Thursday, 24 November 2016

USAFI NI MUHIMU.


Jambo moja ambalo kila siku hulalamikiwa na wanawake kuhusu waume zao ni suala la mwanaume kuwa mchafu, kuingia kitandani huku ananuka kama soksi chafu na wakati huohuo unataka kuwa karibu na mke wako kimapenzi kila sehemu ya mwili wako.
Sidhani kama hilo ni jambo la kistaarabu!

Kuna siku kilirushwa kipindi redioni kinachowaomba wanawake kuuliza maswali au kutoa malalamiko kuhusu usafi na tendo la ndoa kuhusu waume zao, tofauti na nchi zinazoendelea ambazo wanawake huogopa kuongea kwa uhuru (in public) kuhusu waume zao, kwa kuwa ilikuwa katika nchi zilizoendelea wanawake waliongea kwa mfululizo na kutoa malalamiko yafuatayo:
Kwanza kuna wanaume hata huwa Hawajali usafi, wapo ambao hata kuoga ni kazi, kupiga mswaki kazi, au kujiandaa kiusafi wakati wa kwenda kitandani na matokeo yake mke hujikuta badala ya kusisimka anakasirishwa.
Saa nne usiku, unaingia kitandani na unataka sex, midevu yako haijanyolewa vizuri na matokeo yake inamchoma mke utadhani kidevu kina sandpaper, hujaoga na jasho la ofisini kupitia kwapa zako linanuka kama compost pile.
Kucha ndefu na chafu kwa ndani utadhani ni kucha za monkey.
Katika utafiti uliofanywa baada ya kuwauliza wanafunzi (chuo) 332 kile ambacho huwavutia zaidi kwa wanaume, iligundulika kwamba namna mwanaume ananukia huvutia zaidi kuliko namna anavyoonekana kwa mwanamke.
“Hii ina maana kwamba ni mwanaume hata kama umepiga pamba za uhakika huku unanukia kama panya aliyeoza huna maana”.
Hivyo ni muhimu sana kwa mwanaume kujifunza kutumia kipande cha sabuni, ni vizuri kuoga kabla ya kujirusha kitandani hata kama ulikuwa na busy day.
Pia Kumbuka kujinusa mwenyewe na kuamini kila kitu kipo shwari si gauge nzuri.
Pia Kumbuka mwanamke ana uwezo mkubwa kunusa kuliko mwanaume.
Usafi na sex ni vitu vinavyoendana huwezi kuvitenganisha.

Monday, 21 November 2016

UKAGUZI WA NAMNA.HII KTK NDOA.

Uwezo wa kumwamini na kujisikia salama na kutulia kati ya wanandoa ni moja ya misingi ya kila mmoja kutoa upendo kwa mwenzake. Bila msingi imara katika kuaminiana au bila kuweza kuimarisha kuaminiana huweza kuleta mzozo mkubwa kwenye ndoa.

Mume na mke hujisikia raha na furaha ya ajabu wakati kila mmoja akifahamu kwamba mwenzake anamwamini (trust) na hii furaha hudumu kwa muda wote ingawa kwa wale wasioaminiana hujikuta wanajiingiza kwenye migogoro na kukwaruzana au mmoja kumkalia mwenzake na kumnyima uhuru na kuwa mtumwa.

Inawezekana wewe ni mwanamke umeolewa na mwanaume ambaye hakuamini kwa lolote, hata ukiondoka na gari ukirudi nyumbani anaanza kukuuliza sehemu zote ulizoenda, umekutana nani, na mmeongea kitu gani ikiwezekana je kwenye gari ulimpakia nani nk.
Haishii hapo bali hujumlisha umbali ambao umemwambia na anaenda kulinganisha na ule umbali ambao gani limesafiri ili ajue ni kweli vinalingana, kama hiyo haitoshi kwa kuwa kuna tofauti na Km 5 anarudi tena kukuuliza imekuwaje ulikoenda na umbali vinatofautiana?

Au umemuomba fedha kwa ajili ya kununua vitu vya kutumia katika familia naye amekwambia kwanza uandike list ya mahitaji yote na bei zake, anakupa pesa kiasi kilekile sawa na vile umeonesha kwenye orodha yako.
Unaporudi anakuomba umuoneshe vitu vyote umenunua na anaomba umpe risiti zote alinganisha kama bei inalingana na vitu umenunua kama haitoshi kila tofauti iliyopo kwenye risiti na orodha ya kwanza inabidi ujieleze.
Anakagua kuhakikisha je vitu umenunua vinalingana thamani na pesa kama kuna kitu umekosea au kina hitilafu anakwambia ukarudhisha au umlipe fedha zake kwani yeye si mtu kwamba anatikisa pesa zinadondoka tu, Kama vile haridhiki anasahihisha hadi spelling za kwenye risiti ilimradi tu aonekane yeye yupo sahihi na si vinginevyo.
Je, hapo kuna kuaminiana?

Inawezekana wa kwako hafanyi hayo hapo juu ila naomba hebu jaribu kujiuliza maswali yafuatayo:
Tafadhari tulia na uwe mkweli na Shahidi ni wewe mwenyewe na moyo wako.
Je, Kila wakati anataka kila kitu kifanyike katika namna anayotaka yeye na si vinginevyo?

Je, Kila wakati yeye ndiye yupo sahihi na si vinginevyo?

Je, Hutafutiza vimakosa hadi vipatikane na hakuna siku anaweza kusifia (compliments)?

Je, Hakupi nafasi kujieleza au kutoa maelezo pale kosa likifanyika?

Je, Hujisikia wivu na kutojiamini hata kama hakuna sababu?

Je, Anakakikisha unajisikia hatia (guilt) kwa kila kitu unafanya?

Kukaliwa na mwenzi kwa namna hii huweza kusababisha mmoja hujiona yupo jela, hana uhuru na mtumwa na hana nafasi kujiachia (express) na matokeo yake ni Kujiona anaishi in hell na hujiona kama anaishi na adui badala ya mume au mke na hujiona kila siku hafai.

Sunday, 20 November 2016

JINSI YA KUFANYA ILI KUMVUTIA MWANAUME MNAPOKUTANA KWA MARA YA KWANZA.

Ukweli kila mwanamke hutuma signal kwa mwanaume na wanaume wengi huweza kufanya detection ya hizo signal kwa sekunde tu na signal za kwanza ambazo mwanamke huzituma na kupokelewa na mwanaume ni mwonekano na lugha ya mwili.

Ni rahisi mno kwa mwanamke kumvutia mwanaume kwani wanaume huvutiwa sana kwa kile wanaona, hata hivyo jambo la msingi kwa mwanamke ni kufahamu kwamba ni aina gani ya attention anahitaji kutoka kwa mwanaume kwani wavuvi huamini kinachodhihirisha aina ya samaki utakayemkamata ni aina ya chambo unayotumia.

Je, unahitaji mwanaume kuvutiwa na wewe kama mwanamke (person) au kama chombo cha starehe (an object) hivyo basi ni muhimu kuzingatia mambo ya msingi ili kupata kile unahitaji.

Mwanamke kujiamini ni jambo la kwanza na msingi kabisa kwa kumvutia mwanaume, kujiamini wewe mwenyewe na mazingira yanayokuzunguka huweza kumvutia mtu anayefanana na wewe, pia utajisikia na kuona watu wanavutiwa na wewe pia.

Mwonekano wako (appearance) ni jambo la msingi sana, mwonekano wako na jinsi unavyotumia mwili wako kuongea huvutia sana hata hivyo ili uliyemvutia abaki na wewe unahitaji personality na uchangamfu.

Pia Kumbuka kwamba jinsi unavyoonekana na kufanya pale mnakutana kwa mara ya kwanza ni muhimu sana kwani akikutana na wewe wakati upo ovyo kuliko wakati wote hawezi nkupoteza muda kuwa na wewe tena (first impression)

Pia hakikisha unampa mwanaume sababu ya msingi ya yeye kukufikiria wewe, hapo inabidi uwe mbunifu kuhakikisha milango yake ya fahamu itafanya akukumbuke, mwanamke hupendeza akivaa nguo soft, pia kuvaa smile usoni kiasi kwamba inakuwa ngumu kwa yeye kukuondoa kwenye mind yake.

Jitahidi kuhakikisha anajisikia yeye ni very important, elekeza akili yako kumsikiliza na pia respond kwa kile anaongea na ku-respect mawazo yake. Cheka wakati anatoa jokes zake hata kama jokes zake hazina kichwa wala miguu hapa ni kuwa na interest kwenye interest zake.

Na mwisho usithubutu kuvaa kitu kingine na ukasababisha yeye ku-fall in love na sanamu kwani siku akikugundua wewe halisi hapatatosha. Onyesha originarity yako na kwamba ni wewe kamili na si mwingine katika haiba, akili na tabia.

Thursday, 10 November 2016

TALAKA UHUMIZA


Talaka huumiza kuliko kifo, hata hivyo kwa baadhi ya wanawake walioolewa sasa wanaona talaka ni uhuru na maisha.
Hujiona wao young and beautiful, hakuna mtu wa kumwambia fanya hili au kile, no demands, hakuna kulaumiwa, kuonywa, kusemwa, kuamrishwa, hakuna kumpikia dinner wala lunch, hakuna utumwa, na akiangalia nje ya ndoa anaona mwanga ni mzuri unaopendeza, anajiuliza kwa nini kuteseka wakati huko nje kuna wanaume wengi tu wananihitaji.
Anafikiria namna anaweza kurudi kwenye maisha ya ujana upya, ulimwengu mpya kwani hakuna kuzozana tena, hakuna kulalamikiana tena, hakuna kuulizana umetumiaje fedha.
Mwanamke anafanya kweli, anaachana na mume wake na kila mtu kuanza kivyake.
Kwa mara ya kwanza anaona mambo ni mazuri, baada ya kusuguana na mume kwa muda mrefu sasa anajiona amepata ahueni, uhuru kwa kwenda mbele.

Sasa nikueleze ukweli wenyewe!

Kawaida wanawake wengi (siyo wote) wanaoachana na waume zao umri wao mara nyingi ni kuanzia miaka 28 – 40.
Maana yake huko nje wanakoamini kuna wanaume wa kuwaoa wapo wanaume wa aina mbili tu, kwanza ni wale ambao nao wameachana na wake zao na pili ni wale ambao ni single (hawajawahi kuoa).
Mara nyingi hawa wanawake huwaogopa sana wanaume wa kwanza hapo juu kwa kuwa ndo walewale ambao wameachana nao, hivyo Hujiuliza swali “kwa nini ameachana na mke wake?”
Hii ni dalili kwamba anaweza kuwa ni big trouble!
Hii ina maana sasa amepunguza idadi ya wanaume ambao anaweza kuoana nao tena kwani tumebakiwa na wanaume ambao hawajawahi kuoa yaani wapo single.
Hapa anamtafuta mwanaume ambaye ana sauti nzuri, mtaalamu wa kuongea, romantic, tender, passionate, mwelewa, mwenye fedha za kutosha, mwenye taaluma nzuri kama vile lecturer, Diplomat au millionaire, mwanaume ambaye hata
Watoto wake watajiona wana baba wa uhakika, ambaye si mlalamikaji, anayeweza kuwafanya kusafiri kila Mahali wanapotaka duniani na mwanaume ambaye atavutiwa na yeye tu na si vinginevyo.
Tuseme wewe mwanamke uliyeamua kutimka kwa mume wako sasa una miaka 38, je unadhani ni rahisi kumpata mwanaume wa aina hii ambaye amekuzidi umri au mnakaribia au sawa.
Ni mwanaume gani mwenye sifa kama hizo anaweza kukubali kuoana na mwanamke aliyeachana na mume wake?
Kama amekuzidi umri na wewe una miaka 38 inakuwaje hadi sasa awe hajaoa, utasema alikuwa anasoma PhD, yaani na PhD yake aje akuoe wewe uliyeachika na mume wako?
Si rahisi kama unavyofikiria!
Ukweli ni kwamba mwanaume wa aina hii anapatikana kwenye TV na Movies!
Anapatikana kwenye mawazo, anapatikana fantasy land na si kwenye maisha halisi!
Nafasi ya kumpa mwanaume wa aina hii ni moja kati ya milioni moja.
“Don’t permit the possibility of divorce to enter your thinking, even in a moment of great conflict and discouragement, divorce is not a solution”
Unaweza kujikuta wewe mwanamke ndiye unawawinda wanaume, kwa taarifa yako mwanaume hayupo wired kuwa kuwindwa badala yake yeye hufurahia kuwinda.
Utajikuta ni lonely na unazeeka haraka kuliko ulivyotegemea.
Wanawake walioolewa ambao walikuwa rafiki zako wataanza kujisikia uncomfortable na wewe, wanakuona ni mwanamke loose na dangerous kwa waume zao na wanaanza kukukwepa na kuweka ulinzi mkali kwa waume zao, na wanaume ovyo nao wanaanza kukushangaa mboni hutaki kulala nao, wanakuona wewe ni cheap target!
Kutafuta talaka ni kupoteza uraia wako, hadhi yako na uhuru wako.
Utajikuta unakaa nyumbani mwenyewe peke yako usiku hadi usiku, hofu itaanza kukuingia, kujiamini kunaanza kupotea, unaanza kujiona huvutii tena na watu wanakudharau.
Talaka ni kubadilisha matatizo ya zamani na kujipa matatizo mapya.
“Guard your relationship against erosion as if you were defending your very lives”
Kumbuka ukishirikiana na mume wako mnaweza kurudi tena kwenye raha ya maisha kama vile mwanzo mlipoanza ndoa yenu.

Sunday, 6 November 2016

NI MAKOSA KUMPA MCHUMBA HUDUMA ZA MKE/MUME


Kawaida huwezi kumpa kila mwanaume huduma za mume wakati bado ni mchumba tu.
Vijana wengi leo wanapochumbiana au kutafuta urafiki wa kawaida kati ya kaka na dada (dating) wengi hawajajua kwamba hiyo ni hatua ya mwanzo kabisa na ni kama usaili tu wa kumpata mtu wa kuoana naye.

Ndoa na uchumba (girlfriend/boyfriend) ni vitu viwili tofauti kabisa uchumba huhusisha kumfahamu mwenzako kama anafaa kuwa mke au mume na ndoa ni agano na kumkubali mtu kuishi naye “ hadi kifo.

Hata siku moja uchumba si ndoa na ndoa si uchumba.

Ukimpa mchumba haki za mume au mke siku mkiachana na huo uchumba (kitu ambacho ni kawaida kama ukiona candidate uliyenae katika uchumba hawezi kwa excellent material ya ndoa) utaumizwa zaidi hasa mwanamke kwani mwanaume anaweza kumpata binti mwingine jioni yake au usiku huohuo na akaendelea na maisha.

Kinachoshangaza pia ni kwamba hata relationship inapovunjika mara nyingi mwanaume huumia kidogo kwa kuwa mwanaume siku zote anapoingia kwenye mapenzi huingia na “open mind”, wakati mwanamke akimpata mwanaume (uchumba) anajiona amampata “the Special one”.

Utasikia akina dada wengi wanasema “Nipo kwenye committed relationship” wakati ni ugirlfriend na uboyfriend tu, ni kweli uposahihi hata hivyo unatakiwa kuacha nafasi kwa ajli ya kuchunguza na si kumfanya huyo mwanaume ni mume wako na kumpa haki zote au services zote kiasi kwamba mahusiano yakivunjika unaanza kusaga meno.

Si busara kumpa mwanaume kila kitu katika mahusiano ya uchumba wakati hujaoana naye. Unamfulia nguo, unalala kwake, unampikia chakula wakati yeye ni boyfriend tu!

Swali ambalo mwanaume anajiuliza ni kwa nini aingie gharama za kukuoa kama umeshakuwa mke hata bila ring kwenye kidole?

Kwa nini akuoe wakati tayari ameshajua kila kitu kuhusu wewe?

Kwa nini anunue ng’ombe kama maziwa na nyama vyote anapata bure?

Kumbuka wazazi wetu walikuwa makini sana na hayo na mwanamke yeyeyote hakujifanya mke wakati ni mchumba tu. Uchumba ni daraja tu la kupita kufikia ndoa. Huwezi kugawa zawadi zote ambazo zipo kwenye begi kabla ya kufika kwa mwenyeji wako katika safari ya kuelekea kwenye ndoa.

Wanaume ni binadamu si Mungu na kila binadamu ana sifa ya kugeuka nyuma pale anapoona njia anayoenda si yenyewe.

Uwe na lengo lakuhakikisha unaweza kuweka mipaka na usimfanye huyo mwanaume ndo kila kitu hapa duniani kwani kuna siku anaweza kubadili uamuzi ndipo kujuta kutakuja.

Ni busara kwa wewe mwanamke hata kama una mchumba uendelee kujihusisha na kazi yako, taaluma yako kiasi kwamba hata ikitokea amekuacha huwezi kuchanganyikiwa.

Kama umewekeza kwa mchumba upendo na mapenzi ya asilimia 100 Je, baada ya kuoana utawekeza kiaasi gain?

Saturday, 5 November 2016

MAMBO HUBADILIKA MKISHAOANA NA KUANZA KUISHI PAMOJA.


Watu wawili wanaopendana na kuishi kila mmoja kivyake ni tofauti sana na watu wanaopendana na kuishi nyumba moja.
Wapo ambao hujiuliza inakuwaje wapenzi wawili waliokuwa wanapendana na kuwa na moto wa mapenzi wa kiwango cha juu sana wakianza kuishi pamoja mambo huanza kubadilika? Pia wapo ambao hukubaliana kwamba baada ya kuoana na kuishi pamoja watajitahidi sana kuhakikisha wanapendana kama mwanzo hata hivyo baada ya kuanza kuishi pamoja hujikuta wamekuwa dada na kaka na hakuna moto wa mapenzi tena.

Jambo la msingi unatakiwa uwe makini kwani kuishi kila mpenzi kwake ni tofauti na kuishi na mpenzi nyumba moja na kitanda kimoja.
Pia wapo wanaume au wanawake baada ya kuoa au kuolewa hufikiria na kuamini kwamba wale wameoana nao si wazuri kama wale walioko nje hata hivyo ukweli ni kwamba kwa kuwa huishi naye masaa 24 kwa siku Ndiyo maana unaona ni mzuri, ukiishi naye kwa saa 24 siku 365 kwa mwaka ndo utajua ni tofauti kabisa.

Inawezekana wakati mnaishi tofauti na mpenzi wako ilikuwa ni kulala saa sita au nane usiku kwani mlikuwa mnapigiana simu na kutumiana sms kiasi ambacho hamkulala hata hivyo baada ya kuoana sasa kila mmoja anakuwa sehemu ya maisha ya mwenzake kila siku inayopita duniani.

Sasa unalala naye, unaamka naye na kula chakula naye. Mnamiliki sebule moja, chumba cha kulala kimoja na kitanda kimoja, frji moja nk. Unajifunza tabia zake kwa undani, unajifunza nini anapenda na nini anachukia, unajifunza udhaifu wake na uimara wake unajua nini anapenda kwenye TV na zaidi rafiki zake watakuja kwenu upende usipende na kufanya au kuongea mambo yao.
Simu za rafiki zake zitapigwa kwenu, utakuwa domesticated man au domesticated woman.

Unapoishi na mtu mwingine taratibu hubadilika, masuala ya sex yatabadilika kwani utalazimika kufahamu hisia zake kimapenzi mahitaji na kile anapenda siku zote na wewe kuwa mbunifu maana unaye kila siku.

Pia unatakiwa kuripoti kila siku kama utachelewa kurudi nyumbani utalazimika kumwambia mapema. Lazima utambue kwamba sasa utakuwa na mtu ambaye ana hofu na wewe kuchelewa au kutokupata habari zako ndani ya saa 6 mchana na huruhusiwi kwenda kimya hadi sita usiku bila yeye kujua upo wapi na kama ni salama.

Pia kuishi pamoja ni kujifunza kuwa kitu kimoja na usipokuwa makini unaweza kujikuta excitement zote za nyuma zinaisha na maisha yanakuwa tofauti na yale kabla ya kuishi pamoja.
Unahitaji kuwa mbunifu wa namna ya kufanya kila siku inayokuja duniani ili mambo mazuri yanayofanya kila mmoja kuwa excited na mwenzake la sivyo badala ya kuishi kama wapenzi mtaishi kama dada na kaka wanaolala pamoja na ambao moto wa mapenzi umezima.

Friday, 4 November 2016

KUACHANA SI SULUHISHO.


Wewe ambaye umeoa au kuolewa na upo unafikiria kuachana na mwenzi wako.

Fikiria upya uamuzi wako.
Fikiria hao watoto mlionao, Fikiria nyakati zote nzuri mlizokuwa nazo pamoja kama mke na mume, Fikiria sehemu tofauti ambazo mlitembelea pamoja, marafiki wazuri mliokuwa nao wote wawili kama mke na mume.
Iepuke talaka kwa gharama zote, sababu zinazokufanya uamue kuachana na huyo mume wako au mke wako zinaweza kuwa ndizo zitakazokuwa sababu mara nyingine tena mbele ya safari kama utaamua kuoa au kuolewa tena.
Sasa unaachana na Jimmy kwa kuwa umechoka na tabia zake za kulewa sana pombe, au kukutaka sex mara nne kwa siku na next time unaweza kujikuta unaachana na John kwa kuwa anakupiga mingumi usiku kucha na yeye sex kwa mwaka mara moja.
Inawezekana unataka kuachana na mary kwa sababu ni msumbufu na anakusema hata kwa vitu vidogo, hata hivyo unaweza kujikuta unaacha na Joyce baadae kwa sababu si mwaminifu katika fedha.
Sasa utaishia wapi na hiyo project ya kuachana na kila unayeoana naye?
Ukiangalia kwa makini kinachobadilika ni tabia na mhusika tu ila wote ni binadamu na binadamu asiye na kasoro bado hajazaliwa hadi leo.


Maisha ni matamu sana kiasi cha kuyapoteza kwa kupeana talaka.
Wanaume wote duniani wanafanana pia wanawake wote duniani wanafanana , na sote ni binadamu.

Wapo wanandoa ni wazembe kiasi ambacho huacha kutumia kila alichonacho kuhakikisha ndoa inarudi kwenye mstari, kukimbilia talaka si jibu bali ni kusukuma tatizo mbele na matokeo yake utakuja kukutana nalo tena mbele ya safari.
Hata kama kuna mtu amekuahidi kwamba ukiachana na huyo uliyenaye basi yeye atakufanya uwe mtu mwenye furaha, hatakuumiza wala kukuacha, ni mwongo na anakudanganya kwani katoka sayari gani na binadamu gani.
Anaonekana anakufaa kwa kuwa huishi naye ukianza kuishi naye utajikuta umeruka mikojo.


Jiulize mwenyewe upya.
Hivi kweli nimetumia uwezo kiasi gani kuhakikisha mwenzi wangu anajua namna tunahitaji kuirudisha ndoa yetu kwenye mapenzi upya kama tulivyoahidiana siku tunaoana?

Je, ni kweli nimefanya kila linalowezekana kusamehe na kusahau?

Je, ni kweli tunataka kuachana na kupeana talaka kwa sababu za msingi?

Kabla ya kuwasiliana na ndugu zako, rafiki zako, washauri wako, wanasheria au wachungaji wako Jaribu kukaa mwenyewe, na mwenzako kujadili upya na kwa upendo namna ya kutatua tatizo lenu na hakuna anayejua shida ya ndoa yako isipokuwa wewe na mwenzi wako.
Usifanye uamuzi wa kuachana kwa haraka ukiamini unaingia kwenye uhuru.
Dawa ya kuachana au talaka ni kusamehe bila masharti.