kabisa moto wake kitandani.