Wednesday, 18 November 2015

MWANAUME HUMTENGENEZA MWANAMKE.

Wakati wa sex Mwanamke huwa kama pasi huchelewa kupata joto na hutunza joto kwa muda zaidi hata baada ya kumaliza kupiga pasi.Inatokea mwanaume anafika nyumbani kutoka kazini anamkuta mke naye yupo nyumbani anamsalimia then anaenda zake chumbani kubadilisha nguo za kazini.
Anapata chakula cha usiku then anaanza kutazama TV au kupitia magazeti yake na kuyasoma.
Muda wa kulala umefika anaenda kuoga na kuvaa pajama zake; mke naye anaenda kuoga na kufanya sawa na mume.
Wanapanda kitandani, mume anampapasa mke, mke naya anajua mzee anataka maana ndiyo sex code yake akinigusa kwa mtindo huu maana yake anataka tuwe mwili mmoja na anajisikia kama kusumbuliwa maana alikuwa hajui kama mzee atataka kutokana na kutowasiliana hata hivyo anamkubalia.
Baada ya dakika chache wamemaliza, wapo kimya na mzee anapiga usingizi.
Mke anajiona kama ametumiwa tu kwani hakukuwa na raha yoyote ni kuumizwa tu kwani mwili haukuwa connected hisia.

Kuna tofauti gani na chura hapa?
Kuwa na mahusiano na kimapenzi kwa mtindo huu ni sawa na kuiba akili ya asili ya chura.

Mwanaume ni rahisi kusisimka kimapenzi wakati mwanamke huhitaji kusisimuliwa. Mwanaume husisimuliwa na moja ya mlango wake wa fahamu kupitia kuona wakati nwanamke husisimuliwa kupitia milango yote mitano ya fahamu Kuguswa, kusikia, kuona, kuonja, kunusa na wororo wa mwanaume.

Mwanaume ni mfano wa bulb ya umeme uki-switch tu mara moja inawaka wakati mwanamke ni mfano wa pasi ya umeme ambayo huchukua muda hadi ipate joto na hutumia muda zaidi to cool off.
Hii ni muhimu sana ukitaka kuwa mpenzi mzuri na mpenzi mzuri hujua na kuzingatia jinsi ya kumridhisha mwenzake.

Mwanamke anaongozwa na highway ya emotions, atajisikia vizuri sana kama alikuwa na idea kwamba kutakuwa na kuwasha pasi yake ya umeme mapema.
Itakuwaje kama wakati wa kuondoka asubuhi mume akampa mke busu la uhakika na kumnong’oneza mkewe kwamba “vipi unaonaje leo usiku ukawasha pasi mapema kwani nina hamu sana kupiga pasi nguo kwani naona bulbu yangu ina mwanga wa uhakika leo".
Nahisi mke atashinda anaweza jinsi ya kuhakikisha pasi yake inawaka chapchap usiku na ikitokea na mchana akaambiwa neno lingine mwororo inaweza kuwa jioni yenye mwako wa mahaba.

Kwa mawasiliano mazuri na kupeana quality time mwanamke huweza kufunguka kiakili, kimwili na kiroho na kuwa tayari kwa usiku wa kufurahisha na kuridhishana.
Ndiyo maana wakati mwingine ukipapasa usiku unaambiwa “baba nanii leo kichwa kinaniuma sana” au “nimechoka sana” au “unapata zero participation na kuambiwa maliza haraka” au pasi inakuwa kavu kabisa matokeo yake ni pasi inagoma kuwaka na kuanza kuumizana.

Jifunze kuwa mwanaume mwororo (tenderness) wasiliana na mke, tafuta muda wa kumsikiliza, cheka naye, cheza naye, ongea naye, mpe mgusu (touch), mkumbatie na kumbusu hata kama si wakati wa sex ni wako na ni wewe uliamua kuishi naye.

Mwanaume humtengeneza mwanamke!

MWILI MMOJA.

Kuambatana!
Wanahitaji kuongea uso kwa uso!

Tumeona kwamba mwanamke anatakiwa (lazima) amheshimu mume ili mume naye ampende na matokeo yake kila mmoja aridhike na mwenzake na hatimaye kuwa na uhusiano mzuri idara zote.

(Efeso 5:33)

Mke anahitaji mume anayempenda na kumuonesha upendo kuanzia asubuhi, mchana na jioni wakikutana mume anahitaji kuwa karibu na mke wake ili mke ajisikia anapendwa na hatimaye ajisikie relaxed na kuwa tayari hata kwa activities zingine usiku.

Je, mume kuwa karibu na mke wake ina maana gani?

Maana ya kuwa karibu kwa mke na mume ni kuambatana, shikamana, kushikana, ng’ang’aniana, fungamana, kaa jirani jirani, songamana, karibiana, kuwa pamoja (cleaving, cling or intimate)
Kuwa karibu ni kuungana uso kwa uso na kuwa mwili mmoja.

“Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja”.
(Mwanzo 2:24)

Katika uimbaji wa Mungu ni Binadamu peke yao ambao huweza kuwa karibu kimapenzi uso kwa uso.
Kuambatana kati ya mke na mume ni zaidi ya kuwa mwili mmoja.
Kuambata kwa mke na mume ni kuwa karibu au mwili mmoja kiroho na kimwili.
Kama wewe ni mwanaume inakupasa ufahamu kwamba mke wako hufurahia na kujiona anapendwa na wewe pale unapomkaribia na kufanya ajione unataka kuwa karibu kwa namna unavyomtazama, unavyomgusa, unavyomkumbatia, unavyotabasamu na kumbusu na kumwambia NAKUPENDA.

Katika ulimwengu wa sasa ni rahisi sana kwa mke na mume kuchukuliwa na kuwa busy na kujisahau kujenga ukaribu ambao ndiyo msingi wa mwanamke kujisikia anapendwa na mume wake.
Wanandoa wenye busara huchukua dakika si chini ya 15 kila siku wakikutana jioni baada ya kazi; huhakikisha kila mmoja anajihusisha na mwenzake kwa ukaribu wa kimaongezi na sharing ya information za namna siku ilikuwa kwao wote na matokeo yao jioni na usiku vinakuwa exciting.
Mke akirudi anataka connections, anataka involvement na mume, anataka face to face talks na Mume akirudi kazini anataka kwenda pangoni hata hivyo jambo la msingi ni mwanaume kuhakikisha anapata muda wa kutosha ili kufanya connection na mke na hasa kama unataka mambo yawe safi kuanzia jikoni, sebuleni hadi chumbani huo usiku pia usigande kwa TV au Gazeti au pangoni bila kuongea na mke na kusaidia kazi ndogondogo hapo nyumbani.
Kuna ubaya gani kama utakuwa unapiga story na yeye anaandaa dinner au na wewe unasaidia kupika (kama hamna wafanyakazi wa ndani)

KUMBUKA KUWA KARIBU NA MKE SI GHARAMA BALI MUDA:

Mke atafurahi kama mara kwa mara:
Utamshika tu mikono,
Utamkumbatia na kumbusu wakati wowote,
Unapokuwa affectionate bila wazo la sex,
Kufanya kitu kinachosaidia kuwa na “togetherness”
Pale unapomwambia unampenda, yeye ni mwanamke mzuri (mrembo).
Kumbusu mke kwa sababu unataka sex tu ni turn off.
Pale mnapoangaliana na kupeana story zinazowafanya kuwa na kicheko.
Unapotumia muda wa kutosha kuwa na yeye katika kazi ndogondogo kama kupika, kufua nguo, kuogesha watoto, kusafisha nyumba nk.
Pale unapomfanya ajisikie unafurahia kujadili vitu mbalimbali na yeye.
Pale unapoendelea kuongea naye, au mkumbatia na mbusu baada ya tendo la ndoa.

SEX NI KITU CHA AJABU SANA.

SWALI
Kaka Jeffy,
Kwanza nashukuru sana kwa hii blog kwani nimejifunza mambo mengi sana kuhusiana na masuala ya mahusiano.

Mimi ni mwanamke mwenye miaka 29 na ni mwaka wangu wa 3 kwenye ndoa hata hivyo nilitaka kuuliza swali lifuatalo kama unaweza kunisaidia.

Mume Wangu anatabia ya kunikaba au kunikwida shingo wakati tukifanya mapenzi (sex) sijajua tabia kama hii ina maana gani.

Nimevumilia kwa muda mrefu hata hivyo imefika Mahali sijisikii kuwa comfortable na hii tabia yake.

Je, ni kitu cha kawaida kwa mwanaume kukukwida shingo wakati wa tendo la ndoa bila kuleta madhala yoyote?


JIBU:

Asante sana kwa swali zuri na pia kupita hapa ili kujifunza tips mbalimbali za maisha ya mahusiano.

Swali lako la msingi linasema

Je, ni kitu cha kawaida kwa mwanaume kukukwida shingo wakati wa tendo la ndoa?

Ukweli ni kwamba linapokuja suala la mapenzi (sex) Binadamu (mke na mume) huonesha tabia nyingi ambazo hushangaza sana (binadamu ni kiumbe wa ajabu sana).

Wapo ambao wakati wa sex hufanya vitendo au kuonesha tabia zifuatazo;
kama vile kufinyana, kuumana kwa meno, kupiga kelele na wengine yowe as if kuna msiba (hadi majirani wanawajua), kupeana matusi ya nguoni, kupigana makofi (kuzabana vibao), kufungana kamba au pingu na kuchapana viboko, wapo wanaume akilifuma kufuli la mke wake hulifakamia na kulinusa kwa dakika kadha na kujisikia raha, wapo ambao hukomalia kunusa kwapa, wengine ni kupeana ahadi kama kununuliana magari au kujengeana ghorofa Mbezi beach (wakiamka asubuhi wanajikuta wapo nyumba ya kupanga manzese jijini Dar es Salaam), sijawasikia hao wa kukwidana shingo na viungo mbalimbali vya mwilini (hii naona inahatarisha maisha zaidi)
Tabia zote hizi wao wanasema ni “to have fun” na kusherehekea mapenzi, hata hivyo inawezekana kwako zisikubalike na kwao zikakubalika.
Usiige!
Napenda ufahamu kwamba kuvumilia tabia au kitu ambacho hukipendi siyo jambo zuri katika uhusiano wa mapenzi kati ya mke na mume, uwe wazi na mweleze ukweli wa vile unajisikia.


Ni muhimu Sana kuweka mipaka kwa vitu ambavyo huvifurahii katika tendo la ndoa na pia muulize mume wako naye ni vitu gani anavipenda na vitu gani havipendi.
Otherwise, nilitakiwa kumuuliza huyo mume wako huwa anasukumwa na kitu gani hadi anakukwida wakati sensitive kama huo au ndo kuzidiwa na mahaba!

NI VIZURI KUFAHAMU HAYA.

Ili Mke awe available kwa mume kimwili na kiroho inampasa mume awe sifa zifuatazo:
Ukaribu, uwazi katika mambo yake, anayeeleweka, mtu wa amani, anayempa uhakika mke kwamba ni yeye peke yake ndiye anapendwa na mume wake na pia kumpa uhakika kwamba yeye ni mwanamke mwenye sifa anazozipenda kimwili (beauty) na kiroho.

Je, unawezaje kuwa mume ambaye mke anakuelewa (understanding)?

Ili mke akuelewe mume unahitaji kutumia secret weapon ya sikio lako.
Kumsikiliza tu mke huweza kuonesha kwake kwamba umemuelewa kuliko hata kabla hajamaliza kuongea wewe unamkatiza na kusema ulikuwa unajua anataka kusema kitu gani.

Tofauti kubwa ya mwanamke na mwanaume ni kwamba mwanaume kawaida yupo wired kusikilizwa na si kusikiliza, na mara nyingi mwanaume hupenda kutatua tatizo au matatizo au kutoa jibu kwa ajili ya tatizo lolote, hivyo anapoongea na mke wake kwa kutomfahamu anakuwa na haraka ya kutaka kutoa majibu badala ya kusikiliza tu.
Narudia tena;
Si mara zote mwanamke anapouliza swali au kukwambia kitu anahitaji majibu, mara nyingi anakuwa katika harakati ya kujihusanisha (connection) na wewe na anachahitaji ni sikio lako tu na si namna ya kupata majibu.
Unachotakiwa kufanya ni kumsikiliza na kushiriki katika kuzungumzia hiyo shida yake na kuliona kama tatizo lenu wote.
“The first duty of love is to listen”.
Mwanamke huhitaji mtu wa kumsikiliza tu na sikio lako wewe mume ndilo analihitaji na si uwezo wako wa kutatua tatizo.
Ukimsikiliza, atajisikia vizuri tofauti na ukirukia kukatiza kile anaongea au kuanza kupendekeza solutions kwa kile anakwambia.

Wanaume kujitahidi kutoa solutions za kile mke anaongea au hata kukatiza kile anaongea kwa mume kujifanya anajua mke alitoka kuongea kitu gani ni moja ya matatizo sugu ya kwenye ndoa.
Hata kama wewe ni mwanaume maarufu kutatua matatizo ya wanaume wenzako bado ukiwa na mke wako unatakiwa kumsikiliza tu na sikio lako hadi aridhike.

NI SEX TU?

Kila unaporudi nyumbani unakutana na mkeo anatabasamu namna hii mlangoni?????

Sex si sababu ya msingi au motivator kwa ajili ya mwanaume kutoka nje ya ndoa yake bali ni kukosa emotions, feelings katika ndoa yake.
Yapo magazeti, TV, Movies, blogs, radio na media zingine zinapiga kelele kwa sauti kwamba kukosekana kwa great sex ndiko kunawafanya wanaume kutoka nje ya ndoa zao hata hivyo tafiti ambazo zinakubaliana na Biblia na sayansi pia zinaonesha si sex bali emotions.
Ni kweli kwamba sexual skills, au ufundi wa kufanya sex huleta ladha na utofauti chumbani hata hivyo linapokuja suala la ndoa mambo ni tofauti.
Hitaji kubwa la mwanaume ni kuheshimiwa (respect, appreciation) kutoka kwa mke wake.
Mwanaume yupo wired kujiona ni winner na kitendo cha kukosa respect au appreciation nyumbani humfanya kujiona ni loser, failure na matokeo yake hujiona hapendwi na hujiweka mbali na mke.
Hii ina maana mwanamke anapoona mambo hayaendi sawa ndani ya nyumba kubadilisha sexual style si move nzuri ukilinganisha na kubadilisha namna unavyompa respect na appreciation.
Ili kumlinda mume asitoke nje jambo la msingi ni mara ngapi mume anapata sex na si ufundi au umaridadi ulionao katika kumzungusha kitandani.
Kabla ya kujikanyaga ili kupunguza uzito, dieting au kufahamu style mbalimbali za love makini ni muhimu sana wewe mwanamke kujua unakuwa available kwake mara ngapi kwa wiki au mwezi.
Hujasikia huu msemo:
Mume akipewa sex anakuwa so nice kwa mke wake na asipopata sex anakuwa jeuri.
Mwanaume akiwa appreciated na respected anajiona ni winner na moja ya sababu ya kumpa appreciation ni kumpa sex mara nyingi achana na suala la skills kwanza.
Je, anapokuwa nyumbani unaongea naye vipi?
Hasira, kukefyakefya au kunung’unika na kulalamika tu kwa kila jambo?
Je, unamshukuru na kumpa appreciation kwa kazi zile Anafanya hata kama ulitegemea uwe wajibu wake?
Je, unamsukuma kwa kila jambo unalotaka wewe afanye na hakuna tofauti kati ya mtoto na yeye?
Je, anapofika mlangoni jioni anaoporudi kazini unaonesha sura ya huzuni, hasira, kukata tamaa hadi anajisikia vibaya na kujiona hapo nyumbani yeye ni failure.
Kumbuka wewe mwanaume usipomfanya ajisikia vizuri basi mwanamke mwingine anaweza kufanya ajisikia vizuri na ikawa hatua moja kuelekea kuzamisha ndoa yako.

DALILI KWAMBA ANA "NYUMBA NDOGO"

Dalili za mwanaume anayechepuka

1. ANATUMIA MUDA MWINGI NJE NA NYUMBANI
Huwezi kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja na kila mmoja ukampa muda sawa.
Wengi huanza kubadilika na kukwepa kuwepo nyumbani na mke wake hata kabla ya affair.
Mwanaume kutumia muda mwingine nje ya nyumbani haina maana kwamba ana-cheat bali inaweza kuwa dalili kwamba ana cheat hasa kukiwa na dalili zingine.
Hata hivyo ukigundua mapema unaweza kuzuia na kuepuka maumivu ya cheating.
Wakati mwingine hawa wanaume huwafunga kamba wake zao kwamba
“Nikitaka kutoka nje, naweza hata muda wa kawaida hivyo nikichelewa haina maana na-cheat”
uwe makini na huo usemi kwani ukweli ni kwamba wanaume wengi hutumia muda wa ziada na si muda wa kazi kufanya cheating zao.
Ukiona mume ana dalili za kukwepa kuwepo nyumbani kama ilivyokuwa kawaida, basi inabidi uwe makini na kuchunguza kujua nini kinaendelea.

NINI CHA KUFANYA:
Ni vizuri kukaa pamoja na kujadili pamoja kuangalia kama kuna issues ambazo haridhiki nazo zirekebishwe haraka ili arudi kwenye mstari.
Pia jiulize:
Je, hapo nyumbani kuna amani, heshima, upendo, na utulivu?
Na je, namna unaongea na mume wako kuna respect? Au ni kulalamika, hasira, huzuni na yeye anajiona ni failure na loser?
Inawezekana huko anaenda kunampa kile anakikosa hapo nyumbani au kwako wewe mke.

2. TENDO LA NDOA MARA CHACHE
Kupunguza kwa kiwango cha sex kati ya mke na mume ni dalili mojawapo kwamba kuna kitu hakipo sahihi na mojawapo inaweza kuwa mume anachepuka kwa “yule mwanamke”.
Pia unaweza kuijua hii dalili mapema na ukazuia huzuni kutokea katika ndoa yako kwa kupiga gia ya reverse kwa kuongeza frequency za sex kati yako na mumeo.
Wapo ambao ni wajanja zaidi ambao huendelea na sex kama kawaida ili wasishtukiwe hata hivyo kutokana na kuwekeza kwa “yule mwanamke” automatically akiwa na mke wake hamu hupungua na matokeo ni kupungua kwa uhitaji na kiwango cha sex hushuka.

NINI CHA KUFANYA:
Kwanza jiulize swali hili:
Je, kiwango cha sex ni mara chache kuliko kawaida? Kama ni chini ya kiwango ni vizuri wewe mwanamke pia kulianzisha uone nini kinatokea.
Kama mwanamke Jitahidi kutengeneza mazingira ambayo yatakufanya usijisikie kuchoka sana na kama inawezekana unaweza kumuomba mume wako kukusaidia kazi ndogondogo za pale nyumbani.
Pia fikiria ni kitu gani unaweza kuongeza (kipya) ili kuimarisha sex na kama inawezekana mnaweza kwenda nje ya hapo nyumbani kwa ajili ya kuwa na intimacy zaidi.

3. ANAANZA KUKUKWEPA WEWE MWENYEWE MKE WAKE
Anaweza kukukwepa kwa njia zile mnatumia kuwasiliana iwe mchana au usiku huanza kupunguza.
Unaweza kujikuta simu hazijibiwi, sms hazipewi majibu na mara simu imefungwa.
Kama ana simu ya mkononi anaanza kutembea nayo hadi anapenda kuoga, anapoi-charge kama ni nyumbani basi ataisimamia kama FBI wanaomsimamia terrorist aliyekamatwa kabla ya kujilipua.
Na kuna simu akiipokea No matter what ataenda kuongelea nje au kwenye uchochoro wowote.
Kama upo makini utajua tu something is not right!
Kikubwa zaidi hapendi kuwa na wewe “closer” kitendo hiki hufanya muwe mbali kihisia.

NINI CHA KUFANYA:
Jaribu kuchunguza kama simu unazompigia sinamsumbua kazini au ni jeuri yake tu na ukorofi kwa sababu ya “yule mwanamke”
Ongea naye namna ya kuwa na muda pamoja kwa kila wiki.
Wakati mwingine mpigie simu ya kumpa appreciation kwa ajili ya kitu chochote amefanya badala ya simu za kulalamika na kumfanya ajione failure na loser.
Kama una hints chunguza simu yake ya mkononi na kama huna hints achana nayo kwani hakuna mwanaume anapenda kutembea huku amefugwa video camera usoni kuchunguzwa kila kona anayopita.

4. ANAKUWA CRITICAL
Alikuwa anapenda mapishi yako, unavyoonekana (sura na maumbile), mapenzi yako, namna unapenda bajeti; ghafla from nowhere anaanza kulalamika na kukulaumu kwa kila unachofanya.
Inawezekana tatizo ni yule mwanamke!
Kiti kidogo kikikosewa inakuwa kama kapatia sababu ya kuanzisha mgogoro au vita ya tatu ya dunia.
Wakati mwingine anaweza kuwa mwonezi (harassing)

NINI KIFANYIKE:
Jadili kwa nini mume wako anakuwa critical na wewe muulize kwa upendo bila wewe kuwa critical pia.
Pia jadili kujua tatizo lipo wapi ili lirekebishwe huku wote mkiwa positive.

UMUHIMU WA SALAAMU KWA WANANDOA.

Je, ni muhimu wanandoa kusalimiana mnapoamka asubuhi?

Kwanza fahamu kwamba wanandoa wanapokaa muda mrefu baadhi ya vitu huanza kuchakaa kimapenzi. Hata hivyo upendo na wema husaidia kurudisha moto wa mapenzi na wanandoa kujiona wapya kila umri unavyozidi kuongezeka.
Matendo yanayoonesha wema kwa wanandoa ni gundi inayoshikisha wawili kujiona wapo karibu na moja ya tendo la wema ni kumsalimia mwenzako wakati mnaamka hata kama mmelala kitandani kimoja na hata kama mlikumbatiana usiku mzima au ulimuweka mwenzi wako kifuani usiku mzima.
Anayesalimiwa hujiona anapendwa, ana thamani na pia appreciated.

Tupo kwenye new millennium kiasi ambacho watu tupo busy hata kuamka tunahitaji kuweka alarm ituamshe hata hivyo badala ya kukimbia bathroom kuoga ni muhimu kumpa kwanza salamu mwenzi wako ndipo uendelee na kazi zingine au na ratiba yako.
Tafiti zinaonesha wanandoa ambao husalimiana asubuhi wanajiona ndoa yao ni nzuri sana na wana mahusiano yanayoridhisha.


Je, nini kinafanya maneno ya salaamu ya asubuhi kuwa muujiza katika ndoa na mahusiano?

Unapomsalimia mwenzi wako maana yake unamwambia na kumpa ujumbe kwamba ni asubuhi njema tumeamka pamoja katika upendo na furaha na kwamba unajisikia vizuri kuanza siku mpya na mtu wako na pia unaweka msingi mzuri wa mawasiliano kwa hiyo siku mpya.