Kuna mambo mengi ambayo unaweza kuyaona katika uso wa mtu na yatakupa mwongozo wa kujua kama mtu huyu kweli anafaa au la.
(A) PENZI MASILAHI
Hao ni wale ambao ukikutana naye ni lazima umpe nauli,au la hata meseji ya kukwambia nimefika hawezi kukutumia,tena hata ukimpigia anaonyesha kutofurahia,ni kwa sababu tu umeachana naye hujampa fedha.
Huenda ni kweli hana nauli,lakini kuonyesha kwamba anafaa au hafai ni pale ambapo hata ukimpa nauli bado anataka zaidi.Ainhii ya mpenzi,hafai,anaonyesha yuko kibiashara zaidi...hayo mtaani wanaitwa akina PENZI MASILAHI.
(B) KUKUPIGIA SIMU HADI AWE ANATAKA "NANIII"
Kuna wanaume,hata kumtumia ujumbe mwenzi wake ni shida,kisa anakwambia niko bize,lakini siku akiwa anataka ngono,atawasiliana hadi hadi basi..haya si maisha sahihi,maisha sahihi ni watu kuwa karibu wakati wote kwa maana ya kujuana hali,si zaidi.Kuna wengine pia kusema nakupenda awe kwenye ngono.Tunapaswa kuwa wenza ambao kweli wanatujali muda wote,kwamba ukiumwa ukimwambia mtu anaonyesha kuumia,kwamba ukimwambia mtu nina tatizo anaonyesha kuumia na kuwa nawe daima pembeni kutaka kujua nini hasa kinaendelea.Mtu yeyote ambaye hakujali,huyo hafai katika maisha.
Fuatilia Part 2 yake ...